Mmiliki wa mtandao wa matukiodaima kulia akipunga mkono sanjari na mwandishi wa Mjengwa Blog na Kwanzajamii baada ya kuweka rekodi ya aina yake kwa wanahabari Iringa kwa kupanda mlima Kilimanjaro kutoka Getini hadi kituo cha kwanza cha Mandara kwa saa 1.45 badala ya masaa 3 kama ilivyokawaida huku mzee wa matukiodaima Bw Francis Godwin akishika nafasi ya kwanza kufika eneo hilo akifuatiwa na Daniel Mbega kutoka Mjengwa blog na Abukarim Mshana kutoka radio QBRATEN huku baadhi ya wanahabari kutoka Iringa wakishindwa kushuka na kulazimika kushushwa na gari la wagonjwa (AMBULENCE)
Pamoja na kudai mlima kilimanjaro upo Kenya,hapa wasnafunzi kutoka nchini Kenya wakipanda mlima Kilimanjaro sanjari na wanahabari Iringa kama walivyonaswa na kamera ya matukiodaima ,kama mlima yungekuwa Kenya si wangepanda mlima huu kupitia Kenya?
Vijana waongoza watalii katika mlima Kilimanjaro wakimsaidia kumshusha kutoka mlimani mmoja kati ya watalii watano kutoka nje ya Tanzanie aliyepoteza fahamu kwa kupanda mlima huo kama walivyokutwa na kamera ya matukiodaima wakiwa eneo la kituo cha kwanza cha MANDARA
Baadhi ya wanahabari kutoka mkoa wa Iringa wakiwa ktk picha kabla ya kuanza kupanda mlima Kilimanjaro.
katibu wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa Bw. Francis Godwin ama mzee wa matukiodaima wa pili kulia ,mwanahabari Abukarim Mshana wa radio Qbra Ten Fm na mwandishi wa Mjengwa BLOG kushoto wakipongezana na watalii wa nje baada ya kufanikiwa kuweka rekodi ya kupandisha mlima huo kwa mwendo wa kukimbia na kutumkia saa 1 .45 kutoka getini hadi kituo cha kwanza cha MANDARA badala ya masaa matatu na kushuka kwa dakika 45
Mwanahabari Mbega akiwa eneo la Mandara
Mzee wa matukio Daima kulia ambae aliongoza kupanda mlima Kilimanjaro akiwa na mpiga picha mkuu wa TANAPA Mussa Mandia ,Mwandishi wa Nuru Fm Victor Meena na mwandishi wa Mwananchi Iringa Hakim Mwafongo ambao walijitahidi kumfukuza mzee wa matukio daima ktk kupanda mlima Kilimanjaro
Bw Mussa Mandia akiweka sahihi kitabu cha wageni baada ya kufika kituo cha kwanza cha Mandara mlima Kilimanjaro
Mzee wa matukiodaima akipongezwa na waongoza watalii mlima Kilimanjaro baada ya kupanda mlima kwa muda mfupi zaidi