KAIMU MKURUGENZI MTENDAJI WA TANESCO eNG. FELCHESMI MRAMBA AKIFAFANUA JAMBO KUHUSU UHAKIKA WA UMEME KATIKA JIJI LA DARESALAAM |
Shirika la TANESCO limelihakikishia shirikisho la viwanda na wafanyabiashara CTI kuwapatia umeme wa uhakika na kwamba kwa kuanzia wameanzisha idara itakayoshughulika na wanachama wa shilikisho hilo moja kwa moja kutatua kero zao zinazowakabili
Akizungumza katika mkutano maalum uliowashirikisha wanachama wa shirikisho hilo la CTI na uongozi wa kampuni ya Tanesco mapema hii leo, Mkurugenzi mtendaji wa Tanesco Eng Felchesmi Mramba amesema hatua ya kuwa na kitengo cha huduma kwa wateja wanaotumia kwa kiasi kikubwa umeme wa Tanesco umefikiwa ili kuweza kuwa karibu na watumiaji hao na wao pia kuweza kutoa kero zao kwa muda muafaka na kupatiwa ufumbuzi wa harakaEng Mramba ameendelea kusema kuwa kwa sasa wamiliki wa viwanda, na wafanyabiashara wakubwa wamekuwa wakitumia takribani asilimia 60 ya umeme wote unaodhalishwa na Tanesco hivyo ili kuweza kuwajali na kusikia kero zao kwa karibu tumeamua kuweka kitengo hicho ambacho tunaamini kitasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza kero ambazo walikuwa wanakumbana nazo
“Tunaamini kwa ushirikiano tutakaouonyesha utaweza kuwawezesha wamiliki wa viwanda na wafanyabiashara wakubwa kuongeza uzalishaji wao kwa kiasi kikubwa na hivyo kuweza kuinua uchumi wa taifa letu” aliongeza Eng Mramab
Eng. MRAMBA AKIFUATILIA MOJA YA MAWASILISHO YA MIRADI MBALIMBALI INAFANYIWA KAZI NA KAMPUNI YAKE,WADAU WA CTI WALIPATA FULSA YA KUSIKILIZA MIRADI HIYO NA KUTEMBELEA BAADHI YA JIJI LA DARESALAAM |
Aidha katika hatua nyingine Eng Mramba amebainisha miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa na ile ambayo bado haijaanza rasmi kutekelezwa hiyo ikiwa ni jitihada za kuwahakikishia wanachama hao wa CTI kuona ni jinsi gain Kampuni imejipanga kuwepo kwa umeme wa kuaminika hapa nchini na kuwapa wanachama hao fulsa ya kujipanga namna gain wanaweza kuongeza uzarishaji wa bidhaa zao,
Miongoni mwa miradi iliyowasilishwa kwa wamiliki hao wa viwanda ni pamoja na ile miradi ya kujenga vituo vyenye megawati kubwa ya pale Ubungo,Kurasini Gongo la mboto na Kinyerezi ambapo ikimalizika hakutakuwa na tatizo la umeme kabisa katika jiji la Daresalaam
MWENYEKITI WA SHIRIKISHO LA VIWANDA NA BIASHARA CTI AKIFAFANUA JAMBO KWA WANACHAMA WA CHAMA HICHO MAPEMA HII LEO KATIKA OFISI ZA TANESCO |
Naye kwa upande wake Mwenyekiti wa shirikisho la viwanda na wafanyabiashara CTI BW. Felex Mosha amepongeza hatua zilizochukuliwa na uongozi wa Tanesco kwa kuandaa idara itakayoshughulika moja kwa moja na wanachama wake kwani hatua hiyo inategemewa kuongeza tija kwa wafanyabishara na wamiliki wa viwanda kwa kupatiwa umeme wa uhakika
MMOJA WA WANACHAMA WA CTI AKIFAFANUA JAMBO MBELE YA MKURUGENZI WA TANESCO MAPEMA HII LEO |
Aidha Bw. Mosha amepongezajuhudi za kuwaleta pamoja wadau wa umeme na kukaa meza moja kuzungumzia pamoja kero za umeme katika viwanda vyetu na kwamba kuanzia sasa sisi kama wamiliki wa viwanda tutakuwa katika nafasi nzuri ya kujua kinachoendelea katika suala zima la umeme na kuwataka viongozi hao wasiishie kuwaita tu katika mikutano na badala yake watoe taarifa za umeme kwa haraka zaidi ili waweze kuchukua tahadhari mapema
“Tunawomba nyinyi kama tanesco kutupatia taarifa ya katizo la umeme mapema iwezekanavyo ili tuweze kujiandaa, na tunaamini kwa sababu ninyi ni sura mpya basi hata matendo yenu yatakuwa mapya na ndio maana hata leo tumeanza ushirikiano mpya na nynyi” aliongeza Bw Mosha
HAPA WADAU WA CTI WAKIONYESHA MOJA YA VITUO VYA KISASA CHA UBUNGO AMBACHO KITASAIDIA KUPUNGUZA TATIZO LA UMEME HAPA JIJINI, KINADHALISHA JUMLA YA KW 180 |
CTI WAKIWA WANAANGALIA MITAMBO YA KUZALISHA UMEME WA UHAKIKA |
Wamiliki hao pia wamepata fulsa ya kujionea miradi mbalimbali inayoendelea katika jiji la Daresalaam
mwishooo
mwishooo