Hivi karibuni, Benki ya NMB imeukabidhi Uongozi wa shule ya msingi Makuburi Jeshini jijini Dar es Salaam msaada wa madawati yenye thamani ya shilingi million tano. Madawati ambayo yatasaidia kupunguza upungufu wa madawati katika shule hiyo.
Meneja wa NMB Mlimani City Bw. Leonard Ngaya (kushoto) akikabidhi sehemu ya madawati 55 yenye thamani ya shilingi milioni tano kwa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Makuburi Jeshini Bi. Stella Kaluse (kulia). Wakishuhudia makabidhiano hayo ni Mwenyekiti wa Kata ya Makuburi Bw. Moshi Kaftanyi (katikati) na Meneja wa NMB tawi la University Bw. Charles Mapunda .Hafla ya Makabidhiano haya ilifanyika hivi karibuni katika viwanja vya shulehiyo
Wawakilishi toka NMB pamoja na uongozi wa shule wakiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi baada ya kukabidhi madawati yaliyotolewa na benki ya NMB kwa ajili ya kupunguza uhaba wa madawati katika shule hiyo.Hafla ya makabidhiano ilifanyika katika viwanja vya shule ya makuburi jeshini hivi karibuni