Quantcast
Channel: MATUKIO NA VIJANA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 20290

Makunga, Kibanda wana kesi ya kujibu

$
0
0
Meneja Uendeshaji Biashara wa Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd (MCL), Theophil Makunga (katikati) akizungumza na Mwanasheria wa Kampuni hiyo, Doris Marealle nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jana baada ya kuahirishwa kwa kesi inayomkabili pamoja na aliyekuwa Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Tanzania Daima, Absalom Kibanda (kushoto). Picha na Maktaba 
Meneja Uendelezaji Biashara wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Theophil Makunga na wenzake wawili, wamepatikana na kesi ya kujibu katika kesi ya makala ya uchochezi inayowakabili.Makunga na wenzake Absalom Kibanda na Samson Mwigamba wanakabiliwa na kesi ya uchochezi dhidi ya askari wa majeshi ya ulinzi kwa kuchapisha makala kwenye Gazeti la Tanzania Daima yenye maneno yaliyolenga kuwashawishi wasiwatii viongozi wao.Makala hayo ya Novemba 30, 2012 yaliyokuwa na kichwa cha habari `Waraka maalumu kwa askari wote’ yaliandikwa na mshtakiwa wa kwanza, Mwigamba ambaye ni mwandishi wa makala katika safu yake ya `Kalamu ya Mwigamba’ katika gazeti hilo.Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Warialwande Lema jana aliwaamuru washtakiwa hao kujiandaa kupanda kizimbani kujitetea baada ya upande wa mashtaka kufunga ushahidi wake.Wakili wa Serikali Beatha Kitau, alisema upande wa mashtaka haukuwa na shahidi mwingine zaidi hivyo kuiomba mahakama kufunga ushahidi wao. Kabla ya kufunga ushahidi wake, upande wa Jamhuri uliwaita mashahidi watatu kutoa ushahidi.
Mashahidi hao ni pamoja na Mkurugenzi Msaidizi wa Usajili wa Magazeti, Raphael, Hokororo, Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Magereza (ACP) kutoka Kitengo cha Sheria cha jeshi hilo, George Mwambashi na Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi (SSP), David Hizza.Baada ya Jamhuri kufunga ushahidi wake, mawakili wa utetezi wakiongozwa na Isaya Matambo waliiomba mahakama iwapatie mwenendo wa kesi hiyo kwa ajili ya kuandaa hoja kama washtakiwa wana kesi ya kujibu au la.Mbali na Matambo, mawakili wengine wa utetezi ni Nyaronyo Kicheere na John Mhozya ambao wote watatu wanawatetea Mwigamba na Kibanda na Imam Daffa kwa niaba ya Makunga.Hata hivyo, Hakimu Lema aliwakatalia akisema kuwa hawezi kutoa nafasi ya kufanya majumuisho ya hoja kama washtakiwa wana kesi au la.Hata hivyo, Hakimu Lema hakufafanua sababu ya kukataa ombi hilo, badala yake alitoa uamuzi papo hapo kuwa washtakiwa wote wana kesi ya kujibu.“Baada ya prosecution (upande wa mashtaka) kufunga ushahidi wake na kwa kuzingatia ushahidi ulioko mahakamani, Mahakama hii imeona kuwa washtakiwa wote wana kesi ya kujibu na wanatakiwa wajiandae kwa utetezi,” alisema.
Kutokana na uamuzi huo, Hakimu Lema aliamuru washtakiwa waanze kujitetea Septemba 3, mwaka huu.Na Mwananchi

Viewing all articles
Browse latest Browse all 20290

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>