Quantcast
Channel: MATUKIO NA VIJANA
Viewing all 20290 articles
Browse latest View live

TASWIRA YA UFUNGUZI WA MATEMBEZI YA UVCCM ZANZIBAR HUKO MICHEWENI, PEMBA, LEO

$
0
0


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,akisalimiana na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Sadifa Juma Khamis,alipowasili katika uwanja wa Mpira Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba,katika ufunguzi wa matembezi Umoja wa Vijana wa CCM Zanzibar katika kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar Shaka Hamdu Shaka,alipowasili katika uwanja wa Mpira Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba,katika ufunguzi wa matembezi Umoja wa Vijana wa CCM Zanzibar katika kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi.[
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,(katikati) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai,(kulia) Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Sadifa Juma Khamis,(kushoto) wakifuatana na Viongozi wengine, mara alipowasili katika uwanja wa Mpira Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba,katika ufunguzi wa matembezi Umoja wa Vijana wa CCM Zanzibar katika kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi
Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Sadifa Juma Khamis,(kutoka kushoto) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, Mke wa Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Seif Ali Iddi,na Dr.Mauwa Daftari,mjumbe wa halmashauri Kuu wa CCM Taifa (NEC) wakiwa katika hafla ya ufunguzi wa Matembezi ya Umoja wa Vijana wa CCM Zanzibar katika kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi,Michweni Mkoa wa kaskazini Pemba
Vijana wa Chama cha Mapinduzi,UVCCM wa Mikoa na Wilaya wakiwa katika uwanja wa Mpira wa Micheweni kwa Shaamemata,Mkoa wa Kaskazini Pemba,wakisubiri ufunguzi wa matembezi ya umoja huo ya kuadhimisha Miaka 50 ya Mapinduzi,na kufunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar.

Vijana wasoma Utenzi Saumu Mohammed,na Rehema Juma,wakiwaburudisha wanachama wa Chama cha Mapinduzi waliohudhuria katika ufunguzi wa Matembezi ya Umoja wa Vijana UVCCM Zanzibar ya kuadhimisha Miaka 50 ya Mapinduzi,ambapo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,atafungua matembezi hayo yatakayoanza Micheweni ,Mkoa wa Kaskazini Pemba
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,akipokea risala ya Veterani wa Umoja wa Vijana UVCCM Zanzibar,kutoka kwa Mzee Mohamed Hassan Ali, katika ufunguzi wa Matembezi ya Umoja huo, ya kuadhimisha Miaka 50 ya Mapinduzi, katika uwanja wa Mpira Micheweni kwa Shaamemata,Mkoa wa kaskazini Pemba leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,akipokea risala ya UVCCM Zanzibar,baada ya kusomwa na naibu katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Zanzibar Shaka Hamdu Shaka, katika ufunguzi wa Matembezi ya Umoja huo, ya kuadhimisha Miaka 50 ya Mapinduzi, katika uwanja wa Mpira Micheweni kwa Shaamemata,Mkoa wa kaskazini Pemba leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,akipokea risala ya UVCCM Zanzibar,baada ya kusomwa na naibu katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Zanzibar Shaka Hamdu Shaka, katika ufunguzi wa Matembezi ya Umoja huo, ya kuadhimisha Miaka 50 ya Mapinduzi, katika uwanja wa Mpira Micheweni kwa Shaamemata,Mkoa wa kaskazini Pemba leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,akisalimiana na Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Sixtus Mapunda,baada ya kutoa salamu za Jumuiya, katika ufunguzi wa Matembezi ya Umoja huo, ya kuadhimisha Miaka 50 ya Mapinduzi, katika uwanja wa Mpira Micheweni kwa Shaamemata,Mkoa wa kaskazini Pemba leo
Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Sadifa Juma Khamis,akizungumza na Wanachama wa CCM na Wananchi wakati alipokuwa akimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, kuzungumza na Umoja wa Vijana ili kuyafungua Matembezi ya Maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar, katika uwanja wa Mpira Micheweni kwa Shaamemata,Mkoa wa Kaskazini Pemba leo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,alipokuwa akizungumza na Umoja wa Vijana wa CCM Zanzibar na Wanachama wa CCM Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba leo,pamoja na kuyafungua Matembezi ya Umoja huo ya Maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar, katika uwanja wa Mpira Micheweni kwa Shaamemata, (kushoto) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,(wa pili kushoto)akiongoza Maandamano ua Umoja wa Vijana CCM Zanzibar yaliyoanzia Michweni kelekea Wete Pemba,leo katika ufunguzi rasmi,Makamo wa Rais wa Zanzibar na Mjumbe wa kamati Kuu Balozi Seif Ali Iddi,(kushoto) Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Sadifa Juma Khamis,(katikati) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai,na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa NEC Dk.Mauwa Daftari
Vijana wa CCM Zanzibar,UVCCM wakiwa katika Matembezi ya maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,yaliyofunguliwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,(hayupo pichani)yaliyoanzia Micheweni kuelekea Wete Mkoa wa Kasakazini Pemba.


Vijana wa UVCCM wakiwa wamebeba Pich za Viongozi wa Chama katika Matembezi ya Madhimisho ya miaka 5o ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, yaliyofunguliwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,(hayupo pichani)kuanzia Micheweni kuelekea Wete Mkoa wa Kasakazini Pemba. 

Kikundi cha Brass Band cha Umoja wa Vijana CCM Zanzibar,kikiongoza matembezi ya maadhimisho ya miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar,yaliyofunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,leo kuanzia Micheweni kuelekea Wete Mkoa wa Kasakazini Pemba.Picha zote na Ramadhan Othman, Ikulu.

POMBE SI CHAI!!: CHEKI JAMAA ALIVYOLEWA HADI KUWEKWA KWENYE MKOKOTENI.

$
0
0



Ni aibu sana mtu kunywa pombe mpaka kushindwa kujua kiwango chako cha kusema basi.Unalewaaa mpaka akili inagota njia ya kwenda kwako unaisahau,mbele huoni unaanguka mpaka kutembea unashindwa mwisho unabebwa kwa style hii kurudishwa kwako.



Kunywa kwa kiasi ili uweze kujimudu kwa style hii wahuni awachelewi kukufanyia vitu vya aibu.....mbayaaa(kwa sauti ya mchungaji Lwakatare)

WASHAURI KUWA RAIS KIKWETE AUNDE SUK

$
0
0
3058713_orig_60bc2.jpg
Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba akifungua mkutano wa Baraza Kuu la Uongozi la CUF huko Buguruni, kulia ni Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad na Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Hamad Masoud
Khamis Haji OMKR — Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF, Profesa Ibrahim Lipumba amesema nchi inakumbwa na msukosuko mkubwa wa kiuongozi na Rais wa Jamhuri ya Muungano, Jakaya Kikwete anapaswa kuchukua maamuzi ya busara ya kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa hivi sasa, ili kulinusuru Taifa.
Profesa Lipumba amesema hayo leo (21/12/2013) wakati alipokuwa akifungua mkutano wa Kawaida wa Baraza Kuu la Uongozi la CUF, unaofanyika Makao Makuu ya chama hicho Buguruni, Dar es Salaam.Amesema msukosuko huo unaonekana wazi kufuatia taarifa ya Ripoti ya Kamati ya Bunge ya Maliasili, Ardhi na Mazingira, Hali ya kukosekana kwa uwazi katika Mchakato wa katiba na Hatma ya Uchaguzi Mkuu 2015, pamoja na malalamiko ndani ya CCM kwamba kuna Mawaziri wengi ndani ya Serikali ni mizigo.
Mwenyekiti Lipumba amesema hali iliyopo inaonesha Serikali ya CCM inayoongozwa na Rais Kikwete hivi sasa imekosa kusimamia uadilifu na Utawala bora na kwamba ni vigumu kuweza kusimamia haki na utawala bora kwa wananchi wake.
Amesema maamuzi ya busara yatakayoweza kuinusuru hali hiyo ni kwa Rais Kikwete kuunda Serikali ya Umoja wa
Kitaifa itakayoweza kuleta maridhiano na kuiepusha nchi na madhara makubwa yanayoweza kujitokeza kutokana na hali iliyopo sasa.
Amesema ripoti ya Kamati ya Bunge ya Maliasili, Ardhi na Mazingira iliyotolewa juzi Bungeni na kusababisha Mawaziri wanne kupoteza nyadhifa zao, inathbitisha hali si shwari na kwamba nchi imekumbwa na uvunjifu mkubwa wa haki za binaadamu na kukosekana utawala bora.Amesema watu waliokwenda kutokomeza ujangili, badala yake wamekuwa wavunjaji wakuu wa haki za binaadamu kwa kutesa watu wasiokuwa na hatia na kusababisha baadhi ya watu hao kupoteza maisha na mali nyingi za wananchi wakiwemo wafugaji kupotea.

Profesa Lipumba amesema vitendo kama hivyo imekuwa ni vya kawaida kufanya hapa nchini na vinahusisha zaidi watendaji wa vyombo vya ulinzi na usalama, ikiwemo katika opresheni za kijeshi zinazoendeshwa mara kwa mara, kama ambavyo pia ilitokea mkoani Mtwara."Kuachishwa kazi Mawaziri wanne, huku Katibu Mkuu wa CCM akilalamika kuwepo Mawaziri wengine ambao ni mzigo, kuna maanisha kuna msukosuko mkubwa ndani ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na kwamba hivi sasa hali ni mbaya sana", amesema Mwenyekiti Lipumba.
Akizungumzia mchakato wa Katiba na hatma ya uchaguzi mkuu ujao, amesema, wakati inaonesha wazi Katiba Mpya haitaweza kupatikana katika muda uliopangwa awali ifikapo mwezi April mwakani, bado wananchi hawaelewi utaratibu gani utatumika kuwawezesha kupiga kura ya maoni na kushiriki katika uchaguzi mkuu wa 2015.
Amesema tangu mwaka 2010 ulipofanyika uchaguzi mkuu daftari la wapiga kura halijafanyiwa mapitio, wakati utafiti unaonesha katika kipindi hicho hadi sasa kuna Watanzania wapatao milioni nne watakuwa wametimiza miaka 18 na kuwa na haki ya kupiga kura.Amesema wakati daftari hilo halijafanyiwa mapitio nao mpango wa Serikali wa kuwapatia wananchi vitambulisho vya uraia, ambavyo vilieleza vingetumika kupigia kura unakwenda kwa kusuasua na kwamba hadi sasa hakuna mkoa hata mmoja uliokamilisha kuwapatia wananchi wake vitambulisho hivyo.
"Mambo haya yako katika hali ngumu, hatuwezi kuingia katika uchaguzi mkuu 2015 na katiba ambayo wananchi wengi wameshapoteza imani nayo. Ni vyema Rais Kikwete aunde Serikali ya Umoja wa Kitaifa hivi sasa", amesema Profesa Lipumba.
Mapema akizungumza katika mkutano huo, Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad kikao hicho kitajadili ajenda zipatazo 13 zote zikiwa na maslahi kwa chama hicho pamoja na Taifa.Amesema jumla wajumbe 40 wa Baraza Kuu la Uongozi la CUF wanahudhuria kikao hicho, kati ya wajumbe wote 54, na hivyo kikao hicho maamuzi yatakayoweza kufikiwa ni halali. Aidha, Maalim Seif alitangaza kwamba chama kimepata msiba mkubwa kufuatia kifo cha mjumbe wa Baraza Kuu, Zainab Nyumba kutoka Mwanza ambaye alifariki juzi baada ya kuugua Malaria na alitarajiwa kuzikwa jana huko Mkoani Mwanza.
Source: http://www.wavuti.com

MANJI AMKINGIA KIFUA KASEJA, ASEMA SIMBA KUMTUNGUA MATATU SIO KIGEZO CHA KUSHUSHA THAMANI YAKE

$
0
0
KASEJA32Juma Kaseja `Tanzania One` amekingiwa kifua na bosi wake ,Yussuf Manji baada ya kufungwa mabao matatu jana kwenye mechi ya Nani Mtani Jembe
Na Baraka Mpenja 
MWENYEKITI wa klabu ya Yanga, Yussuf Manji amemkingia kifua mlinda mlango wao mpya, Juma Kaseja baada ya kufungwa mabao matatu jana akiwa langoni katika mchezo wa Nani Mtani Jembe dhidi ya watani zao wa jadi, Simba Sc ambao Mnayama alishinda 3-1.
Mbao ya Simba sc katika mechi ya jana yalifungwa na Amis Tambwe aliyepiga mawili na kiungo Juma Awadh Issa, wakati la Yanga lilifungwa na Emmanuel Okwi.
Akizungumza leo na waandishi wa habari, Manji amasema hawakumsajili Kaseja kwa ajili ya kuifunga Simba SC, bali malengo yao ni kupata msaada wake katika michuano mikubwa ya soka barani Afrika.
Baada ya Yanga kufungwa jana, huku Kaseja akiwa langoni, katibu mkuu wa baraza la wazee la klabu hiyo, Mzee Ibrahim Akilimali, iliulaumu uongozi kwa kusema kuwa  usajili wa kipa huyo ni makosa na hauna baraka zao.
Manji amejibu mapigo na kueleza kuwa umri unazidi kumtupa mkono mzee Akilimali  kwani ameshindwa kukumbuka kuwa , huyo Ivo mwenyewe aliondoka Yanga akiwa anatumikia adhabu ya kufungiwa miezi sita na uongozi wa wakati huo kwa tuhuma za kufungisha kwenye mechi dhidi ya  Simba SC.
Pia Manji alihoji wakati Simba ikisawazisha mabao yote matatu  katika mchezo wao wa ligi kuu soka Tanzania bara oktoba 20 dhidi ya Simba sc , Kaseja alikuwa langoni?.
Mwenyekiti huyo alisema  si jambo zuri kulaumiana pale yanapotokea makosa, bali ni kuwa na mshikamano kwa ajili ya maendeleo ya Yanga.
“Tunaheshimu uwezo wa Kaseja, thamani yake ni kubwa. Hakuna kipa yeyote nchini aliyedaka mechi nyingi za kimataifa kama kipa huyu. Kamwe hatuwezi kumshusha thamini yake na uwezo wake kwa kufungwa mabao matatu kwenye mechi ya jana ambayo ilikuwa sawa na bonanza tu”. Alisema Manji.
Manji alisema mechi ya jana walicheza kumfurahisha mdhamini wao, TBL, lakini haikuwa na maana yoyote na matokeo ya kufungwa wala hayajawaingia akilini.
Hata hivyo Manji amewapongeza Simba SC kwa kucheza soka safi, hivyo walistahili ushindi katika mchezo wa jana.
 Kuelekea ngwe ya lala salama ya ligi kuu na michuano ya Kimataifa , Manji alisema wataboresha timu pamoja na benchi la ufundi  kwa tafsiri ya kuwaondoa makocha wao Ernie Brandts na wasaidizi wake, Mzawa Fredy Felix Minziro na Mkenya, Mkenya Razack Ssiwa 
“Timu itaenda tena Ulaya kuweka kambini kama walivyofanya waka jana. Naamini tutajivua vizuri na kuwa makali zaidi kutetea ubingwa wetu na kufanya vizuri michuano ya kimataifa”. Alisema Manji.
Ili kuongeza makali, Yanga imesajili wachezaji watatu katika dirisha dogo la usajili ambao ni mlinda mlango, Juma Kaseja, kiungo Hassan Dilunga na mshambuliaji mahiri raia wa Uganda, Emmanuel Anord Okwi.

Wachezaji hao walitumika jana, lakini hawakufua dafu mbele ya kikosi cha Simba Sc kilichoonekana kuwa bora zaidi Yanga.

MAGAZETI YA MICHEZO NA BURUDANI

MAGAZETI YA UDAKU LEO

MAGAZETI YA LEO JUMATATU TAREHE 23.12.2013

REAL MADRID WASHINDA 3KWA 2,RONALDO AVUNJA REKODI YA KUFUMANIA NYAVU REAL MADRID

$
0
0
Cristiano Ronaldo ameifungia bao Real Madrid jana usiku na kuvunja rekodi ya mmoja wa washambuliaji waliopo katika orodha ya kufunga mabao mengi zaidi enzi zao wakisakata soka.
Mshambuliaji huyo raia wa Ureno amefunga mabao 164 katika michezo 151 na kuvunja rekodi ya mshambuliaji wa zamani wa Mexico, Hugo Sanchez aliyefunga mabao 164 katika mechi 207.
Ronaldo ameingia katika orodha ya wafungaji wanne wa juu waliowahi kufunga mabao mengi katika historia ya Real, lakini amebakiwa na rekodi tatu kuzivunja, yaani ya Santillana mwenye magoli 186,  Alfredo Di Stefano magoli  216 na Raul aliyetia kambani magoli 228. 
Real Madrid waliwafunga Valencia mabao 3-2 jana, shukurani zimwendee Ronaldo kwa kichwa chake mahiri dakika ya 40  kufuatia mpira mzuri wa adhabu uliochongwa na Agel Di Maria alimbadili Gareth Bale katika mchezo huo.
Madrid walipata bao la tatu na la ushindi kupitia kwa kinda wao mwenye miaka 20 Jese Rodriguez katika dakika ya 84.
Bao la kwanza lilifungwa na Angel Di Maria katika dakika ya 28 kufuatia kuwazidi ujanja mabeki wa Valencia.
 Mabao ya Valencia yalifungwa na Pablo Piatti dakika ya 34 na Jérémy Mathieu dakika ya 62.
Kikosi cha Valencia jana: Guita, Pereira, Ruiz, Mathieu, Romeu, Feghouli, Bernat, Parejo (Banega, 84), Cartabia, Piatti (Guardado, 80), Jonas.
Kikosi cha Real Madrid: Lopez, Arbeloa (Carvajal, 80), Ramos, Nacho, Marcelo, Alonso, Modric, Di Maria (Illarramendi, 87), Isco (Jese, 73), Ronaldo, Benzema.
Record: Cristaino Ronaldo's goal against Valencia saw him become the joint fourth top scorer in Real's history 
Rekodi: Bao la Cristiano Ronaldo jana usiku dhidi ya  Valencia limemfanya aungane na wafungaji wanne waliowahi kufunga mabao mengi katika historia ya Real Madrid
Jumping for joy: Ronaldo scored Madrid's second goal of the evening during the 3-2 win over Valencia
Akiruka kwa furaha: Ronaldo aliifungia bao la pili Real Madrid katika ushindi wa mabao 3-2 jana usiku
Team effort: Ronaldo is congratulated by his team-mates after his goal gave Madrid a half-time lead 
Jitihada ya timu: Ronaldo akipongezwa na wachezaji wenzake baada ya kufunga bao la pili lililowafanya waende mapumziko wakiwa mbele kwa mabao 2-1
Ahead: Angel di Maria celebrates with left back Marcelo after opening the scoring for Real Madrid against Valencia 
Kifua mbele: Angel di Maria  na beki wa kushoto Marcelo  wakishangilia bao la Margentina huyo
Leveller: Valencia's Pablo Piatti (centre) celebrates with his team-mates after equalising at the MestallaAmesawazisha: Mchezaji wa Valencia,  Pablo Piatti (katikati) akishangilia na wachezaji wenzake baada ya kusawazisha bao
Game on: Valencia French defender Jeremy Mathieu clenches his fist after scoring on the hour mark 
Kipute kinaendelea: Beki wa Valencia, Mfaransa , Jeremy Mathieu akishangilia baada ya kusawazisha bao la pili dakika ya 62
Winner: Striker Jese (left) celebrates with team-mate Luka Modric after clinching the victory for Madrid 
Mshindi: Mshambuliaji  Jese (kushoto) akishangilia  na mchezaji mwenzake Luka Modric baada ya kuifungia Madrid bao la ushindi
So close: Real Madrid defender Sergio Ramos puts his hands on his head after missing a good chance to score 
Aaaah! nimekosaje?: Beki wa Real Madrid,  Sergio Ramos akishika kichwa chake baada ya kupoteza nafasi ya wazi  kufunga  bao

Challenge: Real Madrid midfielder Xabi Alonso gets the better of Valencia winger Pablo PiattiChangamoto: Kiungo wa Real Madrid ,  Xabi Alonso akimtoka winga wa Valencia  Pablo Piatti katika mchezo wa jana usiku

Polisi wakiri makosa Operesheni Tokomeza

$
0
0
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Isaya Mungulu

JESHI la Polisi, limekuwa la kwanza kati ya taasisi saba zinazohusika moja kwa moja, kukiri udhaifu katika utekelezaji wa Operesheni Tokomeza Ujangili, iliyowaondoa mawaziri wanne katika nafasi zao.
Mawaziri ambao uteuzi wao ulitenguliwa na Rais Jakaya Kikwete Ijumaa iliyopita kutokana na kadhia hiyo kwa Taifa, ni Balozi Khamis Kagasheki (Maliasili na Utalii), Dk Emmanuel Nchimbi (Mambo ya Ndani ya Nchi), Shamsi Vuai Nahodha (Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa) na Dk David Mathayo (Maendeleo ya Mifugo).
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Isaya Mungulu, alisema yaliyojiri katika Operesheni hiyo, ni moja ya changamoto kubwa zilizowasibu kwa mwaka huu.
“Operesheni Tokomeza Ujangili, ni moja ya changamato ambazo zimetusibu kwa mwaka huu. Kama kujisahihisha basi tutajisahihisha. “Yaliyotokea tumeyaona … operesheni hazitakiwi kuleta madhara makubwa na kama yanakuwapo basi yanapaswa kuwa kidogo,” alisema.
Alisema kwa kuwa mchakato wa kujirekebisha kutokana na makosa yaliyofanyika katika Operesheni hiyo unaendelea, wananchi watarajie mabadiliko.
“Kuhusu nini kifanyike pia ni suala la kufuatilia. Tunachukua taarifa kama ilivyotolewa na kwa vile mchakato unaendelea, nadhani tutaona mabadiliko zaidi,” alisema Mungulu.
Mungulu ametoa kauli hiyo wakati Rais Kikwete akisubiriwa na umma wa Watanzania, kuchukua hatua ya kujaza nafasi hizo, ambazo zinatarajiwa huenda zikahusu mabadiliko zaidi katika wizara zaidi ya hizo nne huku Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akitangaza hatua zaidi zitakazofuata.
Katika hatua hizo, Pinda alisema itaundwa Tume ya Uchunguzi wa Kimahakama, ambayo Mwanasheria Mkuu, Jaji Frederick Werema alisema ndiyo itakayomaliza mzizi wa fitina.
*Taasisi nyingine
Tume hiyo inatarajiwa katika uchunguzi wake, kufikia Jeshi la Polisi lililokuwa na askari 440 katika Operesheni hiyo.
Taasisi zingine zinazotarajiwa kufikiwa na Tume hiyo, ambayo Rais Kikwete ameagiza uundwaji wake uharakishwe, ni Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), ambalo lilikuwa na askari 885 katika Operesheni hiyo.
Zingine kwa mujibu wa ripoti hiyo ya James Lembeli, ni Kikosi Dhidi ya Ujangili askari 440, Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa), lililokuwa na askari wa wanyama pori 383.
Pia kuna Wakala wa Huduma za Misitu (TFS), iliyokuwa na askari 99, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), iliyokuwa na askari 51, Wizara ya Sheria na Katiba iliyokuwa na waendesha mashitaka 23 na Idara ya Mahakama iliyokuwa na mahakimu 100.
Mbali na taasisi hizo, tayari jana kulitolewa kauli za viongozi na mashirika mbalimbali yakitaka watendaji zaidi katika wizara husika, wachukuliwe hatua baada ya viongozi wao kuwajibika kisiasa.
*Haki za binadamu
Ripoti hiyo ya Operesheni Tokomeza Ujangili imeainisha ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu kuwahi kutokea katika historia ya nchi.
Mbali na kutokea mauaji ya watumishi sita na watuhumiwa 13, ripoti hiyo ilibainisha udhalilishaji na mateso kwa binadamu yaliyofanyika.
Miongoni mwa mateso hayo, ripoti hiyo ilibainisha kuwa viongozi wa vijiji na vitongoji na watumishi wa Serikali walikamatwa na kudhalilishwa mbele ya wananchi wanaowaongoza.
“Baadhi ya watuhumiwa waliokamatwa, walidai walidhalilishwa mbele ya wanafamilia kwa kupewa adhabu wakiwa uchi na wanawake kushikwa sehemu zao za siri bila ridhaa yao.“Ndugu Ali Nyenge (38) wa Kata ya Iputi, Wilaya ya Ulanga, alidai kuvuliwa nguo, kumwagiwa maji yaliyochanganywa na chumvi na kuchapwa viboko huku mwanawe wa kiume wa umri wa miaka 11 akishuhudia,” ilieleza taarifa hiyo.
Nyenge pia kwa mujibu wa taarifa hiyo, alidai kutakiwa kuchora picha ya chatu kwa kutumia wembe kwenye paja lake.
“Baadhi ya akinamama walidai kubakwa na kulawitiwa, mfano kata ya Iputi, wilaya ya Ulanga, mwanamke mmoja alidai kubakwa na askari wawili usiku. “Mama mmoja mkazi wa kata ya Matongo, wilayani Bariadi, alibakwa na askari watatu huku akiwa ameshikiliwa mtutu wa bunduki,” taarifa hiyo ilieleza.
Kwa viongozi, Diwani wa kata ya Sakasaka wilayani Meatu, Peter Samwel, alidai kuadhibiwa akiwa mtupu, kuning’inizwa kichwa chini miguu juu, kupigwa kwa nyuma na kulazimishwa kufanya mapenzi na mti.
“Baadhi ya kambi za mahojiano zilipewa jina kama vile Guantanamo (Ruaha), Goligota (Ngorongoro), Duma na Andajenga (Serengeti),” ilieleza ripoti hiyo.
*Wizara nyiingine kukumbwa?
Ripoti ya Operesheni Tokomeza Ujangili, imewaondoa katika nafasi zao mawaziri hao wanne, huku kukiwa na vuguvugu la tuhuma za mawaziri wasiowajibika ipasavyo waliopewa jina la mawaziri ‘mizigo’ na chama chao cha CCM.
Vuguvugu hilo lilianzia katika ziara ya zaidi ya mwezi mmoja ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana mikoani ambapo inadaiwa wananchi walibainisha mawaziri wasiowajibika kuwa ni pamoja na Christopher Chiza (Kilimo, Chakula na Ushirika), na Naibu wake, Adam Malima.
Wengine walitajwa ni William Mgimwa (Fedha), Dk Shukuru Kawambwa (Elimu na Mafunzo ya Ufundi) na Abdallah Kigoda (Viwanda na Biashara).CHANZO HABARI LEO

TAARIFA TOKA TFF LEO DESEMBA 23, 2013

$
0
0
Boniface Wambura Mgoyo
Kaimu Katibu Mkuu TFF

MECHI YA MTANI JEMBE YAINGIZA MIL 422/-
Mechi ya Nani Mtani Jembe kati ya Yanga na Simba iliyochezwa juzi (Desemba 21 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na Simba kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 imeingiza sh. 422,611,000.

Mapato hayo ni kutokana na washabiki 52,589 waliokata tiketi kushuhudia mechi hiyo kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 40,000. Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo walikuwa 19,044.
Asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa kutokana na mapato hayo ni sh. 64,466,084.75 wakati gharama za kuchapa tiketi ni sh. 7,488,000.
Mgawo mwingine ilikuwa kama ifuatavyo; kila klabu imepata sh. 117,470,066.61, asilimia 15 ya uwanja ni sh. 52,598,537.29, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 35,065,691.53 wakati gharama za mchezo zilikuwa sh. 28,052,553.22.
MALINZI, MKUTANO WA WAANDISHI WA HABARI
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi atakuwa na mkutano na waandishi wa habari utakaofanyika kesho (Desemba 24 mwaka huu).

Mkutano huo utafanyika saa 6 kamili mchana kwenye ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
 Boniface Wambura Mgoyo
Kaimu Katibu Mkuu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

YANGA YAMTEMA RASMI BRANDTS, BIN KLEB AWEKA MAMBO HADHARANI LEO JANGWANI!!

$
0
0
binklebkatabaro (1)Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano Abdallah Bin Kleb (katikati) akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu ya Yanga, kushoto ni Musa Katabaro na kulia Afisa Habari Baraka Kiziuguto. Picha kwa Hisani ya Young Africans Official Website
Na Baraka Mpenja
KIMENUKA jangwani!. Siku mbili tu baada ya Yanga kupata kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Simba SC katika mechi ya Nani Mtani Jembe, uongozi wa klabu hiyo umetangaza kuachana na kocha wake, Mholanzi, Ernie Brandts.
Mwenyekiti  wa Kamati ya Mashindano wa klabu ya Yanga Abdallah Bin Kleb amesema Uongozi umempatia taarifa (Notice) ya siku  thelathini (30) , Brandts juu ya kusitisha mkataba wake kuanzia jana Disemba 22 mwaka huu.
Bin Kleb amesema maamuzi hayo yanafuatia muenendo wa matokeo mabaya katika michezo iliyopita ya Ligi Kuu, kirafiki na bonanza la Nani Mtani Jembe dhidi ya Simba SC mwishoni mwa wiki.

“Hatua ya Yanga kusitisha mkataba  na Brandts isichukuliwe kama chuki bali ni moja ya sehemu ya kuhakikisha tunaboresha benchi la ufundi ili tuweze kupata matokeo mazuri katika Mashindano yanayotukabili”. Alisema Bin Kleb.
 Bin kleb aliongeza kuwa Ukitazama uwezo wa mchezaji mmoja mmoja wa Yanga SC na wapinzani wao Simba Sc, na soka walilocheza kwenye mechi ya Nani Mtani Jembe  ni dhahiri kocha amefikia mwisho kimbinu na hana njia mbadala.
“Yanga imekua ikicheza chini ya kiwango katika michezo ya Ligi Kuu hali iliyoplekea kupata ushindi kwa tabu na wakati mwingine timu kupoteza pointi”. Alisema Bin Kleb.
 Mwenyekiti huyo alisema kuwa Kufuatia kupewa taarifa ya siku 30, Brandts ataamua mwenyewe kama ataendelea kusimamia mazoezi ya timu au kuondoka moja kwa moja kabla ya muda huo ukiwa haujakamilika. 
Bin kleb aliongeza kuwa Ikiwa Brandts ataondoka mapema timu itaendelea na mazoezi kama kawaida  kila siku asubuhi katika uwanja wa bora kijitonyama kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu na mashindano ya kimataifa chini ya kocha msaidizi Fred Felix “Minziro”.
 “Ili kuhakikisha timuYanga  inafanya vizuri katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom na mashindano ya kimataifa uongozi unakamilisha maandalizi ya safari ya kambi nje ya nchi na taratibu zote zitakapokamilika tutawajulisha”. Alisema Bin Kleb.
BRANDTSErnie Brandts amepewa `Notice` ya kusitishwa kwa mkataba wake.
Aidha uongozi upo katika mchakato wa kumapata mrithi wa Brandts ambaye ataungana na timu kwa ajili ya maandalizi ya mzunguko wa pili na Mashindano ya klabu Bingwa Afrika.
 “Tunawaomba wanachama, wapenzi na washabiki wa Yanga wasivunjike moyo kufuatia matokeo ya bonanza mwishoni mwa wiki, uongozi unajipanga kuhakikisha timu inaimarika kwenye benchi la ufundi na kurudisha furaha katika mzunguko wa pili wa VPL”. Alisema Bin Kleb.
Katika hatua nyingine , Bin Kleb amethibitisha ushiriki wa Yanga katika Kombe la Mapinduzi Januari mwakani visiwani Zanzibar.
Mwaka huu Yanga haikushiriki kombe la mapinduzi kufuatia kuwa na ziara nchini Uturuki ambako iliweka kambi ya wiki mbili.

BREAKING NEWS: TRESOR MPUTU AIHAMA RASMI TP MAZEMBE

ANGALIA PICHA ZA VURUGU ZA WAFUGAJI NA WAKULIMA YALIOTOKEA MALINYI ULANGA

$
0
0
 Kituo cha Polisi Kilichovamiwa na wananchi ambapo Walifanya uharibifu mkubwa wa mali pamoja na kuchoma moto gari moja lilokuwa kituoni hapoa na katika vurugu hizo  watu watau walifariki dunia 

 Picha ya mmoja wa marehemu kutokana na Vurugu za wafugaji na wakulima ambapo wananchi walitaka kuvamia kituo cha polisi malinyi.Katika vurugu hizo watu watatu walipoteza maisha.CHANZO MATUKIO BLOG


SERIKALI KUENDELEA KUWEKA MAZINGIRA WEZESHI YA UWEKEZAJI NCHINI.

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji Dkt. Mary Nagu akieleza kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu mafanikio ya serikali ya awamu ya nne katika maeneo yanayohusu Idara ya Maendeleo ya Sekta binafsi, Uwekezaji na Uwezeshaji,wakati wa mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi(NEEC) Dkt. Omar Issa.
Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi (NEEC) Dkt. Anacleti Kashuliza na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Uzalishaji na Usambazaji wa Vifaa vya Ufugaji Nyuki Tanzania (NBS) Bw. David Camara wakitia saini mkataba wa Programu Endelevu ya Ufugaji Nyuki na Uzalishaji wa Asali katika kanda ya Mashariki,Kati na Magharibi mwa Tanzania leo Jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa kampuni ya ya GS1Tanzania Bi. Fatma Kange (kushoto) na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi (NEEC) Dkt. Anacleti Kashuliza wakitia saini Mkataba wa Programu Endelevu ya Ufugaji Nyuki na Uzalishaji wa Asali katika kanda ya Mashariki,Kati na Magharibi mwa Tanzania leo Jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa kampuni ya ya GS1Tanzania Bi. Fatma Kange (kushoto) na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi (NEEC) Dkt. Anacleti Kashuliza wakibadilishana hati ya  mkataba wa Programu Endelevu ya Ufugaji Nyuki na Uzalishaji wa Asali katika kanda ya Mashariki,Kati na Magharibi mwa Tanzania leo Jijini Dar es Salaam.
Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi (NEEC) Dkt. Anacleti Kashuliza na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Uzalishaji na Usambazaji wa Vifaa vya Ufugaji Nyuki Tanzania (NBS) Bw. David Camara wakibadilishana hati ya Mkataba wa Programu Endelevu ya Ufugaji Nyuki na Uzalishaji wa Asali katika kanda ya Mashariki,Kati na Magharibi mwa Tanzania leo Jijini Dar es Salaam.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi (NEEC) Dkt. Anacleti Kashuliza akieleza malengo ya Programu Endelevu ya Ufugaji Nyuki na Uzalishaji wa Asali katika kanda ya Mashariki,Kati na Magharibi mwa Tanzania ikiwa ni kuanzisha na kuendeleza ufugaji kisasa wa nyuki unaojali mazingira, unaozalisha bidhaa bora za ufugaji nyuki zitakazomwingizia mfugaji kipato cha kutosha na kumwezesha kuchangia kikamilifu pato la Taifa. Kulia ni Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Uzalishaji na Usambazaji wa Vifaa vya Ufugaji Nyuki Tanzania (NBS) Bw. David Camara.

Mtendaji Mkuu wa kampuni ya ya GS1Tanzania Bi. Fatma Kange akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) juu ya mipango iliyowekwa katika kuhakikisha sekta ya ufugaji wa nyuki na uzalishaji asali inaendelea kukua, wakati wa hafla ya utiaji saini kwa ajili ya programu endelevu ya ufugaji nyuki na uzalishaji wa asali katika kanda ya mashariki,kati na magharibi mwa Tanzania.kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi(NEEC) Dkt. Anacleti Kashuliza.

Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Uzalishaji na Usambazaji wa Vifaa vya Ufugaji Nyuki Tanzania (NBS) Bw. David Camara akieleza kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) jinsi serikali ya awamu ya nne inavyoendelea kusaidia mpango wa ufugaji nyuki na uzalishaji wa asali ili kuhahakikisha ukuaji katika sekta hiyo, wakati wa mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.kushoto ni katibu mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi (NEEC) Dkt. Anacleti Kashuliza
(Picha zote na Hassan Silayo-MAELEZO)
Na Hassan Silayo-MAELEZO
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendelea kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji ili kuhamasisha na kuvutia miradi ya uwekezaji nchini kwa mujibu wa sheria ya uwekezaji ya mwaka 1997.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji Dkt. Mary Nagu wakati wa hafla ya utiani saini wa hati ya mkataba wa Programu Endelevu ya Ufugaji Nyuki na Uzalishaji wa Asali katika kanda ya Mashariki,Kati na Magharibi mwa Tanzania leo.
Dkt. Nagu alisema kuwa serikali itaendelea kuhamasisha uwekezaji nchini kwa kuboresha na kutekeleza sera na sheria zitakazovutia uwekezaji kwani inasaidia kuongeza pato la taifa na kuongeza fursa za ajira kwa watanzania. 
“kutokana na jitihada za serikali za kuweka mazingira wezeshi na kuhamasisha wawekezaji wa ndani na nje ya nchi, idadi na thamani ya miradi iliyoidhinishwa na kituo cha uwekezaji Tanzania imeendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka na hii inasaidia kuongeza pato la taifa na kuongeza fursa za ajira kwa watanzania”Alisema Dkt.Nagu.
Dkt. Nagu aliongeza kuwa ili kuendelea kuboresha Sera na Sheria za uwekezaji ili ziendane na mazingira na mahitaji ya uwekezaji serikali imeshakamilisha maandalizi ya Taarifa ya Mapitia ya Sera zinazohusu uwekezaji yaliyofanyika kwa kutumia mfumo wa kutathmini Sera za Uwekezaji unaotumiwa na shirika la Kimataifa la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo(OECD).
Katika ushiriki wa Serikali katika utoaji elimu ya ujasiriamali Dkt. Nagu alisema kuwa serikali inaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika utoaji wa elimu na mafunzo ya ujasiriamali nchini hasa wale wa vijijini.
Serikali imetekeleza Mpango wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Kuongeza Ajira ambapo tathmini iliyofanyika inaonesha mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 50.03 imetolewa kwa utaratibu wa serikali kutoa Dhamana ya mikopo kwenye benki za CRD NA NMB, mpango ulionufaisha wajasiriamali 74,701.Posted By Blogger to THE GOVERNMENT OFFICIAL BLOG

VIJANA WAIOMBA SERIKALI KUWAJENGEA CHUO CHA SARAKASI

$
0
0
001Kocha wa Sarakasi Bw,Innocent Mathew akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani), jijini Dar es Salaam kuhusiana na Mchezo wa sarakasi.002Innocent Mathew akiwa kwenye moja ya picha na vijana wenzie.

HABARI,  PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE DAR ES SALAAM
 
KOCHA wa Sakatari,Innocent Mathew ameiomba Serikali kuanzisha Chuo cha mafunzo ya mchezo huo ili kutoa nafasi kwa vijana wa kitanzania kupata ujuzi utakaofanikisha kujiajiri wenyewe.
Akizungumza Dar es Salaam jana na waandishi wa habari, alisema Tanzania ina vijana wengi wenye vipaji katika michezo mbalimbali ila kinachowakwamisha ni kutokuwa na sehemu ya kuwaendelea ili kuwa na ufanisi mkubwa utakaoendana na ushindani kimataifa.
Mathew ni miongoni mwa vijana 12 wanaounda kundi la Hakuna Matata ambalo linafanya shughuli za maonesho ya sanaa za jukwaani, ikiwemo uigizaji na Sarakasi katika visiwa vya Macau pamoja na nchi ya China, alifafanua kuwa ikiwa Serikali na wadau wa michezo watafanya hivyo itasaidia vijana wengi kupata fursa ya kujifunza na kuondokana na kuikaa vijiweni.
“Naamini ikiwa Serikali na wadau wa michezo watatoa hudumu hiyo kwa kuwajengea vijana vyuo vya aina hiyo itafanya kuwapa fursa ya kujitengenezea ajira mara baada ya kuhitimu mafunzo yao kwa kuna soko kubwa la mchezo huo nje ya nchi,” alisema.
Alisema mfmno unaoweza kutumia ni kwa kutumia kundi lao ambalo lilianzishwa mwaka 2000 na tangu mwaka 2003 walinza kusafiri katika nchi mbalimbali kama vile Ujerumani, Australia,Seoul Korea,Ufaransa, Ubelgiji, Uholanzi, Korea Kusini kwa mkataba wa miaka mitatu na baadae kutua huko Macau, China.
“Kama Tanzania inahitaji vijana wake wapate fursa ya kuondokana na umasikini ni vema ikawatengenezea fursa hiyo ili kufukia mafanikio katika malengo ya milenia mwaka 2015,” alisema.
Mathew hivi karibuni alirejea nchini kwa ajili ya mapumziko akitokea China alikokuwa katika mafunzo mbalimbali ya mchezo huo, amewaomba wadau wa mchezo huo kujitokeza kumpa sapoti ili kufikia malengo.

POLISI YAZINDUA BODI YA SHIRIKA LA UZALISHAJI

$
0
0

pereira-silima-feb02-2013
Mhe. Pereira Silima
Na  Frank Geofray-Jeshi la Polisi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dr. Jakaya Mrisho Kikwete ameridhia kuundwa kwa bodi ya Shirika la Uzalishaji la Jeshi la Polisi itakayosaidia kuongeza mapato ya Jeshi la Polisi ili kuendelea kuboresha huduma ndani ya Jeshi la Polisi na hatimaye kuongeza ufanisi katika kutoa  huduma bora kwa wananchi.
Akizindua bodi hiyo ya Shirika la Uzalishaji la Jeshi la Polisi yenye wajumbe nane, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mheshimiwa Pereira Silima alisema, moja kati ya vipaumbele ambavyo bodi inapaswa kuviangalia ni pamoja na kuboresha makazi ya askari ili waweze kutoa huduma bora kwa jamii.
Mheshimiwa Pereira alisema kuwa, kuwepo kwa shirika hilo kwa upande wa jeshi la polisi kutasaidia kuongeza kipato kwa Jeshi ili liweze kuboresha mazingira ya kazi kwa askari wake, huku akitolea mfano wa shirika la Suma JKT pamoja na J`eshi la Magereza 
Nae Mwenyekiti wa bodi hiyo, Bwana Emmanuel Umba alisema yeye pamoja na wajumbe wenzake wa  bodi hiyo, wataifanya kazi waliyokabidhiwa na Serikali kwa weledi na kuhakikisha kuwa wanaleta mrejesho wenye mafanikio ili watanzania wawe salama kwani kwa kuboresha mazingira ya kazi kwa askari wa jeshi la  polisi kutaongeza ufanisi katika utendaji kazi zao.
Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Said Mwema alisema usalama, amani na utulivu vina gharama kubwa na kwamba majeshi mengine katika mataifa makubwa na yaliyoendelea, wanatumia mfumo huo wa kuwa na mashirika ya uzalishaji mali katika kujipatia kipato cha ziada ili kuboresha huduma katika majeshi yao ikiwa ni pamoja na kutoa huduma bora kwa wananchi.

ALEX MSAMA AKABIDHI ZAWADI YA VYAKULA KWA VITUO MBALIMBALI VYA WATOTO YATIMA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
1aMkurugenzi wa Msama Promotion inayoandaa Tamasha la Krismas Bw. Alex Msama akikabidhi zawadi ya vyakula mbalimbali kwa Halima Mpeta wa kituo cha Mwandaliwa  cha Boko kwa ajili ya sikukuu ya Krismas, Msama amesema kama ilivyo kawaida ya kampuni hiyo imeamua kutoa kiasi fulani cha mapato yake ya tamasha hilo na kununua vyakula kwa ajili ya kuwapa zawadi watoto yatimu ili na wao washerehekee sikukuu ya Krismas vizuri kama wenzao, vituo vilivyopata zawadi hiyo ya vyakula leo ni Honorata Temeke, Mwandaliwa Boko, Malaika Kinondoni, Yatima Group Trust Fund ya Chamazi na Mahabusu ya watoto Upanga vyote vya jijini Dar es salaam, Makabidhiano hayo yamefanyika katika ofisi za kampuni hiyo Biafra Kinondoni jijini Dar es salaam.2aMkurugenzi wa Msama Promotion inayoandaa Tamasha la Krismas Bw. Alex Msama akikabidhi zawadi ya vyakula mbalimbali kwa Mwanaidi Ramadhan wa kituo cha yatima Malaika cha Konondoni.3aMkurugenzi wa Msama Promotion inayoandaa Tamasha la Krismas Bw. Alex Msama akikabidhi zawadi ya vyakula mbalimbali kwa Alex Mulumba wa kutuo cha  Honorata Temeke 4aMkurugenzi wa Msama Promotion inayoandaa Tamasha la Krismas Bw. Alex Msama akikabidhi zawadi ya vyakula mbalimbali kwa Haruna Mtandika wa kituo cha Yatima Group cha Chamazi wilayani Temeke.5aMkurugenzi wa Msama Promotion inayoandaa Tamasha la Krismas Bw. Alex Msama akikabidhi zawadi ya vyakula mbalimbali kwa Ramadhan Yahya wa  Mahabusu ya watoto Upanga.6aMkurugenzi wa Msama Promotion inayoandaa Tamasha la Krismas Bw. Alex Msama akifafanua jambo kwa waandishi wa habari mara baada ya  kukabidhi zawadi ya vyakula mbalimbali.

HALI NI MBAYA…! LUNYAMILA ANAPUMULIA MASHINE HOSPITALI YA MWANANYAMALA!!

$
0
0
WINGA wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, Edibily Lunyamila leo hii asubuhi amekimbizwa katika hospitali ya Mwananyamala baada ya kusumbuliwa na kifua na sasa anapumua kwa msaada wa mashine. Mtandao huu ulifanikiwa kufika hospitalini hapo muda mfupi baada ya winga huyo kukimbizwa hospitalini hapo baada ya kuzidiwa tangu jana usiku akiwa nyumbani kwake Mbezi jijini Dar es Salaam. Shaffihdauda.com imemshuhudia Lunyamila akiwa amelala kitandani katika wodi ya wanaume namba namba 5 kitanda namba 16 katika hospitali hiyo ya rufaa ya Kinondoni.
Daktari Madirisha Pascal anayemuhudumia winga huyo wa zamani, Lunyamila anasumbuliwa na tatizo la kifua ambalo linamfanya ashindwe kupumua vizuri. “Kama mnavyomuona anapumua kwa msaada wa mashine na bado tunaendelea kumfanyia uchunguzi ili kubaini nini kinachomsumbua zaidi,” alisema Pascal. Mmoja wa ndugu wa Lunyamila, Lameck John alisema kwamba, mchezaji huyo wa zamani alianza kujisikia vibaya jana Jumapili na leo asubuhi hali yake ilibadilika ndipo walipomkimbiza hospitali.
 
 Lunyamila alivyokuwa enzi anaichezea Yanga.. 
“Alianza kulalamika hawezi kupumua na kifua kinamsumbua pia mbavu zilikuwa zikimuuma, baada ya majibu ya vipimo tutajua kinachomsumbua zaidi,” alisema Lameck. 
Kutokana na hali iliyoonekana hospitalini hapo, Lunyamila anahitaji huduma ya haraka ili kuweza kuokoa uhai wake kwani anapumulia mashine akiwa katika sehemu yenye joto kali hivyo anapambana na vitu vingi kwa wakati mmoja…
Taarifa za kiuchunguzi zilizofanywa na mwandishi wetu zimebaini Lunyamila anasumbuliwa na ugonjwa wa moyo.
”Nilikuja jana hospitali ya mwananyaala ikagundulika moyo wangu umekuwa mkubwa,hivi sasa naenda muhimbili kwa ajili ya vipimo zaidi nikifika na kukutana na daktari nitakujulisha ”
ilipofika mchana wa leo mwandishi alipokea simu kutoka kwa Lunyamila akimwambia ameambiwa arejee tena hospitali ya Mwananyamala.
CHANZO: Shaffih Dauda in Sports

REDDS MISS TANZANIA 2013 KUSHEREHEKEA SIKUKUU YA X MASS NA WATOTO YATIMA KITUO CHA MGOLOLE MOROGORO.

$
0
0
Redds Miss Tanzania 2013 Happiness Watimanywa (pichani), tarehe 25 Desemba 2013 atajumuika na watoto yatima wa kituo cha Mgolole Orphanage kilichopo Bigwa nje kidogo ya Mji wa Morogoro. 
Mrembo huo ataungana na warembo wengine watatu, akiwemo Miss Tanzania mshindi wa pili Latifa Mohamed, Miss Tanzania mshindi wa tano Elizabeth Perrty, na Sabra Islam Miss Morogoro 2013 ambaye ndie atakae kuwa mwenyeji wao wakati wote wakiwa mkoani hapo. 
Ni kawaida kwa Mrembo wa Taifa, Miss Tanzania kila mwishoni mwa mwaka kula X Mass na Watoto Yatima, wasiojiweza pamoja na wale waishio katika mazingira magumu. 
Baada ya shughuli hiyo Miss Tanzania Happiness Watimanywa atajumuika pia na watoto wa aina hiyo jijini D’salaam siku ya Mwaka mpya tarehe 1 January 2014 katika vituo vingine atakavyopangiwa na  Kamati ya Miss Tanzania. 
Pamoja na shughuli hiyo, Mrembo Happiness Watimanywa pia anakusudia kusaidia jamii wenye matatizo ya Maji kwa kuwachimbia visima vya maji safi katika mikoa ya Dodoma na Singida. 
Miss Tanzania Happiness Watimanywa ambaye pia ni Miss Dodoma na Miss Kanda ya Kati 2013, ambaye pia ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu  nchini Scotland ameahirisha masomo yake kwa muda wa mwaka mmoja hadi hapo atakapovua Taji la Mrembo wa Taifa mwishoni mwa mwaka ujao 2014.
  
HIDAN .O. RICCO.
PUBLIC RELATIONS OFFICER
LINO INTERNATIONAL AGENCY

BODABODA DAY: ASILIMIA 90 WAJIUNGA NA MPANGO WA UCHANGIAJI HIARI WA PSPF

$
0
0
 Watumishi wa PSPF wakitoa maelezo ya namna ya kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari (PSS) kwa waendesha bodaboda waliohudhuria kwenye tamasha la siku ya bodaboda
Meneja wa mpango wa uchangiaji wa hiari (PSS) wa PSPF, Mwanjaa Sembe akitoa maelekezo ya namna ya kujaza fomu za kujiunga na PSS
Afisa mwandamizi wa fedha wa PSPF, Hidaya Mganga akimsaidia kujaza fomu mmojawa waendesha bodaboda aliyejitokeza kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari wa PSPF
Afisa wa mpango wa uchangiaji wa hiari Mwajuma Ali akipitia fomu za usajili wakati wa tamasha hilo
Afisa wa uendeshaji PSPF, Halima Isaa akiwaelekeza namna ya kujaza fomu za kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari PSS
Mtumishi wa PSPF akigawa vipeperushi kwa waendesha bodaboda vinavyoeleza namna ya kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari

Waendesha bodaboda wakisoma fomu za kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari kabla ya kujaza maelezo yao na kujisajili


Afisa fedha wa PSPF, Reginald Msafiri akigawa vipeperushi
Waendesha bodaboda wakisoma vipeperushi vya PSPF wakati wa tamasha
Afisa masoko wa PSPF, Queen Edward

Afisa Fedha wa PSPF, Mohamed Madenge akigawa vipeperushi
Msanii Linex akifanya yake Viwanjani hapo
Watumishi wa PSPF katika picha ya pamoja

Zaidi ya asilimia 90 ya waendesha bodaboda waliohudhuria tamasha la siku ya waendesha bodaboda lililopewa jina la siku ya waendesha bodaboda wamejiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari (PSS) wa mfuko wa Pensheni wa PSPF.

Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari, Mwanjaa Sembe amesema udhamini wao katika tamasha hilo ni moja ya mikakati yake ya kuwafikia watu mbalimbali walio kwenye sekta isiyorasmi ili wajiunge na mpango wa uchangiaji wa hiari (PSS).


Wakati tamasha hilo lililofanyika jumapili ya desemba 22 mwaka 2013 likiendelea waendesha bodaboda wengi walifurika kwenye banda la mfuko wa pensheni wa PSPF kujisajili na kujiunga na mpango wa hiari wa uchangiaji PSS.
Viewing all 20290 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>