Quantcast
Channel: MATUKIO NA VIJANA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 20290

Hali ya usalama ya Mogadishu yaibua swali

$
0
0
Ofisa usalama akiwa amesimama karibu na eneo ambalo bomu la kujitoa muhanga lililipuka tarehe 5 Mei katika msafara wa serikali huko Mogadishu ambalo liliua watu 11. Ulipuaji huu wa bomu ni moja ya mashambulio kadhaa yaliyosababisha vifo ambayo yalilenga mji mkuu katika siku za karibuni, ikiibua maswali kuhusu ufanisi wa vikosi vya usalama vya Mogadishu. 
Kulingana na upigaji risasi uliosababisha kifo wiki iliyopita huko Mogadishu ambao ulimlenga mwanasiasa wa Swideni, wachunguzi wasema serikali ya shirikisho ya Somalia inahitaji kufanya zaidi kuimarisha usalama na kulinda wageni wa nje ambao msaada wao ni muhimu katika ujenzi wa nchi.
Tarehe 21 Agosti, mwanaume mwenye silaha alimpiga risasi na kumjeruhi mwanasiasa wa Swideni Ann-Margarethe Livh, ambaye aliripotiwa kuwa alikuwa anarudi hotelini kwake kwa gari baada ya kutoa mhadhara kuhusu demokrasia kwenye chuo kikuu cha Somalia huko Mogadishu.

Wanaume wawili waliokuwa wakisafiri naye, mwanaume mwenye asili ya Kisomali na Kiswideni ambaye anaaminika kuwa alikuwa mkalimani na polisi wa Somalia ambaye alikuwa mlinzi binafsi wake, waliuawa katika shambulio hilo.

Gari hilo lilishambuliwa nje tu ya eneo la chuo, karibu na njia ya mzunguko ya KM4 yenye magari mengi. Eneo la chuo liko nyuma ya makao makuu ya Idara ya Upelelezi wa Uhalifu siyo mbali kutoka ubalozi wa Uturuki, ambao ulishambuliwa na wapiganaji wa al-Shabaab tarehe 27 Julai.


Wanaume hao walikimbia na hakuna kundi liliodai kuhusika.

Serikali ya Somalia ililaumu shambulio hilo na kutangaza kwamba ilianzisha uchunguzi.

"Ninalaumu shambulio hili kwa nguvu zote na kutuma salamu zangu za rambirambi kwa familia za mwanasiasa wa Swideni aliyeshambuliwa Mogadishu jana," Waziri Mkuu Abdi Farah Shirdon alisema katika kikao cha baraza la mawaziri tarehe 22 Agosti. "Ninatoa wito kwa vikosi vya ulinzi kuwalinda marafiki zetu na wabia wetu wanaotembelea na kufanya kazi Somalia."

Hata hivyo, kushupaa kwa mashambulizi, kumeonyesha mapengo katika kinga ya usalama ya mji mkuu, profesa wa sayansi ya siasa wa Chuo Kikuu cha Mogadishu Abdikarim Daud Nur aliiambia Sabahi.

Polisi ya Somalia na vikosi vya Misheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM) walipaswa kuwa wameondoa mashambulizi, alisema.

"Ilikuwa sio haki kuwaleta watu kama hivyo, ambao wanaunufaisha umma, katika hoteli na kuwaacha humo. Inaonyesha ulazima wa kuitegemea AMISOM kuwalinda wanadiplomasia," alisema Nur, ambaye pia alikuwa kanali wa Jeshi la Taifa la Somalia.

Katika maoni yake, ukosefu wa usalama ulitokana na mambo kadhaa yaliyolimbikizwa.

"Sababu za kutofaa kwa ulinzi ni wanajeshi ambao hapewi mishahara yao ipasavyo, kutokuwa na uwezo kwa kikosi cha upelelezi cha serikali [uwakala] kukusanya data muhimu zinazohusiana na usalama na ukosefu wa mafunzo endelevu ya kiutaalamu," Nur alisema.

Nur alitoa wito kwa serikali kutafuta msaada wa ziada wa majeshi kutoka jamii ya kimataifa kupitia mafunzo zaidi ya mara kwa mara kwa vikosi vya Somalia.

"Ili vikosi vya usalama viwe na viwango vya kimataifa, inabidi msaada utafutwe kutoka katika mataifa yenye kiwango cha juu cha [maarifa] katika usalama na ambayo ni marafiki wa Somalia ili yaweze kuvisaidia mara kwa mara vikosi vya usalama vya serikali katika usalama," alisema.

Kutofuata utaratibu kwa vikosi vya usalama vya Somalia
Shambulizi la tarehe 21 Agosti lililotokana na uzembe na kutofuata utaratibu kwa upande wa vikosi vya usalama vya Somalia, alisema Mohamed Nur Galal, jenerali mstaafu na aliyekuwa naibu waziri wa ulinzi katika utawala wa Mohamed Siad Barre.

"Makao makuu ya Mahakama ya Mkoa wa Benadir yalishambuliwa wakati serikali ilipokuwa ikituambia kwamba ilikuwa ikifanya jambo fulani kuhusiana na usalama. Makao makuu ya UN yalishambuliwa wakati walikuwa wakisema hivyo, na sasa wanasiasa wa Sweden ambao usalama ulipaswa kuwa kipaumbele kwao walishambuliwa," Galal aliiambia Sabahi. "Kwa hiyo, maneno ya kiongozi wa utawala na hali iliyopo ya usalama ipo katika wasiwasi."

Galal alisema tukio la hivi karibuni limeshusha hadhi uwezo wa upungufu katika majeshi ya usalama ya Somalia.

"Wanaume waliomshambulia [Livh] inaonyesha walikuwa na taarifa ya kutosha kuhusu mahali alipokuwa," alisema. Hata hivyo, watumishi wa usalama ambao sasa wanafuatiliwa na wamekuwa wakipingwa kwa kutompa ulinzi hawana hata mafunzo ya kutosha kufanya kazi yao, aliongeza.

Ili kuzuia mashambulio kama haya yasitokee tena siku zijazo, serikali inapaswa kuwarejesha baadhi ya wanajeshi wa zamani, ambao watahudumia kama wafundishaji wa jeshi, alisema Galal.

Kanali mstaafu Ali Ibrahim Afey, hata hivyo, alisema usalama umeboreshwa kwa kiasi kikubwa huko Mogadishu kwa miaka michache iliyopita na hilo halipaswi kupuuzwa.

Shambulio la Livh lilipeleka ujumbe wa uongo kwamba kikundi kisichotaka amani kimefanikiwa kupita usalama katika mji mkuu, alisema, wakati rushwa katika mahakama ni kiini cha tatizo.

"Nchi haiwezi kufanikiwa katika usalama kama matawi ya mahakama zake yamejaa na ufisadi, kwa sababu wakati ofisa anapomkamata mtu fulani na kumpeleka katika kituo cha polisi, mtu huyo anaachiwa kesho yake ama kwa njia ya ukabila au fedha," Afey aliiambia Sabahi. "Sijui jinsi usalama unavyoweza kuboreshwa bila kubadilisha matawi ya mahakama au kuyachukulia kama yanawajibika kwa kiasi kikubwa."


Viewing all articles
Browse latest Browse all 20290

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>