Quantcast
Channel: MATUKIO NA VIJANA
Viewing all 20290 articles
Browse latest View live

ANGALIA PICHA NA VIDEO YA MGONJWA ANAYEISHI HOSPITALI KWA MIAKA 45 SASA

$
0
0

                                  Paulo Henrique

Paulo Henrique Machado, raia wa Brazil ameishi hospitalini kwa kipindi cha miaka 45 sasa kutokana na kupooza kulikosababishwa na ugonjwa wa polio alioupata baada ya kuzaliwa na mama yake kufariki.

Paulo na watoto wengine walipatwa na ugonjwa huo baada ya kutokea mlipuko nchini humo miaka ya 70, na tangu wakati huo, Paulo amekuwa akipumulia mashine saa 24 kwa siku, huku watoto wenzake wengi wakiaga dunia miaka michache baadaye. 


Pamoja na masaibu mengi aliyoyapitia, yote hayo hayajawa kikwazo cha kumzuia Paulo kutumia ubongo


na akili yake kwani ameweza kupata elimu na kubobea katika masuala ya utengenezaji vikaragosi/vibonzo kwa kutumia kompyuta (computer animator) na sasa ameanza kutengeneza tamthiliya kuhusu maisha yake inayotokana na kitabu kilichoandikwa na rafiki yake --ambaye pia ni mgonjwa, Eliana-- ambayo itaonekana kwenye runinga.



Anatamani sana angeweza kucheza soka kama watoto wengine, lakini kwa kujikubali kuwa haiwezekani, ameweza kutumia akili yake kuwaza (imagination) na kufurahia mchezo huo na mengineyo.

ANGALIA PICHA NYATI AZAA MTOTO ANAEFANANA NA BINADAMU.

$
0
0

Unbelievable+Human-like+Buffalo+BirthNchini Thailand, Nyati  amezaaa mtoto anayefanana sana na mwanadamu. 

Hizi ni picha ya nyati zikionyesha uso  na wa binadamu hasa yake ambayo ni sawa . Hata hivyo, mikono yake na miguu inafanana  zaidi na  nyati. Lakini kwa ujumla nyati anafanana sana na ng’ombe, Lakini sio kwa binadamu.


Kwa bahati mbaya kiumbe huyu alikufa muda mfupi baada ya kuzaliwa. 

Hli jambo limeleta gumzo na mtafarukiu mkubwa katiak kijiji hicho kuna imani kwamba tukio kama hilo linata baraka kwa watu wote wa sehemu tukio lilipotokea.

kutokana na imani hii watu wengi wameonekana wakiomba na kusali ili wapate baraka. uso wa kiumbe  huyu huwezi kutofautisha ni binadamu au ni nyati alisikika mwanakijiji mmoja.

ANGALIA PICHA YA MTU ALIYEIFADHI MAITI NDANI KWA MIAKA KUMI

$
0
0
A 62 year old retired vice-principal has been arrested by the Imo state police for allegedly killing his mother and hiding her corpse in his house since 2003.

Dr. Chimezie Osuigwe was arrested after the embalmed body of his mother was discovered hidden in a cupboard in his house yesterday Monday April 14th by another family member.

Police say the body of the woman, Lucy Osuigwe, who was declared missing in 2003, 'was found in a large cupboard inside a shrine in a private room in a circumstance depicting ritual practice.'

The police believe the retired educationist and devotee of the Guru Maharaji sect, killed his mother for ritual purposes. Dr. Chimezie Osuigwe is being held for first degree murder.

ANGALIA PICHA ZA MAITI ILYOFUKULIWA HUKO INDONESIA

$
0
0

Maiti ikipambwaDuna hii imejaa matukio mengi sana na ya ajabu,huko Indonesia kuna utamaduni ambao si wa kawaida na pengine ni wa ajabu wa kufufua maiti kaburini  na kisha kuwapamba upya na kuwavisha nguo za thamani wavalie kama walivyokuwa hai.
Wakazi hao wa Jimbo la Twaraj huko  Indonesia wanakusanyika na kumfanyia sherehe kubwa maiti kabla ya kuanza msafara wa kumtembeza katika mitaa na kumrejesha kaburini alipokuwa amezikwa, wakazi hao wanamini kwamba watu waliyokufa wanahaki ya kuendelea kuishi na kujumuika nao.

 Na ili   kufanikisha zoezi hilo la kihistoria ambalo wanaimani kwa lazima kufanya ili kuonesha hishima kwa maiti na kulinda mapenzi ya kweli kwa mtu aliyekufa, kabla ya kumzika maiti anavishwa kitambaa maalum ili kuzuia mwili wa marehemu kuoza.



Kweli dunia ina mambo

ANGALIA PICHA : SIMBA NA MAMBA WAZICHAPA KUGOMBEA MZOGA WA KIBOKO.

$
0
0
Lion fights crocs over hippo

Ni jambo la nadra sana kuona wanyama wanaosifika kwa kuwala wenzao mbugani kuonekana wakipambana, katika picha hizi zilizopigwa na mtaalam wa masuala ya teknolojia kutoka San Francisco nchini Marekani, Richard Chew aliyekuwa kwenye mapumziko na mke wake  kwenye mbuga ya Maasai Mara iliyopo Kenya aliweza kunasa tukio la mamba akipambana na Simba mwenye njaa wakigombea mzoga wa kiboko aliyekufa, nisikuchoshe ,
Lion fights crocs over hippo

Lion fights crocs over hippo
Lion fights crocs over hippo
Lion fights crocs over hippo
Lion fights crocs over hippo
Lion fights crocs over hippo
Lion fights crocs over hippo
Lion fights crocs over hippo
Lion fights crocs over hippo
Lion fights crocs over hippo
Lion fights crocs over hippo
NA LARRY BLOG

ANGALIA PICHA YA MWANAMKE ALIYEOA WANAUME WAWILI

$
0
0
MWANAMKE mkazi wa kijiji cha Ikandamoyo, wilayani Katavi, Veronica Saleh ‘Mama Kaela’ (50), amefanya uamuzi adimu wa kuolewa na wanaume wawili ambao anaishi nao kijijini hapo.

Kijiji hicho kipo umbali wa takribani kilometa 30 kutoka mjini hapa katika Jimbo la Katavi linalowakilishwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

Pamoja na ndoa hiyo iliyowezeshwa na mume mkubwa kukubali kuishi na mume mdogo, imeelezwa kuwa mwanamke huyo ndiye ‘aliyewaoa’ wanaume hao kwa zaidi ya miaka saba sasa, huku akiwa na amri kuu katika nyumba, kama ilivyo katika ndoa za kawaida.

Wanaume hao ni Paulo Sabuni ‘Baba Kaela’ (60) ambaye ndiye mume mkubwa na Arcado Mlele (45) ambaye ni mume mdogo.

Taarifa za kuwapo kwa ndoa hiyo ya aina yake, ziliifikia Globu ya Jamii na kufanyiwa uchunguzi kwa zaidi ya wiki tatu, na hatimaye katikati ya wiki hii, wahusika walikubali wao wenyewe kuzungumzia suala hilo. Kwa mujibu wa maelezo ya mwanamke huyo ambaye alionekana kuwa msemaji wa familia hiyo, yeye na mumewe mkubwa, walifika kijijini hapo miaka 24 iliyopita, wakitoka kijiji cha Usumbwa mpakani mwa Chunya, Mbeya na Tabora.

Wakiwa kijijini hapo mume wake aliendelea kufanya kazi ya ukulima wakati yeye mama (Veronica), pamoja na kilimo hujihusisha na upishi na uuzaji wa pombe ya kienyeji iitwayo kayoga.

Mwanamke huyo ambaye amesema ana watoto wanne, Alfred (20), binti mwenye miaka 16 (ambaye ameolewa) na wengine wawili wa kiume, mmoja akisoma darasa la sita na mdogo ana miaka saba, amesema hana shida na waume wake.

Ingawa wanandoa hao walizungumza kwa hadhari, majirani walikiri kuwa mwanamke huyo anaishi na wanaume hao wawili kwa amani na kwamba mwanamke huyo ndiye mwenye sauti na si waume zake.

“Si siri tena sasa, tumeshawazoea, kwani wanaishi kwa amani ila yule mume mdogo anaishi kwenye nyumba aliyoachiwa na marehemu baba yake, lakini anashinda kwa mume mkubwa, ambapo inajulikana kijijini hapa kuwa ni nyumba kubwa. “Basi pale ni mambo yote, kula na kunywa, mama huyu amewapangia zamu wanaume hao kama afanyavyo mume mwenye wake wengi. 

Ama kweli ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni,” alisema mkazi mmoja kwa masharti ya jina lake kutoandikwa gazetini. Ilielezwa, kwamba wanaume hao wana akili timamu na hawatumii kilevi cha pombe kama ilivyo kwa mke wao.

Hata hivyo, mume mkubwa anapewa sifa za upole tofauti na mume mdogo anayetajwa kuwa mkorofi kiasi cha mara kadhaa kumchapa makofi mkewe anapomuudhi.

Majirani wanadai kwamba Mama Kaela na mumewe Paulo, walipofika kijijini hapo, walipokewa na kuishi maisha ya kawaida, lakini baadaye mama huyo alianza kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Arcado, ambaye naye alilazimika kuachana na mkewe wa ndoa anayefahamika kijijini hapo kwa jina la Mama Pere.

Ilielezwa na mashuhuda hao kwamba mume mkubwa alipobaini uhusiano huo, alikuja juu, lakini mwanamke huyo inadaiwa alimweleza mumewe huyo, atake asitake lazima wataishi wawili, vinginevyo ataachana naye, ndipo mume mkubwa alipokubali kuishi na mume mwenza.

Katika maisha ya kawaida katika familia hiyo, inaelezwa kwamba katika baadhi ya siku ikitokea kuwa mama huyo amechoka kupika, mume mdogo huchukua jukumu la kupika na kumwandalia chakula na maji ya kuoga mume mkubwa.

“Lakini mara nyingi kwa mfano, ikiwa ni zamu ya mama huyo kulala kwa mumewe mkubwa, basi humfulia nguo zake kisha anakwenda kwa mumewe mdogo nako anamfulia nguo.

“Ndivyo wanavyoishi, nasi sasa tumewazoea ila yule mama ni mkali na ana sauti pale kwake kwa wanaume wale ila tunaona kama ana wivu sana kwa huyu mdogo ambaye naye pia ana wivu kwa mkewe huyo, labda anahofia kuwa mama huyo anaweza kuongeza mwanamume mwingine,” anasema mmoja wa majirani hao.

Hakuna mazuri yasiyokuwa na machungu, japo familia hiyo inaelezwa kuwa na amani, mtoto wao mdogo nusura avuruge uhusiano wa wanandoa hao, baada ya kuibuka mzozo wakati wa maandalizi ya ubatizo wake.

Kwa sababu anazojua mama, ingawa inafahamika kuwa wote ni watoto wa mume mkubwa, mke huyo katika hati za ubatizo aliandikisha ubini wa mtoto huyo kuwa ni Mlele (akimaanisha kuwa mtoto wa mume mdogo), lakini mume mkubwa aliweka pingamizi kanisani akidai yeye ndiye baba halali wa mtoto huyo.

Kwa mujibu wa mwanamke huyo, yeye na Arcado ni waumini wa madhehebu ya Katoliki wakati Paulo ni Mpentekoste. Madai ya mzozo wa uhalali wa `ubaba’ wa mtoto huyo, yalithibitishwa na baadhi ya wakazi wa kijiji hicho, akiwamo mwalimu wa dini wa Kigango cha Kanisa Katoliki Uruira, Mashaka Abel. Walisema miaka sita iliyopita, mtoto huyo akiwa na umri wa mwaka mmoja, alifanyiwa taratibu za ubatizo, lakini ilishindikana, kutokana na wanaume hao, kila mmoja kudai ndiye baba mzazi wa mtoto.

“Lilikuwa jambo la kustaajabisha sana, kwani familia hiyo ilifanya maandalizi yote ya sherehe ya ubatizo wa mtoto huyo, lakini siku hiyo kanisani wakati huo ilikuwa ni kigango cha Katumba ambacho sasa ni Uruira, sakata lilianzia pale Padri alipomwuliza mama wa mtoto huyo ubini wa mtoto naye akasema ni Mlele.

“Hapo ndipo mume mkubwa alipopinga na kudai kuwa mtoto yule si wa Arcado bali wake na yeye ndiye baba halali. Padri hakuamini, aliuliza tena na tena na majibu yakawa ni yale yale, ndipo ubatizo ukashindikana,” alisema Katekista Abel.

Kazi ya kutafuta undani wa ndoa hiyo haikuwa rahisi kutokana na mazingira ya woga na usiri uliokusudiwa kubaki, ambapo awali mama alisema kwamba mume wake ni Paulo pekee japo siku ambayo mwandishi wa habari hizi alifika kijijini hapo na baadaye nyumbani kwa wanandoa hao na kumkuta mume mdogo (Arcado akimsaidia mkewe kukoroga pombe. Awali katika utambulisho, walidai kuwa ni mtu na mdogo wake na kusita kuzungumzia maisha yao ya kifamilia.

Mke wao ambaye alionekana wazi kuwa ni msemaji mkuu alifoka na kuja juu, akidai kuwa hayuko tayari kuzungumzia uhusiano wake na wanaume hao wawili, ingawa alikiri kuwa wanaishi pamoja.

"Kwa hiyo umefunga safari yote hii kutoka huko ulikotoka ili uje kwangu mie Veronica … nasema sitaki kabisa mtu kuja hapa na kutaka kunivurugia mpangilio wa maisha yangu, kwanza nani alikueleza hayo, wambea wakubwa hao yanawahusu nini watu hao?” alihoji.
“Mie mume wangu ni huyu Paulo basi … sasa leo umeniachia vurugu ndani ya nyumba nitapigwa na huyo mume wangu Paulo, kwani mmenishikisha ugoni?” alifoka Mama Kaela. Hata hivyo, mume mkubwa alidai kuwa hatamwadhibu mkewe huyo na kwamba wataendelea kuishi pamoja na mdogo wake Arcado kwa amani. Hata hivyo, akina mama wengi kijijini hapo wanalaani kitendo cha mama huyo kuishi na wanaume wawili ambapo waliomba uongozi wa Kanisa uingilie kati, ili mama huyo aweze kufunga ndoa na mume mmoja.

Lakini kwa upande mwingine, baadhi walimpongeza mwanamke huyo wakidai kuwa kitendo hicho ni cha kijasiri kwa mwanamke, kumudu kuishi na wanaume wawili na kuwa na mamlaka juu yao.

ANGALIA PICHA ZA AJALI ZA NDEGE ZA KUTISHA

RAIS PUTIN AKAMILISHA MADAI YA TALAKA YA MKEWE

$
0
0

RAIS wa Urusi amekamilisha madai ya talaka kutoka kwa mkewe waliyeishi naye kwa miaka 30, Lyudmila Aleksandrovna Putina baada ya kutengana kwao, majira ya joto mwaka jana.

Wasifu wa Putin uliotolewa hivi karibuni unaonesha ana watoto wawili bila kutajwa kwa jina la mke wa rais (fisrt lady).
Msemaji wa Rais huyo, Dmitry Peskov amethibitisha kukamilika kwa talaka hiyo katika chombo cha habari kinachomilikiwa na serikali hiyo cha Itar-TASS.
Katika hali iliyowashtua wengi, Juni mwaka jana, Putin alitangaza kuachana na mkewe huyo baada ya kudumu katika ndoa yao kwa miaka 30.
“Ni makubaliano yetu sote,” Putin alisema wakati mkewe akisema kwamba ndoa yao imefika mwisho kwasababu “hatukutani tena katika tendo la ndoa” akiita talaka yao ni ya kiungwana.
Baada ya hapo Lyudmila Putina hakuonekana tena kwenye hadhara za kiserikali, huku watoto wake wawili nao wakiwa hawaonekani hadharani.
Maisha binafsi ya Putin (61) yamezua uvumi nchini humo, huku akihusishwa kuwa na mahusiano na mwanamichezo Alina Kabayeva.

Hata hivyo uvumi huo ulikanushwa na chombo cha habari kilichotoa taarifa hiyo kilifungiwa mwaka 2008.

ANGALIA PICHA NDEGE SITA ZILIZOWAHI KUPOTEA DUNIANI HIZI HAPA

$
0
0

1. Amelia Earhart - 1937

Rubani wa Kimarekani, Amelia Earhart alikuwa mwanamke wa kwanza kuvuka Bahari ya Atlantic kuchunguza dunia, alipotea na ndege yake miongo saba iliyopita. Inahisiwa kuwa ndege yake iliishiwa mafuta na kuanguka. 
2. Airbus A330 - 2009
  Mwaka 2009 ndege ya Shirika la Ndege la Ufaransa, Airbus A330 iliyokuwa na abiria 228 ikitoka Rio de Janeiro, Brazil kwenda Paris, ilipotea kwa siku tano. Ilipatikana ikiwa imeanguka na kuungua. Hadi sasa maiti za abiria 74 bado hazijatambulika.

3. Flying Tiger 739 - 1962
 Mwaka 1962 ndege ya kijeshi ya Marekani ilipotea ikiwa na watu 90 waliokuwa wanakwenda Ufilipino. Rubani wa ndege hiyo hakuwahi kutoa taarifa yoyote ya dharura na hadi sasa haijaonekana licha ya wataalamu 1,300 kushiriki kuitafuta.
4. South American Airways - 1947
 Ilichukua miaka 50 kupata fununu za ndege ya Amerika ya Kusini iliyopotea mwaka 1947 ikiwa na abiria 11 na kupatikana mwaka 1998 katika Milima ya Andes. Ndege hiyo ilifunikwa kwenye barafu ya milima hiyo.
5. Bermuda Triangle - 1948 na 1949
 Ulikuwa ni mfuatano wa matukio ya kupotea kwa ndege mbili katika eneo la baharini linaloitwa Pembetatu ya Shetani (Devil’s Triangle) katika maeneo ya Florida, Puerto Rico na Bermuda ambalo limekuwa na matukio mengi ya kupotea kwa ndege na meli kimiujiza. Katika matukio hayo mawili, ndege hizo zikiwa na jumla ya abiria 51 zilipotea na hata wanaanga 13 waliotumwa kuitafuta pia walipotea.
6. Uruguay 571- 1972
 Ndege ya Shirika la Ndege la Uruguay, 571, ilipotea mwaka 1972 ikielekea Santiago, Chile. Ndege hiyo ambayo ilikuwa na abiria 45, ilianguka milimani na watu 12 walikufa. Walionusurika walitafutwa kwa zaidi ya siku 72. Kabla ya kuokolewa, majeruhi hao walilazimika kula nyama za wenzao waliokufa ili kuishi.

ANGALIA PICHA ZA KUTISHA WATU WANAVYOJICHUKULIA SHERIA MKONONI

$
0
0
 KUMRADH kwa picha mbaya na za kutisha.Tunaungana na Jeshi la Polisi nchini kupinga unyama huu wanaofanyiwa binadamu wenzetu licha ya kwamba wanakuwa waharifu hii ni kosa kisheria.



WATANZANIA TAKRIBANI MILIONI 3.3 HUTUMIA HUDUMA ZA KIBENKI : GAVANA BENNO NDULU

$
0
0
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Profesar Benno Ndulu akikata utepe kuzindua kitabu cha ripoti ya utafiti Tanzania katika masuala ya uchumi uliofanyika leo Aprili 2, 2014 katika ukumbi wa Makao Makuu ya Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Profesar Benno Ndulu akikata utepe kuzindua kitabu cha ripoti ya utafiti Tanzania katika masuala ya uchumi uliofanyika leo Aprili 2, 2014 katika ukumbi wa Makao Makuu ya Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Profesar Benno Ndulu akiongoza wageni waalikwa kuonyesha kitabu cha utafiti mara baada ya kumaliza kuzindua.
Wageni waalikwa waliohudhuria katika mkutano huo wa kutangaza ripoti ya utafiti Tanzania katika masuala ya uchumi.
Wageni waalikwa waliohudhuria katika mkutano huo wa kutangaza ripoti ya utafiti Tanzania katika masuala ya uchumi.
Wageni waalikwa waliohudhuria katika mkutano huo wa kutangaza ripoti ya utafiti Tanzania katika masuala ya uchumi.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Profesar Benno Ndulu akizungumza katikamkutano na waandishi wa habari leo Aprili 2, 2014 katika ukumbi wa Makao Makuu ya Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam mara baada ya kumaliza kuzindua ripoti ya utafiti Tanzania katika masuala ya uchumi iliyotolewa na taasisi ya Financial Sector Deepening Trust (FSDT). Katikati ni Mkurugenzi wa Ufundi wa taasisi ya Financial Sector Deepening Trust (FSDT), Sosthenes Kewe na Mtakwimu Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Slyvia Meku.
Waandishi wa habari waliohudhuria katikamkutano na waandishi wa habari leo Aprili 2, 2014 katika ukumbi wa Makao Makuu ya Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam mara baada ya kumaliza kuzindua ripoti ya utafiti Tanzania katika masuala ya uchumi iliyotolewa na taasisi ya Financial Sector Deepening Trust (FSDT).
Mkurugenzi wa Ufundi wa taasisi ya Financial Sector Deepening Trust (FSDT), Sosthenes Kewe akikazia jambo.

Mtakwimu Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Slyvia Meku akieleza waandishi wa habari (hawapo pichani) jinsi utafiti huo ulivyofanyika na kupata matokeo. Mkutano huo ulifanyika leo Aprili 2, 2014 katika ukumbi wa Makao Makuu ya Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam. Katikati ni Mkurugenzi wa Ufundi wa taasisi ya Financial Sector Deepening Trust (FSDT), Sosthenes Kewe na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Profesar Benno Ndulu.
---
Benki Kuu ya Tanzania (BOT) imethibitisha kuwa watu takribani watu milioni 3.3 ni kwa kutumia huduma za kibenki, kulingana na matokeo ya FinScope 2013 utafiti uliofanywa na Financial Sector Deepening Trust (FSDT ).

Hayo yamesemwa na jijini Dar es Salaam na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Prof Benno Ndulu , wakati akitoa hotuba wakati wa uzinduzi wa utafiti wa ripoti ya FinScope Tanzania 2013; habari zilizomo katika utafiti huu thamani ni muhimu kwa ajili yetu maendeleo ya kiuchumi. Utafiti huu wa FinScope ni wa tatu tangu mwaka 2006.

Hata hivyo, alisema nusu ya Watanzania wote watu wazima - watu milioni 12 - sasa kutumia simu zao kwa kuondoa , kupokea na kuokoa fedha, au kulipa bili. Wanaume na wanawake katika maeneo ya mijini na vijijini katika nchi nzima na upatikanaji wa haraka kwa aina mbalimbali ya huduma za kifedha katika bonyeza ya kifungo chache .

 Alisema hii ni mapinduzi ya utulivu ambayo ni kuwa na madhara makubwa kwa mazingira ya fedha katika Tanzania . Mtandao wa simu operators kuendelea kufanya kazi na baadhi ya benki yetu ya kibiashara na kuendeleza bidhaa na huduma iliyoundwa na kukutana kutarajia kuongezeka kwa mahitaji katika muongo ujao.

Mkurugenzi wa Ufundi wa FSDT, Sosthene Kewe alisema zaidi ya nusu ya watu katika nchi kutumia huduma rasmi za kifedha, ikiwa ni pamoja na akiba na mikopo vikundi vidogo , maduka, ugavi mikopo na wakopeshaji fedha , ambayo bado ni mkubwa sana muhimu kwa nchi na mara nyingi pamoja na huduma nyingine.

" Ingawa hakuna miongoni mwao pia umewekwa au inasimamiwa na taasisi rasmi za fedha, akiba na mikopo ya vikundi inamilikiwa na kuendeshwa na watu ambao matumizi yao . Hii , kama vile bidhaa na huduma ambayo ni makini kulengwa kwa soko yao, inaweza kuelezea umaarufu wao "alisema.

Alisema matokeo ya utafiti inaonyesha kuna ongezeko la kuingizwa fedha na ufahamu juu ya huduma za benki za Mkono, ambapo zaidi ya watu 6.6m katika nchi kwa kutumia simu za kibenki.

WATALII MABILIONEA WA MAREKANI WAMALIZA ZIARA SERENGETI

$
0
0
8880ca0dedL
HIFADHI ZA TAIFA TANZANIA
logo-tanapaTAARIFA KWA UMMA
Watalii Mabilionea 42 kutoka Marekani wamemaliza  ziara yao ya utalii ya siku nne katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na kuelezea kufurahishwa kwao na uzuri wa hifadhi pamoja na maajabu ya wanyama mbalimbali wanaopatikana Serengeti ikiwemo msafara maarufu wa wanyama wahamao aina ya nyumbu.Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu alipata fursa ya kuwaaga watalii hao walipokuwa wakiondoka nchini kuendelea na ziara ya utalii katika nchi nyingine za Afrika wakitumia ndege binafsi aina ya Boeing BBJ 737 HB-11Q inayomilikiwa na Kampuni ya Utalii ya Abercrombie  & Kent ya nchini Marekani.Watalii hao walioingia nchini Machi 28, mwaka huu wakiongozwa na Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Kampuni ya Abercombie & Kent, Geoffrey Kent wameelekea katika nchi za Italia, Botswana, Malawi, Zambia, Uganda, Namibia, Ethiopia na Afrika Kusini ikiwa ni muendelezo wa ziara yao ya kitalii katika nchi za Afrika.Hili ni kundi la pili likifuatia ziara iliyofanywa na kundi jingine la mabilionea waliotembelea Serengeti mapema mwezi wa tatu mwaka huu kwa siku tatu na makundi yote yalifuatana na wanahabari kutoka kituo cha Televisheni cha Marekani cha CNBC ambao wamekuwa wakichukua picha na matukio mablimbali ya ziara hiyo kwa ajili ya kurusha katika kituo hicho kupitia kipindi chao maarufu kinachofahamika kama “Secret Lives of the Super Rich.”

Kipindi hiki hurushwa kupitia kituo hiki katika mataifa ya Marekani, Asia, Ulaya, Mashariki ya Mbali na Afrika.
Kwa upande wake Waziri Nyalandu alisema ujio wa watalii hao matajiri ni faraja kwa sekta ya utalii kwa kuwa itajenga imani kwa wenzao ambao hawajafika nchini kutembelea vivutio vya utalii.
Hivi sasa sekta ya utalii inachangia asilimia 17 ya Pato la Taifa na Marekani ndiyo nchi inayoongoza kwa kuleta watalii wengi nchini wanaofika kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo nchini. Waziri Nyalandu alibainisha kuwa malengo ya wizara yake ni kuhakikisha sekta hiyo inachangia asilimia 25 ya Pato la Taifa.
Nyalandu alisema Serikali inakusudia kuhamasisha utalii wa makundi kwa kutumia ndege binafsi na mabasi kulingana na uwezo wa watalii wenyewe.
Imetolewa na Idara ya Mawasiliano
Hifadhi za Taifa Tanzania
02.04.2014

Tangazo la nafasi za kazi kutoka Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma

$
0
0


Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo ambacho kimeundwa kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1). Kwa mujibu wa Sheria hiyo, chombo hiki, pamoja na kazi zingine kimepewa jukumu la kutangaza nafasi wazi za kazi zinazotokea katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Waajiri (Taasisi za Umma).
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma anakaribisha maombi kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 482 za kazi kwa waajiri mbalimbali
kama ifuatavyo:
MASHARTI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania.
ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.

iii. Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za
kazi kwa Waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
iv. Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe katika kichwa cha habari cha barua na juu ya bahasha, kutozingatiwa hili kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.
v. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)

watatu wa kuaminika.


vi. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka au kupotea.
    - Shahada ya juu/Shahada/Stashahada ya juu/Stashahada/Astashahada.
    - Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
    - Cheti cha Kompyuta
  - Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from  respective boards)
  - Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.

vii. “Transcripts”, “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.

viii. Waombaji wawe na umri usiozidi miaka 45.
ix. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
x. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
xi. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xii. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 15 Aprili, 2014

xiii. Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya Ajira HAURUHUSIWI.
xiv. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na NECTA).
xv. Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza na yatumwe kupitia posta kwa anuani ifuatayo;-
Katibu,
Sekretarieti ya Ajira katika
Utumishi wa Umma,
SLP.63100, 
Dar es Salaam. 

 ************************

ANGALIA NAFASI MPYA YA KAZI KUTOKA CRDB

SPIKA WA BUNGE LA A.MASHARIKI MASHAKANI

$
0
0

Vikao vya bunge la Afrika Mashariki
Mgogoro wa uongozi umezuka katika Bunge la Afrika Mashariki ambapo wabunge wa bunge hilo wanakusudia kumwondoa madarakani spika wa bunge hilo.
Tayari wabunge hao wameshakusanya saini 36 kutoka kwa wabunge 45 wa bunge hilo ambazo zinatakiwa kwa mujibu wa kanuni.
Wabunge hao wanamlaumu Spika huyo kwa kukiuka kanuni za bunge pamoja kushindwa kuwashirikisha wabunge kwenye baadhi ya uamuzi.
Akiongea na waandishi wa habari kiongozi wa wabunge hao kwa niaba ya wabunge wenzake wa bunge hilo Abudulla Ali Hassani Mwinyi, amesema wabunge hao wamefikia hatua hiyo ya kumwondoa spika huyo Margareth Zziwa kufuatia kukerwa na mwenendo wake.
Tayari wabunge hao wameshapeleka hoja ya kumwondoa spika huyo kwa Katibu wa Bunge hilo ikiwa na sahihi za wabunge 36 ili kutimiza matakwa ya utaratibu unaotakiwa kwa mujibu wa kanuni za bunge hilo ili kuanzisha hoja ya kumwondoa spika.
Je wabunge hao hawakuwa na njia nyingine kumaliza mgogoro huo hadi kufikia hatua ya kutaka kumwondoa spika huyo.
Mgogoro huu wa uongozi ndani ya bunge hilo umesababisha kuahirishwa kwa bunge hilo tangu jana kwa muda usiojulikana baada ya spika huyo kuamua kuliahirisha kwa muda usiojulikana.
Hii inafuatia malumbano yalijitokeza ndani bunge hilo ambapo mmoja wabunge alisema hoja hiyo isingeweza kujadiliwa.
BBC ilifanya juhudi za kuwasiliana na spika huyo Margareth Zziwa kwa simu yake ya mkononi ili kujibu tuhuma hizo hata hivyo alikataa kusema chochote ambapo alishauri apigiwe afisa habari wa bunge hilo ili atoe ufafanuzi.
Mgogoro huu wa uongozi ndani ya bunge hilo bado haijajulikana utamalizika lini lakini kwa vyovyote vile utakuwa umeathiri shughuli za Bunge hilo la Afrika Mashariki.Chanzo BBC Swahili

ANGALIA PICHA ADHABU ZA KIJESHI

$
0
0
Kwa haraka haraka hao ni wakosaji,walidharau amri za mahali fulani kwa bahati nzuri wakakutana na aliyetunga amri hizo,sasa wameambiwa wapige mbizi  ambaye hataonekana kabisa nikimaanisha atakayezamia kwa sekunde kumi atakuwa amepona.angalia hapo kila mtu ana style yake.




CHANGAMKIA NAFASI ZA SCHOLARSHIP

$
0
0

University of Bath Tanzanian Commonwealth Scholarships , 2014

15 full fee scholarships are available to Tanzanian nationals for study on either:
MSc International Construction Management or MSc Integrated Environmental Management
Eligibility – Candidates must meet all the following criteria:
• CSC Criteria: Must be Commonwealth citizens of a developing Commonwealth country, refugees or British protected persons AND be permanently resident in a developing Commonwealth country.

• Must be Tanzanian national AND able to attend 2 residentials in Dar Es Salaam, Tanzania.
• Provide evidence of a first degree from a recognised University or hold a professional qualification such as MCIOB, MRICS, RIBA, MIC• Meet the University's minimum requirement for non-native English speakers is IELTS 6.5 (with no less than 5.5 in each band) or PTE Academic 62 (both online tests). Applicants who have undertaken significant work experience or study, where English was the main language of communication, may be accepted if evidence is provided.

Your first residential will be held 1 -7 October 2014 in Dar Es Salaam, Tanzania and you must be available to attend for the full duration.

In order to apply you must submit an application to the University of Bath and also to the Commonwealth Scholarship Commission.  We are not able to consider any candidates unless both completed applications have been received by the deadline

Deadline: 30 May 2014.

ANGALIA PICHA ANACHOKIFANYA HUYU JAMAA NA MFALME WA PORI SIMBA NI HATARI TUPU.

$
0
0
He trusts lions enough to stick his arm in their mouth!





Kevin leverages his ability to help prevent these lions from being poached. As you can see from video below, these cats have a much gentler side as well.

ANGALIA PICHA ZA WEMA ALIVYOFANYA VURUGU OFISI ZA GLOBAL PUBLISHER

$
0
0

HOVYOOO! Wema Isaac Sepetu aliye pia Miss Tanzania 2006, amejitoa fahamu kwa kupandisha mzuka na kutinga makao makuu ya Kampuni ya Global Publishers, Bamaga-Mwenge, Dar na kuzua timbwili la aina yake kisa kikiwa ni kuandikwa kwa habari zake na mpenziwe, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
Tukio hilo la kumchoresha staa huyo mwenye vituko kila kukicha, lilijiri Jumatatu iliyopita kwenye ofisi za Global ambao ni wachapishaji wa gazeti hili (Amani), Uwazi, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Championi na Risasi majira ya mchana kweupe hivyo kufunga mtaa huku wapita njia wakimzodoa kwa maneno ya kejeli.


Wema akiwa ndani ya ofisi za Global na sura ya 'kuua mtu', mkononi akiwa na gazeti la Ijumaa Wikienda lenye stori: DIAMOND ATAMANI USHOGA. Kushoto ni mpambe na mfanyakazi wake Petit Man Wakuache.
ATINGA NA WAPAMBE DHAIFU

Akiwa na kundi la wapambe dhaifu na goigoi wakiongozwa na meneja wake, Martin Kadinda waliosimama nje ya ofisi hizo, Wema alifika kwa upole akionekana mkarimu kwa mlinzi ambapo aliomba kuonana na mwandishi nguli wa magazeti pendwa, Imelda Mtema.

 Mlinzi alimruhusu kwa vile Global ni mjengo wa mastaa na watu wasio mastaa, huwa hawakauki kuingia na kutoka kwa mambo mbalimbali.
 Wema alipofika mapokezi, pia aliomba kuonana na mwandishi huyo lakini tofauti na utaratibu ambapo huwa mgeni akifika huulizwa kama ana ‘apointimenti’ ili aitiwe anayemhitaji, Wema alipitiliza kwa nguvu hadi chumba cha habari akifuatana na kijana aliyekuwa akimrekodi.

Wema akiwa ndani ya News Room akimtafuta mwandishi wa Global Imelda Mtema, huku akisema yeye ni chizi!

 Akiwa ndani ya chumba cha habari, Wema aliuliza kwa sauti ya juu na ya kujiamini: “Imelda yupo wapi? Nauliza Imelda yupo wapi?”
WEMA NA IMELDA
Katika kumtafuta Imelda kwa macho kwa sababu chumba cha habari ni kikubwa huku akionywa na wahariri kwamba atulize mzuka kisha aeleze shida yake, Wema alimuona Imelda akitoa maelezo kwa Mhariri Kiongozi wa Magazeti Pendwa ya Global, Oscar Ndauka kuhusu habari aliyokuwa ameifuatilia.
 Cha kushangaza, Wema alimfuata Imelda mpaka kwenye meza ya mhariri huyo kisha kuanza kufoka kwa sauti ya juu.
 MSIKIENI WENYEWE
“Kwa nini mnafuatilia maisha yangu? Kila siku mnaniandika na Diamond. Kwa nini Imelda unaniandika kuwa mimi msagaji?”

"Mimi ni chizi, nakwambieni mimi ni chizi zaidi ya machizi wote"....Wema alikuwa akifoka mwanamke!
ATULIZWA, AGOMA

Katika kuhoji huko, mhariri kiongozi alijaribu kumtuliza Wema ambaye alikuwa kama amewehuka: ”‘Wema tuelewane, eleza shida yako kwa utaratibu kwani hakuna ofisi isiyokuwa na utaratibu.”

 Pamoja na kuambiwa hivyo bado Wema aliyekuwa ameshika Gazeti la Ijumaa Wikienda toleo la Jumatatu iliyopita, aliendelea kumng’ang’ania Imelda ambaye alikuwa akijaribu kumtuliza:
 “Wema twende tukakae pale kwenye meza ya mkutano uwaeleze viongozi wangu tatizo lako. Hiyo stori kuwa wewe ni msagaji mbona haipo, ni gazeti gani?”

"Mimi ni chizi, msinitanie ohhh!!
Licha ya kupewa mwongozo huo, Wema aliendelea kufoka:

“Hivi mnajua mimi ni chizi? Kwa taarifa yenu mimi ni chizi zaidi ya machizi wote, ohooo!”

MLINZI ATONYWA, ATIA TIMU
Baada ya hali kuwa tete, mlinzi wa geti kuu alipigiwa simu ya mezani na kujulishwa juu ya Wema kusababisha kazi kusimama ambapo alifika haraka tayari kwa kumtoa nje kwa hiyari yake au lazima.
Ndipo kukatokea timbwili kubwa, wapambe wake ‘goigoi’ nao waliingia wakitaka kufanya vurugu ili kumteka mwandishi huyo lakini kikosi imara cha Global kikiongozwa na Mhariri Kiongozi wa Magazeti ya Championi, Saleh Ally kilijiimarisha na kutuliza fujo hizo huku kikiwa makini kuhakikisha Wema na timu yake hawajeruhiwi hata kidogo.
WEMA ATUMIA GAZETI KAMA SILAHA

Katika purukushani hiyo, Wema alionesha udhaifu wa kumudu varangati pale alipotumia gazeti aliloshika kumpiga nalo mwandishi Imelda, jambo lililodhibitiwa kama Waasi wa M23 wa Kongo walivyodhibitiwa na Majeshi ya Umoja wa Mataifa, akatolewa nje.

Wema akiwa nje ya ofisi sasa baada ya kutolewa kwa nguvu, yeye pamoja na wapambe wake
MBALI NA WEMA

Ukiachia mbali Wema kutulizwa kwa kutolewa nje kwa nguvu, vijana wake walegevu nao waliwekwa chini ya himaya ya Global kwa kunyang’anywa  kamera ya video iliyokuwa ikitumika kuchukua matukio huku nao wakipigwa picha za kutosha na wapiga picha wetu.
VITA KUBWA, WEMA AVUA VIATU

Nje ya ofisi, ‘vita’ kubwa kati ya Wema na walinzi wa Global (alifika mwingine kutoka lindo la mbali) ilizuka ambapo staa huyo alivua vile viatu vyake virefu vya rangi ya bluu bahari na kuanza kumpiga navyo mmoja wa walinzi hao akiamini anamkomesha lakini pia akadhibitiwa!

Wema akiwa ameshika viatu vyake vya mchuchumio mkononi baada ya kutolewa nje ya ofisi na wapambe wake akiwemo meneja wake, Martin Kadinda (kulia).

 Wema akiwa anarandaranda kwenye geti kuu akiwa peku, alidondosha matusi ya nguoni ambayo hayaandikiki gazetini kwa namna yalivyokuwa makali. Ilikuwa si rahisi kuamini kuwa yeye ni kioo cha jamii.
 Timbwili la Wema na wapambe wake akiwemo Petit Man, ambao hawakufua dafu kwa walinzi na vijana wa Global nje ya ofisi hizo, lilichukua zaidi ya nusu saa huku likikusanya kadamnasi na kusababisha mtaa kujifunga wenyewe.

Wema akiwa kafura ka' faru aliyekoswa koswa kung'olewa kipusa na majangili, kulia ni mpambe na mfanyakazi wake Petit Man Wakuache.
POLISI HAO

Hata hivyo, uongozi wa Global uliwasiliana na Polisi wa Kituo cha Kijitonyama ‘Mabatini’, Dar ambao walifika na kumkuta Wema na timu yake wakiwa wamepoa mlangoni, wakaambiwa timbwili limetulia hivyo wakatimua zao.

'Baby' wa Diamond Platnumz alikuwa hashikiki viatu viligeuka kuwa 'mzigo mzito' akivibagwa chini huku akitoa mkwara akiwa pekupeku na kufunga mta
a.

Ilibidi askari polisi waitwe kuja kuhakikisha utulivu unakuwepo huku wapita njia wakiwa hawaamini macho yao kuwa wanayemuona mbele yao 'peku peku' akimwaga mitusi ni Miss Tanzania, Wema Isaac Sepetu!

APEWA KAMERA, KADI NOOOO!
Baadaye Wema aliomba kupewa kamera yake ambapo zoezi hilo lilifanyika lakini ‘memori kadi’ yenye picha walizoanza kurekodi, ilitolewa ili kupisha maridhiano kwanza. Waliambiwa kadi hiyo ilitolewa kwa sababu walirekodi bila idhini au kibali cha Kampuni ya Global.

Miongoni mwa watu waliokuwa kwenye msafara wa Wema ni pamoja na Ammy Nando (kushoto), mshiriki wa Big Brother Africa 'The Chase' ya mwaka jana ambaye alikuwa akificha sura kukwepa kamera za Global.
WEMA AGOMA KUONDOKA

Baada ya kugundua kadi ya kamera ipo chini ya ulinzi wa Global, Wema alitaka kulianzisha tena akidai hawezi kuondoka hadi apewe kadi hiyo lakini uongozi uliweka ngumu. Baadaye aliondoka kimyakimya. Wakati huo wapambe wake walishaondoka kitambo.

WEMA: CHIZI in action......

 Hadi gazeti hili linakwenda mitamboni, kadi ya kamera hiyo bado ilikuwa inashikiliwa na uongozi wa Global ili kumthibitishia Wema kuwa hawezi kufanya umafia wowote dhidi ya waandishi wa kampuni hiyo yenye nguvu kihabari nchini Tanzania.

ANGALIA VIDEO ZIKIONYESHA JINSI BIASHARA ZNAVYOFANYIKA NYAKATI ZA USIKU:

Viewing all 20290 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>