Polisi inasema ililazimika kutumia gesi ya kutoa machozi baada ya ghasia zilizotokea ndani na nje ya msikiti huo. Polisi inasema Msikiti huo wa Mussa unatumiwa kama kituo cha kueneza fikra na misimamo ya makundi yenye misimamo mikali.
Vilevile maafisa wa Kenya wanadai kuwa msikiti huo unatumia kusajili wapiganaji a kundi la al Shabab la Somalia.
Hata hivyo makundi ya kutetea haki za binadamu yameikoa utendaji wa polisi katika tukio hilo.

Vijana waliotiwa mbaroni baada ya police kuvamia Msikiti wa Musa, jijini Mombasa
Watu walioshuhudia wanasema waliona maiti za watu wawili waliopigwa risasi na polisi na kwamba makumi ya Waislamu waliokuwa katika msikiti huo wametiwa nguvuni.
Mkurugenzi Mtendaji wa kundi la kutetea haki za binadamu la Haki Africa lenye makazi yake Mombasa, Khalid Hussein amesema polisi haikuwa na haja ya kutumia nguvu ziada kwa ajili ya kukabiliana na watu waliokuwa msikitini hapo. Hussein amesema polisi ilipaswa kuwa na uvumilivu kwa ajili ya kuzuia umwagaji damu.
