Quantcast
Channel: MATUKIO NA VIJANA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 20290

Wayne Rooney kubakia Man Utd

$
0
0

Karibu kwenye bodi: David Moyes amefanya Mkutano wake wa kwanza na Waandishi wa Habari kama kocha wa Manchester United 


KOCHA David Moyes amesema kwamba Wayne Rooney hatauzwa na Manchester United na hili ni sawa na pigo lingine kwa Arsenal, ambayo ilikuwa inamtaka mchezaji huyo.
Kocha huyo mpya wa Old Trafford amekutana na Waandishi wa Habari leo kwa mara ya kwanza tangu athibitishwe kuwa mrithi wa Sir Alex Ferguson, kiasi cha miezi miwili iliyopita na akakutana na maswali kibao kuhusu mustakabali wa mshambuliaji huyo wa England.

Moyes amethibitisha kwamba Rooney – ambaye inafahamika alimuambia Ferguson anataka kuondoka– amebadilisha mawazo yake na amesema atabaki klabuni hapoWayne hauzwi," amesema. "Ni mchezaji wa Manchester United na atabakia kuwa mchezaji wa Manchester United,".

"Tumezungumza mara kadhaa. Vyovyo ilivyotokea kabla, na Wayne tunafanya kazi pamoja sasa. Nimeona nuru katika macho yake, anaonekana mwenye furaha na kama anayekwenda kukita chini. Nasonga mbele kufanya naye kaziI na hatauzwa.

"Kulikuwa kuna kikao cha faragha baina ya Wayne na Sir Alex. Nasona sasa. Sijui kilichozungumzwa katika kikao chao cha faragha. Kama ninavyosema, nasonga mbele katika kumuweka Wayne Rooney katika kiwango sahihi,"alisema.


Sakata la Rooney linaonekana kufikia tamati baada ya Moyes kusema mshambuliaji huyo hatauzwa
 


Moyes akiwa ofisi mpya, Old Trafford anaonekana mwenye furaha

Viewing all articles
Browse latest Browse all 20290

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>