Quantcast
Channel: MATUKIO NA VIJANA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 20290

Ubakaji waongezeka katika mkoa wa Somaliland huku wakosaji wakipata msamaha

$
0
0
Wahamasishaji wa haki za binadamu wamesema idadi kubwa ya wanawake katika mkoa wa Somaliland wanakabiliwa na mawindo ya ubakaji. Juu, wanwake wakiwa wamejipanga mstari nje ya kituo cha kupigia kura huko Hargeisa tarehe 26 Juni, 2010, wakati Somaliland ilipofanya uchaguzi wake wa urais wa mkoa. 
Kuingilia kati kwa wazee wa kimila na kukosekana kwa utekelezaji wa sheria kunakwamisha mashtaka dhidhi ya idadi inayoongezeka ya matukio ya ubakaji katika mkoa wa Somaliland.
Takribani wanawake na watoto 180 wa Somaliland walibakwa kuanzia Januari hadi tarehe 8 Agosti, kwa mujibu wa kumbukumbu zinazotunzwa na kituo cha Baahi-Koob, ofisi ya rufaa za mashambulio ya kingono katika Hospitali kuu ya Hargeisa. Kituo hicho huwanasihi waathirika, kinawapima afya, na kupeleka kesi zao kwa polisi na mahakamani.
"Ukiukaji katika ubakaji unaongezeka kila mwezi na kila mwaka," alisema meneja wa programu wa Baahi-Koob Abdikadir Ahmed Mohamed. Alisema asilimia 30 ya matukio yaliyoripotiwa yalikuwa ya ubakaji unaofanywa na genge na asilimia 55 ya waathirika walikuwa na umri wa chini ya miaka 15.
Kituo hicho kilianzishwa 2009, kina rasilimali chache na kinafanya kazi katika eneo moja tu. Dhamira kuu ya kituo inakabiliwa na vikwazo kadhaa, kama vile kuingiliwa kitamaduni, msamaha wa kisheria katika mashtaka inayowakabili wabakaji na umma kukosa uelewa wa jumla kuhusu kutoa ripoti za matukio ya ubakaji kwa wakati, Mohamed said.
Aidha, wafanyakazi wa afya katika Baahi-Koob hawana vifaa au mafunzo ya kutosha ya namna ya kukusanya vizuri ushahidi wa kimwili ambao unaweza kutumiwa mahakamani. Robo ya matukio ambayo Baahi-Koob inayashughulikia huishia kukosa ushahidi kama huo wakati inapopelekwa mahakamani, Mohamed alisema.

Ni matukio machache chini ya asilimia 20 hupelekwa kwenye mamlaka na Baahi-Koob na kusababisha hukumu za mahakama kwa sababu wazee wa kimila hushughulikia kesi hizo hata wakati zikiwa zinasikilizwa na mahakama, alisema.

Kuna mifumo mitatu sambamba ya kutoa hukumu ya mizozo huko Somaliland -- moja ni ule unaoegemea katika desturi na kuongozwa na wazee wa kimila, mwingine unaegemea kwenye sheria za sharia na mwingine unaegemea kwenye mfumo wa sheria wa Somaliland -- ambayo inawawezesha wakosaji kutafuta hukumu katika mfumo ambao unawafaidisha.

Ingawaje sheria inayoainisha makosa na adhabu inataja adhabu ya hadi miaka 15 kwa kubaka, hakuna mahakama katika Somaliland ambayo imewahi kutoa kifungo cha muda mrefu kama huo kwa mshtakiwa wa kubaka, Mohamed alisema.

"Kinachotokea ni adhabu ya mwaka mmoja dhidi ya mkosaji, ambaye badala yake analipa faini hapo hapo," alisema.

Hata hivyo, Mohamed, aliifurahia adhabu ya miaka 10 iliyotolewa tarehe 4 Agosti na Mahakama ya Mkoa ya Marodi Jeh kwa wanaume 20 kati ya 21 walioshtakiwa kwa ubakaji wa kikundi wa wanawake wawili wa Hargeisa mwezi Julai 2012. Mshtakiwa wa mwisho alihukumiwa kifungo cha miaka mitano.

"Hiyo ilikuwa ni hukumu nzuri ambayo imetolewa na serikali dhidi ya wakosaji wa ubakaji wa kundi, na pia hukumu kali dhidi ya kesi yoyote ya ubakaji," alisema. Hata hivyo, serikali inapaswa kujitahidi kuanzisha na kutekeleza mfumo mmoja wa sheria, alisema, ukionyesha ukweli kwamba kwa sasa hakuna sheria inayokataza wazee wa kimila na wengine kuingilia kesi kama hizo.

Ndoa za kubaka
Kesi zilizoandikwa na Baahi-Koob ni chache sana kuliko jumla ya idadi ya ubakaji ambao ulifanyika huko Somaliland mwaka 2013, kwa mujibu wa Ahmed Yusuf Hussein, mkuu wa Shirika Kuu la Haki za Binadamu lenye makao yake Hargeisa.

"Hii ni kwa sababu kituo hicho kinafanya kazi Hargeisa tu, aidha [matokeo yake] kinawataja waathirika tu wanaokubali kuripoti kesi zao huko," Hussein aliiambia Sabahi. "Ubakaji haukuwahi kuwa wa kiwango cha juu kiasi hiki, na umekuwa ni tatizo kubwa la ukiukaji wa haki za binadamu katika Somaliland."

Hakuna aliye na uhakika kuhusu ni ubakaji mwingine kiasi gani unaotokea Hargeisa au sehemu nyingine za Somaliland, alisema. "Tunatafuta suluhisho la haraka kwa tatizo hili," Hussein alisema.

"Wakati kundi la vijana au wanaume wanambaka mwanamke mmoja, familia za wahalifu zinagawana gharama na kuifidia fedha familia ya muathirika," alisema, akiongeza kwamba baadhi ya waathirika wanalazimishwa hata kuolewa na wabakaji kama sehemu ya suluhu nje ya mahakama kati ya familia iliyosuluhishwa na wazee wa mila.

Fidia ya kubakwa inategemea suluhisho la kimila kwa kawaida haizidi shilingi milioni 5 za Somaliland (dola 760), alisema Hussein.

"Kwa jinsi tunavyojua, ndoa nyingi zilizopatikana kwa njia hii kwa haraka huishia katika talaka na hazidumu kwa zaidi ya miezi sita," alisema. "Hii ni kwa sababu ya kuchanganyikiwa mwanawake huyo kutokana na uhalifu unaofanywa dhidi yake."

Bado, kuna baadhi ya viashirio kwamba kuna maendeleo yanayofanyika kuhusiana na mashtaka ya kesi za ubakaji, kwa mujibu wa Hussein Jama Guled, mwanasheria na mshauri wa kitaalamu katika ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Somaliland.

Washtakiwa 134 katika kesi 67 za ubakaji walihukumiwa kati ya mwezi Mei 2012 na Mei 2013, Guled aliiambia Sabahi. Idadi hii inawakilisha ongezeko la asilimia thelathini katika hukumu za kuanzia mwaka uliopita.

"Inaonyesha maendeleo yanafanyika katika kupambana na suala hili," alisema.

Maendeleo yamefanyika kwa jitihada za ushirikiano kati ya ofisi ya mwendesha mashtaka na Programu ya Maendeleo ya Umoja wa Mataifa (UNDP) iliyokusudia kuendeleza mfumo wa kisheria wa Somaliland, alisema.

Sheria zipo ambazo zinaweza kutumika kushtaki kesi za ubakaji, Guled alisema. "Hakuna utekelezaji wa sheria, lakini kuna utekelezaji wa hukumu," alisema.

"Mara kesi ya ubakaji inapofika katika ofisi ya mashtaka, ni vigumu kwa [wazee wa mila] kuzipeleka katika njia ya kiutamaduni," alisema, akikiri kwamba kuingilia katika hatua za awali bado ni kikwazo kikubwa katika kuwafikisha wahalifu wa ubakaji mbele ya sheria.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 20290

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>