Quantcast
Channel: MATUKIO NA VIJANA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 20290

Waumini wa kishia wauawa Misri

$
0
0

Umati wa washambuliaji walijaribu kuiteketeza nyumba walimokuwa viongozi wa kishia
Kiongozi wa madhehebu ya kishia nchini Misri ametoa wito wa kimataifa kuwa waumini wa kishia walindwe , siku moja baada ya viongozi wa kishia kuuawa karibu na mji mkuu wa Misri, Cairo.
 serikali ya Misri imekosa kulinda jamii ya kishia kwa sababu haiwezi hata kujilinda yenyewe.
Maafisa wanasema kuwa shambulizi hilo lililotokea Jumapili, lililenga kundi la waumini waliokuwa wamekusanyika kwa maombi.Waisilamu wanne wa kishia waliuawa nchini Misri baada ya kuvamiwa na kundi la watu katika kijiji kimoja mjini Cairo.
Washambuliaji waliwatuhumu waliokuwa wamekusanyika kwa kujaribu kueneza imani za kishia.

Idadi ya waisilamu wa kishia ndogo sana ikilinganishwa na wasunni nchini Misri, lakini matamshi ya kupinga washia yameongezeka hivi karibuni kwa sababu ya mgogoro wa Syria.
Walioshuhudia shambulizi hilo,  kundi la watu wanaowapinga washia na ambao idadi yao ilikuwa watu miamoja, walikusanyika na kuizingira nyumba hiyo.
Kisha wakawataka washia kuondoka katika nyumba hiyo kabla ya kuivamia na kuiteketeza.
Picha za mashambulizi hayo, zinaonyesha waathiriwa wakibururwa kwenye barabara za mji.
Mmoja wa waliouawa alikuwa kiongozi wa kishia Hassan Shehata.
Maafisa wanasema kuwa watu wengine wanane walijeruhiwa kwenye shambulizi hilo.
Afisaa mmoja katika wizara ya afya nchini humo , aliambia shirika la habari la Mena kuwa miili ya waathiriwa ilionyesha majeraha mabaya zaidi.
Sawa na katika nchi zengine, katika eneo hilo, matamshi yanayopinga washia yamekuwa yakisikika sana nchini Misri, kwa sababu ya vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria nchi ambayo imekuwa na sifa ya mapigano ya kidini.
Mapema mwezi huu, mhubiri mmoja wa kidini aliwaasa waisilamu wa Sunni kwenda Syria kusaidia katika vita dhidi ya utawala wa rais Bashar al-Assad

Viewing all articles
Browse latest Browse all 20290

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>