Askofu wa Jimbo la Njombe Alfred Maluma akieleza malengo ya Kuusaidia Mkoa wa Njombe.
Mama Tunu Pinda naye apongeza Jitihada za Wakazi wa Wilaya ya Wanging'ombe.
Mratibu wa Ujenzi wa Chuo cha Kilimo na Mifugo wilaya ya Wanging'ombe Padre Evodius Msigwa akisoma Taarifa ya Chuo Hicho kwa Waziri Mkuu.
Mbunge wa Jimbo la Njombe Magharibi ambaye Pia ni Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Gerson
Lwenge
Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe Bi.Esterina Kilasi akisoma taarifa ya Wilaya Hiyo kwa Waziri Mkuu Akiwa Katika Kijiji cha Ilembula.
Waziri Mkuu Pinda akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe Leo wakati wa Ziara yake ya Wiki Moja Mkoani Njombe.
Waziri Mkuu akiweka Jiwe la Msingi Katika Ujenzi wa Bweni la Wasichana katika Shule ya Sekondari ya Igwachanya
Chief wa Kabila la Wabena ambao ndio Wataalamu wa Kimila Mdandu na Msitu wa Nyumbanitu Mzee Mbeyela.
Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Kilimo Mkoa wa Njombe NADO Bwana John Wihallah Akisoma taarifa ya Shirika Hilo Kwa Waziri Mkuu wakati alipotembelea na kukagua maonesho ya Wajasiliamali Igwachanya.
Mbunge wa Viti Maalumu wa Vijana Bi.Msigwa
Hii Ni Bendera ya Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe
Na Gabriel Kilamlya Wanging'ombe.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda Amewataka Wakuu wa Wilaya na
Wakurugenzi wa Halmashauri Mkoani Njombe Kutafuta Namna ya
Kupunguza Tatizo la Maji Linaloonekana Kuwa Sugu Mkoani Hapa.
Aidha Waziri Mkuu Amewataka Viongozi Hao Kutafuta Wafadhili
Mbalimbali Watakaosaidia Kujenga Miradi Mbalimbali ya Maji Kama Vile
ya Visima Ambayo Inaweza Kuanza Katika Hatua za Muda Mfupi za
Kupunguza Tatizo Hilo.
Akizungumza Wakati wa Kuweka Jiwe la Msingi Katika Chuo Cha Kilimo
na Mifugo Mayale Ikiwa ni Siku Yake ya Kwanza ya Ziara ya Wiki Moja
Mkoani Njombe,Waziri Mkuu Mizengo Pinda Amesema Bila Maji ya
Uhakika ni Vigumu Kupata Maendeleo ya Kilimo.
Aidha Amewataka Maafisa Ugani Kuhakikisha Wanawafikia Wakulima na
Wafugaji Mashambani Badala ya Kuendelea Kukaa Ofisini Kwa Kisingizio
Cha Ukosefu wa Usafiri.
Sanjali na Hayo lakini Pia Ameagiza Mkurugenzi Pamoja na Mkuu wa
Wilaya ya Wanging'ombe Kuhamia Igwachanya Mwishoni Mwishoni mwa
Mwezi Huu.
Awali Akisoma Taarifa ya Chuo Hicho Mratibu wa Chuo Hicho Mchungaji
Evodeus Msigwa Amesema Chuo Hicho Kinajengwa Chini ya Ufadhili wa
Nchi ya Italy na Lengo Hasa ni Kwaajili ya Kuwasaidia Watu Wenye
Ulemavu na Vijana.
Ziara ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda Imeanza Leo Mkoani Njombe na
Kutarajiwa Kudumu Kwa Wiki Moja Huku Akitarajiwa Kutembelea Maeneo
Mbalimbali Mkoani Hapa