Quantcast
Channel: MATUKIO NA VIJANA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 20290

BREAKING NEWZZZ : BUNGE LAAHIRISHWA KUTOKANA NA HOTUBA YA CHADEMA

$
0
0
Naibu Spika Wa Bunge Mh Job Ndugai Amelihairisha bunge mchana huu kabla ya muda wake mara baada ya kutokea mgongano.Hali hiyo imesababishwa na hotuba ya msemaji mkuu wa upinzani bungeni ya ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa iliyokuwa inasomwa na Mbunge wa chadema Mh Ezekia Wenje ambayo ilikuwa ina maneno yasiopendeza kwa chama cha wananchi CUF.

Wakati Mh Ezekia Wenje akisoma hotuba hiyo ndipo mbunge wa cuf kutoka zanziba Mh Masoud aliposimama Kuomba mwongozo wa Spika na  Ndipo Naibu spika Mh Job Ndugai kumpana nafasi .Katika maelezo yake Mh Masoud alisema hotuba hiyo ni ya kihuni na inaizalilisha chama cha CUF ,Ndipo Naibu Spika alipompa nafasi Mh wenje ajitetet wakati anafanya hivyo ndipo wabunge kutoka chama cha CUF waliposimama wakipinga hotuba hiyo na kutaka waombwe radhi hali iliyolazimu naibu spika kuliahirisha bunge mpaka saa 11 jioni ya leo na ametisha kamati ya bunge ya maadili kukutana mara moja kujadili hotuba hiyo

Viewing all articles
Browse latest Browse all 20290

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>