Mwenyekiti wa CCM Taifa Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akifungua kikao cha siku moja cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kilichofanyika leo mjini Zanzibar ,pamoja na mambo mengine Kamati Kuu imeipongeza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, na wananchi wake kwa kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimtambulisha mgombea wa nafasi ya uwakilishi wa jimbo la Kiembesamaki Ndugu Mahmoud Thabit Kombo mara baada ya Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kumteua kuwa mgombea wa nafasi uwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki kwa tiketi ya CCM.
Picha na Adam H. Mzee