Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akimjuilia hali Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi na Utumishi wa Umma Mhe. Haroun Ali Suleiman katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amefika katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam kuwajuilia hali Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi na Utumishi wa Umma Mhe. Haroun Ali Suleiman, pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu Mzee Cleopa David Msuya waliolazwa katika hospitali hiyo.
Viongozi hao wamelazwa katika hospitali hiyo wakisumbuliwa na matatizo ya moyo. Wakizungumza na Makamu wa Kwanza wa Rais, wamesema wanaendelea vizuri na kwamba afya zao zinaendelea kuimarika siku hadi siku, tofauti na walipofikishwa hospitalini hapo.
Waziri Haroun anatarajiwa kupelekwa nchi Afrika ya Kusini kwa uchunguzi na matibabu zaidi. Kwa upande wake Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amewaombea viongozi hao wapone haraka ili waendelee na majukumu ya kulitumikia taifa.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akimuombea dua Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi na Utumishi wa Umma Mhe. Haroun Ali Suleiman, alipokwenda kumjulia hali katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akimjuilia hali Waziri Mkuu mstaafu Mzee Cleopa David Msuya katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akimjuilia hali Waziri Mkuu mstaafu Mzee Cleopa David Msuya katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Picha na Salmin Said, OMKR
Picha na Salmin Said, OMKR