Quantcast
Channel: MATUKIO NA VIJANA
Viewing all 20290 articles
Browse latest View live

SPIKA MAKINDA AFUNGUA GYM YA MAZOEZI YA BUNGE KWA AJILI YA WABUNGE

$
0
0

DKT.SHEIN AFUNGUA MADRASA QAMARIA MATEMWE

$
0
0
IMG_3150Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt .Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Sheikh Yakob Mfadhili wa Madrasa Qamaria wakati alipowasili katika Kijiji cha Kijini Matemwe Mkoa wa Kaskazini Unguja leo kuifungua rasmin Madrasa hiyo.[Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]

IMG_3165Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt .Ali Mohamed Shein,akifungua pazia kuashiri  ufunguzi wa Madrasa Qamaria katika kijiji cha Kijini Matemwe Kaskazini Unguja leo,madrasa hito iliyojengwa na Jumuiya ya ALFATAH ambapo itawanufaisha watoto wa kijiji hicho kujipatia Elimu ya Qurani na hadith mbali mbali,(wa kwanza kulia) mwenyekiti wa CCM Mkoa Kaskazini Mhe,Haji Juma Haji na Mkuu wa Mkoa huo Mhe, Pembe Juma Pembe .[Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]
IMG_3188 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt .Ali Mohamed Shein,akipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Alfatah Rashid Salim,ambayo imejenga madrasa Qamaria katika kijiji cha Kijini Matemwe Mkoa wa Kaskazini Unguja,wakati  alipotembelea vyumba vya   Madrsa hiyo baada ya kuifungua rasmin leo ,[Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]
IMG_3216 Baadhi ya wanafunzi wa Madrasa Qamaria ya Kijiji cha Kijini Matemwe  Mkoa wa Kaskazini Unguja,wakimsikiliza  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt .Ali Mohamed Shein,alipokuwa akitoa nasaha zake kwa wananchi na wanafunzi hao ,katika suala zima la Elimu ya Quran,baada ya kuifungua rasmi madrasa Qamaria iliyojengwa kwa usimamizi wa Jumuiya ya ALFATAH,ufunguzi huo ulifanyika leo.[Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]
IMG_3246Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Omar Kabi,alipokuwa akimkaribisha  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt .Ali Mohamed Shein (kushoto) kuzungumza na wananchi na wanafunzi wa madrasa Qamaria ya Kijiji cha Kijini Matemwe Mkoa wa kaskazini Unguja baada ya kuifungua leo,(kutoka kulia) Mfadhili wa Ujenzi Sheikh Yakub ,Katibu wa Mufti Sheikh Fadhil Suleiman Soraga na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe,Haji Juma Haji.[Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]
IMG_3300ais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt .Ali Mohamed Shein (wa tatu kushoto) pamoja na Viongozi wengine na Mfadhili ujenzi wa Madrasa Qamaria Sheikh Yakub (kulia) wakiitikia Dua iliyoombwa baada ya kumalizika kwa hafla ya ufunguzi wa madrasa Qamaria katika Kijiji cha Kijini Matemwe Mkoa wa kaskazini Unguja leo.[Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]

PROF. MAGHEMBE AKUTANA NA UJUMBE WA SERIKALI YA SINGAPORE

$
0
0
???????????????????????????????Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe akiwa na mgeni wake, Waziri Mwandamizi anayeshughulikia Mambo ya Nje na Ndani wa Singapore, Masagos Zulkifli wakielekea kwenye chumba cha mkutano.

???????????????????????????????Baadhi ya wataalam waliombatana na ugeni kutoka Singapore uliomtembelea Prof. Maghembe
???????????????????????????????Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe (katikati) akiwa na, Waziri Mwandamizi anayeshughulikia Mambo ya Nje na Ndani wa Singapore, Masagos Zulkifli (kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Inj. Bashir Mrindoko (kulia).
???????????????????????????????
Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe na Waziri Mwandamizi anayeshughulikia Mambo ya Nje na Ndani wa Singapore, Masagos Zulkifli, wakibadilishana zawadi.
………………………………………………………
Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe leo mchana amekutana na Waziri Mwandamizi anayeshughulikia Mambo ya Nje na Ndani wa Singapore, Masagos Zulkifli kuzungumzia Maendeleo ya Sekta ya Maji nchini ofisini kwake Ubungo Maji Dar es Salaam.
“Tunatekeleza miradi mikubwa mitatu Nchini, mmojawapo ni ujenzi wa Bwawa kubwa la Kidunda, mkoani Morogoro ambalo litasaidia kuongeza upatikanaji wa maji jijini Dar es Salaam kwa miaka 20 ijayo,” alisema Waziri Maghembe.
“Hivyo, tunahitaji Ushirikiano wa Taasisi za Kibinafsi na Kiserikali kwa Maendeleo ya Kiuchumi Nchini (PPP) katika kuhakikisha tunatekeleza miradi ya maji na kuinua sekta hii, maana kutegemea bajeti ya Serikali pekee haitoshelezi kufikia malengo makubwa tuliyojiwekea kama Wizara.” alisisitiza Prof. Maghembe.
Pia, Waziri Maghembe alizungumzia changamoto tatu kubwa zinazoikabili Wizara yake katika kuhakikisha maji yanafika katika kila nyumba kwa wakazi karibu milioni 3.3 wa Dar es Salaam, ujenzi wa miundombinu ya majitaka na upotevu wa maji na kusisitiza ni jambo la kupatiwa ufumbuzi haraka iwezekanavyo.
Katika mazungumzo hayo, Waziri Maghembe alimuomba mgeni wake kuhakikisha nchi yake inawekeza katika Sekta ya Maji ambayo ni muhimu katika nchi hii, na ikizingatiwa eneo la Kusini mwa Tanzania linategemea kushamiri kwa viwanda na wingi wa watu baada ya kugundulika gesi na hivyo uhitaji wa maji utaongezeka kwa kasi.
Aidha, Waziri wa Singapore, Masagos Zulkifli alisema watahakikisha wanawekeza na kuleta maendeleo katika sekta ya maji na kutumia wataalamu na uzoefu walionao kutoka nchi yao. Huku akisisitiza kufanikisha zoezi la uunganishaji mabomba kwa kila nyumba, kujenga miundombinu ya majitaka nchi nzima na upotevu wa maji.
Waziri huyo wa Singapore aliambatana na ujumbe mkubwa uliojumuisha wataalamu mbalimbali wa sekta tofauti nchini humo, ambao wapo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tano.

LUPITA NYONG’O NA FAMILIA YAKE KUTUA TAMASHA LA 17 LA ZIFF

$
0
0
DSC_0021
Mkurugenzi Mkuu wa ZIFF, Profesa Martin Mhando (wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kuzindua rasmi Tamasha la Filamu la nchi za Majahazi la 17 maarufu kama Zanzibar International Film Festival (ZIFF). Kulia Msaidizi wa Kitengo cha habari ZIFF, Lara Prieston, Kushoto ni Meneja wa Tamasha la ZIFF, Daniel Nyalusi (Dean), Afisa Mawasiliano wa ZIFF, Hassan Musa "Has T" (wa pili kushoto) na Music Coordinator wa ZIFF, Edward Lusala (katikati). Picha na Zainul Mzige wa modewjiblog (FS)

Na Andrew Chale
DUNIA inatarajia kushuhudia tukio kubwa na la kihistoria ndani ya viunga vya Ngome Kongwe ndani Mji Mkongwe wa Stone Town, Unguja, kwa watu wa mataifa yote watakapoungana na kushuhudia ‘Hatma ya Pamoja’ (A common Destiny) Juni 14 hadi 22, 2014, katika Tamasha la Kimataifa la filamu la Zanzibar (ZIFF).
Tamasha hilo maarufu kama filamu la nchi za Majahazi ZIFF, kwa mwaka huu linatarajiwa kufanyika kwa mara ya 17, tokea kuanzishwa kwake.
Akizungumza mapema leo jijini Dar es Salaam, kwenye halfa maalum ya uzinduzi wa tamasha hilo la 17, kwa wandishi wa habari iliyofanyika Goethe Institut kituo cha utamaduni, Mkurugenzi Mkuu wa tamasha hilo, Profesa Martin Mhando, alisema tamasha hilo msimu wa mwaka huu linatarajiwa kuwa moto kwani linakuja na mambo mbalimbali yenye kuleta mabadiliko ya hali ya juu.
Ni kutokana na mabadiliko hayo, Profesa Mhando anasema tasnia ya filamu kwa Tanzania inahitaji kubadilika ikiwemo wasanii wenyewe kujituma na hata kuingia darasani ili kufanya kazi zenye uhakika.
Akimaanisha kila msanii wa filamu aweze kufikia malengo yake, hana budi kujifunza na kushirikisha wale waliotangulia katika tasnia hiyo.
Anazungumziaje kaulimbiu ya ‘A Common Destiny’
Prof. Mhando amesema kauli mbiu ya mwaka huu yenye kusema Hatma ya pamoja yenye maana ya ‘A common Destiny’, ina lengo la kuwakutanisha watu wa mataifa mbalimbali kuwa kitu kimoja na kufurahia kwa pamoja ikiwemo kubadilishana mawazo kwa pamoja kwa tasnia ya filamu, muziki, kwa mlengo ya kujenga.
“Tukiwa na haja moja, kuishi kwa amani na kuleta mapinduzi ya kiuchumi, kifikira na maendeleo kwa amani, ZIFF kwa kutumia dira hiyo hasa kupitia filamu zetu za ndani zenye mchanganyiko wa utamaduni na asili yetu.
“Wazanzibari na hata wageni watakaoshuhudia filamu hizi wataweza kuchukua utamaduni huo na kuupeleka nje kwa furaha kubwa katika kufikia hatma ya pamoja” amesema Prof. Mhando.
DSC_0082
Music Coordinator wa ZIFF, Edward Lusala akisisitiza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na wasanii watakaotoa burudani kwenye tamasha hilo.
Lupita-Nyong-o-729-620x349
Lupita Nyong’o, Genevieve ndani ya nyumba
Tukio kubwa ambalo kwa sasa Tanzania hasa kwenye viunga vya Zanzibar na nchi nyingine duniani katika tamasha hilo la 17, ni ujio wa msanii wa Kenya na Mexico, Lupita Nyong’o, atakayeudhuria utoaji wa tuzo hizo za ZIFF mwaka huu.
Lupita ambaye ametwaa tuzo za Oscar na nyingine nyingi na kupelekea kutikisa Hollywood kwa sasa ni miongoni mwa mastaa watakaokuwa kwenye tamasha hilo huku akitarajiwa kuambatana na wazazi wake wote wawili pamoja na wadogo zake.
Prof. Mhando amesema tayari wazazi wote wawili wa Lupita akiwemo Dorothy na Peter Anyang’ Nyong’o, watakuwapo kwa siku zote 10 kwenye tamasha hilo huku Lupita mwenyewe akiahidi kuangalia uwezekano wa kuhudhuria japo katika utoaji wa tuzo kama ratiba za shughuli zake hazita mbana.
Prof. Mhando alisema Lupita ni zao la ZIFF na ndiyo iliyomfungulia mwanya wa kujulikana na baadaye alienda kusoma zaidi masuala hayo ya filamu, ambapo alishiriki ZIFF 2007 kama Volunteer.
Mara nyingi staa huyo amekua akihudhuria matamasha na halfa mbalimbali za utoaji wa tuzo na zawadi zingine huku akiwa ameambatana na wazazi wake wote wawili.
Lupita mbali na tuzo hiyo ya Oscar, kupitia filamu ya ‘12 Years a Slave’ pia filamu hiyo imempatia tuzo mbalimbali zikiwemo: tuzo ya Steve McQueen kama mwigizaji mwenye mvuto, mwigizaji bora wa kike aliyeshirikishwa, ‘Academy Award’, ‘Screen Actors’ Guild Award’, ‘NAACP Image Award’, ‘Independent Spirit Award’, ‘Broadcast Film Critics Association Award’, na nyingine nyingi.
Genevieve-Nnaji-Cover
Genevieve Nnaji.
Mbali na Lupita, katika kuongeza utamu wa tamasha hilo, mastaa wengine nguli wa Afrika kwa mwaka huu wanaotarajiwa kuwapo katika ushuhudiaji wa utoaji wa tuzo hizo ni pamoja na muigizaji na mwanamitindo nyota wa Nigeria, Genevieve Nnaji.
Wengine ni Amr Waked (Misri), Faouzi Bensaidi (Morocco), Nadia Buari, Richard Mote Damijo ‘RMD’, John Dumelo, Desmond Eliot na Florence Masebe.
DSC_0067
Afisa Habari wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Mpango wa Chakula Duniani (WFP), Fizza Moloo akizungumzia kuhusiana na Filamu iliyopewa jina la "Women with Altitude" iliyoandaliwa na WFP ambapo ndani yake imeshirikisha wanawake wa kitanzania watatu waliofanikiwa kufika kilele cha Mlima Kilimanjaro wakiwa wameambatana na wenzao nane kutoka Nepal na kuzungumzia changamoto mbalimbali wakati wa kupata elimu na maisha kwa ujumla itakayoonyeshwa kwenye tamasha hilo tarehe 17/6/2014 saa 19:15 jioni ukumbi wa Old Fort visiwani Zanzibar.
Filamu ya Mandela kufungua pazia
Jumla ya filamu 79, kutoka mataifa mbalimbali zinatarajiwa kuonyeshwa huku filamu iliyoingia kwenye tuzo za Oscar, ya Mandela: ‘A Long Walk to Freedom’ ndiyo itakayofungua pazia kwenye tamasha hilo, Juni 14.
“Katika filamu hizo 79 za kimataifa zitaoneshwa ZIFF, nyingi zikiwa zinatoka katika nchi za Kiafrika na filamu ya Mandela imepata bahati ya kuwa ya ufunguzi”, amesema Profesa Mhando.
Pia Profesa Mhando amesema kuwa zitakuwepo filamu zinatoka katika nchi 35 zikiwemo filamu fupi 38, filamu ndefu za kuburudisha 24 na makala 17.
DSC_0137
Meneja wa Tamasha la ZIFF, Daniel Nyalusi "Dean" akionyesha kitabu chenye ratiba nzima ya tamasha hilo litakalorindima visiwani Zanzibar kuanzia Juni 14 hadi 22 mwaka huu.
Burudani zitakazopamba
Kwa upande wake, Edward Lusala anayeshughulikia muziki kwenye tamasha hilo la 17, anasema kuwa, wamejiandaa kutoa burudani ya aina yake ambayo itaacha historia kwa mwaka huu.
Lusala amesema jumla ya makundi 18 yanatarajiwa kutumbuiza. Huku kwa wasanii gwiji wakiwemo pia Didier Awadi kutoka nchi ya Senegal na Habib Koite (Mali) wanatarajiwa kuja kuishika Zanzibar na viunga vyake.
“Wasanii Koite na Didier ni miongoni mwa wasanii wakubwa sana na wenye heshima kubwa hasa kwa muziki wao kwani wanapiga kimataifa hasa katika matamasha makubwa na wamekuwa wakipiga miziki ya kipekee. Hivyo watu wote watafurahia” amefafanua Lusala.
Ameongeza kuwa, wasanii wengine ni pamoja na Farid Kubanda ‘Fid Q’, Ambwene Yesaya ‘ Ay’, Sauti Soul, Mzungu Kichaa, Ras Inncent Nganyagwa, Grace Matata na wengine wengi ambao watatoka Tanzania.
Na kuongeza kuwa kwa sasa AY yupo nchini Malawi akijifua na moja bendi maarufu ya muziki wa Live ambapo anatajiwa kukaa jukwaani kwa zaidi ya lisaa limoja na nusu huku akiimbaLIVE.
Pia vikundi vya muziki nguli toka Tanzania, Egypt, Kenya, Uganda, Malawi na Afrika ya Kusini vitatumbuiza kila siku katika tamasha hilo.
Aidha, Lusala amesema kuwa, kwa mwaka huu wanatarajia kufanya ‘surprise’ kwa kumleta msanii mkubwa ambaye bado wapo kwenye mazungumzo na msanii huyo kutoka Afrika kusini.
Kwa upande wake Meneja wa tamasha hilo, Daniel Nyalusi amewataja wadhamini wa tamasha hilo ni pamoja mdhamini mkuu ZUKU Pay tv, huku wengine ni Ethiopian Airlines, Tanzania Media Fund TMF, ComNet, Cello, Air Uganda, Gina Din, FASTJET and United Petroleum. Wengine ni shirika la Rosa Luzemburg Foundation, Arterial Networking, Steps International, Azam marine, Prime Time Promotions, Goethe Institut na wengine wengi.
ZIFF moja kati ya matamasha ya filamu makubwa duniani hukutanisha wadau katika tasnia ya filamu. Wakiwemo waigizaji wa siku nyingi na maarufu, waongozaji, waigizaji wachanga na wanafunzi kutoka ulimwenguni kote
DSC_0119
Meneja wa Biashara wa shirika la ndege la Fastjet, Jean Uku akizungumzia udhamini wao kwenye tamasha hilo ambapo wametoa tiketi za safari ya washiriki kutoka Afrika Kusini watakaoshiriki kwenye tamasha hilo.
DSC_0084
Msanii wa Hip Hop, Harry Kaale kutoka kundi la One "The Incredible" akielezea namna watakavyotoa burudani na elimu kwa vijana kwenye tamasha hilo.
DSC_0105
Msanii Mzungu Kichaa akiwashukuru ZIFF kwa kutoa nafasi kwa wazalendo kuonyesha vipaji vyao kwenye tamasha la ZIFF.
DSC_0108
DJ maarufu Kahlil Jacobs-Fantauzzi kutoka Puerto rico akisisitiza kutoa burudani ya aina yake kwenye tamasha hilo.

WASANII WATAKAOPIGA SHOW KESHO KILI TOUR WAMEWASILI NDANI YA KAHAMA,TAZAMA PICHA 8 HAPA WAKIHOJIWA NA KAHAMA FM

$
0
0


Wasanii watakaopanda jukwaani katika Kilimanjaro Music Tour wamewasili mjini Kahama kwa ajili ya show.
Wasanii hao ambao ni Shilole, Christian Bella, Madee, Mwana FA, AY, Rich Mavoko, Jambo Squad na Weusi wanatarajiwa kupanda jukwaani siku ya Jumamosi katika uwanja wa halmashauri ya Kahama kwa kiingilio cha Sh 2500. Mara baada ya kuwasili Mwana FA, AY, Rich Mavoko na Shilole walifanyiwa mahojiano na Kahama FM ambapo walielezea namna walivyojipanga kwa ajili ya show.

Ay na Mwana FA wakitaniana ndani ya Kahama FM leo
 Ay akiongelea show ya kesho ndani ya kahama Fm

 Shilole akiongea na mashabiki wake kupitia Kahama FM leo
Shilole na Ay wakipiga picha ya Pamoja ndani ya kahama FM

Mh. Lowassa azindua bwawa kubwa la maji MONDULI

$
0
0




Waziri mkuu mstaafu an mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa akifungua kitambaa kuashiria uzinduzi wa bwawa kubwa la maji la Leken katika kata ya Seleli wilayani Monduli leo Ijumaa.Bwawa hilo ambalo limegharimu kiasi Cha shilingi bilioni moja unusu, lina ukubwa wa kilomita tatu.





Mh Lowassa na mkewe wakivishwa nguo za kimasai ikiwa ni ishara ya shukrani kutoka kwa wananchi wa Seleli,kwa kufanikisha ujenzi wa bwawa hilo ambalo ni mkombozi mkubwa kwa wakaazi wa eneo hilo an maeneo ya jirani


Ribery nje ya Kombe la Dunia

$
0
0
Ribery nje ya Kombe la Dunia
Mkufunzi wa Ufaransa amedhibitisha kuwa mshambulizi Frank Ribery hatashiriki kombe la dunia kutokana na jeraha.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 na anayechezea klabu ya Bayern Munich alijeruhiwa mgongoni wakati wa mazoezi siku ya Ijumaa.
“Ilimbidi kuwacha kufanya mazoezi kwa kuwa alikuwa akihisi uchungu mwingi sana,” Deschamps aliwaambia wanahabari baadaye.
‘’Hataweza kufanya mazoezi wala kucheza kwa majuma kadhaa.”
Ribery amejeruhi mgongo mazoezini
Lyon's Clement Grenier pia atakosa mashindano hayo kwa jeraha la nyonga.
Kiungo cha kati wa Southampton Morgan Schneiderlin na mshambulizi wa Montpellier Remy Cabella wamejumuishwa kikosini ili kucheza kwa niaba ya wawili hao.
Ribery alipelekwa kupigwa picha ya MRI, ambayo ilidhibitisha kiwango cha jeraha hilo.

Riberi alichaguliwa kuwa mchezaji wa tatu bora zaidi duniani mwaka wa 2013 nyuma ya mshindi wa Ballon d’Or Christiano Ronaldo wa Real Madrid na mshambulizi wa Barcelona Lionel Messi.

Emirates yatoa punguzo maalumu la bei za tiketi kwa Watanzania wanaokwenda Chicago, Marekani

$
0
0

Wasilisha ombi la tiketi kabla ya Agosti 5 kwa safari za hadi Novemba 30, 2014


Shirika la Ndege la Emirates, linalosifika kwa kutoa huduma bora za usafiri wa anga kwa abiria kwa mataifa mbalimbali, limetangaza ofa maalumu kwa Watanzania watakaokwenda Chicago nchini Marekani, kupitia Dubai wakitokea Dar es Salaam. Punguzo hilo au ofa hiyo maalumu ni kwa madaraja ya abiria wa kawaida yaani Economy Class na daraja la wafanyabiashara ‘Business Class’.

Emirates ilitangaza ofa hiyo mapema Februari mwaka huu na ndege zake zitakuwa zikitua kwenye Uwanja wa  Ndege wa Kimataifa wa Chicago O’Hare. Safari hizo za kila siku zitaanzia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai, Terminal 5 ifikapo Agosti 5, 2014 na ndege ya Emirates itakayotumika ni aina ya Boeing 777-200 LR na hivyo kutoa fursa kwa Watanzania kutembelea jiji hilo la tatu kwa ukubwa nchini Marekani.

Gharama za tiketi ni kuanzia dola za Marekani 1,309 4,285 kwa tiketi ya daraja la abiria wa kawaida kwenda na kurudi na kwa abiria wafanyabiashara gharama ya tiketi ni dola za Marekani 4,285.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Emirates maombi ya ununuzi wa tiketi yafanywe kabla ya Agosti 5 na ununuzi wa tiketi hizo za ofa utafanywa kati ya Agosti 5 hadi Novemba 30, 2014. Kwa habari zaidi kuhusu gharama za tiketi na masharti mengineyo, wateja wanaombwa kufuatilia katika tovuti: http://www.emirates.com/tz.

Chicago iliyopewa hadhi ya jiji tangu mwaka 1837, ina idadi ya watu milioni 2.7na ni jiji linalosifika kwa mambo ya utamaduni na sanaa mbalimbali. Lakini pia jiji hilo linafahamika kwa kuwa bora katika michezo na hivyo hivyo kuwavutia watalii wengi kila mwaka. Inakadiriwa kuwa watalii wanaotembelea jiji hilo kila mwaka ni milioni 46.

Shirika la Ndege Emirates linafanya safari mbalimbali nchini Marekani na baadhi ya miji ambayo Watanzania wengi wamefikishwa na shirika hilo ni pamoja na Boston, Dallas Fort Worth, Houston, Los Angeles, New York City, San Francisco, Seattle na Washington D.C.

Abiria wa daraja la kawaida, pia wanaweza kununua tiketi kutoka Dar es Salaam kwenda Boston kwa dola za Marekani 1,534, kwenda Dallas Fort Worth 1,519, Houston 1,518, Los Angeles 1,854, New York City 1,533, San Francisco 1,854, Seattle 1,854 na Washington D.C dola 1,533. Gharama hizo ni kwenda na kurudi.

Kwa abiria wanaotaka kusafiri kutoka Dar es Salaam kwa daraja la wafanyabiashara kwenda na kurudi katika miji ya Marekani, gaharama ya tiketi ni kama ifuatavyo. Kwenda Boston dola 5,170, Dallas Fort Worth dola 5,810, Houston dola 5,810.

Kwenda Los Angeles ni dola 6,540, gharama ya New York ni dola 5,170 huku tiketi ya San Francisco ikiuzwa kuanzia dola 6,540 kwenda Seattle ni dola 6,540 na dola 5,170kwenda Washington D.C.

Emirates ilianza kusafirisha abiria kila siku kwenda Marekani mwaka 2004 na safari zake ni za moja kutoka Dubai hadi New York JFK. Kwa sasa safari zake zimepanuka na kuifikia miji ya Washington, Houston, Dallas, Seattle, San Francisco, Los Angeles. Huduma za kuelekea Chicago zitazinduliwa Agosti. Wasafiri ni mashuhuda kuwa tuzo ya ubora wa huduma iliyopewa Emirates inadhihirishwa kwa ubora wa huduma na uzoefu kutoka kwa wafanyakazi kutoka nchi 120 mbalimbali.

Abiria awapo safarini huburudishwa kwa aina tofauti za muziki wa kusikiliza na video. Mteja anaweza pia kuomba muziki autakao kulingana na matakwa yake. Ndege yenye namba EK 725 huondoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa kila sikua kuanzia saa 04:50 asubuhi na hutua Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere saa 09:15 mchana. Ndege hiyo huruka kurejea Dubai saa 10:45 jioni na kuwasili saa 05:20 usiku.

Kiongozi wa kidini afariki Nigeria

$
0
0
Marehemu Emir Al-Haji Ado Bayero
Kiongozi wa waisilamu katika jimbo la Kano nchini Ngeria,Al-Haji Ado Bayero, amefariki.
Kiongozi huyo mwenye kuheshimiwa sana miongoni mwa viongozi wengine wote nchini humo , amethibitishwa kufariki nchini humo.


Tangu wakati huo Nigeria imekabiliana na misukosuko ya mapinduzi ya kijeshi na ghasia zingine.Al-Haji Ado Bayero, alikuwa mtawala wa Kano tangu mwaka 1963 na alifariki baada ya kuugua kwa mda mrefu.

Alikuwa na umri wa miaka 84 na kutambuliwa kama kiongozi wa muda mrefu sana na mkongwe zaidi wa waisilamu katika jimbo hilo na pia alitambulika kama kiongozi wa pili mwenye ushaiwishi zaidi kwa waisilamu Nigeria
Emir akiwa kwa Maombi katika jimbo la Kano
Marehemu Emir pia alitambuliwa kama kiongozi aliyependa amani.
Miaka miwili iliyopita alinusurika kwa tundu la sindano baada ya msafara wake kushambuliwa ambapo dereva wake na walinzi wake wawili walifariki.
Ilishukiwa kuwa kundi la wapiganaji wa kiisilamu wenye itikadi kali, Boko Haram, ndio waliomshambulia.
Emir akiwa na mwanamfalme wa Uingereza Prince Charles
Boko Haram wamewashutumu viongozi wa kijadi nchini Nigeria kwa kuwa vibaraka wa wanasiasa. Juma lililopita Emir wa Gwoza aliuliwa na kundi hilo ambalo limetekeleza mashambulizi mengi Kaskazini Mashariki mwa nnchi hiyo.
Mwandishi wa BBC Sa'ad Abdullahi mjini Abuja anasema kuwa emiralikuwa amerejea tu kutoka mjini London ambako alikuwa anapokea matibabu.

Maishani mwake alikuwa mfanyakazi wa banki, polisi, mbunge , balozi na mfanyabiashara maarufu.

Lupita kuigiza katika Americanah

$
0
0
Lupita kuigiza katika Americanah
Muigizaji nyota kutoka Kenya Lupita Nyong'oamejumuishwa katika wasanii watakaoigiza katika filamu ya Americanah inayotokana na kitabu cha mwandishi Chimamanda Ngozi Adichie.

Filamu hiyo kama ile ya ''12 Years a Slave'' iliyompelekea kichuna huyo kushinda tuzo la Oscars mwezi Februari itatengenezwa na kampuni ya Plan B inayomilikiwa na Muigizaji nyota na mtayarishi msimamizi wa filamu Brad Pitt .

Muigizaji huyo aliwaambia mashabiki wake kuwa ni heshma kubwa kwake kupewa nafasi ya kuigiza katika filamu hiyo inayotokana na kitabu cha bi Adichie.Filamu hiyo mpya ya Americanah inaelezea mada ya mapenzi kati ya raiya wawili wa Nigeria ambao licha ya penzi kuchanuka kati yao wanatenganishwa na maswla ya uhamiaji .

Kitabu hicho cha Americanah, kiachoelezea maisha ya wapenzi wawili Ifemelu na Obinze, chenyewe kinasifa si haba.
Kitabu hicho kilishinda tuzo la ''US National Book Critics Circle Award mwaka uliyopita.
Lupita kuigiza katika Star Wars na Americanah
Aidha kimeteuliwa kuwa moja kati ya vitabu kumi bora na jopo la 'The New York Times Book Review.
Nyongo aliiambia BBC kuwa baada ya kukisoma kitabu hicho , alitamaushwa na jinsi Ifemelu na mpenzi wake Obinze,walivyostahimili majaribu mengi katika uhusiano wao .
Hali ambayo inawakumba waafrika wengi ambao kutokana na tamaa ya mafanikio wanakwenda ughaibuni kutafuta ajira na wengine kwa masomo ya juu.
Mbali na Americanah ,Adichie anajivunia tajriba ya uandishi wa vitabu vingine kama vile Purple Hibiscus na Half of a Yellow Sun,ambayo pia imefasiriwa na kuigwa katika filamu na muigizaji nyota katika 12 Years a Slave , Chiwetel Ejiofor.
Nyong'o aliwatamausha wapenzi wa filamu kote duniani aliposhirikiana na Ejiofor na kutwaa taji la Oscar katika 12 years a slave.

Nyongo vilevile amejiunga na wasanii katika filamu ya Star Wars

CHUO KIKUU CHADAIWA KUWATAPELI WANACHUO 115

$
0
0
TAASISI ya Sayansi ya Afya ya Chuo Kikuu cha Eckernforde Tanga, inatuhumiwa kuwatapeli wanachuo zaidi ya 115 iliyowadahili na kukaa chuoni hapo miezi sita kisha kuwafukuza kwa madai kuwa hawana vigezo vinavyotakiwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Hata hivyo, wanachuo hao walifukuzwa baada ya kuwa wamelipa ada, fedha ya chakula, malazi na michango mingine.
Kwa mujibu wa nyaraka mbalimbali ambazo Tanzania Daima limeziona, chuo hicho kilitangaza nafasi hizo kupitia gazeti la Mwananchi la Oktoba 31, 2012.
Tangazo hilo lilisomeka; “Wito wa maombi kwa ajili ya kujiunga na kozi za cheti na stashahada za sayansi za afya mwaka wa masomo 2012/2013.”
Kwa mujibu wa tangazo hilo, waombaji wangesoma kozi hiyo kwa miaka miwili ngazi ya cheti, huku wale ngazi ya stashahada wakisoma kwa miaka mitatu.
Sifa zilizoainishwa katika tangazo hilo ni kwamba mwanafunzi atakayesajiliwa ni aliyefaulu masomo manne, likiwemo moja la sayansi.
“Mwombaji lazima awe na ufaulu wa pasi tatu katika masomo ya sayansi, walau daraja ‘D’ katika kemia, biolojia na hisabati au kidato cha sita akiwa na pasi moja daraja ‘E’ katika somo lolote la sayansi,” lilisomeka tangazo hilo.
Kila fomu ya kujiunga ilinunuliwa kwa sh 20,000 ambapo fedha hizo zililipwa kupitia benki ya NBC Tawi la Tanga, akaunti na 0201030006036.
Baada ya wanachuo hao kudahiliwa kwa sifa zilizoanishwa, walisoma kwa miezi sita na wakati wakiendelea na masomo, Wizara ya Afya ilileta vigezo tofauti na vile vilivyokuwa vimeainishwa kwenye tangazo la awali.
Hatua hiyo ilisababisha wanachuo 115 kuonekana hawana sifa, na hivyo kutakiwa kuondoka au kufanya mitihani upya ili kuweza kukidhi sifa stahiki.
Badala ya kufuata masharti ya wizara, Januari 2013, uongozi wa chuo uliwatoa wasiwasi wanachuo kwa kuwaeleza kuwa hakuna suala la kujisajili kwa mara nyingine kwa kuwa chuo hicho kipo chini ya Baraza la Elimu ya Ufundi (NACTE), na kwamba wanatambuliwa.
Licha ya kupewa matumaini hayo, lakini Juni mwaka huo, walionekana hawana sifa na hivyo kuondolewa chuoni hapo kwa mizengwe.
Chanzo chetu kilidokeza kuwa waliombwa na uongozi wa chuo kutofanya fujo ili madai yao yashughulikiwe kwa utaratibu, hivyo walipewa hundi kwenda benki kuchukua fedha.
Hata hivyo, walipofika benki ya CRDB Tawi la Tanga, walielezwa kuwa hundi hizo ni feki na waliporejea chuoni, walikuta ulinzi umeimarishwa, wakalazimishwa kuondoka maneo hayo.
Baada ya kufanyiwa utapeli huo, wanachuo hao walitoa taarifa kwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Tanga Mjini, wakiomba kuandamana ili wafike kumwona Mkuu wa Mkoa kumweleza kilio chao.
Licha ya maandamano hayo, hakuna hatua iliyochukuliwa na Serikali ya Mkoa wa Tanga dhidi ya chuo hicho, hali iliyowalazimu kuondoka kurejea majumbani kwao wakiwa wanadai fedha hadi leo.
Wanachuo hao wanadai fedha walizolipa kwa ajili ya chakula, malazi na vifaaa vya darasani ni sh 1,987,500 kila mmoja.
Pia zipo gharama za usafiri kwa kila mmoja kutegemeana na mahali alikotoka, fedha za usumbufu na hivyo kufanya madai yote kwa pamoja kufikia sh 353,069,600.
Mbali na madai yao kufikishwa kwa mkuu wa mkoa bila kupatiwa ufumbuzi, pia wanachuo hao wamewahi kumwandikia barua Waziri Mkuu, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii na Baraza la Elimu ya Ufundi, ingawa hakuna walikosikilizwa.
Alipotafutwa Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Chuwa Kiango, alitetea kuwa suala linaloulizwa silo bali kuna tatizo jingine, huku akiomba apewe muda kwa vile alikuwa akiingia kikaoni.


“Chunguza upya, muulize aliyekupa taarifa hii, nitakupa maelezo nikitoka kwenye kikao,” alisema Prof. Kiango ingawa baadaye alipopigiwa simu hakupokea.

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI TAREHE.07.06.2014

ANGALIA PICHA ZA DIAMOMOND AKIHOJIWA NA MASHIRIKA MAKUBWA YA HABARI KWENYE MAANDALIZI YA TUZO ZA MTV

WAANDISHI WA HABARI WAPATA AJALI MBAYA WAKIKWEPA TEMBO

$
0
0

Ajali mbaya imetokea juzi usiku katika moja ya maeneo mto Rubana wilayani Bunda kuingia mbuga ya Serengeti ikihusisha watu wanne baadhi yao wakiwa ni waandishi wa Habari.
Napata fursa yakufanya mahojiano na mmoja wa majeruhi katika ajali hiyo Fredrick Katulanda mwandishi wa habari wa gazeti la Mtanzania ambaye alisema kuwa ajali hiyo ilitokana na kumkwepa tembo aliyejitokeza ghafla akivuka barabara. .CDT: sengoblog

Mwili wa Mwanasoka Nguli wa Zamani Marehemu Gebbo Peter waagwa leo nyumbani kwake Vingunguti,Kuzikwa kijijini kwao Kigurunyembe mkoani Morogoro

$
0
0


Sehemu ya wachezaji mpira wa sasa na wazamani wakiwa wamesimama pembeni ya Jeneza lenye Mwili wa aliyekuwa Mchezaji wa Timu ya Simba miaka ya nyuma,Marehemu Gebbo Peter aliefariki jana kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.hapa wakiwa nyumbani kwake Vingunguti tayari kwa safari ya kwenda kwenye maziko yake Kigurunyembe mkoani Morogoro (Picha na Evance Ng'ingo)




Wadau mbali mbali wa soka wakiwemo viongozi wa soka wakipita kutoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa Marehemu Gebbo Peter,Nyumbani kwake Vingunguti,jijini Dar es Salaam kabla ya kuanza safari ya kuelekea Kigurunyembe mkoani Morogoro kwa mazishi.


Ibada ikifanyika.


Mbunge wa Jimbo la Ilala,Mh. Mussa Azzan Zungu akitoa heshima za Mwisho.


Mwili ukiwasili nyumbani.Chanzo Mtaa Kwa Mtaa Blog

RIDHIWANI KIKWETE, I.G.P MSTAAFU MAHITA,WAONGOZA MAMIA WA WANANACHI WA MORO KUMZIKA MWENYEKITI WA YANGA

$
0
0
 Umati wa watu uliofulika nyumbani kwa
mama mzazi wa mwenyekiti wa Tawi la Yanga marehemu Hamis Katoto
                Baadhi ya Umati huo
 Jeneza lililobeba mwili wa marehemu Katoto

                      Waombolezaji
 Watu wakikimbilia magari kuelekea makaburini
 Kwa sheria za dini ya kiislama wanawake hawafiki makaburini hivyo baadhi ya kina mama hao walijazana kwenye tulubai wakiwafariji wafiwa
 Katibu wa tawi la yanga mkoa wa Morogoro Hamisi mkingie mwenye bagharashia akiwa na hudhuni kubwa ya kuondokewa na mwenyekiti wake tawi hilo
                       Kina mama wakipokea duwa
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Morogoro ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Morogoro Kusini lnnocent Karogerezi akitoa salam za Chama ambapo marehmu pia alikuwa kada wa chama hicho
 Salma za mbunge huyo ziliishia njiani baada ya kushindwa kujizuia na kuangua kilio,lkumbuke jimbo la morogoro kusini analoongoza mbunge huyo iliki wilaya ya Morogoro Vijijini ambapo marehemu Katoto alikuwa lnjini wa barabara ya halmashuri ya Morogoro Vijijini,chini ya Ungozi wa Karogerezi jimbo la Morogoro kusini kwa sasa mbali ya kuwa na umeme lina barabara nzuri zilizosimamaiwa na Mbunge huyo na marehemu
 Kalogerezi akiendele kuangua kilio, huku kaka yake Wencelaus Karogerezi[kushoto] ambaye ni Diwani wa kata ya Mji Mpya naye akimsapoti mdogo wake kwa kuangua kilio vigogo hao wa CCM na marehemu wote ni wamezaliwa na kukulia kata hiyo ya Mji Mpya

 Mkuu wa Wilaya ya Kusini Unguja ambaye alifika kwenye maziko hayo na ujumbe wa watu wanne akitoa salamu kutoka kwenye wilaya yake
 Katibu wa tawi la Yanga Safi Morogoro Hamiss Mkingie ambalo marehemu katoto alikuwa mwenyekiti akitoa salama za tawi hilo
 Kigogo wa CCM kata ya Mji Mpya Jitihada Kitogo'Kitonsa'anaye alishindwa kutoa salama za CCM kata na kuangua kilio kwa uchungu ambaposehemu ya maneneo yake alisema" CCM Mji Mpya kulikuwa kwenye maandalizi ya kumuanda lnjini Katoto kuwa mbunge wa moja ya majimbo ya mkoa wa Morogoro lakini bahati mbaya mungu amemchukua"alisema Kitonsa na kuangu kilio
                Kitonsa akizidi kulia
 Mama mzazi wa marehemu akiangua kilia kwa uchungu,wa kuondokewa na mwanae ambaye alikuwa nguzo muhimu kwenye familia hiyo.
 Mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiniwa Kikwete[kulia] ambaye pia ni mtoto wa rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete 
 Aliyekuwa mkuu wa jeshi la Polisi Tanzania ambaye kwa sasa amestaafu I.G.P Alhaji Omar ldd Mahita naye alikuwepo kwenye msiba huo
 Hamis Rajabu Kibangula[kushoto]
 Beki mahiri wa yanga Juma Abdul[kati] anaye alikuwepo kwenye mazishi ya mwenyekiti wa timu yake
 Kaimu Sheikh mkuu wa mkoa wa Morogoro Sheikh Ally Omar naye alikuwepo kwenye msiba huo
 Tawi la yanga safi ambaye lilianzsihwa na marehemu mbali ya kutoa rambirambi ya shilingi lakini mbili pia kwenye kikao chaom cha juzi walikubalia pia kukodi basi ambalo lilibeba wanachma wote wa tawili hilo,huku basi hilo likipambw ana bendera za timu yao
 MTANI JEMBE,Mwanachma wa Simba Frank Mwarabu'maarufu kwa jina la Samora ambaye kwenye msiba huo alikuwa mtani alipanda kwenye basi hilo huku akiwa na jezi yenye rangi nyekundu na nyeupe ambazo ni rangi 'Boko Haramu'kwa yanga baadhi ya wananga wakimzuia Samora kupanda basi hilo mwanachma huyo wa simba alikomaa na kufanikiwa kupanda kwenye basi hilo
 Baada ya kureha kutoka makaburini walipiga picha ya pamoja na mwanachma huyo wa simba
Mahita akitoka msibani na kukatiza mitaa ya Mji Mpya huku akiwa na Sheik Koba ambaye ni Sheikh kiongozi wa Msikiti wa Mahita ulipo pande za Mafika mkoani hapa.
Na Dustan Shekidele,Morogoro.
MTOTO wa Rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete, Ridhiwani Kikwete ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Chalinze na mkuu wa jeshi la polisi mstaafu I.G.P Omar ldd Mahita jama jioni waliongoza umati wa wananahci kutoka pande mbali mbali za nchini ya Tanzania kumsika mwenyekiti wa Tawi la Yanga Safi Morogoro marehemu lnjnia Hamis Selema Katoto aliyekufa juzi kwa ajari ya gari eneo la Kihonda maghorofani majira ya saa 6 usiku.

lnjini Katoto ambaye ni miongoni mwa waandisi walioapishwa juzi kati Dodoma na waziri wa Ujezi John  Pombe Magufuri amekwa jana katika makaburi ya Makambalani nje kidogo ya Mji wa Morogoro.
marehemu ameacha mke na watoto watatu 

BRAZIL 1 vs 0 SERBIA: FRED AWAOKOA, LAKINI MASHABIKI WAZOMEA KIWANGO `MBOFU MBOFU` YA SAMBA

$
0
0
To the rescue: Fred scored the only goal of the game in Brazil's final warm-up before the World Cup
Fred flicked the ball home in the 58h minute to open the scoring at Morumbi Stadium
 Fred akichukua mpira katika dakika ya 58 na kufunga bao kwenye uwanja wa  Morumbi
Helpless: Branislav Ivanovic watches on but can't prevent the Brazilian forward from scoring
WAZEE wa Samba, Brazil,  jana usiku walibanwa mbavu na kuanza vibaya kipindi cha kwanza katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Serbia na kupata ushindi mwembamba wa bao 1-0 wakati huu zikisalia zimesalia siku tano tu kuanza fainali za kombe la dunia.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mashabiki waliofurika uwanjani waliwazomea wachezaji wa Brazil baada ya Fred kufunga bao hilo pekee katika dakika ya 58.
Mchezo huo ulilalia kwa Serbia ambao walitengeneza nafasi nyingi hususani kipindi cha kwanza, lakini walikosa umakini.
Brazil walikoswa katika dakika ya 30 baada ya Aleksandar Mitrovic kupiga kichwa cha hatari na kutoka nje kidogo na  katika kipindi cha pili, Milos Jujic aliwakosa baada ya mpira wake kugonga mwamba.
 Hulk alifunga bao katika dakika ya 73 lakini lilikataliwa baada ya mwamuzi kuonesha alikuwa ameotea, lakini video za uwanjani zilionesha kuwa mwamuzi hayakuwa sahihi.
Mechi hiyo ya kirafiki ilikuwa ya mwisho kwa wenyeji Brazil kabla ya kucheza mchezo wa ufunguzi dhidi ya Croatia wiki ijayo katika uwanja wa Corinthians arena .
Brazil wanahodhi michuano ya kombe la dunia kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1950 na wapo kundi A na timu za Cameroon, Mexico na Croatia.
 Kikosi cha Brazil: Julio Cesar, Dani Alves (Maicon 71), Luiz, Thiago Silva, Marcelo (Maxwell 74), Gustavo, Paulinho (Fernandinho 64), Oscar (Willian 46), Hulk, Fred (Jo 75), Neymar.
Wachezaji wa akiba: Jefferson, Dante, Henrique, Ramires, Hernanes, Bernard, Victor.
Goli: Fred 58.
Kikosi cha Serbia: Stojkovic (Lukac 88), Basta (Tomovic 86), Ivanovic, Aleksandar Mitrovic, Kolarov, Dusko Tosic, Matic, Jojic, Tadic (Zoran Tosic 69), Petrovic (Mrdja 86), Markovic (Gudelj 81).
Wachezaji wa akiba: Pejcinovic, Djuricic, Stefan Mitrovic, Ljajic, Bisevac, Vulicevic, Lazovic, Brkic.
On the move: Neymar (right) fights for the ball with Serbia's Dusan Basta
Challenge: Brazilian forward Neymar is closed down by Chelsea's Ivanovic
 Huendi fundi: Mshambuliaji wa Brazil, Neymar akizuliwa na beki wa Chelsea, Ivanovic.
Partisan: Brazilian fans in Sao Paulo cheer their team's last game before the World Cup
 Mashabiki wa Brazil wakiishangilia timu yao katika mchezo wa mwisho wa kirafiki kuelekea kombe la dunia.
Passionate: The Sao Paulo crowd booed their team off at half-time after an uninspiring first period
 Walikosa uzalendo: Mashabiki wa The Sao Paulo waliwazomea wachezaji wao baaada ya kuonesha soka bovu kipindi kizima cha kwanza.
Message: Serbia players held up a banner as the two teams lined up before the game

MGONJWA WA SARATANI ALIYETELEKEZWA AFARIKI DUNIA

$
0
0

Mgonjwa wa saratani ambaye alidai kupewa tiba feki za mionzi katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (OCRI), Pendo Shoo amefariki dunia  juzi wilayani Karatu akiwa safarini kuelekea Kirua Vunjo, Kilimanjaro kwa wazazi wake.
Mdogo wa Pendo, Digna Shoo, alisema dada yake alifariki juzi, saa nne usiku wakati wanafamilia wakimfanya maombi.
“Alianza kubadilika ghafla wakati tukiwa katikati ya maombi, alilegea na mgongo wake ukawa kama unapinda hivi, tukamshika na tukamweka kitandani,” alisema.
 Digna alisema kwamba baada ya kumweka kitandani  mtumishi wa Mungu aliyekuwa nyumbani hapo alimwombea na hazikupita dakika nyingi akakata roho. Alisema Pendo alikwenda Karatu akitokea Dar es Salaam mwishoni mwa mwezi uliopita, kipindi ambacho hali yake ilikuwa imeshatetereka sana kiasi cha kushindwa kutembea mpaka apate msaada wa mtu karibu.
“Wakati tunatoka Dar es Salaam kuja Karatu, hali yake ilikuwa imeshakuwa mbaya, alikuwa hawezi kutembea bila kumpa ‘support’ (msaada) alikuwa anapepesuka,” alisema Digna.
Digna alisema safari ya dada yake haikuwa imelenga kuishia Karatu, bali walikuwa wanaelekea Kirua Vunjo, Kilimanjaro ambako ni nyumbani kwao alipozaliwa, lakini mauti yalimkuta msichana huyo kabla hajafika.
Kwa maelezo ya Digna, Pendo alikuwa amekata tamaa ya kuishi kutokana na saratani hiyo kusambaa katika matiti yake mawili na kumsababishia vidonda vilivyompa maumivu makali.
Itakumbukwa kwamba gazeti hili liliwahi kuripoti mara mbili taarifa kuhusu Pendo; kwanza ni ile iliyohusu mgonjwa huyo kupewa dawa feki ambazo badala ya kumtibu zilimsababishia madhara zaidi na pili ni kuhusu kunyanyapaliwa baada ya taarifa ya awali kuandikwa gazetini.
Pendo alianza kupata tiba OCRI Novemba mwaka jana baada ya kupata rufaa kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili lakini katika mchakato wa tiba yake,  alitozwa kiasi cha Sh1.34 milioni na mtumishi wa OCRI, Almasi Matola kinyume na taratibu.
Baada ya gazeti hili kuchapisha habari hiyo, Mei 20 mwaka huu alikwenda katika hospitali hiyo kupata tiba zaidi, lakini alinyanyapaliwa na wahudumu wa OCRI na akielezwa kwamba vipimo alivyochukuliwa awali vilikuwa havionekani.
 “Niliamua kurudi hospitali nikapime tena na nilitoa damu kwa ajili ya vipimo, lakini nilipokwenda tena kuchukua majibu walidai damu yangu imepotea. Kwa hiyo nililazimika kuanza upya, nilitoa damu tena na vipimo vyote vikawa tayari kama X-ray, Ultra sound na nikavipeleka kwa daktari,” alisema Pendo kabla ya kukutwa na mauti.
Alisema alipatwa na hofu zaidi baada ya kwenda kwa daktari wake Dk Dominista Kombe, ambaye alipaswa kumpa matokeo ya vipimo, lakini alishangaa daktari huyo alipomjibu kwamba, “Majibu yako utayajua hukohuko,” akimaanisha kwenye chumba cha tiba ya mionzi.
Alisema alipofika chumba cha tiba ya mionzi muuguzi aliyekuwapo alimwambia asubiri kwenye foleni hadi atakapoitwa jina, lakini alikaa zaidi ya saa nzima bila faili lake kuitwa. Alisema baadaye muuguzi alirudi na kumwambia aende nyumbani kwa sababu wagonjwa ni wengi. Lakini wagonjwa wengine waliokuwa kwenye foleni hawakupewa maelekezo hayo na waliendelea kusubiri.
Kutokana na hali hiyo, Pendo aliapa kwamba asingeweza kwenda tena OCRI na badala yake kuamua kusaka tiba asili na kwenda makanisani kwa ajili ya maombi na maombezi. Mara ya mwisho, marehemu aliwasiliana na gazeti hili akiwa safarini kwenda Karatu ambako amefikwa na mauti.
Uongozi wa OCRI
Mkurugenzi wa OCRI , Dk Twalib Ngoma alisema suala la Pendo lilishafanyiwa kazi na  ripoti ya tukio lote ipo kwenye bodi na matokeo ya ripoti hiyo huenda yakatolewa hivi karibuni.
“Mimi nipo likizo...lakini suala hilo lilishafanyiwa kazi kwa sababu hatuwezi kuacha hivihivi lipite bila kuchukua hatua. Tunalifanyia kazi kwa undani kitaasisi,” alisema Dk Ngoma jana kupitia simu yake ya mkononi.
Aliongeza: “Tunajua kuwa gazeti la Mwananchi lilikuwa na nia njema, lakini siwezi kuhukumu na lazima taasisi ifanye uchunguzi.”
 Mkurugenzi wa Tiba wa OCRI, Dk Diwani Msemo alisema uongozi ulichukua hatua za kumpigia simu Pendo na kumwambia arudi hospitali ili akabadilishiwe daktari na dawa, lakini Pendo aliwaambia kwamba yuko Karatu.
“Tulimpigia simu Pendo ili aje atoe na maelezo yake, tusingeweza kuhukumu kwa maelezo ya upande mmoja tu,” alisema Dk Msemo.
Alisema nia ya OCRI ilikuwa ni kusimamia matibabu ya Pendo ikiwemo kumpa tiba akiwa nyumbani kwa sababu taasisi hiyo ina kitengo cha kutoa tiba ya aina hiyo.
Alisema sambamba na hilo, uongozi ulichukua maelezo ya madaktari waliomhudumia Pendo na muuguzi anayedaiwa kupokea fedha na kutoa dawa feki.
Alisema maelezo ya Matola aliyoandika kwa uongozi wa OCRI, ni kuwa dawa aliyompa Pendo ilibakizwa na mgonjwa mwingine ambaye alitaka kurejeshewa fedha zake ndiyo maana alichukua fedha hizo kwa mgonjwa.
Hata hivyo, Dk Msemo alisema OCRI haina mamlaka ya kuchukua fedha kwa mgonjwa ili kumpa tiba na badala yake, dawa zilizobaki hutakiwa kurudishwa kwenye kitengo cha dawa.
“Tumewapa barua za maonyo, wengine tumewabadilisha vitengo na hatua zaidi zilikuwa zinaendelea kuchukuliwa lakini mauti yamemkuta kabla,” alisema.

WAANAOTESA WATOTO SASA MOTO WAANZA KUWAWAKIA, SHUHUDIA HAPA

$
0
0

Jeshi la Polisi Changombe, Dar linamshikilia mwanamke aliyetajwa kwa jina moja la Neema na babu Ramadhan kwa RB namba CHA/RB/4645/2014 UNYANYASAJI WA MTOTO wakidaiwa kumsulubu mjukuu wao (jina linahifadhiwa kimaadili). 

Mke na mume wanaodaiwa kumfanyia ukatili mtoto huyo
Tukio la kuwatia nguvuni wahusika hao lilijiri Mei 29, mwaka huu maeneo ya Buza jijini Dar, baada ya ya majirani kusikia kilio cha mtoto huyo akiomba msaada ili kunusuru maisha yake kutokana na kipigo kizito alichodaiwa kupewa na wawili hao.
MAJIRANI WAZINGIRA 
Kwa mujibu wa majirani waliozingira nyumbani hao, siyo mara ya kwanza kwa mtoto huyo ambaye ni yatima kupigwa hivyo waliamua kuivamia nyumba hiyo kwa kuwataka wazee hao waache kumpiga mtoto huyo jambo ambalo lilishindikana.
Mtoto akionyesha majeraha baada ya kipigo
Majirani hao waliokerwa na kitendo hicho walitishia kuchoma moto nyumba hiyo ndipo wazee hao wakaacha kumpiga mtoto huyo na kutoka nje wakijitetea kuwa walikuwa wakimpiga kwa kuwa alifanya kosa.
Walipohojiwa sababu za kumpiga mtoto huyo mara kwa mara, wazee hao walijitetea kuwa mtoto huyo ni mtukutu.
Moja ya majeraha aliyosababishiwa baada ya kipigo
Majirani hao walidai kuwa siku za nyuma wazee hao walishawahi kuandamana kuhusu unyanyasaji wa mtoto huyo ambapo walishawahi kumripoti polisi Chang’ombe.
MAJIRANI WAANDAMANA
Ilielezwa kuwa majirani hao waliripoti kuhusu unyanyasaji huo kwa Mjumbe na Afisa Mtendaji wa eneo hilo, Mary Patrick ambaye alitoa taarifa kwa mwanaharakati wa kutetea haki za watoto kutoka TUHIMIZANE, Cleophace Simioni ambaye alimchukua mtoto huyo na kumpa huduma ya kwanza kabla ya kumpeleka Ustawi wa Jamii kwa ajili ya matunzo.
WAANDISHI WASHUHUDIA
Waandishi wetu walifika nyumbani hapo na kushuhudia mtoto huyo akiwa na majeraha ya kuchanwa mgongoni, makovu ya moto na uvimbe usoni na kichwani.
Akizungumzia sakata hilo, mwanaharakati huyo alisema atapambana hadi hatua ya mwisho kutetea haki ya mtoto huyo.
Naye Afisa Mtendaji wa Kata ya Buza, alisema kuwa anapinga vikali unyanyasaji wa watoto katika eneo lake na kuapa kufuatilia kwa upande wake ili kuhakikisha wanatoa mfano kwa watu hao.
Mwishowe wazee hao walifikishwa katika kituo cha polisi Chang’ombe ambapo walifunguliwa shitaka hilo wakisubiri kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

BUNGENI DODOMA: PICHA ZA MH. VICKY KAMATA AKIWA NDANI YA UKUMBI WA BUNGE.. SIKU CHACHE BAADA YA KUTOKA HOSPITALI.

$
0
0

Mh. H. Kigwangala akiwa amemkumbatia Mh. Vicky Kamata baada ya kuingia ukumbi wa Bunge mjini Dododma
 Mh. Vicky Kamata aliwasili Bungeni Dodoma na kama ilivyo ada alipokewa vizuri na kila mbunge aliyekutana nae. Wabunge wengi walimpa pole baada ya kuugua siku chache kabla ya ndoa yake na kumtakia kila la kheri, huku wengi wakiamini kilichotokea ni mpango wa Mungu na kua Ndoa yake ipo na itakuwepo siku yoyote Mungu akiamua kulitimiza kusudi lake juu ya Mh. Vicky Kamata..       Wakati wabunge wengi wakimuhurumia na kudhani kua kutofungwa kwa ndoa yake kungemgharimu siku nyingi kurudi katika hali ya kawaida, ilikua ni tofauti kabisa kwa upande wa Mh. Vicky Kamata kwani muda wote alikua na amani na kwamba hakujiskia vibaya kama wengi walivyodhani na ndio maana ilichukua muda mfupi sana na aliweza fika Bungeni na kazi ya kuwatumikia wananchi wake wa Geita na Tanzania kwa ujumla ilianza mara moja na kwamba bado anaamini kilichotokea ni mpango wa Mungu na kwamba Mungu hakosei na anamini Muda si mrefu atafunga ndoa na kila mtu atashuhudia na mkono wa Mungu utasiamama juu ya ndoa yake

Mh. Vicky Kamata akiteta jambo na baadhi ya wabunge wenzake ndani ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma
Mh Vicky Kamata akiwa amekumbatiwa na mbunge mwenzake
Viewing all 20290 articles
Browse latest View live




Latest Images