Naye mkurugenzi wa uwanja huo Bw Moses Malaki amesema uwanja unakidhia matakwa ya kiusalama wa kimataifa ila jambo kubwa ni uwepo wa watau wachachae ambo wanafanya kazi kinyume na mfumo huo.
Akihitimisha ziara hiyo Mh Mwakyembe amesema amebaini mambo mengi ikiwemo kuwa katika uwanja huo kuna taasisi nyingi za kiusalama ambazo zinafanya kazi hivyo na kusema kuwa hakuna sababu yeye wala watumishi wengine wa uwanjani huo kuendelea kufanya kazi uwanjani hapo.
Hivi karibuni uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wa jijini Dar-es-Salaam, uligubikwa na wingu la kukamatwa kwa kiasi kikubwa cha madawa ya kulevya yaliyo kamatwa nchini Afrika ya kusini yakihusishwa na vijana kutoka Tanzania, jambo lililopelekea Watanzania kukaguliwa ki ziada katika mataifa ya nje ikiwemo Afrika ya kusini hivyo kuchafua jina la Tanzania katika medani ya kimataifa
Chanzo:ITV