Hadi sasa hakuna kundi lililojitokeza kudai kutekeleza mashambulizi hayo lakini polisi wanashuku kuwa yalitekelezwa na wapiganaji wa Kisunni. Waislamu wa Kisunni wanasema kuwa wanatengwa na serikali ya Waziri Mkuu Nouri Maliki ambaye anaongoza serikali ya Kishia tuhma ambazo serikali inapinga na kusema kuwa wapiganaji hao wanatumiwa na makundi ya kigaidi. Tangu kuanza kwa mwaka huu, zaidi ya watu 4,000 wameuawa na zaidi ya 10,000 kujeruhiwa kutokana na mashambulizi hayo ya mabomu. Takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonesha kuwa mwezi Julai ullikuwa mbaya sana kwa raia wa Iraq baada ya watu 1,057 kupoteza maisha yao wengi wao wakiwa mjini Baghdad.
↧
ZAIDI YA WATU 50 WAUAWA KWA BOMU IRAQ
↧