Quantcast
Channel: MATUKIO NA VIJANA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 20290

Mkuu mpya wa kikundi cha maslahi ya biashara cha Nairobi aeleza dira

$
0
0
Mmiliki wa hoteli David Gachuru ni mwenyekiti mpya wa Chama cha Biashara cha Wilaya cha Kaunti ya Nairobi. 
Chama cha Biashara cha Wilaya cha Kaunti ya Nairobi (NCBDA) kimewakutanisha pamoja wamiliki wa biashara na watendaji wakuu katika mji mkuu wa Kenya kuzishawishi serikali za kaunti na taifa kuhusu masuala ambayo yanaathiri jamii ya biashara, kama vile kuzuia uhalifu na maendeleo ya miundombinu, pamoja na mambo mengine.
Mwezi Julai, shirika liliweka chapa mpya, kubadilisha jina lake na kumchagua David Gachuru kama mwenyekiti wake mpya. Gachuru, meneja mkuu wa Sarova Stanley, hoteli ya nyota tano, alichukua nafasi ya Timothy Muriuki.
Gachuru alizungumza na Sabahi kuhusu dira yake kwa Nairobi, ikiwa ni pamoja na shughuli zinazohusiana na usalama na uchumi.

Sabahi: Vijana wengi wanasema ni vigumu zaidi kupata kazi Nairobi kuliko katika miji mingine. Mpango wa NCBDA ni upi kwa ajira ya vijana?

David Gachuru: Nairobi inakumbwa na tatizo la ukosefu wa ajira kwa sababu katika kaunti nyingine vijana wanakuja kutafuta ajira Nairobi.

Tunawashawishi wanachama wetu kuajiri vijana zaidi katika makampuni yao, ili mradi wana vyeti sahihi vya masomo, bila ya kusisitiza kuwa na uzoefu kwanza, akama ilivyo kwa sasa. Pia tunasaidia biashara kubwa na ndogo za vijana zinazozalisha kipato kwa kufadhili warsha za kuwezesha vijana wajasiriamali.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 20290

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>