
Mshambuliaji wa Manchester United, raia wa Uholanzi, Robin Van Persie, amemtetea Kocha wake David Moyes kwa kusema kwamba anahitaji muda zaidi kujenga kikosi imara zaidi na cha ushindi.Manchester wakiwa chini ya Moyes,wanashikilia nafasi ya 7 katika ligi kuu ya Uingereza [English Premier League] huku wakiwa na kikosi ambacho hakina uhakika wa ushindi mara kwa mara kama ilivyokuwa enzi za kocha Alex Ferguson.
Van Persie ambaye yupo nje ya uwanja kwa mwezi mmoja kutokana na kusumbuliwa na misuli ya kwenye paja amesema, “ Moyes anahitaji muda zaidi.Bado ni mgeni. Kocha wetu ndio kiongozi wetu na nina uhakika atabadilisha uelekeo hivi karibuni”. Katika mahojiano hayo na BBC Van Persie aliongeza kwamba, “ Tumeshapoteza pointi nyingi sana katika msimu huu lakini tunajitahidi kufanya kila linalowezekana kubadilisha hali hiyo”
Mpaka hivi sasa Moyes hajawaridhisha mashabiki na viongozi wa club hiyo ya jijini Manchester japokuwa tangu achukue mikoba ya Ferguson ameshinda Kombe La Ngao Ya Jamii mwezi August. Bado hajajishinda kombe lolote la maana kitu ambacho mashabiki wa Man U wanasema “walishazoea”