Quantcast
Channel: MATUKIO NA VIJANA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 20290

Nairobi yadhamiria kushughulikia uhaba wa maji unaojitokeza kwa mabwawa mapya

$
0
0

Wakaazi wakijaza maji kwenye mapipa kutoka kwenye bomba katika makaazi duni ya kibera ya Nairobi Machi 2007.
Wakati serikali ya Kenya ikianzisha ujenzi wa mabwawa ya maji mawili mapya ili kukidhi mahitaji ya maji safi huko Nairobi, wataalamu wa tasnia hiyo wamesema hili litatatua tatizo kwa muda mfupi labda usimamizi mzuri wa rasilimali ya maji utekelezwe.
Serikali ilialika zabuni kutoka kwa makampuni ya ndani na ya kimataifa katika tangazo lililochapishwa katika magazeti ya ndani tarehe 9 Desemba kwa ajili ya ujenzi wa mabwawa ya Maragwa na Ndarugu. Tarehe 14 Machi ni ya mwisho ya kuomba zabuni, ambapo baada ya hapo itachagua kampuni ndani ya muda wa wiki.
Mabwawa haya mapya yanatarajiwa kuongeza usambazaji wa maji huko Nairobi na kurahisisha msukumo katika bwawa la Ndakaini, ambalo linasambaza asilimia 80 ya maji yanayotumika katika jiji hilo, kwa mujibu wa Mbaruku Vyakweli, meneja wa masuala ya ushirika kwa Maji ya Jiji la Nairobi na kampuni ya uwekaji wa mabomba ya maji machafu. (Maji ya Nairobi).
Ujenzi wa mabwawa hayo mawili umepangwa kukamilika ndani ya kipindi cha wiki 42 toka tarehe ya kuanza na ni sehemu ya mpango mkuu endelevu wa serikali kwa jiji hilo, Usambazaji Mkubwa wa Maji kwa Nairobi, ambao unalenga kuwezesha asilimia 80 ya kaya za jiji hili kupata maji safi na maji ya bomba yasiyoingiliwa.

"Mabwawa hayo mawili yatasaidia kuondoa tatizo la bomba kukauka maji wakati wa kipindi cha ukame," Vyakweli aliiambia Sabahi. "Mabwawa ya ziada ya maji yatatupa kiasi cha maji cha kutosha katika sehemu zote za jiji. Hili litatuwezesha kusimamisha programu kali ya usambazaji wa maji ambayo kwa sasa inatumika."

Viewing all articles
Browse latest Browse all 20290

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>