Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Siprian Kiwango,mwenye umri kati 60-70 mkazi wa Shimbi amefariki dunia papo hapo baada ya pikipiki aliyokua akiendesha kugongana na gari ndogo.
Duru za Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanajaro zinaeleza kuwa, ajali hiyo ilitokea Julai 24 majira ya saa nane mchana ikihusisha gari aina ya suzuki lenye namba za usajili T 771 CKE na pikipiki yenye namba T 659 AVX.
Mashuhuda wa ajali hiyo wamesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa gari, pia wamesema kuwa dereva wa gari alikua mlevi na hivyo kushindwa kumudu gari hali iliyomfanya kukosa uelekeo na kusababisha ajali. na jaizmelaleo