Quantcast
Channel: MATUKIO NA VIJANA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 20290

WANAMUZIKI WATAKAOSHIRIKI TAMASHA LA PASAKA KUPIGIWA KURA NA MASHABIKI

$
0
0
1Bw. Alex Msama Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa Tamasha la Pasaka akizungumzia maandalizi ya tamasha hilo ambapo amesema utaratibu wa kuwapata waimbaji katika tamasha hilo mwaka huu waimbaji wote watakaoshiriki watapigiwa kura na mashabiki wa muziki wa injili ili kuleta ushindani kati ya waimbaji, lakini pia kuwaachia mashabiki wenyewe wachague ni mwimbaji gani wanamuhitaji katika tamasha hilo badala ya kutumia utaratibu wa mwanzo.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)2Bw. Alex Msama Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa Tamasha la Pasaka akisisitiza jambo wakati alipokuwa akihojiwa na waandishi wa habari kutoka TV Tumaini ya jijini Dar es salaam.
3Tamasha la Pasaka ndiyo tamasha pekee kubwa la muziki wa inijili linalofanyika kila mwaka nchini Tanzania likishirikisha waimbaji mbalimbali kutoka ukanda wa Maziwa Makuu, Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika na limekuwa ni kivutio kikubwa kwa mashabiki na wapenzi wa muziki wa injili.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 20290

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>