
Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani Tanzania,Mohamed Mpinga akiongea na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Mapambano , kuhusiana na masuala ya Usalama Barabarani katika kuadhimisha wiki ya Umoja wa Mataifa ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambayo huadhimishwa Mei 6 hadi 12 ,ambapo wafanyakazi wa vodacom waliambatana na mkuu huyo katika kutoa elimu kwa watoto wa shule hiyo na Uzuri zote za Sinza jijini Dares Salaam na kutoa msaada wa madafutari na vitabu mbalimbali vya kujisomea,anaeshuhudia kulia ni Meneja uhusiano wa nje wa Vodacom Tanzania,Bw.Salum Mwalim.

Meneja wa Vodacom anaye husika na masuala ya elimu Grece Lyon akimkabidhi mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi ya Uzuri Tandale jijini Dar es Salaam, Vitabu vya Sayansi wakati wa Maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Mataifa ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambayo huadhimishwa Mei 6 hadi 12 ,ambapo wafanyakazi wa vodacom waliambatana na mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani Tanzania,Mohamed Mpinga (hayupo pichanini).
Vodacom yaungana na UN wiki ya nenda kwa usalama
Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom nchini, leo inaungana na Shirika la Umoja wa Mataifa chini ya Shirika la Afya Duniani, Makamishna wa Kanda wa Umoja wa Mataifa na Wadau mbalimbali wa masuala ya Usalama Barabarani katika kuadhimisha wiki ya Umoja wa Mataifa ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambayo huadhimishwa Mei 6 hadi 12 kila mwaka duniani kote.
Aidha, katika maadhimisho hayo, yenye kauli mbiu "Usalama wa Waenda kwa Miguu" na ambayo yanafanyika kwa msaada wa Shirikisho la Kimataifa la Mashindano ya mbio za Magari (FIA), lengo hasa ni kutoa elimu kwa watumiaji wa vyombo vya usafiri na watembea kwa miguu juu ya tahadhari wanazopaswa kuchukua wawapo barabarani.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkuu wa Kitengo cha Vodacom Foundation,Bw.Yessaya Mwakifulefule, alisema katika maadhimisho hayo wanatarajia kutoa huduma kadhaa zikiwemo uwezeshaji wa mafunzo ya elimu ya usalama barabarani, na ugawaji wa zawadi za vitabu kwa wanafunzi wa shule za msingi Tandale Uzuri na Mapambano, jijini Dar es Salaam.
"Ajali za barabarani zinaongezeka kwa kasi na kusababisha upotezaji wa nguvu kazi huku zikiacha maafa makubwa kwa taifa, ni jukumu la kila Mtanzania kuwa sehemu ya kusimamia na kuzingatia sheria za barabarani huku tukijikita zaidi kuchukua tahadhari kwa waenda kwa miguu kama kauli mbiu ya mwaka huu inavyotuagiza," alisema Mwakifulefule na kuongeza:
Kama Vodacom na Vodafone duniani kote tumeichagua siku hii kati ya siku saba za mwendelezo wa maadhimisho haya, ili kujumuika na makundi mbalimbali ndani ya jamii, katika kuelimishana na kubadilishana mawazo, kwa mantiki ya kila mmoja kuchukua tahadhari, sanjari na kuzungumza na wanafunzi ambao hasa wengi wao hupata madhara ya kuuawa na kujeruhiwa kutokana na kugongwa na vyombo vya usafiri wawapo barabarani,"
Aidha, alibainisha kuwepo kwa ongezeko la vifo vya watembea kwa miguu vinavyotokana na ajali za barabarani kila siku, huku akisisitiza kuwa ni kadhia inayoleta simanzi na kusababisha kupotea kwa nguvu kazi ya taifa, sambamba na kuwasihi watanzania kila mmoja kutoa sauti itakayosaidia kupunguza maafa hayo na ajali nyingine za barabarani kama kauli mbiu ya mwaka huu inavyotuagiza
Kamuhanda, akizungumza kwa niaba ya Vodacom na Vodafone duniani, alisema inapaswa kueleweka kuwa tafiti zilizopo zinaonesha zaidi ya watembea kwa miguu laki 3, sawa na robotatu ya watu milioni 1.3 duniani kote hufa na wengine kujeruhiwa katika barabara mbalimbali duniani kwa mwaka, huku wengine wapatao 5000 ambao wengi wao ni watoto hufariki kila wiki kutokana na kugongwa na vyombo vya usafiri duniani.
"Hivyo tunaamini kwa kutumia njia ya elimu na hamasa juu ya masuala ya usalama barabarani ni dhahiri itakuwa njia bora na rahisi katika kufikisha ujumbe" alisema Mkuu huyo wa Kitengo cha Mahusiano ya jamii na Mawasiliano Vodacom Tanzania.
Mwisho ...CHANZO:MATINA NKURLU.