Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali Eliezer Feleshi amesema tukio la kumwagiwa tindikali kwa raia wawili wa Uingereza sio la kigaidi. "matukio haya yasichukuliwe jumla jumla, sisemi moja kwa moja kuwa tukio hilo ni la kigaidi ila naomba tuhamasishe jamii ya watanzania utii wa sheria bila shuruti, na tusaidie vita dhidi ya matumizi mabaya ya tindikali" - Alikuwa anajibu swali kama tukio la Tindikali nalo ni la kigaidi kama yale aliyopitisha ofisini kwake yafunguliwe mashtaka ya Ugaidi yaliyokataliwa na Mahakama
↧