Quantcast
Channel: MATUKIO NA VIJANA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 20290

Kaunti za Kenya kuwaondoa wafanyakazi hewa zaidi ya 10,000

$
0
0
Mamia ya wauguzi kutoka hospitali za umma na kliniki za afya waliandamana jijini Nairobi tarehe 9 Machj, 2012, katika kudai malipo mazuri siku moja baada ya serikali ya Kenya kuwafukuza watu 25,000 wanaoshiriki katika migomo. 
Ukaguzi unaoendelea wa kaunti 47 za Kenya umeonyesha kwamba serikali ya kitaifa inalipa mishahara kwa maelfu ya wafanyakazi ambao walishafukuzwa, ambao kwa sasa hawatimizi majukumu yao, na katika baadhi ya matukio, ambao walishafariki dunia miaka mingi iliyopita.
Kutoka Julai, kaunti za Kenya zimekuwa zikifanya uhesabuji mkuu wa wafanyakazi kuwaondoa "wafanyakazi hewa" hawa, kuondoa mishahara yao na kuboresha utoaji wa huduma, alisema mwenyekiti wa magavana wa Wilaya Isaac Ruto.
"Tulikuwa tunajua kwa muda mrefu kwamba serikali imekuwa ikilipa wafanyakazi hewa, lakini kinachoshtua ni kwamba mwezi mmoja tangu [tangu] zoezi hili lianze, wafanyakazi hewa zaidi ya 10,000 wamebainishwa," aliiambia Sabahi.

Ukaguzi huu umekuja wakati mfumo wa serikali ya Kenya imegatuliwa kutoka iliyokuwa muundo wa majimbo kwa kutoa madaraka zaidi kwa kaunti mpya.

"Tunatarajia serikali ya kitaifa kuhamisha kazi zote za msingi, ikiwa ni pamoja na malipo ya mishahara ya wafanyakazi, kwenda kwenye kaunti ifikapo Januari mwaka ujao. Ukaguzi wa wafanyakazi ni kuhakikisha kwamba kaunti zinaendelea na kazi hii zikiwa na rejesta safi ya malipo" alisema Ruto, ambaye pia ni gavana wa kaunti ya Bomet County.

Hadi sasa, ukaguzi umeonyesha kwamba zilizokuwa halmashauri za majimbo na manispaa, pamoja na taasisi za afya zinazoendeshwa na serikali, zilikuwa zimejaa wafanyakazi hewa, alisema.


"Tunawalenga wafanyakazi ambao wameonekana tu mwishoni mwa mwezi kuchukua mishahara. Wafanyakazi hewa ndio wanaongoza maandamano dhidi ya serikali pale panapokuwa na kuchelewa kidogo kwa mishahara, lakini wakati wote hawako kwenye vituo vyao vya kazi walivyopangiwa," Ruto alisema, akiongezea kwamba ugatuzi huo ungehakikisha kwamba kaunti za Kenya zinaachana na vitendo vya ajira za rushwa viilivyokuwepo siku zilizopita.

Kwa kuongezea kuwatafuta wafanyakazi hewa, ukaguzi unakagua vyeti vya masomo vya wafanyakazi wa kaunti ili kuhakikisha wana sifa kwa kazi zao. Kila bodi ya utumishi wa umma ya kaunti itaamua hatua itakayofuata kwa wale walioajiriwa bila ya sifa zinazofaa, Ruto alisema.

Baadhi ya wafanyakazi ambao hawana sifa kwa kazi maalumu waliajiriwa kupitia rushwa au urafiki, alisema.

"Tunaelewa kwamba kulikuwa na njama katika kuwaajiri watu kwa kubadilishana na utoaji rushwa, lakini baada ya zoezi hilo tutaanzisha uchunguzi na kuwashtaki wakosaji," Ruto alisema.

Ukaguzi hautawatambua wafanyakazi wa kaunti ambao wamechukua likizo za masomo au ambao wamepangiwa kazi maeneo mengine kama wafanyakazi hewa, Ruto alisema.

Zaidi ya hayo, ukaguzi utasaidia kubainisha taasisi ambazo huduma zake zinahitaji kuboreshwa kwa kuwa wanaojifunza na wenye ufanisi zaidi, kwa sababu wasiofaa au watu wasiokuwepo katika orodha ya malipo ya mshahara vinawazuia waombaji wenye sifa kupata nafasi hizo.

"Kuna taasisi muhimu ambazo zina wafanyakazi wasiotosha, wakati nyingine zinao wengi. Zoezi hili litasaidia katika ugawanyaji upya wa kazi pale inapohitajika," Ruto alisema.

Hata waliokufa walikuwa wakilipwa
Katika kaunti ya Mombasa pekee, ukaguzi uligundua kwamba hadi wafanyakazi hewa 1,000 walikuwa katika orodha ya malipo ya mishahara ya serikali.

Utawala wa kaunti ya Mombasa uliwarithi wafanyakazi hao wasiokuwepo au wafanyakazi waliokufa kutoka kwa iliyokuwa Halmashauri ya Manispaa ya Mombasa, kwa mujibu wa Khalid Walid, ofisa wa fedha wa ndani aliliambia gazeti la The Standard la Kenya. Wafanyakazi hewa katika kaunti hii walipata jumla ya shilingi milioni 50 (dola 577,000) katika mshahara baada ya kulipwa bila ya kutambuliwa kwa miaka mingi, alisema.

Wafanyakazi waliofariki ambao walikuwa wanalipwa kupitia benki waliendelea kupata fedha zilizoingizwa katika akaunti zao baada ya kufariki, aliyekuwa Diwani wa Kata ya Ademsajida Abdirahman Ahmed aliiambia Sabahi. Lakini wakati wafanyakazi wa ngazi ya chini, ambao walikuwa wakilipwa fedha taslimu na zilizokuwa halmashauri za jimbo, walipofariki malipo yao yalikuwa yakichukuliwa na viongozi waliokuwa wanasimamia ulipaji wa mishahara yao, alisema.

Katika Kaunti ya Garissa, ukaguzi ulibainisha watu wapatao 300 ambao walikuwa hawafanyi kazi lakini bado walikuwa wakilipwa.

"Tunawabainisha pia wafanyakazi hewa kama wafanyakazi wa serikali ambao wameamua kufanya biashara zao kwa kutumia muda wa umma. Kimsingi tunatumia Sheria ya [Tume ya Utumishi] Umma na kanuni za maadili za watumishi wa serikali kusahihisha kushindwa kwa mfumo uliopita wa serikali," Gavana wa Kaunti ya Garissa Nathif Jama Adam aliiambia Sabahi.

"[Wafanyakazi hewa] wamekuwa wakidanganya serikali kwa miaka mingi. Kwa lengo la busara, serikali ya nchi haitamlipa mtu yeyote ambaye hatoi huduma" alisema.

Gavana wa Kaunti ya Nairobi Evans Kidero alisema inafuatilia majina ya zaidi ya wafanyakazi hewa 1,000 katika orodha yake ya malipo ya mshahara.

"Kama mtu analipwa basi ni lazima kuzifanyia kazi fedha hizo. Tutaimarisha mfumo huo wa kuhakikisha kwamba wote wanaobaki wafanye kazi au vinginevyo waachishwe kazi," aliiambia Sabahi, akiongeza kwamba malipo makubwa ya ujira na malalamiko kuhusu huduma mbaya kutoka kwa wakaazi wa Nairobi awali yalizindua shaka kwa utawala.

Katika Kaunti ya Wajir, ukaguzi uligundua kwamba wafanyakazi 100 katika orodha ya malipo ya serikali walikuwa hawafanyi kazi, kwa mujibu wa Gavana wa kaunti Ahmed Abdullahi.

Baadhi ya watu hao walikuwa wameshafariki, wengine walikuwa wakifanya kazi katika asasi zisizo za serikali huko Somalia na katika kambi kubwa ya wakimbizi ya Dadaab, na wengine walikuwa wamefukuzwa kazi, aliiambia Sabahi.

"Kosa hilo linasababisha serikali ya taifa kutopeleka watumishi, kama, wafanyakazi wa afya au walimu nchini kwa sababu data zao zinaonyesha kwamba nchi ina wafanyakazi. Hili linasababisha utoaji wa huduma mbaya na ukaguzi utarekebisha uelewa huo mbaya," alisema.

Muuguzi wa hospitali ya eneo la Wajir Mohamed Noor Ali alisema utawala wa Kaunti unapaswa kuwa makini na ukaguzi wake na kufanya usikilizaji wa halali kwa watu kabla ya kuwabainisha kama wafanyakazi hewa, kwani baadhi wanaweza kuwa wamepewa kazi nyingine au kwenda likizo ya masomo.

"Kuna matukio ambapo serikali ya taifa [iliwapeleka] baadhi ya wafanyakazi wake katika asasi zisizo za serikali kufanya kazi katika mashirika ya misaada ya kibinadamu ndani ya nchi kwa kipindi maalumu, kuanzia mwezi mmoja hadi miaka," alisema, akiongeza kwamba serikali ya Kaunti na ya taifa inahitaji kushirikiana ili kuandaa orodha ya mwisho ya wafanyakazi wasiokuwepo kazini.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 20290

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>