Mgambo wa Manispaa ya Morogoro wakimkamata mkazi ambaye hakufahamika jina lake kwa kosa la kuchafua mazingira kwa kujisaidia haja ndogo.Manispaa hiyo imepitisha sheria ya usafi wa mazingira kwa kuweka kiwango cha adhabu ya shilingi 50,000 kwa yeyote atakayekamatwa akichafua mazingira.