

Na Kibada Kkibada -Katavi
Wadau wa maendeleo wa mikoa ya kanda ya ziwa Tanganyika wamelitupia lawama shirika la viwango nchini TBS kwa kuonesha udhaifu katika kuhibiti uingizaji holela wa bidha bandia kutoka nje ya nchi na badala yake kuanza kuwaharibia bidha wananchi ambao wanakuwa wamenunua kwenye maduka hayo hayo ambayo yako kisheria hali inayotia wasiwasi kwa watendaji wa mamlaka hiyo.
Akiongea kwenye mdahalo huo mmoja wa wajumbe alieleza kusikitishwa na utendaji kazi wa mamlaka hiy alieleza kuwa mfano mfanyabiashara ananunua tv zake kumi kutoka kariakoo anazipeleka mikoani wanakuja kumvunjia television hizo inaonekana kuwa mamlaka hiyo utendaji kazi wake hauko makini.
Alieleza kuwa udhibiti mdogo kwa watu waliopewa dhamana bado ni changamoto kubwa kwa watumishi wa mamlaka hii.
wajumbe walishauri uingizaji wa bidhaa kutoka nje ambazo siyo bora na usambazaji udhibitiwe.nakuomba uaminifu wa wafanyabiashara na wale waliopewa mamlaka ya kushughulika na masuala ya udhibiti wa viwango. wakasisitiza sheria itumike vizuri na ipewe nguvu za kutoa adhabu kali ya (kunyongwa) na ianzishwa mahakama maalum iwepo.