Waziri Mkuu wa Zimbabwe Bw. Morgan Tsvangirai amesema muda uliobaki ni mfupi mno kuweza kutimiza siku iliowekwa kwa ajili ya uchaguzi wa kitaifa nchini humo.
Ameongeza kusema kuwa mabadiliko ya msingi ya kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru na haki bado yanahitajika kutekelezwa.
Rais Robert Mugabe wiki iliyopita alisema atakubaliana na muda uliowekwa na mahakama ya katiba.
Uchaguzi huo utaashiria kumalizika kwa muungano ulioundwa na viongozi hao mwaka 2009 baada kura kuvurugiga.
Chama cha Movement for Democratic Change (MDC) cha Bw. Tsvangirai kiliungana na Zanu-PF cha rais Mugabe na kushirikiana kuunda serikali chini ya shinikizo la viongozi wa Afrika kwa nia ya kumaliza vurugu zilizodumu kwa muongo mmoja nchini Zimbabwe.