Makundi ya waokoaji yanaendelea kuwatafuta watu walionusurika katika mafuriko yaliotokea katika jimbo la Uttarakhand nchini India, huku maafisa wakisema karibu watu 300 wamekufa.
Taarifa zinasema zaidi ya watu 13,800 wamepotea na wengine 62,800 wangali wamekwama katika maeneo hayo karibu na miji ya shughuli za hija za waumini wa kihindu ya Badrinath na Kedarth.
Picha za televisheni zimeonyesha watu wakipanda mabonde, huku wakisaidiwa na wanajseshi.
Hadi sasa karibu watu 56,000 tayari wameokolewa. -DW.