|
CHUO KIKUU CHA TUMAINI MAKUMIRA - TAWI LA MBEYA
S L P 3040, MBEYA
TANGAZO LA NAFASI ZA MASOMO YA KOZI ZA UALIMU
Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira Tawi la Mbeya ambacho awali kilijulikana kamaMbeya Lutheran Teachers’ College kinatangaza nafasi za masomo ya kozi ya Ualimu Ngazi ya Cheti,Stashahada na Shahada katika mwaka wa masomo 2013/2014.
1. Sifa za Mwombaji
a) Ngazi ya Cheti
i. Mwombaji awe amefaulu mtihani wa kidato cha Nne kwa kiwango kisichopungua daraja la nne alama ishirini na saba (27) katika mkao mmoja.
ii. Awe amehitimu Elimu ya Sekondari siyo zaidi ya miaka mitano iliyopita.
b) Stashahada
i. Mwombaji awe na ufaulu wa principle moja na Subsidiary moja katika masomo yanayofundishwa Shule za Sekondari. AU
Awe na Cheti cha daraja la tatu A chenye ufaulu wa wastani wa B au “Credit naDistinction”. AU
Awe na cheti cha daraja la Tatu A na uzoefu usiopungua miaka mitano kazini.
Angalizo:Waombaji wote wanaotumia cheti cha Ualimu Daraja la Tatu A wanatakiwa kuwa na ufaulu usiopungua “D” Tano katika mtihani wa kidato cha Nne.
c) Kwa muombaji wa Shahada (Degree) tembelea tovuti ya TCU na chagua TUMA-MBEYA yenye code number MKM01 AU MKM02.
2. Namna ya kutuma maombi.
(a) Fomu za maombi zinapatikana katika Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira tawi la Mbeya kilichopo Uyole. Au tembelea katika tovuti yetu www.shuco.ac.tz.
(b) Mwombaji anatakiwa alipie Tshs. 30,000/= kama gharama za maombi katika akaunti namba:
ELCT-MLTC Computer Building Project (CRDB): 0152421083000
(c) Barua iambatanishwe na Vivuli vya Vyeti vya kuhitimu Elimu ya Sekondari na Chuo.
(d) Waombaji waliosoma Nje ya Nchi wawasilishe Vyeti vya Baraza la Mitihani laTanzania ili vipatiwe utambulisho (kupasishwa).
(e) Hati halisi ya malipo (Pay in Slip) iambatanishwe kwenye barua ya maombi.
3. Muda wa mafunzo
Kozi ya Cheti na stashahada zitatolewa kwa muda wa miaka miwili na kwa kozi za shahada ni miaka mitatu.
KWA NGAZI YA CHETI NA STASHAHADA MASOMO YATAANZA RASMI TAREHE 08/07/2013
4. Maombi yote yatumwe kwa
Mratibishaji wa masuala ya Taaluma
Chuo Kikuu Tumaini Makumira - Kituo cha Mbeya
S.L.P. 3040 MBEYA.
Simu no: + 255 25 2510450
+255 0655 858 527/+255 753 817 274
Nukushi: + 255 25 2510094
Tovuti: www.shuco.ac.tz
Barua pepe: tumashuco2012@gmail.com