![Msofe na Nanyaro Msofe na Nanyaro]()
Nanyaro anasema wakiwa wanawashauri mgambo hao, ghafla walishangaa na yeye amezingirwa na kuanza kupigwa sambamba na Msofe huku mgambo hao wakiwaeleza Madiwani hao kuwa wamekuwa na kiherehere sana.
Hatua za kisheria dhidi ya mgambo hao
Hadi tunaandika taarifa hii, Madiwani hao walikuwa wanaandaa utaratibu wa kushughulikia swala hilo wakidai kwamba mgambo hao wameonesha utovu mkubwa wa nidhamu na ukiukwaji wa sheria kwa kuwapiga waajiri wao. Msofe na Nayaro wamelaani vikali tukio hilo na kuahidi kufuatilia ili sheria ichukue mkondo wake na iwe fundisho wa wengine.