Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi funguo za Trekta kwa Mwenyekiti kwa vijana Tumsume Shemgogo lililotolewa na chama cha Mapunduzi CCM kwa vijana wa mkoa wa Njombe katika makabidhiano yaloyofanyika kwenye Kambi ya vijana iliyopo kwenye kijiji cha Mlengu Kata ya Kiangala Tarafa ya Ikuo mkoani Njombe ambapo kambi hiyo ina eneo lenye ukubwa wa hekta 300 za mashamba, Kinana aliahidi kutoa trekta hilo wakati alipofanya ziara ya kikazi mkoani Njombe mwezi Agosti mwaka huu baada ya kuelezwa jinsi vijana hao walivyojiunga pamoja katika kikundi na kuamua kushughulika na kilimo ili kujkwamua kiuchumi, Leo Abdulrahman Kinana alishiriki kulima kwa trekta kabla ya kukabidhi trekta hilo kama anavyoonekana katika baadhi ya picha akilima shambani kwa trekta. Kushoto anayeshuhudia makabidhiano hayo ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi, Katika Ziara hiyo Kinana pia ameongozana na Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kamataifa na Mbunge wa kuteuliwa.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-MAKETE-NJOMBE) Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akilima shambani kabla ya kukabidhi trekta hilo.Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiliendesha kwa umakini kabisa.Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kamataifa na Mbunge wa kuteuliwa akikumbatiana kwa furaha na Mkuu wa Wilaya ya Makete Josephin Matiro mara baada ya kuwasili katika eneo la mapokezi huko Chimala Mbeya.Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kulia akizungumza na Kapten mstaafu Aseri Msangi mara baada ya kuagana na Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh. Abbas Kandoro wa pili kutoka kushoto na viongozi wengine wakati alipowasili katika eneo la Mapokezi huko Chimala mkoani Mbeya leoKinana akisalimiana na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Njombe.Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe Ndg, Deo Sanga “Jah People” akizungumza wakati wa mapokezi hayo kulia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na kutoka kushoto ni Dr. Asha Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi.Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kucheza ngoma ya kabila la Wawanji huko linalopatikana mkoani Njombe.Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na vijana wa Kambi ya Mlengu kabla ya kukabidhi trekta kwa vijana hao.Wananchi wa kijiji cha Mlengu wakimsikiliza Abdulrahman Kinana hayupo pichani wakati alipokuwa akizungmza nao.Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akifurahia jambo wakati alipokagua darasa la ushonaji wa nguo katika chuo cha Veta mjini Makete Kushoto ni Dr. Asha Rose Migiro na katikati ni Mkurugenzi wa Veta Kanda ya Kusini Monica Mbele,Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozwa na Mkurugenzi wa Veta Kanda ya Kusini Monica Mbele wakati alipokagua chua cha Veta mjini Makete leo kushoto ni Josephin Matiro Mkuu wa Wilaya ya Makete.Injini Asifiwe Swalo mwalimu wa chuo cha VETA Makete akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati alipotembelea chuoni hapo na kukagua shughuli mbalimbali zinazoendeshwa na chuo hicho, kulia ni Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Kusini Monica Mbele.Mwanafuzni wa fani ya ujenzi Abel Mbilinyi akimuelezea Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana jinsi wanavyofyatua matofari yaliyochanaganywa udongo wa kawaida na saruji kidogo na faida zakeMkuu wa mkoa wa Njombe Kapten Aseri Msangi akiuliza swali kwa mwanafunzi Tito Fungo uimara wa matofari hayo huku Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Dr. Asha Rose Migiro wakisikiliza kwa makini.Nape Nnauye akijenga njia zinazopita chuni hapo kwa matofari madogo huku Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na viongozi wengine wakiangalia.Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipanda mti wa kumbukumbu chuoni hapo.Dr. Asha Rose Migiro katikati akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa wilaya ya Makete Josephin Matiro kushoto na Monica Mbele Mkurugenzi wa VETA kanda ya Kusini.Picha ya pamoja ikipigwa