Quantcast
Channel: MATUKIO NA VIJANA
Viewing all 20290 articles
Browse latest View live

HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI MHE. EZEKIAH DIBOGO WENJE (MB) ILIYOSABABISHA BUNGE KUHAIRISHWA LEO

$
0
0

HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI MHE. EZEKIAH DIBOGO WENJE (MB) KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA KWA MWAKA WA FEDHA 2013/2014

1.0 UTANGULIZI
Mheshimiwa Spika, katika hotuba ya Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni katika bajeti ya wizara hii mwaka 2012/13, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na CHADEMA ilibaini mapungufu mengi ya kiutendaji na kiuwajibikaji katika wizara hii, na hivyo kuitaka Serikali kufanya mambo yafuatayo ili kuboresha utendaji na ufanisi:
1. Kuziwezesha balozi zetu nje kwa kuzitengea fedha za kutosha ili ziweze kufanya kazi kwa ufanisi
2. Kutoa idadi ya majengo ya balozi zetu nje (nyumba za mabalozi, nyumba za maafisa wa balozi na ofisi za balozi) kwa mchanganuo wa idadi ya nyumba katika nchi na kama nyumba hizo zina hati miliki au la.
3. Kutoa taarifa ya namna kila ubalozi ulivyotekeleza sera ya Diplomasia ya uchumi kwa kuzingatia kwamba balozi nyingi ziko hoi kifedha kiasi cha kwamba waambata wa kiuchumi wanakosa fedha za kusafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa ajili ya upelelezi wa masuala ya kiuchumi.
4. Kulikarabati jengo la ubalozi wa Tanzania huko Msumbiji lililokuwa limechakaa kwa kutofanyiwa ukarabati tangu 1975 ingawa jengo hilo tulipewa bure na Serikali ya Msumbiji chini ya FRELIMO.

5. Kujenga kitega uchumi katika kiwanja cha Tanzania kilichopo Dubai na kukiendeleza kiwanja namba 19 tulichopewa bure na Serikali ya Uingereza kilichopo Uingereza (Central London) ambavyo vimekuwa maficho ya wezi kwa kutoendelezwa kwa muda mrefu na kusababisha Serikali za nchi hizo kutaka kutaifisha viwanja hivyo.

6. Kufanya uchunguzi kuhusu tuhuma za balozi zetu nchini China, na Uingereza kutoa hati za kusafiria kwa mataifa mengine hasa ya Afrika Magharibi ili kubaini ukweli na kuliondolea taifa aibu kutokana na tuhuma hizi.

7. Kukarabati jengo la ubalozi wetu nchini China ambalo lilikuwa na nyufa na kuvuja nyakati za mvua, na kununua samani na vifaa vya ofisi kama mashine za nukushi na za kurudufu ambazo zilikuwa hazipo,

8. Kununua magari mapya ya ofisi ya ubalozi wetu nchini China kwa kuwa magari matatu yaliyokuwepoyalikuwa yameshapitiliza muda wa miaka 10 ambao kwa mujibu wa sheria za China hayapaswi kutumika tena,

9. Kupeleka mwambata wa kiuchumi (economic attaché) nchini China ili kufuatilia fursa mbalimbali za kiuchumi katika kutekeleza diplomasia ya uchumi kutokana na mahusiano makubwa ya kibiashara kati ya nchi yetu na China

10. Kuwawekea zuio wahusika wa kashfa ya rada kuwa viongozi wa shughuli za kiserekali ili walau kuonesha uwajibikaji wa kimaadili (moral accountability) baada ya kushindwa kuwawajibisha kisheria, ili kuondoa dhana iliyojengeka miongoni mwa jamii kwamba dola imetekwa na mafisadi.

11. Kuchunguza na kuwachukulia hatua watanzania (wafanyabiashara na wanasiasa) waliotorosha kiasi kikubwa cha fedha za nchi yetu (zaidi ya shilingi bilioni 315) na kuzificha katika mabenki ya uswisi

12. Kutoa mchanganuo wa jinsi fedha za rushwa ya rada (chenji ya rada) zilivyotumika

13. Kueleza bayana faida za kiuchumi tunazopata kama taifa kwa kushirikiana na jumuiya mbalimbali za kimataifa ili kuthibitisha kwamba mashirikiano hayo hayatumiki kupora rasilimali za nchi yetu kwa hila ya “uwekezaji”

Mheshimiwa Spika, kabla sijajielekeza kwenye mambo mahsusi kwa kipindi hiki cha bajeti ya 2013/2014, napenda kuchukua nafasi hii kwa niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na CHADEMA, kuitaka Serikali kutoa majibu mbele ya Bunge hili tukufu, kwamba imetekeleza kwa kiwango gani masuala yaliyoorodheshwa hapo juu, tuliyoitaka iyatekeleze (moja baada ya jingine) kwa mwaka wa fedha unaomalizika wa 2012/2013?


1.1 Upotevu wa Fedha za Safari za Rais, Shilingi bilioni 3.5

Mheshimiwa Spika, katika hotuba yangu ya mwaka 2012/2013 nilihoji kuhusu serikali Kuchunguza na kuchukua hatua kwa waliohusika na upotevu wa shilingi bilioni 3.5 kwa ajili ya safari “hewa” za Rais nje ya nchi, ili waweze kubainika na kuchukuliwa hatua stahiki kwa mujibu wa sheria zetu.

Mheshimiwa Spika, fedha hizi ni nyingi sana na hasa ikikukumbukwa kuwa mwaka jana 2012 wapo mawaziri ambao walichukuliwa hatua na Bunge hili kutokana na upotevu ama madhaifu yaliyofanyika kwenye wizara zao, wapo ambao walihukumiwa kutokana na kupotea kwa Twiga kwenye wizara zao, wapo waliohukumiwa kutokana na udhaifu katika kusimamia wizara zao na taasisi zilizoko chini yao. 

Kambi rasmi ya upinzani, inahoji iweje leo waziri aliyeshindwa kusimamia wizara yake na kusababisha upotevu wa fedha hizi mpaka leo bado yupo, wakati wapo mawaziri wengine walioshughulikiwa kutokana na udhaifu walioonyesha kwenye kusimamia wizara zao, au ndio kusema kuwa Serikali hii ya CCM inafanya upendeleo na kuonea baadhi ya mawaziri na kuwaacha wengine? “This clearly indicates the “double standard” nature of this Government in the performance of its functions”

1.2. Kuanzishwa kwa Ubalozi Mdogo Guangzhou -China

Mheshimiwa Spika, mwaka jana Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ilipendekeza kuwa serikali ianzishe ubalozi mdogo katika Jiji la Guangzhou kwa ajili ya kurahisisha biashara kati ya wafanyabiashara wa Tanzania na wale wa China. Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni, inatambua kuwa serikali imelifanyia kazi wazo hili na imeamua kuanzisha ubalozi mdogo katika mji huo ,ila tunataka kujua ni lini ubalozi huu utazinduliwa rasmi, kupata watendaji na vitendea kazi ili uweze kuanza kufanya kazi .

2.0 DIPLOMASIA YA UCHUMI

Mheshimiwa Spika, moja ya matarajio ya ushirikiano wa kimataifa ni kuweza kutafuta, na kunufaika na fursa mbalimbali za kiuchumi zinazoweza kupatikana katika mashirikiano hayo ili kama Taifa, tuweze kujikwamua kiuchumi na kujitegemea.

Mheshimiwa Spika, kinyume na matarajio hayo mazuri, sasa nchi yetu imegeuzwa kuwa kitega uchumi cha nchi zilizoendelea kwa kisingizio cha “ushirikiano wa kimataifa” chini ya mwavuli wa “uwekezaji”. Matokeo ya ushirikiano huu wa kinyonyaji (exploitative relationship) ni kwamba kiwango cha umasikini katika nchi yetu kimeongezeka na hivyo kuifanya nchi yetu kuwa tegemezi zaidi kuliko ilivyokuwa hapo kabla.

Mheshimiwa Spika, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikerwa na unyonyaji na unyanyasaji uliokuwa ukifanywa na wakoloni, hali iliyompelekea kusema maneno yafuatayo:

“Tumeonewa kiasi cha kutosha, tumenyonywa kiasi cha kutosha, tumepuuzwa kiasi cha kutosha. Unyonge wetu ndiyo uliotufanya tuonewe, tunyonywe na kupuuzwa. Sasa tunataka kufanya mapinduzi”

Mheshimiwa Spika, baada uhuru, Mwalimu akaanzisha siasa ya Ujamaa na Kujitegemea. Ujamaa ulilenga kujenga umoja wa kitaifa na umoja wa bara la Afrika dhidi ya unyonyaji wa kibeberu, wakati kujitegemea kulimaanisha kujenga uchumi endelevu ili kulijengea taifa heshima na nguvu ya maamuzi mbele ya mataifa mengine, na kuliepusha taifa na fedheha ya kuombaomba.

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani imesikitishwa sana na kitendo cha Serikali kulidanganya taifa, kupitia Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2010 kwamba: “Katika kipindi cha miaka mitano 2010 -2015, Serikali ya Chama cha Mapinduzi itatekeleza Sera ya Diplomasia ya Uchumi” wakati Ibara ya 98 (i) ya Ilani hiyohiyo ya CCM inasema kwamba Serikali ya CCM itaendelea kushinikiza nchi tajiri kutekeleza ahadi yao ya kutenga asilimia 0.7 ya pato la taifa la nchi zao kwa ajili ya misaada kwa nchi masikini”.

Mheshimiwa Spika, ikumbukwe kwamba ahadi hii ya asilimia 0.7 ya pato la taifa la nchi tajiri ambayo Serikali ya CCM inakodolea macho ni fedha za walipa kodi wa nchi hizo kama ambavyo wananchi wetu wanavyolipa kodi. Aidha ni aibu kwa Serikali hii ya CCM kuchukua ahadi za wahisani na kuziweka kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM kama ahadi kwa wananchi ili kubembelezea kura.

Mheshimiwa Spika, kutokana na uvivu wa kufikiri na kubuni mbinu za kuikwamua nchi hii na umasikini, Serikali hii ya CCM sasa hivi imeachana kabisa na sera ya kujitegemea, ambayo Mwalimu kupitia Azimio la Arusha alisema kwamba “ … Hakika ni ujinga na upumbavu zaidi kwetu sisi, kufikiri kwamba tutaondokana na umasikini wetu kwa misaada ya fedha kutoka nje kuliko rasilimali zetu wenyewe”

Mheshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inaitaka Serikali kulieleza bunge hili, kama inatekeleza Diplomasia ya Uchumi kwa kutegemea ahadi ya misaada ya fedha kutoka kwa wahisani na kama hilo ndio suluhisho la matatizo yanayokumba uchumi wetu kama taifa kwamba tutaweza kuendelea kwa kutegemea hisani na fadhila za wafadhili huku tukishindwa kuzitumia rasilimali zetu kwa ajili ya kujikomboa kiuchumi.

Aidha, Kambi Rasmi ya Upinzani imejiridhisha kwamba kauli mbiu ya ‘Diplomasia ya Uchumi’ imeendelea kubakia kama ilivyo kauli mbiu ya ‘Kilimo Kwanza’ ambayo imebakia kutamkwa na viongozi bila kuwa na mkakati wa utekelezaji wala vigezo vya kupima kiwango cha utekelezaji wake.

3.0. VYAMA VYA SIASA NA MISAADA KUTOKA NJE YA NCHI.

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Umoja wa Mataifa ‘United Nations University’(UNU-WIDER) ya mwezi Aprili 2012 iliyoandaliwa na Aili Mari Tripp ilionyesha kuwa misaada ya wahisani kutoka nje katika mabadiliko ya kisiasa Tanzania ‘Donor Assistance and Political Reform in Tanzania’, inaonyesha kuwa Tanzania imepokea misaada kutoka nje yenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 26.85 toka mwaka 1990-2010.

Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa ripoti hiyo ni kuwa Tanzania ni nchi inayoongoza kusini mwa jangwa la Sahara kwa kupokea misaada mingi kutoka nje ya nchi na hasa kutoka mataifa ya Ulaya na taasisi za nchi za Uingereza, Marekani, Ujerumani, Uholanzi, Norway, Canada, Sweden, na taasisi kama Benki ya Dunia, IMF ,UNDP ,UNICEF na mengineyo. 

Pamoja na misaada yote hiyo, bado tumeendelea kuwa nchi maskini sana duniani pamoja na kuwa na rasilimali lukuki ambazo tumepewa na Mungu ila tunashindwa kuzitumia kwa manufaa ya watanzania na badala yake tumeendelea kudanganywa na vimisaada vidogo vidogo na kubadilishana na rasilimali zetu kama madini, misitu ,wanyama nk kwa ajili ya misaada hiyo.

Mheshimiwa Spika, pamoja na misaada hiyo kwa serikali hii ya CCM bado vyama vya siasa vimekuwa na mahusiano na baadhi ya vyama vingine vya siasa katika mataifa ya magharibi na vimekuwa vikipokea misaada ya aina mbalimbali kama fedha , nyenzo na mengineyo kadiri ya makubaliano na mirengo ya kiitikadi ya vyama husika.Pamoja na ukweli huo bado vipo vyama vya siasa vinavyopotosha umma kuhusiana na misaada vinayopokea kutoka nje ya nchi na vyama hivi vimekuwa mstari wa mbele kueneza propaganda za uongo kuwa vyenyewe havipokei misaada kutoka nchi za magharibi.

Mheshimiwa Spika, CCM wao ‘wanajiita’ kuwa wapo mrengo wa kijamaa/kikomunisti na wamekuwa wakipokea misaada mingi sana ya fedha na nyenzo kutoka Umoja wa Vyama vya Kikomunisti Ulimwenguni ‘Socialist International’ kutoka katika nchi kama za Ujerumani kupitia SDP ,Uingereza kupitia chama cha Labour,China kupitia chama cha Kikomunist ,Marekani kupitia chama cha Democrats. Pamoja na misaada ya kifedha na kiufundi ambayo CCM imekuwa ikipata kutoka nje wamekuwa hawatangazi hadharani hata mara moja kuhusiana na kiasi ambacho wamekuwa wakipokea na hivyo kila kitu kwao imekuwa ni siri kuu ya viongozi wao.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa chama cha CUF, kutokana na itikadi zake za mrengo wa Kiliberali ambazo miongoni mwa misingi yake mikuu ni pamoja na “kupigania haki za ndoa ya jinsia moja, usagaji na ushoga”. Hii ni kwa mujibu wa tangazo lao kwenye mtandao wao wa umoja wa maliberali ulimwenguni, likiungwa mkono na Waziri wa Haki na Usawa wa Uingereza, Lynn Featherstone kutoka chama cha Liberal Democrats wakati chama hicho(www.liberal-international.org) kilipokuwa kinapitisha azimio la kuruhusu ndoa za jinsia moja kama haki ya mtu mmoja mmoja, wanashirikiana na vyama kama vile LPC ya Canada, Det Radikale Venstre cha Norway, FDP cha Ujerumani, Israel Liberal Group cha Israel,PDS cha Senegal na Liberal Democrats cha Uingereza.

Kutokana na umoja huo, CUF wamekuwa wakipata msaada wa kifedha na nyenzo nyingine mbalimbali kutoka kwa vyama hivyo vya mrengo wa Kiliberali na msaada wa mwisho ni hivi majuzi mwezi Machi 2013 waliposaini makubaliano na chama cha Kiliberali kutoka Norway.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa CHADEMA, wapo kwenye Umoja wa Vyama vya Kidemokrasia Ulimwenguni (International Democratic Union - IDU). Huu ni umoja wa vyama ambavyo vipo kwenye mrengo wa kati na ambavyo msingi wake mkuu ni pamoja na kuwa na familia, kama taasisi muhimu katika jamii, ikimaanisha kwamba: “tunapinga vitendo vyote vya ushoga na usagaji”. Tunatetea demokrasia, haki za binadamu na kupambana na ufisadi katika serikali. Vyama wanachama wa umoja huu ni pamoja na Conservative Party cha UK, CPP cha Norway, Republican cha Marekani na vingine vinavyofuata mrengo huo.

Mheshimiwa Spika, Kambi rasmi ya upinzani Bungeni, inavitaka vyama vyote ambavyo vimekuwa na mahusiano na vyama vya nje viweke wazi mikataba yao na malengo ya mahusiano hayo ikiwa ni pamoja na misaada ambayo vimekuwa vikipokea kutoka kwenye nchi hizo .

4.0 MPANGO WA KUJITATHIMINI KIUTAWALA BORA (APRM)

Mheshimiwa Spika, itakumbukwa kuwa mnamo mwezi Januari, 2013 ulifanyika mkutano wa 20 wa wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa ,Ethiopia na ni katika mkutano huo Mhe. Rais Kikwete aliwasilisha taarifa ya nchi yetu kuhusu kujitathimini katika utawala bora kwenye mpango wa nchi zinazojitathimini katika utawala bora (APRM).

Mheshimiwa Spika, baada ya taarifa hiyo (randama uk.15) nchi yetu ilitakiwa kutafutia ufumbuzi changamoto zifuatazo;

i. Migogoro baina ya wakulima na wafugaji
ii. Imani za kishirikiana (uchawi)
iii. Kuhakikisha kuwa manufaa ya kukua kwa uchumi yanawafikia wananchi
iv. Kutoa elimu kwa umma kuhusu mipango na sera za serikali
Mheshimiwa Spika, changamoto hizi ambazo nyingine zinatia aibu taifa letu mbele ya mataifa mengine kama vile sisi kuonekana ni wachawi na hivyo kutakiwa kuchukua hatua dhidi ya uchawi !ni fedheha na aibu kubwa kwa taifa letu .

Aidha , Kambi rasmi ya upinzani Bungeni inataka kujua serikali na wizara imechukua hatua gani mpaka sasa katika kukabiliana na changamoto hizi na hasa tatizo la wakulima na wafugaji na kuhakikisha kuwa manufaa ya kukua kwa uchumi wetu yanawanufaisha wananchi na sio kuwanufaisha baadhi ya viongozi na mafisadi wachache.

5.0 MLIPUKO WA BOMU ARUSHA NA BARAZA LA USALAMA LA UMOJA WA MATAIFA.

Mheshimiwa Spika, mwaka huu tarehe 05 Mei, Kanisa Katoliki Parokia ya Olasiti huko Arusha lililipuliwa kwa bomu. Tukio hili lilitokea wakati akiwepo balozi wa Vatican Nchini na ambaye ndio alikuwa mgeni wa heshima kwenye tukio la kuzindua Parokia hiyo.

Mheshimiwa Spika, mara baada ya tukio hilo, Balozi wa Vatican nchini aliwasilisha taarifa hiyo kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kuonyesha kuwa Tanzania sio nchi salama sana kutembelewa na wageni na kama wakitembelea basi wanapaswa kuchukua tahadhari kubwa kwa kipindi chote watakapokuwa hapa nchini.

Mheshimiwa Spika, Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni, inataka kujua nini kauli ya serikali kuhusiana na tukio hili na hasa kuhusiana na taarifa za hali ya usalama wa nchi yetu na wageni zilizowasilishwa kwenye Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa .

6.0 SAFARI ZA VIONGOZI NJE NA MISAFARA MIKUBWA

Mheshimiwa Spika, tangu mwaka 2011/2012 Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni imekuwa ikihoji suala la misafara ya Viongozi wa kitaifa kuwa mikubwa kutokana na kuambatana na watu wengi ambao wengine wanakuwa hawana hata majukumu ya msingi ya kufanya wakati wa ziara hizo huku wakiliongezea taifa gharama kubwa ya kuwasafirisha na na kulipia malazi yao na starehe zao.

Aidha , tumekuwa tukipendekeza na kushauri kuwa sasa ni wakati muafaka kwa Rais wa nchi kuamua kutuma wasaidizi wake kwenye baadhi ya ziara za nje kama wanavyofanya viongozi wengine wa nchi jirani kama Rais Kagame wa Rwanda na hata Mwai Kibaki, Rais mstaafu wa Kenya alivyokuwa anafanya akiwa Rais, kwani kwa kufanya hivyo atapunguza msururu wa maafisa na viongozi mbalimbali wa kuambatana naye. Tunashauri tena kuwa rais awe anatuma wasaidizi wake kwenye ziara za kawaida na yeye awe na jukumu la kushiriki kwenye ziara rasmi za kiserikali ‘State Visits’ na mikutano maalum ya Kimataifa kama UN na AU.

Hivyo basi Kambi rasmi ya Upinzani inashauri mambo yafuatayo yafanyike ili kupunguza gharama hizi kubwa za kuwasafirisha viongozi na misafara isiyokuwa na tija kama ifuatavyo;

i. Serikali itengeneze kanuni za kuthibiti idadi ya maafisa na watu ambao watakuwa wakiambatana na Rais kwenye ziara za nje (idadi ya wajumbe kwenye misafara iwe wazi na ijulikane)

ii. Pawepo na kanuni za kuainisha kuwa ni nani watapaswa kupanda ndege daraja la kwanza na wale wenye haki ya kulala kwenye hoteli za daraja la kwanza wajulikane.

6.1. Idara ya Protocol na Mabilioni ya Fedha za Safari za Nje.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2011/2012 fungu 221100 ‘travel out of country’zilitumika shilingi 36,121,942,870.00 kwa ajili ya safari za nje ya nchi kwa viongozi wakuu. Katika mwaka wa fedha uliopita wa 2012/2013 kifungu 1010 ambacho ni kwa ajili ya protocol walitengewa shilingi 8,372,581,824 na fedha ambazo zilikuwa zimepokelewa na wizara mpaka mwezi Februari 2013 zilikuwa jumla ya shilingi 26,081,860,727.16! (randama uk.4)jedwali la 2 na zilitumika kwa ajili ya kugharamia safari za viongozi nje ya nchi.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2012/2013 Bunge lilikuwa limetenga na kuidhinisha kiasi cha shilingi 8,372,581,824 kwa ajili ya kifungu hiki cha Protocol ‘travel out of Country’kwa mujibu wa kitabu cha matumizi ya kawaida juzuu ya pili (volume II). Jambo la kushangaza ni kwamba, wizara iliieleza kamati na Bunge hili kuwa walishatumia zaidi ya bilioni 26.081 kutokana na fedha walizokuwa wamejitengea wenyewe wizara ambazo hazikuidhinishwa na Bunge kiasi cha bilioni 29.404

Mheshimiwa Spika, Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na CHADEMA, inataka maelezo ya kina kuhusiana na mamlaka ya wizara hii kwenda kutenga na kutumia fedha nyingi kuliko zilizokuwa zimeidhinishwa na Bunge hili na zilikuwa fedha kwa ajili ya safari za kwenda nje ya nchi, ni nani aliipa wizara mamlaka hiyo na kiburi hicho kiasi cha kupuuza maamuzi ya Bunge hili tukufu.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka huu wa fedha 2013/2014 kitengo hiki cha Protocol kimetengewa jumla ya shilingi 15,155,377,400.00 kwa ajili ya matumizi mengineyo ,ambazo katika mchanganuo wake kwenye kifungu 1010 kifungu kidogo cha 221100 ‘travel out of Country’ zimetengwa shilingi 9,381,328,850.00 kwa ajili ya kugharamia safari za kikazi za viongozi wa Kitaifa nje ya nchi.

Aidha, katika kifungu kidogo cha 220700 ‘rental expenses’ zimeombwa jumla ya shilingi 2,925,445,000.00 kwa ajili ya kukodisha ndege ,magari na kumbi za mikutano kwa ajili ya viongozi wa kitaifa.

Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni, haikubaliani na kamwe haitakubaliana na ufujaji huu wa fedha za walipakodi maskini wa Tanzania . Tunamtaka waziri atoe maelezo ya kina kwa watanzania ni kwanini nchi maskini kama yetu tutumie fedha nyingi kiasi hicho kwa ajili ya safari za viongozi nje ya nchi? Aidha , hatukubaliani na kitendo cha kutenga fedha kwa ajili ya kukodi ndege wakati Rais ana ndege yake ambayo ilinunuliwa na mabilioni ya fedha za watanzania. 

Ikumbukwe kwamba ndege hii ya Rais ilinunuliwa kwa mbwembwe nyingi kiasi kwamba Waziri wa Fedha wa wakati huo Ndugu Bazili Mramba alisema watanzania wafunge mkanda, hata kama watakula majani, lazima ndege ya Rais inunuliwe. Watanzania hawa wamekula majani sasa kiasi cha kutosha, bado tena Serikali inaendelea kuwanyonya ili ipate pesa za kukodisha ndege wakati Rais ana ndege? Hivi Serikali sasa inataka watanzania wale mawe ndio ijue kwamba watu wamefunga mkanda kiasi cha kutosha?

6.2 Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje

Mheshimiwa Spika, mwaka 2012 Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama, ilifanya ziara kwenye balozi takribani zote na iliona matatizo yanayozikumba balozi zetu huko na ilikuwa matumaini yetu kuwa baada, ya ziara ile ya kamati ingehakikisha kuwa fedha zinaongezwa kwenye wizara hii na hasa kwenye fungu la maendeleo ili tuweze kuboresha mazingira ya balozi zetu. Kinyume na matumaini hayo, ni kwamba hakuna jitihada zilizofanyika kuongoeza bajeti ya wizara hasa katika fedha za maeendeleo.

Mheshimimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, inaitaka kamati ya Bunge ya Ulinzi na usalama, kuishinikiza Serikali ili kuhakikisha kuwa katika mwaka huu wa fedha wizara hii inaongezewa fedha kwa ajili ya kuboresha mazingira ya balozi zetu , na hiyo ndio njia pekee ya kuonyesha kuwa kamati haikuenda kufanya utalii bali ilienda kuona matatizo ya balozi zetu na kuchukua hatua.

7.0 UFISADI KATIKA UNUNUZI WA JENGO LA OFISI NA MAKAZI KATIKA UBALOZI WA TANZANIA JIJINI PARIS – UFARANSA.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka huu wa fedha kwa mujibu wa randama ya wizara ni kuwa mwaka huu wa fedha kiasi cha shilingi bilioni 28 (28,000,000,000.00) zimepangwa kwa ajili ya matumizi ya maendeleo na kati ya hizo kiasi cha shilingi bilioni 24 na milioni 188 (24,188,000,000.00) ni kwa ajili ya ununuzi wa jengo la ofisi na makazi ya balozi jijini Paris ,Ufaransa (randama uk 25) na kiasi cha shilingi bilioni 3 na milioni 812 (3,812,000,000.00) ni kwa ajili ya gharama za ukarabati wa majengo ya ofisi na makazi yaliyopo Ubalozi wa Tanzania Maputo,Msumbiji. 

Mheshimiwa Spika, ukisoma randama ya wizara (uk.120) katika kasma 6391 ,kifungu kidogo 411100 kiasi cha fedha kilichoombwa ni shilingi bilioni 23 na milioni 900 (23,900,000,000) kwa ajili ya ununuzi wa jengo la ofisi na makazi ya Balozi jijini Paris, Ufaransa na shilingi bilioni 3 namilioni 700 (3,700,000,000.00) kinaombwa kwa ajili ya ukarabati wa majengo ya ofisi na makazi yaliyopo ubalozi wa Tanzania Maputo,Msumbiji.

Hata hivyo, katika mwaka huu wa fedha 2013/2014 kwenye kasma 6391 katika fungu la Maendeleo (randama uk.120) wizara inaomba kutengewa kiasi cha shilingi milioni 400 (400,000,000.00) (kifungu 221100 ) fedha ambazo hazipo kwenye kitabu cha matumizi ya kawaida juzuu ya pili (volume II) kwa ajili ya posho ya kujikimu na gharama za usafiri kwa ajili ya kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya Wizara, miradi yenyewe ni miwili mmoja wa kununua nyumba Ufaransa na kukarabati jengo Msumbiji.

Mheshimiwa Spika, mkanganyiko huu wa kimahesabu unatia mashaka makubwa sana kuhusiana na dhamira ya serikali na wizara hii hasa fedha zinapotengwa bila kufuata utaratibu wa kibajeti na bila kuingizwa kwenye vitabu vya fedha na mafungu husika.

Kambi rasmi ya Upinzani, inajiuliza tunapitisha mafungu yapi? Kwani kwenye randama fedha zinatofautiana kwenye fungu moja la maendeleo baina ya (ukurasa 25 na 120) , vilevile kwenye kitabu cha matumizi ya kawaida hali ni tofauti kwenye fungu la travel out of the Country kwani sasa wizara imejiongezea shilingi milioni mia nne kwa ajili ya kufuatilia miradi miwili ambayo ni kununua jengo Paris na kukarabati Jengo la ubalozi - Maputo,Msumbiji.

Mheshimiwa Spika, utata wa fedha unaendelea kuonekana kwenye randama ya wizara katika kiambatanisho Na.1 ‘utekelezaji wa ushauri na mapendekezo ya kamati ya kudumu ya Bunge ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa’ katika ushauri/mapendekezo Na.5 kamati iliitaka ‘Wizara itoe mchanganuo wa matumizi ya fedha za bajeti ya maendeleo zilizopokelewa kutoka hazina katika mwaka wa fedha 2012/13’

Maelezo ya wizara yalikuwa kama ifuatavyo; nanukuu randama ya wizara “katika mwaka wa fedha 2012/2013 ,hadi kufikia mwezi Machi ,2013 wizara imepokea kutoka Hazina kiasi cha shilingi 13,261,281,600.00 ambapo kati ya fedha hizo kiasi cha shilingi 9,660,000,000.00 zimetumika kwa ajili ya kulipia malipo ya awali ya ununuzi wa Jengo la Ofisi na Makazi ya Balozi Paris,Ufaransa;shilingi 995,930,000.00 zimetumika kwa ajili ya ukarabati wa jengo la serikali lililopo Maputo,Msumbiji ;shilingi 626,899,155.00 zimetumika kwa ajili ya ukomboaji wa vifaa vya ujenzi bandarini vilivyotumika katika ujenzi wa kituo cha mikutano cha kimataifa cha Julius Nyerere na safari ya kikazi ya wataalam katika balozi za Maputo,Pretoria na Lusaka kwa ajili ya kazi ya upembuzi yakinifu wa miradi ya maendeleo iliyopo katika Balozi hizo; na shilingi 1,978,452,485.20 bado hazijatumika na zinatarajiwa kutumika kwa ajili ya kulipia gharama za ukarabati wa jengo la Serikali lililopo Maputo’

Mheshimiwa Spika, baada ya kufuatilia na kufanya tathimini ya kina kuhusiana na majibu hayo ya wizara kuhusu fedha za maendeleo kwa ajili ya ukarabati wa Jengo la Maputo na kununua Jengo la Ofisi na Makazi ya Balozi Ufaransa na kukuta kuwa ni fedha nyingi sana kuliko uhalisia wenyewe , kwa mfano waziri anataka Bunge na taifa tuamini kuwa kufanya ukarabati wa jengo moja la ofisi Maputo Msumbiji tunahitaji kutumia kiasi cha shilingi 4,695,930,000.00 kwa kutumia fedha inayoombwa mwaka huu wa fedha na zile ambazo tayari zilishalipwa katika mwaka wa fedha wa 2012/2013. 

Aidha wakati wizara inawasilisha majibu yake kwenye kamati ya kudumu ya Bunge walisema kuwa (swali 12 uk.5) ‘kiasi cha fedha kilichotengwa kwa ajili ya ukarabati wa majengo ya Serikali yaliyopo Maputo ni shilingi 3,812,000,000.00……kiasi hicho cha fedha kinatosheleza kukamilisha kazi ya ukarabati wa majengo hayo ya Serikali yaliyopo Maputo, Msumbiji’

Aidha, kununua jengo moja la ofisi na makazi katika Jiji la Paris Ufaransa tunahitaji kutumia kiasi cha shilingi bilioni 33 na milioni 560 33,560,000,000.00.

Mheshimiwa Spika, kwa majibu haya ya wizara ni kuwa tayari wizara imeshafanya malipo ya shilingi bilioni 9.66 kama malipo ya awali kwa ajili ya ununuzi wa jengo la ofisi na makazi huko Paris Ufaransa , na kuwa tayari tumeshafanya malipo ya awali kiasi cha shilingi milioni 995.930 kwa ajili ya ukarabati wa jengo la ubalozi huko Maputo,Msumbiji.

Mheshimiwa Spika, hakika kiasi hiki ni kikubwa kupitiliza na hata utafiti na tathimini ambayo ilifanywa na Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni ilionyesha kuwa kununua jengo la ofisi katika jiji la Paris kwenye mji wa bei ghali kama Co’te d’Azur (most expensive area in Paris) huwezi kutumia fedha nyingi kiasi hicho kwa ajili ya manunuzi ya jengo la ofisi na makazi.

Aidha, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni tunakumbuka sakata la ununuzi wa jengo la ubalozi lililomkumba balozi Prof.Mahalu huko Roma - Italia na yaliyofuatia mpaka kesi na fedha zetu tulizoambiwa kuwa zimepotea hazikuweza kurejeshwa baada ya Prof.Mahalu kushinda kesi hiyo mahakamani.

Hivyo basi, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inataka kupata majibu kuhusiana na mambo yafuatayo;

i. Ni eneo gani ambalo tumepata jengo la kununua kwa ajili ya ubalozi na makazi ya balozi huko Paris, Ufaransa, na ni nyumba ya aina gani .

ii. Je, Serikali inaweza kuonyesha mkataba wa manunuzi wa nyumba hizo (Paris) kwa Bunge na tutalipa kiasi gani kununua jengo hilo?

iii. Ni nani au wakala gani wa serikali aliyefanya tathimini ya hayo majengo na kuamua kuwa tulipe kiasi hicho cha fedha?
iv. Ni kampuni gani iliyohusika katika kufanya makubaliano ya mauziano ya nyumba hizo na tunawalipa kamisheni ya shilingi ngapi?

v. Nani, aliidhinisha kutumika kwa kiasi kikubwa hivyo kwa ajili ya kununua jengo la Ubalozi na makazi huko Paris, je Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, ilishirikishwa katika manunuzi haya?

vi. Ukarabati unaofanywa kwenye jengo la Maputo Msumbiji ni wa aina gani, au tunajenga upya nyumba hizo?
vii. Ni kampuni gani ya ujenzi inayofanya ukarabati wa jengo letu huko Msumbiji na mkataba wa ukarabati huo uko wapi, tungetaka uwekwe hadharani.

Aidha , kambi rasmi ya Upinzani Bungeni , inatoa hoja ya kumtaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kufanya uchunguzi maalum (Special Audit) kuhusiana na ununuzi wa majengo haya na ukarabati unaofanyika kwenye jengo letu huko Maputo, Msumbiji, na kuona kama thamani halisi ya fedha imezingatiwa , na kama sheria ya manunuzi ya umma imefuatwa kikamilifu.

Mheshimiwa Spika, Vile vile, tungetaka sehemu ya fedha hizi zitumike kwa ajili ya kukarabati jengo letu la zamani la ubalozi lililopo Washngton ambalo kwa sasa halitumiki baada ya kutekelezwa kwani likikarabatiwa litaweza kuliongezea taifa mapato kutokana na matumizi ya kibiashara ya jengo hilo.

8.0 MPANGO WA WIZARA WA KUTOA VISA KWENYE BALOZI TU

Mheshimiwa Spika, mpango wa Wizara kutoa visa kwenye balozi tu haukubaliki. Kwa Mujibu wa majibu ya wizara kwenye kamati ya kudumu ya Bunge ya Mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa ilionyesha kuwa ili wizara iweze kukusanya fedha za kutosha kwenye balozi zetu ni kwa kurudisha utaratibu wa utoaji wa viza kufanywa na Balozi zetu tofauti na utaratibu unaotumika hivi sasa ambapo wageni huweza kupatiwa viza pindi wanapowasili katika vituo vya kuingilia nchini (viza on arrival).

Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni, haikubaliani na wazo hili la wizara kwani badala ya kuongeza wageni kuja nchini litapunguza sana hasa ikizingatiwa kuwa ni nchi chache sana ambako tuna ofisi za Balozi na pia kuna nchi nyingine kama Marekani ambapo, kama mgeni yupo Carlifonia na anataka kusafiri kuja Tanzania atalazimika kwanza kusafiri kwenda Washington ambako ndiko kwenye ubalozi atafute visa na ndipo aweze kuja nchini. Utaratibu huu utaongeza gharama kubwa za usafiri kwa wageni na watalii na hivyo kulipotezea taifa mapato yataokanayo na utalii kwani wageni watapungua.

Aidha, tunaikumbusha wizara kuhusiana na Itifaki ya kuwa na“Single Tourist Destination Protocol” na uwepo wa hati ya kusafiria na visa moja ya utalii “Single Tourist Visas” kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, hivyo kama sisi tukifanya huo uamuzi basi wenzetu Kenya wataendelea kupata wageni wengi zaidi kutokana na visa ya pamoja na wageni wataingia Tanzania kutokana na visa za Kenya chini ya Itifaki hiyo.


8.1 Mkutano wa Mabalozi wa Mwaka 2013/2014

Mheshimiwa Spika, wizara inahitaji kiasi cha shilingi bilioni 1 kwa ajili ya kufanikisha mkutano wa mabalozi kwa mwaka wa fedha 2013/2014 , na wizara iliwasilisha maombi ya fedha hizo Hazina kama sehemu ya kipaumbele lakini hazikuweza kupatikana .

Kambi rasmi ya upinzani Bungeni, inaitaka serikali kuiondoa aibu hii na kutenga hizo fedha kwa ajili ya kufanikisha mkutano huo na tunapendekeza kuwa katika fungu la protocol safari za nje ndipo fedha hizo zipunguzwe na kutumika kwa ajili ya mkutano wa mabalozi wetu ili waweze kupeana ushauri na uzoefu,ili kuboresha ufanisi wa majukumu yao.

8.2 Utaratibu wa Kupeleka Fedha kwenye Balozi

Mheshimiwa Spika, kutokana na utaratibu wa kupeleka fedha kwenye balozi zetu kuwa na mlolongo mrefu wa kwanza kutoka Hazina na kupelekwa Wizarani, ndipo wizara isambaze fedha hizo kwenye balozi zetu mbalimbali umesababisha fedha kuchelewa kufikishwa kwa wakati kwenye balozi zetu na hivyo kusababisha usumbufu mkubwa na ucheleweshaji wa kazi kwenye balozi zetu.

Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni, inaitaka serikali kubadilisha utaratibu huu na hazina iwe inapeleka fedha hizo moja kwa moja kwenye balozi husika badala ya kuzipitisha wizarani kama ilivyofanya kwenye fedha za Halimashauri mbalimbali nchini ili kupunguza usumbufu huo.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo kwa niaba ya kambi rasmi ya Upinzani naomba kuwasilisha.



______________________________ __

Ezekiah Dibogo Wenje

MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI

NA

WAZIRI KIVULI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
CHANZO JAMII FORAM

BALOZI BISWARO AWAPA CHANGAMOTO VIJANA WA STARS!!

$
0
0
MAZOEZINa Boniface Wambura
Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Joram Biswaro amewataka wachezaji wa Taifa Stars kuhakikisha wanaipeleka timu hiyo kwenye fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika mwakani nchini Brazil.
Ametoa changamoto hiyo wakati alipotembelea mazoezi ya timu hiyo jana (Mei 29 mwaka huu). Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imepiga kambi nchini Ethiopia na inafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Addis Ababa.
 “Watanzania tunafurahi kutokana na uwezo mnaouonyesha, hasa baada ya kuifunga Morocco mabao 3-1. Kama mliwafunga nyumbani hata kwao mnaweza kuwafunga. Tunataka kuwaona Maracana (Brazil) mwakani, mimi tayari ninayo tiketi mtanikuta kule,” amesema Balozi Biswaro ambaye enzi zake aliwahi kuichezea timu ya Yanga.
Taifa Stars ambayo iko Addis Ababa tangu Jumatatu (Mei 27 mwaka huu) imeweka kambi katika hoteli ya Hilton ambapo Jumapili (Juni 2 mwaka huu) itacheza mechi ya kirafiki na Sudan (Nile Crocodile) kwenye Uwanja wa Addis Ababa.
Balozi Biswaro ameikaribisha Taifa Stars ubalozini Addis Ababa mara baada ya mechi dhidi ya Sudan ambapo itakutana na baadhi ya Watanzania wanaoishi Ethiopia kabla ya kuondoka alfajiri kwenda Marrakech, Morocco kwa kupitia Cairo, Misri.

Kocha Kim Poulsen amesema kikosi chake kinaendelea na mazoezi vizuri na kitaimarika zaidi baada ya wachezaji Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wanaochezea timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) kujiunga nacho Juni 3 mwaka huu jijini Marrakech kwa ajili ya mechi dhidi ya Morocco itakayochezwa Juni 8 mwaka huu.
Wachezaji walioko katika kikosi cha Stars jijini Addis Ababa ni Juma Kaseja, Aggrey Morris, Mwadini Ally, Ally Mustafa, Shomari Kapombe, Kevin Yondani, Erasto Nyoni, Haroub Nadir, Mwinyi Kazimoto, Frank Domayo, Mrisho Ngasa, Khamis Mchana, Amri Kiemba, Salum Abubakar, Simon Msuva, John Bocco, Vicent Barnabas, Mudathiri Yahya, Athuman Idd, Haruni Chanongo na Zahoro Pazi.

KATIBU MKUU WA CCM ABDULRAHMAN KINANA ATEMBELEA MGODI WA CHUMA NA MAKAA YA MAWE LIGANGA LUDEWA

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (wapili kulia) akionyeshwa sampuli mbalimbali za madini ya chuma kwenye kituo kinachofanya utafiti wa awali kuhusu kiwango cha chuma kinachoweza kupatikana kwa kuchimbwa eneo la Liganga, wilayani Ludewa mkoani Njombe alipotembelea karakana ya kampuni ya Kichina ya Tanzania China International Mineral Resorce Ltd, inayofanya uchunguzi huo. Anayempa maelezo ni  Meneja Utawala wa kampuni hiyo, Tao Jian. Kushoto ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, mgodi huo utaanza kuzalisha madini hayo ya Chuma na Makaa ya mawe mwaka 2019.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (wapili kulia) akionyeshwa sampuli mbalimbali za madini ya chuma kwenye kituo kinachofanya utafiti wa awali kuhusu kiwango cha chuma kinachoweza kupatikana kwa kuchimbwa eneo la Liganga, wilayani Ludewa mkoani Njombe alipotembelea karakana ya kampuni ya Kichina ya Tanzania China International Mineral Resorce Ltd, inayofanya uchunguzi huo. Anayempa maelezo ni  Meneja Utawala wa kampuni hiyo, Tao Jian.
 Tao Jian akiwaonyesha Kinana na msafara wake, ramani linalofanyiwa kazi na kampuni yake katika kutafiti aina na kiasi cha Chuma kitakachoweza kupatikana Liganga

 Mabosi wa Kampuni ya Kichina inayofanya utafiti wa aina na kiasi cha chuma kitakachopatikana Liganga, wakitoa maelezo ya jumla kuhusu mradi huo unavyoendelea
Kilima cha madini ya Chuma, kinavyoonekana kwa mbali eneo la Liganga PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO

WADAU WA TCAA WAKUTANA DAR

$
0
0
untitled5 51f77
Mdau kutoka kampuni ya Alia aviation consultants Mahmud Shamt(aliesimama)akitoa ufafanuzi. 
untitled6 52748

untitled7 d153a
Fadhili Manongi (kulia akiongae) MK wa Bodi Juma Mbwana Juma.
untitled8 ce63a

TAARIFA ZAIDI KUHUSU MTOTO ALIYEDONDOKA KWENYWE BOMBA LA MAJI MACHAFU

$
0
0
This frame grab taken from AFPTV footage received on May 28, 2013 shows rescue workers breaking away bits of a pipe to remove a newborn baby boy stuck inside in the city of Jinhua, in the eastern province of Zhejiang.  The newborn baby boy was rescued from a sewage pipe in a Chinese apartment building after being flushed down a toilet, state media said, provoking online outrage on May 28.    CHINA OUT   AFP PHOTO / AFPTV        (Photo credit should read AFPTV/AFP/Getty Images)
Waokoaji wakivunja bomba la maji taka kumuokoa kichanga huyo.
Mtoto mchanga aliyeokolewa kutoka bomba la kupitishia maji taka nchini China amerejeshwa kwa mama yake baada ya maafisa wa polisi kubaini kuwa kutumbukia  kwake katika bomba hilo ilikuwa bahati mbaya.
Tukio hilo la kuokolewa kwa mtoto mchanga katika jimbo la Pujiang  lilizua shutuma kali kutoka kwa raia wa China na wahisani wengi walijitokeza kumsaidia mtoto huyo wa kiume.
Mtoto huyo tayari amechukuliwa na mama yake kutoka hospitali.
Mwanaume mmoja ameomba uchunguzi wa kubaini kama mtoto huyo ni wake na kusema ikibainika ni hivyo, yuko tayari kujadiliana na mama huyo jinsi ya kumlea.
Polisi wameamua kuwa mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 22 hatakabiliwa na mashitaka yoyote.

article-2331941-1A0AF3D2000005DC-345_634x425
Mtoto aliyeokolewa kutoka kwenye bomba la kupitisha maji taka baada ya kupatiwa huduma ya kwanza.

Watoto wawili wa familia moja wauawa kikatili mkoani Singida baada ya kulawitiwa na watu wasiojulikana.

$
0
0
DSC01448
Makaburi walikozikwa wanafunzi wawili waliolawitiwa na kisha kunyongwa hadi kufa. (Picha na Nathaniel Limu).
DSC01402
Mama mzazi wa watoto waliobakwa na kisha kunyongwa hadi kufa Veronica Nuru mkazi wa kijiji cha Lukomo wilaya ya Mkalama, akizungumzia tukio la kuuawa kikatili watoto wake.
DSC01430
Afisa mtendaji wa kata ya Iguguno Josia Pangani akizungumzia tukio la kulawitiwa na kisha kunyongwa hadi kufa wanafunzi wawili wa familia moja wa shule ya msingi Lukomo wilaya ya Mkalama.
Na Nathaniel Limu.
Watoto wawili wa familia moja wameuawa kikatili  mkoani Singida baada ya kulawitiwa na  watu wasiojulikana,  kisha  kunyongwa kabla ya milii yao  kwenda kufungwa kwenye mti porini.
Watoto hao wametajwa kuwa ni Esta Daudi  (14)  na  Anita Shila (9)  wote wanafunzi wa darasa la saba na  tatu katika shule ya msingi Lukomo kata ya Iguguno wilaya ya Mkalama mkoani Singida.
Afisa mtendaji wa kata hiyo Josia  Pangani, amesema tukio hilo limetokea majira ya saa  12 jioni wakati watoto hao  wa kike wakiwa wanachunga mifugo kwenye pori jirani na nyumbani kwao.
Pangani amesema  baada ya  muda  wa kurejesha  mifugo  zizini kufika, wazazi wa watoto hao  walishangaa kutowaona watoto wala mifugo, hali iliyosababisha kuanza juhudi za kuwatafuta.
Amesema juhudi hizo hazikuweza kuzaa matunda siku hiyo hadi kesho yake walipoikuta miili ya watoto hao ikiwa imefungwa kwenye mti.
Baada ya uchunguzi  wa kitaalamu kufanyika, ilibainika kuwa walibakwa, kunyongwa shingo, kisha kufungwa vitambaa usoni na watu wasiojulikana.
Habari za kipolisi zinasema  kuwa watu wawili akiwemo baba mzazi wa watoto waliouawa wanahojiwa kuhusiana na tukio hilo.
Tukio hilo limekuja mwezi mmoja tu baada ya mvulana mmoja mkazi wa kijiji hicho kulawitiwa, kuvunjwa mkono na kutobolewa  macho kisha kuuawa, hali inayozua hofu kubwa kwa wakazi wa eneo hilo.

Diamond afunguka kuhusu Wema, Penny, Jokate, Uwoya, Aunt katika “Take One”

$
0
0
diamond-zamaradi-mketema-wema-sepetu

diamond-zamaradi-mketema-wema-sepetu-0
Msanii Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amefunguka kupitia kipindi cha Take One cha Clouds TV, kuwa hana tena mapenzi na aliyekuwa mpenzi wake, mrembo Wema Isaack Sepetu. Akihojiwa na Zamaradi Mketema katika kipindi hicho, Diamond ameeleza anavyomfeel sana mpenzi wake wa sasa Penny ambaye anadai anamuheshimu na wala hamcheat.Kuhusu kutoka kimapenzi na wasanii wa Filamu Bongo, Irene Uwoya pamoja na Aunt Ezekiel, Diamond ameruka kwa kusema kuwa anamheshimu sana Uwoya wakati akidai kuwa Aunt alikuwa demu wa mshikaji wake.

Mkali huyo ameweka wazi pia kuhusu mapenzi yake na Jokate kwa kummwagia sifa kadhaa na kueleza kuwa yeye ndiye mwenye makosa maana Jokate alikuwa innocent na hakuwahi kumkosea japo aliachana naye na kurudi kwa Wema kabla hajaangukia kwa mrembo Penny ambaye ndiye anataraji awe mama watoto wake.

BREAKING NEWZZZ : MATOKEO YA KIDATO CHA NNE YATOKA, YAANGALIE HAPA


Mwili wa Ngwea watarajiwa kuwasili nchini Jumamosi huku watanzania wakiombwa kuchangia kwa hali na mali.

$
0
0
IMG_6306
Msemaji wa Kamati ya Kuratibu Mazishi ya Msanii Albert Mangwea aliyefariki nchini Afrika Kusini akiwa katika shughuli zake za kimuziki Adamu Juma (kushoto) akitoa taarifakwa vyombo vya habari kuwa kama mambo yatakwenda kama yalivyopangwa mwili wa mwanamuziki huyo unatarajiwa kuwasili nchini siku ya Jumamosi Jioni.

Aidha amesema mwili huo unatarajiwa kuagwa siku ya Jumapili saa 2 asubuhi kabla ya kusafirishwa kuelekea Mororgoro Kihonda kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika tarehe 3 Mwezi wa Sita mwaka huu.
Adamu Juma ametumia fursa hiyo kuwaomba watanzania kujitolea michango ili kufanikisha msiba huo.
Unaweza kutuma mchango wako kwenye Namba ya Kaka wa marehemu Keneth Mangwea +255-754-967738 ambayo imeunganishwa na M-Pesa ili kufanikisha za mazishi ya mpendwa wetu.
Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.

SIKILIZA MJADALA ULIOSABABISHA BUNGE KUHAIRISHWA MCHANA WA LEO HAPA

$
0
0
Za moto moto leo kutoka kwenye tunaloliita Bunge La Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania, sintofahamu imetokea ndani ya bunge baina ya wabunge wa Cuf na Chadema, hali iliyopeleka wabunge wa vyama hivyo kutaka kupigana ndani ya Bunge.Sikiliza ilivyokuwa hapa


RATIBA KAMILI YA MSIBA WA ALBERT MANGWEA

$
0
0

Baada ya kumalizika kwa uchunguzi, uliokuwa ukifanyika katika hospitali ya Hillbrow, mwili wa marehemu Albert Mangwea(Pichani) unatarajiwa kuwasili Jumamosi kwa ndege ya Shirika la Ndege la Afrika ya kusini, ukitokea nchini Afrika ya kusini.
Mwili utapelekwa moja kwa moja katika hospitali ya muhimbili kuhifadhiwa, uletwaji wa mwili huo, ni kwa hisani ya Clouds Media Group. Ndio waliogharimia safari ya mwili wa marehemu.
Jumapili asubuhi, kuanzia saa mbili, mwili wa Albert Mangwea utakuwa unaagwa na hapa kampuni itakayoshughulikia zoezi hili ni Entertainment Masters na zoezi ni katika viwanja vya Leaders Club. Baada ya mwili kuagwa, safari ya kumsindikiza Albert Mangwea kuelekea kwenye maziko itanza, na hii itakuwa ni kuelekea Morogoro.
Push Mobile nao wametoa shilingi Milioni 5 na Bongo records pia wametoa Milioni 5 
Mwili wa Mangwea utazikwa Jumatatu katika eneo la Kihonda, mkoani Morogoro.
Michango zaidi ya wadau inahitajika ambapo kwa tigopesa namba ni 0717 553 905
                                                                                         M pesa namba ni 0754 967 738

Rasimu ya Katiba kuzinduliwa Jumatatu, Juni 3 mwaka huu.

$
0
0
Mwenyekiti-na-Katibu-wa-Tume-ya-Mabadiliko-ya-Katiba-Jaji-Joseph-Warioba-na-Assaa-Rashid
Mwenyekiti na Katibu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba na Katibu, Tume ya Mabadiliko ya Katiba Assaa-Rashid.
Tume ya Mabadiliko ya Katiba inapenda kuwafahamisha wananchi wote kuwa itafanya uzinduzi wa Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania siku ya Jumatatu, Juni 3, 2013, kuanzia saa 8:00 mchana  katika viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam.
Uzinduzi huo utarushwa moja kwa moja na vituo vya redio vya TBC Taifa, ZBC Redio na vituo vya televisheni vya TBC 1 na ZBC TV na vituo vinginevyo vya redio na televisheni.
Rasimu hiyo ya Katiba imetokana na maoni ya wananchi, viongozi na makundi mbalimbali waliyowasilisha kwa Tume kupitia njia mbalimbali zikiwemo mikutano, barua pepe, ujumbe mfupi wa simu za mikononi (sms) na nyinginezo.
Tume inawaomba wananchi na wadau kufuatilia uzinduzi huo kwa makini kupitia vyombo hivyo vya habari.
Imetolewa na:
Assaa Rashid,
Katibu, Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

AAR WITH THE MINISTER OF INFORMATION, CULTURE ANS SPORTS DR. FENELLE MKUNGARA TO SUPPORT TLGU

$
0
0

Ajali ya Gari Mtoni Kwa Kisasi Zenzibar

$
0
0

 Wananchi wakiwa katika harakati za kumuokoa dereva wa gari aina ya Haice yenye namba za usaji Z 239 DX, inayochukuwa Watalii, kikitokea Kiwengwa na kugongana na gari yenye namba za usajili Z920 CP, ikitokea mjini kuelekea bububu, Kwa mujibu mashuhuda walioshuhudia ajali hiyo wamesema ajali hiyo imesababishwa na haraka za madereva hao kila mtu akitaka kuwahi.
Wananchi wakiangalia  jinsi ya dereva wa haice akinasuliwa katika usukani baada ya kutokea ajali hiyo.
chanzo zanz newz

TAARIFA YA UCHUGUZI JUU YA KUTEKWA NA KUUMIZWA KWA ABSALOM KIBANDA HII HAPA

$
0
0
Mhariri Mtendaji wa New Habari (2006) Ltd na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibanda
TAARIFA YA UCHUGUZI JUU YA KUTEKWA NA KUUMIZWA KWA ABSALOM KIBANDA IMEWASILISHWA NYUMBANI HOTEL – TANGA MEI 30, 2013
UTANGULIZI:Usiku wa Jumanne ya Machi 5 kuamkia Machi 6, 2013, Mhariri Mtendaji wa New Habari (2006) Ltd, ambaye pia Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibanda alivamiwa na kujeruhiwa vibaya akiwa nje ya lango la kuingilia nyumbani kwake Mbezi Juu, Dar es Salaam.
Tukio hilo liliishtua na kutikisa taifa kwa kiwango kikubwa si tu katika tasnia ya habari nchini, bali pia jamii kwa ujumla hasa baada ya aina ya utekaji, utesaji na usiri uliotumika katika kufanikisha uhalifu huu kufanana kwa karibu na tukio lilomkuta Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madkatari Tanzania, Dk. Stephen Ulimboka lililotokea karibu miezi tisa kabla ya tukio la Kibanda yaani, usiku wa Juni 26, 2012.
Ukiacha matukio hayo, miezi sita kabla ya Kibanda kutekwa na kuteswa Mwandishi Daudi Mwangosi, aliuawa akiwa mikononi mwa vyombo vya dola Septemba 2, 2012 huko Nyololo, Iringa akiwa kazini.Tukio la Kibanda limekuwa na sura ya mwendelezo wa mauaji au utesaji wa wanahabari, hasa ikitiliwa maanani kuwa Mwandishi Issa Ngumba (45) wa Radio Kwizera aliyekuwa anafanyia kazi zake katika Wilaya ya Kakonko, Kigoma, Januari mwaka huu, alipigwa risasi na kuuawa katika mazingira ya kutatanisha.Kama hiyo haitoshi, tukio la kutekwa na kudhuriwa kwa Kibanda limetokea mwezi mmoja tu baada ya Mwandishi wa Gazeti la Tanzania Daima, Shaaban Matutu kupigwa risasi na polisi akiwa nyumbani kwake Dar es Salaam kwa maelezo kuwa kimakosa polisi walidhani Matutu ni jambazi.Mazingira ya kutekwa na kuumizwa kwa Kibanda yalitia wasiwasi kuwa upo uwezekano, na dalili zilionyesha kwamba waliofanya kitendo hicho cha kinyama hawakuwa wezi wala majambazi kutokana na ukweli kwamba licha ya kuwa na fedha zipatazo shilingi milioni tatu taslimu ndani ya gari, laptop, simu tatu za gharama (ipad, iphone na Blackberry), watekaji hawa hawakuchukua chochote baada ya kukamilisha uhalifu wao.Kibanda aliumizwa kwa kiwango kikubwa. Alitobolewa jicho la kushoto, akaumizwa vibaya kichwani kiasi cha kusababisha kuvunjika kwa baadhi ya mifupa ya kichwa.


Aling’olewa meno mawili na kucha mbili, tena bila gazi. Watekaji hawa, katika unyama wa ajabu kabisa, walimkata pingiri ya kidole cha pete chini ya kucha na kuondokana nayo.Hali hiyo iliibua maswali mengi, watu wengi wakajiuliza na kutafuta sababu za kutekwa na kuumizwa kwa Kibanda kiasi hiki. Kutokana na kuwapo kwa maelezo mengi yanayotofautiana kuhusu tukio hilo, ikabidi Jukwaa la Wahariri Tanzania lifanye uamuzi.Katika kikao cha Machi 8, 2013 Jukwaa la Wahariri Tanzania liliunda TIMU ya watu watano na kuipa hadidu rejea za kufanya uchunguzi wa kihabari juu ya shambulio hilo kubaini limetokana na nini.

Timu hiyo iliundwa kufuatia uamuzi wa Jukwaa la Wahariri kufanya uchunguzi huo na baada ya kukubalika kwa ombi la ruzuku ya kufanya uchunguzi huo wa kihabari kutoka Mfuko wa Vyombo Vya Habari Tanzania (TMF). Ruzuku ya TMF ililenga kiujumla kutumia tukio la Kibanda kuwa chanzo cha kutengeneza mazingira salama zaidi kwa waandishi na wahariri na kwamba kiwango cha matukio ya kuteswa, kupigwa na kuuawa kwa waandishi yanapungua kila mwaka. Timu hii imefanya kazi usiku na mchana kwa kwa zaidi ya mwezi. Timu imezungumza na wadau 26.

Kati ya hawa yumo Kibanda mwenyewe, mke wake, ndugu zake, wasaidizi wake, waajiri wake wa zamani na wa sasa, viongozi wa kisiasa na vyombo vya dola kutafuta ukweli wa jambo hili. Pia tumesoma matamko na habari zilizochapishwa kwenye mitandao ya kijamii na magazeti ya kati ya Machi 5, 2012 na Aprili 5, 2012 kwa nia ya kufanya ulinganishi wa taarifa tulizozipata kutokana na uchunguzi na habari zilizochapishwa baada ya kutekwa kwake.Vyombo vya dola akiwamo Waziri mwenye dhamana walikataa kuhojiwa wakisema kuna tume ya serikali inayofanya kazi hiyo na kwamba kuhojiwa kungeonyesha kutokuwa na imani na tume hiyo.

Leo tunawasilisha muhtasari wa ripoti hii. Ripoti kubwa pamoja na viambatanisho vyake, itachapishwa na kuwekwa katika kitabu kimoja. Utaratibu mwingine wa kuchapisha habari ambazo hazijachapishwa kuhusiana na tukio hili (untold stories) pia utaandaliwa kwa ushirikiano na Jukwaa la Wahariri kwa nia ya kuieleza jamii maajabu juu ya kadhia hii.Tulipewa Hadidu Rejea ziafuatazo:

HADIDU REJEA:1. Kuchunguza mazingira ya kabla na baada ya tukio la kushambuliwa kwake. Kabla ya kushambuliwa kwa maana ya kufahamu kama kulikuwa na viashiria vyovyote vinavyoelekea kuwapo kwa mipango ya mashambulizi dhidi yake.2. Kuchunguza mazingira ya tukio lenyewe kwa kujikitika katika mwenendo wake hasa siku nzima ya Jumanne Machi 5, 2013.3. Kuangalia mazingira ya kazi ndani ya Kampuni ya New Habari (2006), Ltd na nje ya kampuni hiyo kwa kumulika sababu za kuhama kwake kutoka Free Media mwishoni mwa mwaka jana na kuhamia New Habari.4. Kuchunguza jambo jingine lolote linaloweza kutoa mwanga wa sababu za kuvamiwa na kupigwa kwa Kibanda.5. Kuchunguza mazingira ya sasa ya kazi kwa wanahabari na kupendekeza hatua za kuchukua kutokana na kile kitakachobainika

YALIYOJIRI KATIKA UCHUNGUZI:1.0. Kuchunguza mazingira ya kabla na baada ya tukio la kushambuliwa kwake. Kabla ya kushambuliwa kwa maana ya kufahamu kama kulikuwa na viashiria vyovyote vinavyoelekea kuwapo kwa mipango ya mashambulizi dhidi yake.Timu ya uchunguzi ilitumia muda mwingi katika eneo hili, kubaini iwapo kulikuwapo viashiria, sababu au matukio ya wazi yenye mwelekeo wa kujitokeza kwa shambulio hili. Tuliangalia pia iwapo wapo watu au makundi yaliyokwishapata kuonyesha ishara kwa matendo au kwa kauli juu ya uwapo wa nia hii. Uchunguzi umebaini kuwa kuliwapo viashiria vingi, isipokuwa Kibanda au watu wake wa karibu hawakupata kufikiri kuwa huenda vingeweza kuleta madhara makubwa kiasi hiki kama ifuatayo:-

1.1. Wiki tatu kabla ya Kibanda kuvamiwa, kutekwa na kuumizwa, gari la polisi aina ya gofu Na PT 180 liliwafuatilia kwa muda mrefu Absalom Kibanda na Ofisa Mtendaji Mkuu wa New Habari (2006) Ltd, Hussein Bashe likiwa limeegeshwa nje ya ofisi zao Sinza Kijiweni na baadaye likawafuatilia hadi Sinza Makaburini, ambapo walisimamisha magari yao na kuzungumza na polisi hao waliosema walikuwa wanatilia shaka magari yao. Baada ya kuzungumza kwa muda polisi waliondoka.
1.2. Usiku wa Februari 25, mwaka huu majira ya saa 09:00 usiku, Kibanda walivamiwa na watu walioingia kwenye uzio wa nyumba yao wakavunja kioo cha gari analotumia, lakini kioo kilipovunjwa ‘alarm’ ilipiga kelele, Kibanda akatoka nje na watu hao wakakimbia.

1.3. Kutokana na uvamizi huo, Kibanda na wapangaji wengine katika nyumba zilizopo kwenye uzio mmoja, waliona hatari ya kuvamiwa hivyo wakaanza mazungumzo na kampuni ya Ulinzi ya Kiwango, iliyowataka kufunga kamera za usalama na kuweka walinzi watano. Hadi Kibanda anatekwa, walikuwa hawajahitimisha mazungumzo na kampuni hii ya Kiwango.

1.4. Kuna askari anayefanya kazi Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) miezi minane kabla alipata kumpa Kibanda taarifa za kinteligensia, kuwa kulikuwapo mpango wa kumteka na kumuumiza. Taarifa kama hizo pia alipewa na wasamaria wanaofanya kazi katika Jeshi la Polisi. Kwa maneno yake Kibanda alisema:“Kuna rafiki yangu askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), kama miezi minane au tisa hivi aliwahi kuniambia ‘unaandika sana usidhani kama watu wanakupenda. Chukua tahadhari hasa unapofika getini nyumbani kwako’. Tangu wakati huo nimekuwa nikichukua tahadhari sana.“Wiki mbili kabla ya tukio, niliwahi kuhisi kitu kama hicho [cha kuvamiwa] nikiwa getini. Nilipiga honi wakachelewa kuja kunifungulia, niliogopa sana. Hata nilipoingia ndani nilikuwa nimekosa raha kabisa.“Pia kuna rafiki zangu polisi waliwahi kuniambia kwamba ninatafutwa na kwamba watu wananifuatilia na ikibidi wanitengenezee ajali au kunifanyia kama Ulimboka au Kubenea.”

1.5. Ndani ya miezi mitatu mbele ya mlango wa ofisi yake Kibanda (Free Media Limited) ilikuwa mara kwa mara muda wa asubuhi anapofika ofisini anakuta damu. Haikufahamika kama damu hiyo ilikuwa ni ya binadamu, kuku, ng’ombe, kunguru au mbuzi, bali waliipuuza wakidhani ni masuala ya ushirikina. Mhariri Mtendaji wa sasa, Ansbert Ngurumo, amethibitisha kuwapo kwa tukio hilo.1.6. Mfanyakazi mwandamizi wa Kampuni ya New Habari anakofanya kazi sasa Kibanda ndani ya wiki mbili kabla ya kutekwa na kuumizwa kwake alipata kumwabia Kibanda maneno mazito mara tatu, na hapa tunamnukuhu Kibanda:“Aliniambia Danny Mwakiteleko [aliyekuwa Naibu Mhariri Mtendaji wa New Habari] hakufa kwa ajali, bali alikufa kutokana na blood clotting (kuganda kwa damu). Hivyo ikitokea mtu ukapata ajali au ukapigwa na kuumizwa sana sehemu za kichwa hivi au tumbo, ni lazima madaktari wadhibiti sana blood clotting.“Na kweli, nilivyoletwa hapa Milpark hospitalini, madaktari walikuwa wananidunga sindano sita kila siku kwenye kitovu kuzuia blood clotting. …. (jina linahifadhiwa) aliniambia maneno haya mara tatu, katika mazingira yasiliyotarajiwa na kwa msisitizo ambao sikujua maana yake. Nasema …. (jina linahifadhiwa) naye achunguzwe kwa kina. Inawezekana kuna jambo analijua.”Ofisa huyu, alipishana dakika chache na Kibanda muda wa kutoka ofisini baada ya kipindi cha kwanza cha mechi kati ya Real Madrid na Manchester united kumaliza nusu ya kwanza (half time). Dakika ishirini baadaye Kibanda alishambuliwa.

2.0. Kuchunguza mazingira ya tukio lenyewe kwa kujikitika katika mwenendo wake hasa siku nzima ya Jumanne Machi 5, 2013.2.1.Familia ya Kibanda na Kibanda Mwenyewe hawakuwa na wasiwasi wowote siku hiyo kwani hawakuwa na hisia wala wazo kuwa ungetokea uvamizi huo.

2.2. Kibanda alipopiga honi, mlinzi alisogea langoni kumfungulia. Ghafla akasikia kishindo kikubwa. Akasikia kelele za Kibanda akiomba msaada. Kijana huyu Baraka Ibrahim mwenye umri wa miaka 27, aliogopa. Aliogopa kwa mana hakuwa na silaha yoyote mkononi. Hakuwa na panga, kisu, rungu, wala filimbi. Kwa maneno yake anasema:“Nilivyoona ningefungua geti hata mimi ningekufa, nilikimbia kuwaamsha majirani. Sikuwa hata na namba ya simu ya mtu yeyote kati ya mabosi wangu ninaowalinda. Nilikuwa mimi tu, imani yangu na Mungu wangu…. kutokana na maisha naifanya hivyo hivyo tu. Vinginevyo milele nisingefanya kazi hii ya ulinzi.”Mlinzi huyo alikimbilia kwa majirani katika nyumba aliyoamini yumo mwanaume, lakini akaanza kumwamsha House Girl, ili house girl amwamshe baba mwenyenyumba. Kitendo cha kuamshana na kuwapa taarifa kilichukua dakika tano hadi saba, na ndani ya muda huo, Mlinzi anasema watekaji wa Kibanda walifanyafanya unyama na uasi huo na kuondoka ndani ya muda mfupi kiasi hicho. “Watu hawa wana mafunzo maalumu,” anahitimisha.

2.3. Mke wake alikwenda kazini asubuhi na kurejea nyumbani jioni, lakini tofauti na utaratibu wake wa kawaida ambapo huwa anaangalia televisheni sebuleni hadi Kibanda anaporejea nyumbani, siku hiyo alikwenda kuangalia televisheni akiwa chumbani na usingizi ukampitia. Anasema hakusikia honi wala tukio la Kibanda kutekwa. “Hii inanitesa sana moyoni. Najiuliza kwa nini siku hiyo tu sikukaa sebuleni? Kwa nini siku hiyo tu nimelala mapema kabla Baba Joshua hajarudi (machozi yanamlengalenga). Najiuliza sipati jibu.”2.4. Mmoja kati ya wasaidizi wawili wa nyumbani kwa Kibanda, alisikia kelele za Kibanda akiomba msaada. Alimwamsha mwenzake na kumwambia. “Nasikia Baba Joshua anapiga kelele kama amevamiwa hivi.” Mwenzake alimwambia “Unaota maana kuna kelele za mpira.” Siku hiyo kulikuwa na mechi kati ya Real Madrid na Manchester United.Ni kweli zilikuwapo pia kelele za wanaoshangilia mpira siku hiyo, hivyo Kibanda alipoomba msaada, hata waliosikia walidhani watu wanashangilia mpira. Binti aliwaamsha Angela na mwenzake, wakaenda sebuleni, wakakaa na kuchungulia dirishani, wakaona mwanga wa gari getini, lakini baada ya kutosikia kelele yoyote wakarejea kulala wakidhani siye. Lakini binti mmoja alibaki sebuleni. Baada ya muda jirani mmoja akampigia simu Angela kumweleza kuwa mumewe ameshambuliwa.2.5. Kibanda kwa upande wake, anasema alipofika getini, alipiga honi, ghafla akaona watu wawili wamesimama pembeni mwa gari lake na mtu wa tatu akiwa kwa mbali. Kisha akasikia kishindo kikubwa, akidhani wanataka kuiba gari, aliatokea mlango wa abiria na kuanza kukimbia huku akiita. “Mama Joshua nisaidieeeeee.”Katika kukimbia, aliteleza akaanguka. Huku watesaji wake wakisema mara tatu “Afande piga risasi.” Kibanda alijaribu kupambana, akashika rungu, akawahoji amewakosea nini hadi wampige kiasi hicho, lakini hawakumjibu lolote. Waliendelea kumpiga, hadi akapoteza fahamu. Hakujua jicho limetobolewa saa ngapi, meno yameng’olewaje na wala pingiri ya kidole chake imekatawaje. Ifuatayo ni sauti ya Kibanda mwenyewe. Inasikitisha ila tuwe wavumilivu na tuisikilize.

3.0. Kuangalia mazingira ya kazi ndani ya Kampuni ya New Habari (2006) Ltd na nje ya kampuni hiyo kwa kumulika sababu za kuhama kwake kutoka Free Media mwishoni mwa mwaka jana na kuhamia New Habari.

3.1. Mazingira ya kazi ndani ya New Habari (2006) Limited na Freemedia Limited, yanaacha maswali kadhaa yenye kustahili majibu. Kama ilivyoelezwa kwenye Hadidu Rejea Na: 1, ndani ya kampuni ya New Habari imekuwapo misuguano isiyo na afya kwa kazi ya Kibanda kama mwandishi na tasnia ya habari kwa ujumla.

3.2.Mazingira ya kazi ndani ya Kampuni ya New Habari (2006) Ltd ni utata. Uhusiano katika chumba cha habari si mzuri. Ndani ya kampuni hawaaminiani na imefikia hatua wanatuhumiana kuwa huenda baadhi ya viongozi ndani ya New Habari wamehusika kumteka na kumuumiza Kibanda. Haya yameandikwa ndani ya mitandao ya kijamii, ikidai kwamba kiongozi mmoja ndani ya kampuni hiyo alihusika na utekaji wa Kibanda.Mkurugenzi wa Uhariri, Prince Bagenda anasema waliohusika kusambaza taarifa chafu dhidi ya kiongozi huyo wa New Habari wanatoka ndani ya kampuni hiyo.

3.3. Timu ya uchunguzi ilibaini kuwapo mgawanyiko mkubwa ndani ya New Habari (2006) Ltd kwa kuwapo kundi la ‘Habari Wazawa’ na ‘Habari wa Kuja’. Malalamiko mengi yanajikita katika msingi kuwa ajira hazitangazwi na watu wanaajiriwa bila kuzingatia sifa za kitaaluma.

3.4. Kibanda hakuhama Free Media kwa amani. Uchunguzi unaonyesha kuwa miezi kadhaa kabla ya kuondoka kwake alianza kupoteza mamlaka. Mwenyekiti wa Kampuni ya Free Media Ltd, Freeman Mbowe alianza kumsikiliza zaidi msaidizi wake ambaye alikuwa Naibu Mhariri Mtendaji, Ansbert Ngurumo kuliko yeye Kibanda. Kwa maneno yake, anasema:“Nilihofu kuwa Mbowe anaweza kutugombanisha. Nikaona ni bora niondoke nisije nikagombana na Mbowe au Ngurumo.”Anasema alianza kupoteza mamlaka yake na kutoaminika kwa mwajiri wake baada ya kuandika makala kuhusu Abdulrahman Kinana ambayo kabla ya kuiandika hakuwa na wazo la kuondoka. Yaliyofuata baada ya makala hiyo, yalimshukuma aondoke.

4.0. Kuchunguza jambo jingine lolote linaloweza kutoa mwanga wa sababu za kuvamiwa na kupigwa kwa Kibanda.

4.1. Uchunguzi ulifuatilia masuala mbalimbali ikiwamo miendendo ya watu waliotajwa kwa njia moja au nyingine kuhusinaa na tukio hili. Hata hivyo, karibu watu wote waliohojiwa, akiwamo Kibanda mwenyewe aliyeumizwa walimtaja kwa kutilia shaka mwenendo wa kijana Joseph Ludovick. Hofu yao, iliongezwa nguvu na maandishi aliyoyachapisha Ludovick kwenye mitandano ya kijamii siku ya Machi 6, 2013.

4.2. Usiku aliotekwa na kuumizwa Kibanda, Ludovick katika naye alidai kuwa ametekwa katika eneo la Shekilango na kupelekwa hadi Kigogo. Baada ya kutekwa aliibiwa kila kitu, ikiwamo begi, laptop, simu mbili, fedha taslimu Sh 35,000, akavuliwa nguo na kubaki na chupi tu. Pia alieleza kuwa alitoa taarifa hizo kituo cha polisi Mabibo.

4.3. Maelezo ya Ludovick yalitiliwa shaka na watu wengi hasa baada ya kuleeza kuwa watekaji walitumia muda wa saa mbili kumtoa Shekilango hadi Mabibo, umbali ambao kwa kiwaida mwendo wake hauwezi kuzidi dakika 10. 4.4. Daniel Chongolo aliiambia timu kuwa alfajiri ya Machi 6, siku anayodai kutekwa Ludovick yeye alimuona eneo la Mabibo wakati anatoka Muhimbili. Chongolo alikwenda kituo cha polisi Mabibo na kupewa taarifa kuwa Ludovick alitoa taarifa polisi kuwa alikuwa ametekwa ila akarudishiwa mali zake zote. “Alipouliza amefuata nini polisi, akawambia kama raia mwema amefika kuandikisha kumbukumbu kwa nia ya kuonyesha kiwango cha uhalifu kinavyoongezeka nchini,” anasema Chongolo. Timu ya uchunguzi ilikataliwa kupitia leja ya polisi kama itakavyoelezwa hapa chini.

4.5. Pia taarifa za uchunguzi wa timu hii zinathibitisha kuwapo kwa utata juu ya madai ya kuibwa kwa simu za Joseph Ludovick, kwani simu yake ya tigo (inayodaiwa kuibwa) ilitumika saa 01:21 asubuhi siku ya Machi 6, 2013. Muda huu ofisi za Serikali na Kampuni ya Tigo zilikuwa hazijafunguliwa

5.0. Kuchunguza mazingira ya sasa ya kazi kwa wanahabari na kupendekeza hatua za kuchukua kutokana na kile kitakachobainika.

5.1. Uchunguzi umebaini kuwa maisha ya wanahabari yapo hatarini. Hatari hii inatokana na makundi mengi yenye masilahi kuwaona wanahabari wanaosimamia ukweli kuwa maadui wa masilahi yao haramu. Kuna hatari kubwa inayowakabili waandishi wakati nchi inapoelekea kwenye uchaguzi wa mwaka 2015.

5.2. Uchunguzi umebaini kuwa usiri umepungua katika vyombo vya habari. Tofauti na zamani ambapo habari nyeti ziliandikwa kwa kuhifadhi majina ya waandishi wakitumia jina la MWANDISHI WETU. Simu hizi hata habari za kutisha waandishi wanaweka majina yao na hata wasipoweka, ndani ya vyumba vya habari vingi waandishi wapo tayari kutaja nani ameandika habari fulani.

5.3. Usaliti miongoni mwa waandishi wenyewe ndani ya vyumba vya habari unazidi kuongezeka na usipodhibitiwa hali itazidi kuwa mbaya zaidi. Mwenyekiti wa MOAT, Dk. Reginald Mengi anasema: “Hili ni jambo muhimu sana. Tuache usaliti vinginevyo wengi wataumia.”

5.4. Pia alishauri waandishi wa habari kurejea katika msingi wa taaluma, ambayo inawataka wao kuwa ndio wenye kuendesha vyombo vya habari badala ya kutegemea matakwa ya wamiliki au makundi yenye masilahi binafsi.

6.0. KILICHOBAINIKA:
6.1. Uchambuzi uliofanywa ni timu hii umebaini kuwa hoja nne zinazungumzwa kuhusiana na kutekwa na kuumizwa kwa Kibanda. Hoja hizi ni:-(i) Kazi yake ya uandishi wa habari(ii) Uhusiano wa kisiasa na vyama au wanasiasa mbalimbali(iii)Uhusiano wa kijamii ikiwamo mapenzi(iv) Vitendo vya rushwa.

6.2. Timu imejiridhisha kutokana na majibu ya wengi kuwa dhana ya mapenzi na rushwa, havina nafasi yoyote katika tukio hili. Wote waliohojiwa walieleza pasi na shaka kwamba suala hili la kushambuliwa na kuumizwa kwa kiwango kikubwa kwa Kibanda, halina uhusiano wowote na rushwa au mapenzi.

6.3. Kutokana na yaliyotajwa hapo juu kazi yake na siasa vikiunganishwa vimechangia kwa kiasi kikubwa kuvamiwa kwa Kibanda. Timu imebaini kuwa kuna kutupiana mpira kati ya vyombo vya dola na vyama vya siasa. Mchezo huu mchafu unaweza ukawa mwanzo wa kuumizwa kwa Kibanda na waandishin wengine.

6.4. Baadhi ya waliohojiwa walidai kuwa utekaji huu umefanywa na vyombo vya dola ukiwa sehemu ya mpango mkakati wa vyombo hivi kukihusisha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na vitendo vya ugaidi.6.5. Wanayataja matukio ya Uchaguzi Mdogo wa Igunga, maandamano ya Morogoro na Mkanda anaodaiwa kurekodiwa Mkurugenzi wa Usalama wa CHADEMA, Wilfred Lwakatare kuwa vililenga kukifanya CHADEMA kichukiwe na Watanzania kwa kukitaja kama chama cha kigaidi ambacho kinateka watu na kinawaumiza.

6.6. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe anadai kwamba mpango kama huo vyombo vya dola viliutumia kwa NCCR Mageuzi vikakisambaratisha, Chama cha Wananchi (CUF) kilisingiziwa udini kikapoteza mwelekeo na sasa vyombo hivyo vililenga kukifanya CHADEMA kionekane cha kigaidi mbele ya macho ya jamii ndiyo maana imerekodiwa mikanda kwa nia ya kuitumia kujenga hoja hiyo.

6.7. Wakati Mbowe akisema hayo, baadhi ya watu waliohojiwa wanadai kuwa CHADEMA kimepewa mafunzo na ushauri kutoka nje ya nchi kuwa kikitumia baadhi ya watumishi wa vyombo vya dola wasiokuwa waaminifu kuteka, kuumiza na hata kuua baadhi ya watu maarufu nchini wakiwamo waandishi na wanasiasa, basi wananchi wataamini kuwa Chama Cha Mapinduzi na Serikali yake kimeshindwa uongozi na sasa kimeanza kazi ya kuua wanaowapinga.

6.8. Kwa njia hiyo, inaelezwa kuwa hesabu za Chadema ni kuwa wananchi wataichukia CCM na Serikali yake na kukipa nafasi ya kuingia madarakani. Hapa kauli ya Chadema kuwa NCHI HAITATAWALIKA itakuwa imetimia.

6.9. Dhana nyingine iliyojitokeza ni kuwa wapo wafanyabiashara ambao wana vita binafsi, hivyo wanaamua kuumiza watu wasiowaunga mkono katika mipango yao na hilo ndilo limemkumba Kibanda, baada ya kuwa ameepusha mauaji ya mwandishi mmoja na aliyekuwa ameandaa mpango wa kuua mwandishi huyo hakuridhika hivyo akaamua amshughulikie Kibanda.

7.0. MAPENDEKEZO:Baada ya Timu kupata taarifa hizi na nyingine nyingi, inapendekeza yafuatayo:-

7.1. Taarifa hii ichukuliwe kama chanzo cha uchunguzi zaidi wa vyombo husika.7.2.

Yanahitajika marekebisho makubwa na ya haraka katika mifumo ya uendeshaji wa vyumba vya habari kwa nia ya kurejesha misingi ya uandishi wa habari inayokubalika.

7.3. Usalama wa wanahabari unapaswa kupewa kipaumbele na wamiliki, wanahabari wenyewe na jamii kwa ujumla. Hapa Timu inapendekeza yawepo mafunzo ya kuwawezesha wanahabari kutambua viashiria vya hatari na kuchukua hatua mara moja.

7.4. Kwa kiwango alichoumizwa Kibanda iwapo mwajiri wake asingejitolea kugharamia matibabu, hatujui hatima yake ingekuwaje leo hii. Tunapendekeza taasisi na mifuko mbalimbali inayojihusisha na masuala ya wanahabari kama Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) , Baraza la Habari Tanzania (MCT), Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF) na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) kuanzisha mfuko wa pamoja utakaotumika kugharamia matibabu ya waandishi watakaoumia wakiwa kazini.

7.5. Tukio la kutekwa kwa Kibanda limeonyesha mwanga kuwa wahariri tumegawanyika mno. Habari zilizochapishwa katika magazeti mbalimbali na mitandao ya kijamii zimeonyesha haja ya kuwafanya wahariri kuwa kitu kimoja kwa kuondoa tofauti zao zisizo na masilahi kwa tasnia ya habari.

7.6. Kuna viashiria vingi kuwa kuelekea mwaka 2015 matukio ya waandishi kuumizwa au kutekwa yanaweza kuongezeka kutokana na wanasiasa na vyama kuwania madaraka huku wakitumia baadhi ya watumishi katika vyombo vya dola. Kwa mantiki hiyo, vyombo vya habari na waandishi wa habari wachukue tahadhari kuanzia sasa.

7.7. Taasisi za habari zifanye juhudi za makusudi kukutana na vyama viwili vya siasa vya CCM na CHADEMA haraka iwezekanavyo, kuzungumzia viashiria hivi vya hatari vinavyoelekea kuvuruga amani ya Tanzania.

8.0. HITIMISHO:Ni dhahiri kuwa kupigwa na kuteswa kwa Kibanda kumejiegemeza katika siasa na kazi yake, hali inayofanya makundi muhimu kuchukua wajibu wa msingi. Kwa upande wa Serikali ni muhimu kufuatilia viashiria katika taarifa hii kwa nia ya kupata ukweli zaidi na kuchukua hatua stahiki za kisheria dhidi ya wahusika.Na kwa upande wa vyombo vya habari na taasisi za kihabari zinapaswa kutambua viashiria vinavyohatarisha usalama wa waandishi wa habari na wahariri na kutengeneza mazingira yatayokuwa salama zaidi kwa waandishi kufanya kazi zao.

9.0. SHUKRANI:

9.1. Tunapenda kulishukuru Jukwaa la Wahariri Tanzania, kwa kufanya uamuzi sahihi wa kuwezesha kufanyika kwa uchunguzi huu ulioanza kuonyesha mwanga wa nini kilitokea.

9.2. Tunapenda kulishukuru Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwa kushiriki kikamilifu na kuiwezesha timu hii kwa Rasilimali Watu na Mali kufanikisha kazi hii.

9.3. Tunapenda kuwashukuru Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF) kwa uwezeshaji wa ruzuku, uliofanikisha kufanya uchunguzi wa kihabari uliohusisha kwenda nchini Afrika Kusini kufanya mahojiano na Kibanda. Uwezeshaji huo pia unahusisha kutengeneza mwongozo kwa waandishi wenye lengo la kuwaepusha na hatari za kiusalama.

9.4. Tunawashukuru Kibanda, mkewe Angela, wanafamilia, ndugu na jamaa wa Kibanda na wanahabari wote waliohojiwa kwa ushirikiano mkubwa walioutoa kwa Timu hii.

9.5. Tunawashukuru wahariri wote kila mtu kwa nafasi yake, kutokana na ushauri wa mara kwa mara mliotupatia katika kufanikisha uchunguzi huu.

10.0. WAJUMBE WA TIMU:Timu hii iliundwa na wajumbe watano ambalo ni:1. Deodatus Balile – Mwenyekiti2. Pili Mtambalike – Mjumbe3. Jane Mihanji – Mjumbe4. Tumaini Mwailenge – Mjumbe5. Rashid Kejo – Katibu




RAIS AZUNGUMZA NA WANAFUNZI MJINI NANJING JIMBO LA JIANGSU CHINA

$
0
0
IMG_2467Wanafunzi wa Tanzania wanaosoma Elimu za Juu katika Vyuo Vikuu katika Mji wa Nanjing Jimbo la Jiangsu nchini China,wakiwa katika ukumbi wa mikutano wa  Sofitel Luxury Hotel,katika mazungumzo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,[Picha na Ramadhan Othman,China.]IMG_2467Wanafunzi wa Tanzania wanaosoma Elimu za Juu katika Vyuo Vikuu katika Mji wa Nanjing Jimbo la Jiangsu nchini China,wakisikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(hayupo pichani) wakati alipozungumza nao  leo  katika ukumbi wa mikutano wa  Sofitel Luxury Hotel, Mjini Nanjing katika jimbo la Jiangsu akiwa katika ziara  ya Kiserikali.[Picha na Ramadhan Othman,China.]IMG_2482Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(wa pili kushoto) akiwa na Mama Mwanamwema Shein,kushoto pamoja na Mawaziri na Maofisa aliofuatana nao katika ziatra ya Kiserikali nchini China,Rais alipata muda wa kuzungumza na wanafunzi wa Tanzania wanaosoma  katika Vyuo Vikuu mbali mbali, na  aliwaelezea  hali halisi ya Utulivu na Amani Iliyopo nchini Tanzania  ambapo aliwataka kuondokana na wasiwasi,[Picha na Ramadhan Othman China.]IMG_2487Mwanafunzi Sauli Elingarama ,Dkt wa Bianadamu aliokuwa akiuliza swali mbele ya Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,wakati wa mazungumzo na Wanafunzi wa Tanzania wanaosoma Vyuo Vikuu vya Mji wa  Nanjing Nchini China katika jimbo la Jiangsu,Rais yupo  China kwa ziara ya kiserikali.[Picha na Ramadhan Othman China.]

KATIBU MKUU WA CCM ABDULRAHMAN KINANA AZUNGUMZA NA WANANCHI KATA ZA UKWAMA NA INIHO MAKETE

$
0
0
1Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa kata ya Iniho Wilayani Makete wakati alipotembelea kata hiyo katika ziara yake ya mkoa wa Njombe leo, Kinana yuko mkoani Njombe kwa ajili ya shughuli za kuimarisha chama na kukagua miradi ya maendeleo katika kusimamia serikali ili kutekeleza ilani ya chama hicho na kuwahimiza wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo.PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-MAKETE6Naibu Waziri wa Maji na mbunge wa jimbo la Makete Injinia , Dk. Bilinith Mahenge akiwahutubia wananchi wa kata ya Iniho wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kata hio wakati Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana alipotembelea kata hiyo8Mkuu wa Wilaya ya Makete Bi. Josephine Matiro akizungumza na wananchi kuelezea jinsi serikali inavyotekeleza miradi ya maendeleo katika wilaya hiyo.9Wananchi wa Kata ya Iniho wakiwa katika mkutano huo
10Kikundi cha ngoma kikicheza ngoma ya asili ya kinyakyusa inayoitwa Ing’oma.17Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi CCM Ndugu Nape Nnauye akiteta jambo na Mzee Pascal Sangamjumbe wa shina la Singida  katika kata ya Tandala Wilayani Makete wakati katibu mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana alipotembelea katika kata hiyo leo18Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akizungumza na wanachama wa chama cha mapinduazi katika shina la Singida kata ya Tandala wakati alipotembelea katika kata hiyo leo19Mzee Pascal Sanga Mwenyekiti  wa shina la Posta  katika kata ya Tandala Wilayani Makete akifungua kikao hicho baada ya Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana na ujumbe wake kutembelea tawi hilo.22Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana na ujumbe wake akiongozana na Mkuu wa Wilaya ya Makete Bi. Josephine Matiro kutembelea tawi la Singida kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Makete Francis Chaula3Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi CCM Ndugu Nape Nnauye  akiwahutubia wananchi katika kata ya Iniho Wilayani Makete.

MZUMBE SECONDARY YAFUNGWA...WANAFUNZI WAPEWA SIKU MBILI WAPOTEE KATIKA MAZINGIRA YA SHULE

$
0
0

 Wananfunzi wakidato cha kwanza hadi cha sita katika shule ya sekondari Mzumbe Morogoro wamelazimika kuandamana kwenda ofisi ya mkuu wa mkoa wa huo wakishinikiza kuboreshewa huduma muhimu.
Maboresha wanayodai kuboreshewa shuleni hapo ni pamoja na miundombinu, kuondoa ubadhirifu, uongozi mbovu na kukomeshwa vitendo vya lugha chafu zinazo tolewa na baadhi ya walimu.
Maandamano hayo yalizimwa mapema asubuhi baada ya jeshi la polisi kulazimika kufika katika eneo la
sangasanga barabara kuu ya Iringa Morogoro ambapo maandamano hayo yalikuwa yamefika kuelekea katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Morogoro.
Wananfunzi hawa wa shule ya sekondari Mzumbe Morogoro ya wenye vipaji maalum wanadai kuwa maandamano hayo yanatokea baada ya kuvumilia kwa muda mrefu na hivyo wameamua kupaza sauti zao wakibainisha matatizo lukuki yanayo wasibu ambayo yanaweza kushusha kiwango cha taaluma yao.
Mkuu wa shule ya sekondari Mzumbe Dismas Njawa ameelezea namna alivyoweza kutatua baadhi ya matatizo lakini hayakukidhi haja za wanafunzi hao.
Katibu tawala Mkoa wa Morogoro Elia Ntandu alilazimika kwenda kuzungumza na wanafunzi hao akiahidi kuyafanyia kazi yale yatakayo wezekana.
Wanafunzi hawakuelewa, na ndipo Serikali ilipoamua kuifunga shule ya Sekondari ya vipaji maalumu, Mzumbe kwa muda usiofahamika na kuwapa wanafunzi siku mbili, kuanzia leo, kuondoka shuleni hapo
---
Monica Lyampawe, 
TBC Morogoro.

RAIS KIKWETE NA MKEWE MAMA SALMA WAKIWA KATIKA SAFARI YA KIKAZI -JAPAN

$
0
0
IMG_3141 
Rais Jakaya Kikwete akiambatana na mke wake Mama Salma tarehe 30. 5.2013 wakitembelea makumbusho ya karakana ya sayansi ya TOSHIBA iliyoko huko Kawasaki karibu na Tokyo nchini Japan inayohusika na utengenezaji wa injini za treni na vifaa vingine vye elektroniki  wakiangalia laptop ya kwanza  pamoja na calculator iliyotengenezwa  na kampuni hiyo mwaka 1985. Rais Kikwete yupo nchini Japan kuhudhuria mkutano wa tano wa uhusiano wa kiuchumi kati ya Japan na Africa.IMG_3147 
Rais Jakaya Kikwete akiambatana na mke wake Mama Salma tarehe 30. 5.2013 wakitembelea makumbusho ya karakana ya sayansi ya TOSHIBA iliyoko huko Kawasaki karibu na Tokyo nchini Japan inayohusika na utengenezaji wa injini za treni na vifaa vingine vye elektroniki  wakiangalia laptop ya kwanza  pamoja na calculator iliyotengenezwa  na kampuni hiyo mwaka 1985. Rais Kikwete yupo nchini Japan kuhudhuria mkutano wa tano wa uhusiano wa kiuchumi kati ya Japan na Africa.IMG_3210 
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Seneta Tetsuro Yano, Rais wa Association of African Economy and Development  (AFRECO) wakati Mama Salma akifuatana na Rais Kikwete walipohudhuria kwenye chakula cha usiku  (working dinner) kilichoandaliwa na seneta  huyo pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan  kuzungumzia uwekezaji  wa Japan kwa nchi za Afrika . Working dinner hiyo ilifanyika huko Tokyo nchini Japan tarehe 30.5.2013.
 PICHA NA JOHN LUKUWI

CHADEMA, CUF WAOMBA RADHI BUNGENI MJINI DODOMA LEO.BUNGE LAENDELA NA SHUGULI ZAKE KAMA KAWAIDA

$
0
0

CHAMA cha CUF na Chadema hivi punde Bungeni , vimekubali kuomba radhi kutokana na vurugu zilizosababishwa na CUF  yenye mrengo wa Kiliberali  na Chadema imemafanya hivyo kutokana na kuihusisha CUF na masuala ya ushoga na usagaji. 
Vyama hivyo vimeomba radhi baada ya Kamati ya Maadili ya Bunge kufanya kikao  kuanzia saa 11:00 jioni mpaka saa 2:30 usiku na kukubaliana kila chama kumuomba spika radhi na pia kuliomba Bunge radhi kutokana na vurugu za jana.
CUF wamelazimika kumuomba spika radhi; kuomba radhi Bunge na kuwaomba radhi Chadema kwa kumtukana Waziri kivuli wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Ezekeil Wenje wakati akisoma hutuba yake ambayo ndani yake ilieleza sera za mrengo wa Kiliberali ambazo  pamoja na mambo mengine ni ushoga na usagaji.  

Awali Mnadhimu wa Chama cha CUF, Rashidi wakati akiomba radhi aliipongeza Kamati ya Maadili na Chadema kwa kufikia muafaka kwa maslahi ya Taifa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“ Napenda kuomba radhi kwa watu wote walioumizwa na vurugu za jana,” amesema hivi punde Rashidi.

 Naye Kiongozi wa Kambi rasni ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe amesimama Bungeni hivi pinde na kuwaomba radhi CUF, Bunge na Spika kutokana na hotuba ya jana iliyosomwa bungeni jana na Wenje.

Awali kabla ya kuomba radhi leo, Freeman Mbowe jana kwenye kikao cha Kamati ya Maadili ya Bunge, alisema kwamba CUF wanafuata mrengo wa Kiliberali ambao msingi wa sera zao ni shoga na usagaji na kwamba hawakufanya kosa, pia alisema CUF alimdhalilisha Wenje (Chadema), CUF walichana hotuba yao na kuwaudhi na kuwakera Chadema.

Kutokana na hali hiyo CUF walishauriwa kuomba radhi jambo ambali wamelifanya leo asubuhi.

Wakati akisoma taarifa ya kamati hiyo  John Chiligati ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki amesema jana CUF walikiri kwenye kamati hiyo kwamba wao ni wanachama wa mrengo wa Kiliberali, lakini chama chao hakikubaliani na sera zote kama za ushoga na usagaji kwa kuwa serikali imeshatoa msimamo kwamba haiungi mkono masuala hayo.
Viewing all 20290 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>