Pili Pili, mwanaume wa Kenya ambaye anamiliki nyumba kadhaa za bati katika makazi duni ya Tudor Moroto mjini Mombasa, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hofu yake ya kufukuzwa na mamlaka ya halmashauri ya mji.
Maurice Omondi alikuwa fundi seremala katika Mtaa wa Ayany wa Kibera hadi Novemba mwaka jana mwaka uliopita wakati mamlaka ya jiji ilipovamia ghafla biashara zake na kumlazimisha kufunga.
Alisema maofisa kutoka Halmashauri ya Jiji la Nairobi walichukua vifaa vyake vyote na samani zilizokuwa zimekamilika ambazo zilikuwa zikisubiri kuchukuliwa na wateja baada ya kushindwa kuonyesha leseni ya biashara.
"Kutoka uvamizi huo, maisha yangu hayako kama yalivyokuwa mwanzo. Nimelazimika kuchagua kazi za utumishi kupata mahitaji," alisema Omondi, mwenye umri wa miaka 35, ambaye sasa anafanya kazi kama kibarua katika maeneo ya ujenzi.
Alisema angepenga kuanza tena biashara yake ya useremala lakini hayo yote yanategemea kama atapata vifaa vyake na fidia yoyote kwa hasara aliyopata, ambayo ataitumia kama mtaji wa kuanzia.
"Nimeshafuatila suala hili mara kadhaa kwenye mamlaka za jiji lakini hakuna maendeleo yoyote, ukiunganisha na ukweli kwamba siwezi kumudu kuwa na mwanasheria ili tuweze kuishitaki mamlaka na kupata haki katika mahakama" alisema. "Nimekubali hatma yangu." Kesi ya Omondi ni mfano halisi wa kile ambacho Wakenya wengi wanapitia wakati wanapotafuta haki nchini Kenya.
Upatikanaji ulio sawa wa sheria na haki ya huduma za kisheria za bure vimewekwa katika katiba ya Kenya. Pia inaeleza kwamba raia waarifiwe haki yao ya wakili wa utetezi, na atolewe kwa mlalamikiwa na serikali kama inahitajika.
Hata hivyo, haki hizi wakati huwa hazipatikani wakati wote kwa watu wa Kenya walio masikini na waliosahaulika, alisema Getrude Angote, mkurugenzi mtendaji wa Kituo cha sheria cha Kenya (Kituo cha Uwezeshaji Sheria cha Kenya).
Angote alisema Wakenya wengi wenye uwezo wa kupiga kura wanayimwa haki zao za huduma za msingi, zinazoondolewa katika majumba, ardhi na biashara zao, na kutishiwa kupitia kwa watu matajiri na maarufu katika jamii.
"Huu ni mwelekeo unaotia hofu ambao una matokeo hasi katika maendeleo ya jumla ya nchi," aliiambia Sabahi. "Akiondoa asilimia kubwa ya idadi ya watu kutoka katika utawala wa sheria kwa kutowapa kimsingi upatikanaji ulio sawa wa haki ikimaanisha hawana nafasi sawa za kuboresha maisha yao hadi kuondokana na umasikini."
'Mamilioni wanahitaji huduma za kisheria'
Mwanasheria Mkuu Njee Muturi alikiri kwamba tatizo hilo lipo katika nchi, lakini alisema "litabadilika katika miezi inayokuja."
"Wakenya wachache sana wanaohitaji huduma za kisheria wanaweza kumudu kuzilipia, na wengi wao hawajui haki zao za kisheria," Muturi aliwaambia waandishi wa habari tarehe 20 Januari. "Watu ambao hawajui haki zao za kisheria hawawezi ama kudai wala kutekeleza haki hizo. Mamilioni wanahitaji huduma za kisheria lakini hawawezi kumudu elimu maalumu na ujuzi wa wataalamu wa sheria."
Hadi kufikia Agosti, Muturi alisema, serikali inapanga kuanzisha programu ya bure ya msaada wa kisheria ambayo italenga Wakenya masikini na watu waliosahaulika.
Alisema Ofisi ya Mwanasheria Mkuu na Wizara ya Sheria ziliunda Msaada wa Sheria Kitaifa na Programu ya Uelimishaji ambayo iliandaa rasimu ya Mswada wa Msaada wa Kisheria na rasimu ya Sera ya Msaada wa Sheria Kitaifa na Uelimishaji mwaka 2013.
Rasimu zote mbili zinapitiwa na Tume ya Usimamizi wa Katiba na zinatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Agosti, alisema.
"Rasimu ya mswada huo inahusisha haki ya kikatiba ya mashtaka halali kwa watu wote walioshutumiwa na itasaidia katika utekelezaji wa sheria ya kikatiba kuhusu haki ya mashtaka halali mahakamani," Muturi aliiambia Sabahi. "Inafanya hivi kwa kutumia muundo wa kisheria na kiasasi kwa ajili ya kutoa msaada wa huduma za kisheria nchini Kenya na baadaye kupendekeza ugatuaji wa madaraka ya huduma za kisheria katika kaunti na kaunti ndogo kulingana na Ibara ya 6 (3) ya katiba kuhusu kupatikana kwa huduma."
Kuhamasisha utawala wa haki na utawala wa sheria na kuimaisha upatikanaji wa haki ni miongoni mwa kazi za kikatiba na vipaumbele vya ofisi ya Mwanasheria Mkuu na Wizara ya Sheria, alisema.
Dira ya mwaka 2030 ya Kenya inaeleza kwamba kukua kwa uchumi peke yake hakutoshelezi kukamilisha uinuaji mzuri katika ubora wa maisha ya maskini, watu waliosahaulika na watu wanaoishi katika mazingira magumu, alisema. Dira inabainisha kukosekana kwa upatikanaji wa haki kwani kuna uhusiano wa moja kwa moja katika umaskini na, kimsingi, inatambua uhitaji wa upatikanaji wa haki na mhimili wa maendeleo ya uchumi na kupunguza umaskini.
"Nguzo wa kisiasa uliodhamiriwa katika Dira hii kuhusu vipengele mbalimbali vya haki za binadamu na utawala wa sheria ili kuhakikisha utawala bora na uwajibikaji," alisema Muturi. "Msaada wa kisheria ni nyenzo muhimu katika kuimarisha upatikanaji wa haki, hususan kwa maskini, waliotengwa na wanaoishi kaika mazingira magumu."
Muturi alisema serikali imekuwa ikiendesha programu sita za majaribio ya msaada wa kisheria huko Nairobi, Mombasa, Kisumu na Eldoret. Alisema changamoto ya msingi inayoikabili programu ilikuwa ni kukosekana kwa maelekezo ya sera, uungaji mkono au ukaidi wa sheria wa wadau wote watakaohusishwa.
"Lakini tumejifunza somo letu na kuanza mabadiliko ya sheria pamoja na kufikia wadau wote, hivyo tunapoendelea na programu [kitaifa] mwezi Agosti vitaendeshwa kwa pamoja," alisema, akiongeza kwamba, Mahakama, wizara za serikali, Vyuo vikuu, Jumuiya ya Kisheria ya Kenya Kenya na asasi za kiraia zote zimekubaliana kushirikiana.
Roselyne Aburili, ofisa kaimu mkuu wa sheria katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, alisema uanzishaji wa programu ya taifa ya msaada wa kisheria utawawezesha kufanya kampeni nyingi za kujenga uelewa wa haki za watu na kubadilisha mifumo ya utatuzi wa migogoro.
"Hili litafanya baadhi ya kesi kushughulikiwa katika ngazi ya jamii kupitia usuluhishi, [kuliko] kuishia mahakamani, hivyo kupunguza kesi zinazosubiri…ikifanya utoaji wa haki kwa haraka," aliiambia Sabahi.
Source: sabahionline.com