Rami-Hamdallah
Ofisi ya Waziri mkuu wa Palestina Rami Hamdallah (Pichani) imethibitisha kwamba Waziri Mkuu huyo amewasilisha barua ya kujiuzulu.
Hatua hiyo inakuja wiki mbili baada ya msomi huyo anayeheshimika kushika wadhifa huo.
Ofisi ya Waziri Mkuu ilitangaza awali kwamba amejiuzulu kwa sababu ya mvutano kuhusu madaraka yake.
Haikuweza kufahamika kama Rais Mahmoud Abbas ameukubali uamuzi wa Bw. Hamdallah ambaye alichukuwa wadhifa wa Waziri Mkuu kutoka kwa mtangulizi wake Salam Fayyad, aliyejiuzulu mwezi Aprili.
Hata hivyo Hamdallah hakuwa na azma ya kushika wadhifa huo kwa muda mrefu, akisema mara baada ya kuteuliwa, atatawala kwa kipindi cha mpito hadi serikali ya Umoja wa kitaifa kati ya chama cha Abbas cha Fatah na kile cha Hamas kinachotawala ukanda wa Gaza, itakapoundwa.