Quantcast
Channel: MATUKIO NA VIJANA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 20290

MARUBANI WAADHIBIWA KWA KUACHA NDEGE IKIJIONGOZA HUKU WAKIPIGA PICHA NA MREMBO ANGANI

$
0
0

Mmoja wa marubani hao akiweka pozi la picha na mrembo huyo. KULIA: Mrembo Ly Nha Ky.
Marubani wawili wameadhibiwa baada ya kudaiwa kupiga picha na mrembo mmoja ndani ya chumba cha marubani katikati ya safari angani.



Marubani hao wa Shirika la Ndege la Vietnam walipigwa faini na kusimamishwa kazi kwa madai ya kumruhusu mrembo aliyegeukia uigizaji, Ly Nha Ky kukaa kwenye kiti cha rubani msaidizi wakati wa safari ya ndege hiyo kutoka Hong Kong kwenda Hanoi mwezi uliopita.
Watu hao walisimamishwa kazi baada ya picha za balozi huyo wa zamani wa utalii kwa Vietnam kupiga picha ndani ya kiota cha marubani na miwani ya jua ya marubani hao ilikutwa kwenye mtandao na kuchapishwa kwenye tovuti moja ya habari.

Mkaguzi mkuu wa Mamlaka ya Anga ya Vietnam alisema uamuzi wa marubani hao kilikuwa 'tishio kwa usalama wa anga na wanatakiwa kuadhibiwa,' kwa mujibu wa tovuti ya habari ya Toui Tre.
Ndege hiyo ilikuwa ikiruka kwa mfumo wa kujiongoza yenyewe (auto-pilot) wakati huo lakini taratibu za usalama wa anga zilikuwa zimevunjwa sababu rubani huyo msaidizi aliacha kiti chake na marubani hao walikuwa wamemwingiza mtu asiyeruhusiwa ndani ya chumba cha marubani.
Katika picha nyingine, mrembo huyo anaonekana akiwa amewakumbatia wahudumu wawili wa ndege hiyo.
Msemaji wa Shirika la Ndege la Vietnam alieleza vyombo vya habari vya Vietnam kuwa hawakuwa na taarifa kuhusu tukio hilo na kwamba watafanya uchunguzi baada ya ripoti rasmi kutoka kwa wafanyakazi.
Kapteni Nguyen Ngoc Nhu Y alitozwa faini ya Pauni za Uingereza 216 wakati msaidizi wake Nguyen Xuan Hai alitozwa faini ya Pauni za Uingereza 92.
Mfumo wa 'auto-pilot' haumaanishi kwamba rubani anaweza kutoka kwenye chumba chake. Wanatakiwa kuwamo kufuatilia njia inamopita ndege na kuweza kuzima mfumo huo wa auto-pilot kama ikihitajika hivyo.
Tukio hilo limekuja baada ya marubani wawili kuwa wamesimamishwa kwenye Shirika la Ndege la India baada ya kudaiwa kuiacha ndege aina ya Airbus iliyobeba abiria 166 ikijiongoza yenyewe na kumwelekeza mhudumu kubeba majukumu yao wakati wao wakiuchapa usingizi katika sehemu ya abiria wa daraja la pili.
Ndege hiyo mnamo Aprili 12 ilikuwa ikisafiri kutoka Bangkok kwenda New Delhi ndipo marubani wote wasaidizi na rubani huyo walipotoka kwenye chumba chao baada ya kuwa wametumia muda kadhaa wakiwaelekeza wahudumu wawili jinsi ya kurusha ndege.
Lakini wawili hao walilazimika kurudi haraka na kuiweka sawa ndege hiyo A-320 baada ya mmoja wao kuzima kwa bahati mbaya mfumo huo wa 'auto-pilot', vyanzo vya habari vilieleza.
Shirika hilo la taifa la usafiri lilimsimamisha rubani huyo wa Airbus A-320 wa ndege ya Bangkok-New Delhi, msaidizi wake, na wahudumu wawili ambao kwa bahati mbaya walizima mfumo wa auto-pilot kwenye chumba cha marubani hao wakati ndege ikiwa kwenye mwendo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 20290

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>