Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe ACP Fulgency Ngonyani amesema Mitandao ya simu imefanikisha kumkamata Tapeli huyo.ALIYEKUWA AKITAPELI WATU MTANDAONI KWA JINA LA RAFIKIELIMU AJULIKANA.
ALIYEKUWA AKITAPELI WATU MTANDAONI KWA JINA LA RAFIKIELIMU,AJULIKANA...Ni Mhitimu wa Chuo Kikuu Cha Sokoine Morogoro ( SUA ), Mkaazi wa Njombe! Zawadi Nono Ya Fedha Taslimu, Shilingi Laki Tano ( Tsh.500,000/=) Za Kitanzania, kutolewa kwa mtu atakaye fanikishwa kukamatwa kwa tapeli hili la mtandaoni.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Acp Fulgency Ngonyani amethibitishwa kukamatwa kwa Tapeli huyo na kwamba kwa sasa alikuwa akifanya kazi kama Project Cordinator wa Agape Foundationi Asasi isiyo ya kiserikali inayoshughulikia masuala ya Watoto Yatima wilayani Njombe.
Kamanda Ngonyani amesema Mtuhumiwa Huyo kama Jina lake Linavyojieleza kwenye Tangazo na Picha Zake mwenye umri wa Miaka 27 Mkazi wa SIDO Njombe amekamatwa Jana majira ya Jioni hivyo hatua za kumsafirisha kupelekwa makao makuu ya Polisi Jijini Dar es Salaam zinaendelea kutokana na kesi yake kufunguliwa Huko.Aidha amesema kuwa hadi sasa wanamsubiri Askari atakayetumwa toka Makao makuu Jijini DAR Kuja kumchukua.
Taarifa za awali zilieleza kutafutwa kwa Tapeli huyo toka Makao Makuu ya Jeshi la Polisi.INAPOTOKA : Mnamo siku ya tarehe 11 Machi 2013, tuliripoti kupitia blogu yetu na katika blogu mbalimbali nchini kuhusu kuwepo kwa mtu anaye watapeli wananchi fedha kwa kutumia jina la taasisi yetu. Tapeli huyu asiye na hata chembe ya huruma kwa masikini wenzake, aliweka tangazo katika mtandao wa Zoom Tanzania, mnamo mwanzoni mwa mwezi February 2013 akitangaza nafasi za kazi z a kuvolunteer katika mikoa mbali mbali ya Tanzania bara. Baada ya watu kutuma maombi yao, tapeli huyo aliyekuwa akijitambulisha kwa jina bandia la EMMANUEL ALBERT na kwamba yeye ni HR wa RafikiElimu, aliwaambia kuwa wamepata nafasi, na kuwatumia fomu za kujaza kisha kuwataka wamtumie shilingi elfu Tano ( Tshs. 5,000/=) za kitanzania kwa mpesa kwenda namba 0763906931 ( AMBAYO MBAYA ZAIDI AMEISAJILI KWA JINA LA RAFIKIELIMU )..
Baada ya kumtumia pesa , tapeli huyo aliwatumia barua na kuwaagiza kuripoti kazini katika taasisi mbalimbali, huku mmoja kati yao akimuagiza aje kuripoti katika ofisi zetu.
Tulibaini juu ya uwepo wa utapeli huu mara baada ya kutembelewa na mmoja kati ya wahanga wa utapeli huo. Dada huyo aliye jitambulisha kwa jina la HAWA MUSSA ambaye ni Muhitimu wa Chuo Kikuu Cha Dodoma ( 2012 ) aliripoti katika ofisi zetu siku ya tarehe 11 Machi 2013 saa nne kamili asubuhi na kuomba kumuona HR . Baada ya kufanya naye mazungumzo ndipo tulipo baini kuwepo kwa utapeli unao fanyika kwa jina la taasisi yetu. Haraka haraka tukaenda kuripoti uhalifu huu kwenye kituo kidogo cha polisi cha Chuo Kikuu Cha Dar Es salaam, na kukabidhiwa RB namba UD/RB/849/2013 WIZI KWA NJIA YA MTANDAO.
![]() |
Hashim Mkane, tapeli anayetafutwa kwa kosa la Kutapeli mtandaoni kwa jina la RafikiElimu. |
Mara baada ya kupata RB moja kwa moja tulipost taarifa ya kuwatahadharisha wananchi juu ya uwepo wa mtu anaye tapeli watu kwa kutumia jina la taasisi yetu, huku tukiwaachia polisi na kazi ya uchunguzi wa tukio hili la uhalifu. Wakati polisi wakiwa bado wanaendelea na uchunguzi, siku ya Jumatatu ya jana, tarehe 11 Machi 2013 saa sita kamili asubuhi, tulipokea simu kutoka kwa mwakilishi wetu wa Mwanza, Dada HADIJA SEJA akiomba tumpe namba za " MR. EMMANUEL ALBERT " ( HR wa RafikiElimu Foundation ).. Kwa kuwa tayari tulikuwa na taarifa za jina hilo, tulimuomba dada Hadija Seja atutaarifu kitu gani kimetokea. Dada Hadija alitupa taarifa ya kusikitisha sana, kwamba kuna mtu mmoja aliyemtaja kwa jina moja tu la Gerlad kutoka Arusha, amewasili jijini Mwanza kuripoti katika ofisi za taasisi ya RESTLESS DEVELOPMENT kwa ajili ya kuanza kazi. Mtu huyo naye ni muhanga wa tapeli huyu, na baada ya kumtumia tapeli huyo sh. elfu tano, tapeli alimuagiza aende kuripoti jijini Mwanza katika ofisi za RESTLESS DEVELOPMENT ( mabazo kimsingi hazipo Mwanza ). Can You imagine, huu ni unyama wa kiwango gani, kumfanyia masikini mwenzako ushenzi kama huo?.
Baada ya kupata taarifa hii, moja kwa moja tukaamua sisi wenyewe kama taasisi kwenda katika ofisi za VODACOM makao makuu zilizopo Mlimani City ili kuweza kumbaini mtu anaye fanya unyama huu...
Tunashukuru sana Mungu, Vodacom walitupa ushirikiano wa kutosha.. Kutoka kwenye database za Vodacom, tuligundua kwamba, mtumiaji wa 0763906931 anaishi Njombe. Namba hii imesajiliwa MPESA tarehe 02 February 2013, hakusajili kwa kitambulisho chake halisi, bali kwa barua kutoka kwa Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa. Alisajili akiwa NJOMBE na alipokea simu nyingi sana. Zaidi ya watu kumi waliingia katika mkenge wake na kumtumia hizo shilingi Elfu Tano.
Mwanzoni alikuwa ana toa hela zake kwa wakala ambaye alisajilia namba hii, lakini baadaye alisafiri na kwenda tarafa nyingine hivyo basi kushindwa kutoa hela kwa sababu namba ameisajili kwa jina ambalo sio lake. Hivyo basi ili kuweza kutoa pesa ilimbidi, ajihamishie salio kutoka katika namba 076390631 kwenda kwenye namba yake halisi ambayo ni 0765283703. Hapo ndipo tulipo weza kumbaini tapeli huyu.
Jina la huyu mtu anaitwa HASHIM MKANE na namba yake halisi ni 0765283703. Ni mkaazi wa Njombe na amehitimu Chuo Kikuu Cha Sokoine ( SUA ) . Aliwahi kuomba nafasi ya uwakala wa RafikiElimu katika wilaya ya Njombe, mwezi Agosti 2012.
Baada ya kupata taarifa hizi tuliamua kutafuta mbinu za kumkamata kirahisi,ambapo tulimtumia barua pepe, jana jioni kisha ujumbe mfupi wa maneno ( SMS ) tukimwambia aje Dar Es salaam kuhudhuria semina ya siku tano ya mawakala wa RafikiElimu ( Tukamtajia na malipo ). Nadhani alistukia kwamba huenda ameshajulikana, akatuma ujumbe mfupi wa maneno uliosomeka :
" Nashukuru kwa taarifa hii ingawa nitashindwa kuhudhuria kwa kuwa taarifa imechelewa kufika na ukichukulia mimi ni mwajiliwa wa taasisi binafsi hivyo kuweza kupata ruhusa kwa siku moja au mbili ilihali tunafanya evaluation ya mradi ni ngumu. natumai kuhudhuria semina nyingine kama mtaiandaa "

Hapa tukajua jamaa ameshastukia mchezo na uwezekano wa kumkamata kwa njia hiyo usingekuwa rahisi. Hivyo basi tumeamua kuweka taarifa hii mtandaoni pamoja na picha za mtuhumiwa huyu, ili kwa yoyote yule atakaye fanikisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyu aweze kupewa zawadi nono ya shilingi Laki Tano za kitanzania . Taarifa nyingine zitatumwa kwenye magazeti na televisheni ili iwe rahisi kusambaza ujumbe kwa watanzania wengi na hivyo kurahisisha kutiwa hatiani kwa dhalimu huyu . Tafadhali upatapo ujumbe huu, wafahamishe na ndugu jamaa na marafiki zako woote...
UKIMUONA MTU HUYU, TOA TAARIFA KATIKA KITUO CHOCHOTE CHA POLISI KILICHO KARIBU NAWE , KISHA WASILIANA NASI KWA SIMU 0782405936. NA ENDAPO TAARIFA YAKO ITASAIDIA KUKAMATWA KWA TAPELI HUYU, TUTAKUPATIA ZAWADI YA FEDHA TASLIMU ZA KITANZANIA SHILINGI LAKI TANO ( Tsh. 500,000/ =)..
![]() |
Hashim Mkane, mwenye namba 0765283703 tapeli wa mtandaoni, aliyewatapeli makumi ya wananchi kwa jina la RafikiElimu akiwahadaa kuwapatia kazi katika taasisi mbalimbali. |
( KWA TAMAA YA PESA KIDOGO, AMEJIDHALILISHA, AMEDHALILISHA TAALUMA YAKE, AMEDHALILISHA CHUO CHAKE, AMEWADHALILISHA WAZAZI, WAKE, NDUGU , JAMAA NA MARAFIKI ZAKE, KWELI WAHENGA WALISEMA TAMAA ILIMPONZA FISI NA MCHUMA JANGA , HUCHUMA NA WA KWAO. )
Jeshi la Polisi Mkoani Njombe limewataka wananchi kufanya kazi kwa uaminifu bila udanganyifu
.