Mwanadada ''Nisha'' Msanii maahiri kutoka swahili wood Anaekuja kwa kasi ya juu katika tasnia ya filamu hapa nchini Leo Amefanya mahojiano na masainyotambofu.blogspot.com kuhusu Shoping aliowafanyia wafanyakazi wake hivi majuzi, alisema hivi: yaani nikwamba hii shopping ilikuwa ya kuwapongeza wafanya kazi wa kampuni yangu nishaz film production kwa kumaliza vizuri filamu yangu ya ''tikisa'' ambayo itatoka mwisho wa mwezi huu naomba mashabiki wangu wakaemkao wa kula na hiyo shopping nimefanya kwenye duka la ''hussen pamba kali'' lililoko maeneo ya kinondoni, Kwa kweli nna imani kazi hii ikitoka wadau wangu wataifuhia kutoka na ubora wake, Nimeifanya kibunifu zaidi na mbali na hivyo nimeifanya kwa gharama ya juu na nilitumia muda mrefu kuitengeneza pia kabla sijaifanya nilikaa chini na watu kadha wa kadha wenye uelewa wa kutengeneza movie nikasikiliza maoni yao kuhusiana na kazi hii, kwa hio sina wasi wasi nayo kabisa mashabiki wangu isubirieni kwa hamu kwani imesheni mastar kibao wenye uwezo mkubwa wa kuigiza bila kusahau wachekeshaji nguli hapa nchini pia wamo. |