![]() Jackson Makini ‘Prezzo’. Na Lucy Mgina MMOJA lazima akae! Julai 7, mwaka huu katika Uwanja wa Taifa kutakuwa na mpambano mkali wa stejini kati ya wasanii, Nassib Abdul ‘Diamond’ na Mkenya, Jackson Makini ‘Prezzo’. |
![]() | Nassib Abdul ‘Diamond’. Diamond ambaye ni mshindi wa Tuzo ya Msanii Bora wa Kiume ya Kilimanjaro Music Awards, anayetamba na ngoma kibao kama Nataka Kulewa na Kesho, ataiwakilisha Bongo Fleva kwa kupiga shoo kali. Mkali kutoka Kenya, Prezzo anayetamba na wimbo wa For Sho Fo Shizzle na juzikati katoa ngoma nyingine inayoitwa Celebration of Life, naye atawakonga nyoyo mashabiki watakaoamua nani mkali kati yake na Diamond. Mratibu wa Tamasha la Matumaini, Abdallah Mrisho ‘Abby Cool’, alisema Prezzo na Diamond watashusha shoo kali, huku kukiwa na mpambano wa nani mkali wa kutawala jukwaa kati yao. Alisema kila mmoja ameshaanza tambo lakini mashabiki ndiyo watakaoamua siku hiyo ili kuondoa ubishi. Alisema wasanii wengine watakaotoa burudani siku hiyo ni TMK Wanaume Family, TMK Wanaume Halisi, bendi za Msondo Ngoma, Sikinde na Jahazi. “Niwaambie mashabiki waje kwa wingi ili wasipitwe na burudani hii, tutataka watuambie nani kamfunika mwenzake na ili kuondoa utata, wanatakiwa kushuhudia kuanzia mwanzo wa shoo hadi mwisho. “Prezzo yeye anachana na Diamond anaimba Bongo Fleva, tutaona ladha ipi ni tamu na inayopagawisha mashabiki, lakini pia tutakuwa na burudani nyingine kabambe kutoka kwa wasanii wengine kama TMK Halisi na Wanaume Family, bendi za Msondo, Sikinde na Jahazi (ikiongozwa na Mzee Yusuf) zitakuwepo pia,” alisema Abby Cool
|
|