Quantcast
Channel: MATUKIO NA VIJANA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 20290

Adaiwa kubaka kuku wawili na kisha kujiua

$
0
0
WAKAZI wa kijiji cha Rukuma katika eneo bunge la Lari jana walifurika nyumbani kwa mvulana mmoja wa umri wa miaka 17 aliyedaiwa kuwanajisi kuku wawili wa nyanyake kabla ya kuwaua na baadaye kujiua kwa kukunywa sumu.
Wakazi walioshtushwa na kisa hicho walidai mvulana huyo alijiua kwa kunywa sumu kwani kulipatikana chupa ambayo haikuwa na kitu ndani kwenye sakafu ya nyumba yake.
Kulingana na Paul Njenga, kijana huyo alipatikana akiwa amelala kitandani akiwa amefariki huku mizoga ya kuku hao ikiwa kwenye sakafu, suala lililopelekea wakazi kushuku aliwanajisi kwa zamu.
Watoto waliokaribia nyumba hiyo ya chumba kimoja cha mvulana huyo, walifukuzwa na wakazi ili waache kuchungulia maiti ya mvulana huyo na mizoga ya kuku hao.
Bw Njenga alisema waliwaita maafisa wa polisi wa kituo cha Lari waliowasili baada ya muda mfupi na wakaanza uchunguzi wao.


“Mvulana huyu aliwakamata kuku hao wa nyanyake na kuwafungia katika nyumba yake ambako amekuwa akiwachafua. Aliposikia wanatafutwa, aliwaua na akanywa sumu na akafariki,” alisema Bw Njenga. 

Kamanda wa polisi wa eneo hilo Bw Joshua Opiyo hata hivyo alipuuzilia mbali madai kwamba mvulana huyo aliyemtaja kama Samuel Muranja aliwachafuakuku hao kabla ya kufariki.

Bw Opiyo alisema mvulana huyo ambaye alikuwa mwanafunzi wa shule ya upili ya Kirenga alikuwa amekataa shule kwa muda wa miezi miwili kwa sababu ambazo hazikuelezwa na familia.

Alisema aliondoka nyumbani mnamo Agosti 6 na alipatikana Alhamisi asubuhi akiwa katika nyumba yake iliyo kando ya nyanya yake ambaye huwa wanaishi naye akiwa amefariki.

Uchunguzi

Hata hivyo, licha ya Bw Opiyo kupuuzilia mbali habari hizo, alisema mwili wa mvulana huyo ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha City jijini Nairobi, ambako uchunguzi wa kilichotendeka utafanyiwa ili ripoti itakayotolewa ibaini iwapo aliwachafua kuku hao au la ni nini hasa kilichopelekea kifo chake.

Kadhalika, kamanda huyo alisema nayo mizoga ya kuku hao wawili itapelekwa katika maabara ya taasisi ya Kabete Veterinary ambako itachunguzwa iwapo walichafuliwa au la na kilichopelekea vifo vyao.

“Hili ni suala la uchunguzi, hakuna mtu anayehojiwa, walalamishi wamefariki na iwapo wangekuwa hai hawangeweza kuongea. Kijana alipelekwa katika ufuo wa City, Nairobi ambako daktari wa upasuaji ataukagua na atoe ripoti yake itakayoeleza kila kitu. Pia, chupa ambayo iliokotwa katika nyumba yake itakaguliwa pia huko,” alisema OCPD huyo.

Bw Opiyo aliongeza: “Nayo mizoga ya kuku hao, itapelekwa katika Kabete Veterinary ili ikaguliwe ijulikane iwapo walichafuliwa au la na vifo vyao vilitokana na nini.”

Viewing all articles
Browse latest Browse all 20290

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>