
Kikubwa zaidi mtoto huyo alizaliwa kwa njia ya kawaida. Mama wa mtoto huyo anaendelea vizuri.
Ujerumani imepata mtoto mpya anayeshikilia nafasi ya kwanza kwa kuzaliwa na uzito mkubwa zaidi.Jasleen alizaliwa kwenye hospitali ya chuo kikuu cha Leipzig July 26 akiwa na pounds 13.47 sawa na zaidi ya kilo 6 na mwenye urefu wa inchi 22.6.
Hata hivyo Jasleen, si mtoto aliyezaliwa na uzito mkubwa zaidi mwaka huu. Mtoto wa Uingereza George King, aliyezaliwa March alikuwa na uzito wa kilo saba na alizaliwa kwa njia ya kawaida