Quantcast
Channel: MATUKIO NA VIJANA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 20290

Chama kipya chataka kukabiliana na changamoto zinazowakabili waandishi wa habari wanawake

$
0
0

Waandishi wa habari wakihudhuria uzinduzi wa chama cha Waandishi wa habari Wanawake wa Somalia mjini Mogadishu hapo tarehe 25 Novemba, 2013. 

Na Abdi Moalim, Mogadishu

Chama kipya cha waandishi wa habari wa Somalia kinakusudia kushughulikia changamoto maalumu zinazowakabili waandishi wa habari wanawake kutokana na ukosefu wa elimu na mafunzo pamoja na majukumu ya kifamilia na shinikizo za kijamii.Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake wa Somalia (SWJ) kilizinduliwa tarehe 25 Novemba na kina zaidi ya wanachama 70 wanaofanya kazi kama waandishi wa habari katika Somalia ya kusini na kati.
Chama hicho kiliundwa ili kuchunguza mahitaji ya waandishi wa habari wanawake na changamoto zinazowakabili, na kuwaandaa kutumikia taaluma, kwa mujibu wa mwenyekiti wa SWJ, Farhia Mohamed Kheyre .
Wanawake wowote wenye nia katika uandishi wa habari au ambao sasa wanafanya kazi katika fani hii wanaweza kujisajili katika chama, Kheyre alisema, na hakuna ada zinazohitajika kutoka kwa wanachama.
"Wanawake hawabakii katika uandishi wa habari kwa muda mrefu kwa vile baadhi yao huacha kazi wakati wanapoolewa au kuwa na watoto," Kheyre aliiambia Sabahi, akiongeza sababu kuu ni ukosefu wa msaada. "Wanawake wengi wenye elimu ndogo pia hujiunga na fani hiyo ya uandishi wa habari na kisha kushindwa. Tatizo lingine linalowakabili wanawake ni kwamba hawapewi nafasi muhimu katika vyombo vya habari vya Somalia kama vile majukumu ya wahariri au wakurugenzi."
SWJ itafanya kazi ya kuondokana na changamoto hizo kwa ajili ya maendeleo ya wanawake katika uwanja wa uandishi wa habari, Kheyre alisema.
"Tufungua kituo cha kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari kike na pia kuwaelimisha wanawake juu ya jinsi ya kushughulikia masuala yanayosababisha waache taaluma yao," alisema. "Kwa mfano, tutawaelimisha juu ya jinsi ya kusawazisha majukumu yao ya kikazi na kazi za nyumbani kama wataolewa."


SWJ itatoa nafasi kwa ushirikiano na mashauriano miongoni mwa wanawake, na itakuwa ikitetea haki za waandishi wa habari wa Somalia, alisema.

Kheyre alisema pia watazungumza na wamiliki wa vyombo vya habari kuhusu kutoa nafasi kwa wanawake nafasi kuonyesha uwezo wao uandishi wa habari na ubunifu.

"Wamiliki wa vyombo vya habari inabidi wakiri uwezo wa waandishi wa habari kike na kuwachukulia kuwa ni watu wenye uwezo ambao wanaweza kukamilisha kazi zozote ambazo zinaweza kufanywa na wanaume," alisema.

Waandishi wa habari wanawake wanaweza kufikia uwezo wao
Nasro Kiin Hashi Nurre, mwenye umri wa miaka 21 na mwanachama wa SWJ ambaye anafanya kazi kama mtangazaji wa michezo katika kituo cha redio cha ndani Goal FM na Royal TV yenye makao yake mjini London, alisema wahariri ni nadra kuwapa wanawake kufuatilia na kuandika hadithi muhimu kama vile michezo au siasa.

"Hawaamini kuwa mwanamke anaweza kufanya kazi ngumu kama hiyo, kwa hiyo hawawapi wanawake nafasi," alisema. "Hata hivyo, sasa tutajaribu kuonyesha jinsi gani waandishi wa habari wa kike wana uwezo wa kutekeleza kazi yoyote katika uandishi wa habari. "

Nurre alianza kuandika matukio ya michezo mwaka 2009, na alisema wasikilizaji wake walikuwa na shauku sana katika kipindi chake kwa sababu walimuona kama mtu anayefanya kitu ambacho wanawake wengine wengi walikuwa hawakifanyi.

Haijawahi kuwa rahisi kufanya kazi katika uwanja unaodhibitiwa na wanaume, Nurre aliiambia Sabahi. "Mimi ni msichana pekee katika kundi la waandishi wa habari wa kiume," alisema, akiongeza kuwa kutangaza michezo kunaongeza seti ya ziada ya changamoto kama vile upatikanaji wa kuhoji wachezaji ambao wanapendelea kuzungumza na wenzao wa kiume.

"Changamoto nyingine ninayokumbana nayo ni kuandika baadhi ya michezo kwa sababu inafanyika wakati wa usiku," alisema, akisema kuwa mameneja wa kituo hawafanyi mipango maalum ili kuhakikisha usalama wake wakati wa kusafiri usiku kwa ajili ya kazi .

Hata hivyo, Nurre aliwapa moyo wanawake wengine kudumu katika taaluma. "Waandishi wa habari wa kike lazima wawe na ujasiri katika uwezo wao na wanaamini kwamba wanaweza kufanya kazi yoyote," alisema.

Amina Muuse Weheliye, aliyekuwa mwandishi wa habari wa idhaa ya BBC ya Kisomali na sasa ni katibu SWJ kwa mahusiano ya nje na haki za binadamu, alisema chama kina nafasi kubwa ya kuboresha hali ya waandishi wa habari wanawake.

"[SWJ] ni kikundi cha watu wenye mahitaji ya kawaida, ujuzi wa kawaida na maslahi ya pamoja. Kwa hiyo, kitafanya mabadiliko makubwa katika hali ya sasa ya waandishi wa habari wa kike wa Somalia," aliiambia Sabahi.

Weheliye alisema kuwa kulikuwa na mashirika yaliyokwishaimarika yenye moyo wa kuisaidia SWJ kifedha, lakini sisi tutalenga kaitka kufikia malengo muhimu kabla ya kuwafikia wafadhili.

Ni muhimu kwa ajili ya shirika kwanza kusimama juu yake yenyewe na kuonyesha dira yake na uwezo yake, alisema, akiongeza kuwa fedha zitakuja baada ya wao kujithibitisha wenyewe. "Kama SWJ watatumika katika majukumu ambayo iliundwa kufanya, basi kuna mashirika ambayo husaidia vikundi kama chetu wenyewe. Tutatafuta msaada wao wakati tunasaidiana."

Weheliye alisema kuwa SWJ inahitaji fedha katika kutekeleza misheni hii, lakini haichangishi fedha katika hatua hii.

"Lengo letu si kupata fedha kutoka [chama] hiki, lakini hatimaye fedha inatoa usalama wa kuwapatia mafunzo wanawake hawa, kujenga ajira kwa wanawake hawa maskini baada ya ujuzi wao uandishi wa habari kuimarika, na kujenga nafasi ili wanawake hawa wapewe haki sawa na kutendewa sawa kama wanaume kwa ujuzi kama huo, "alisema. "Hii haipo kwa wakati huu."

Mapambano makali
Abdinasir Hirsi Idle, mkuu wa zamani w avyombo vya habari vya kujitegemea Radio Xurmo na HornAfrik, alisema wanawake wanaweza kuleta maendeleo katika uandishi wa habari wakiwa na elimu bora na kuamua kwa umahiri kukaa katika taaluma hii hata kama wakutana na changamoto nyingi.

Alisema wakurugenzi wanakabiliwa na matatizo wakati waajiri wanawake kwa sababu wengi wao hawako tayari kufanya kazi kwa muda mrefu na wengi wao hawaendelee na elimu na ujuzi wao.

"Tumeona wanawake waliopewa talaka kwa kuwa waandishi wa habari wakati walipokataa kuacha taaluma ya uandishi wa habari," alisema. "Kwa hiyo, ni muhimu kwa wanaume waliooa waandishi wa habari wanawake kuwasaidia katika taaluma yao badala ya kuwawekea shinikizo."

Kiin Omar Markaan, mwenye umri wa miaka 25, ambaye amekuwa akifanya kazi kama mwandishi wa tangu mwaka 2007, alisema wanawake mara nyingi wanakatishwa tamaa nyumbani kwao na kupuuzwa katika kazi.

"Mwanamake mwandishi wa habari ni aibu," alisema jamaa zake walimuambia. "Kwa nini hubaki nyumbani?"

Markaan alisema pia anakabiliwa na mapambano makali, baada ya daima kuthibitisha mwenyewe kwa wakubwa wake. "Mameneja Mpango wananipa hadithi za burudani na matangazo ya michezo ya kibiashara, jambo ambalo huathiri vibaya hatima yangu ya baadaye."

Markaan, ambaye sasa anafanya kazi katika Royal TV, alisema alijiunga na SWJ kwa matumaini kwamba yeye sawa na waliokuja wapya watapata msaada kushughulikia baadhi ya mambo haya.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 20290

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>