Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizindua rasmi mwongozo mpya wa huduma za kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, (PMTCT OPTION B+) kwa Mkoa wa Dar es Salaam katika sherehe iliyofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere tarehe 22.1.2014.
Washiriki waliohudhuria sherehe za uzinduzi wa mwongozo mpya wa huduma za kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto wakisikiliza na kushangilia hotuba ya uzinduzi iliyokuwa ikitolewa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete aliyekuwa Mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo uliofanyika kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere tarehe 22.1.2014.