Quantcast
Channel: MATUKIO NA VIJANA
Viewing all 20290 articles
Browse latest View live

MBWANA SAMATTA NA THOMAS ULIMWENGU KUTUA DAR JUMAMOSI KUICHEZEA TAIFA STARS DHIDI YA ZIMBABWE

$
0
0

 http://kandanda.galacha.com/wp-content/uploads/2014/04/Samata.jpg

Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
RAIS wa shirikisho la soka nchini Tanzania, Jamal Malinzi imepigana kiume kuwasiliana na mwenyekiti na mmiliki wa klabu ya TP Mazembe, Moise Katumbi  na taarifa njema juu ya mawasiliano hayo ni kwamba washambuliaji wawili wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta na Thomas Ulimwengu watawasili jumamosi mchana kwa ajili ya mchezo wa jumapili.
Taarifa za uhakika kutoka ndani ya TFF zinaeleza kuwa Rais Malinzi amethibitisha ujio wa wanandinga hao tegemeo kwa Taifa stars na kuibua matumaini ya Taifa stars kufanya vizuri kwasababu Samatta na Ulimwengu ni wachezaji mahiri zaidi kwa sasa.
Nyota hao wawili watatumiwa kwa mara ya kwanza na kocha wa Taifa stars, Mart Nooij katika mechi ya raundi ya awali kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika mwakani nchini Morocco dhidi ya Zimbabwe kwenye uwanja wa Taifa, jijini Dar es salaam.
 http://1.bp.blogspot.com/-eS4uaRKjA4Y/UjWrRwt7Y3I/AAAAAAAAwC4/jFrQDx9PAbE/s640/1.jpg
TP Mazembe aliwazuia wachezaji hao kuja Tanzania kwasababu wanawahitaji katika michezo ya makundi ya ligi ya mabingwa barani Afrika.
Matajiri hao wa DRC walipo kundi         A wanatarajia kucheza mechi ya kwanza  dhidi ya El Hilal Omduran siku ya ijumaa mjini Khartoum nchini Sudan, hivyo baada ya mechi hiyo wachezaji hao wa Tanzania watatua nchini jumamosi na kucheza mechi siku ya jumapili.
Hata hivyo baada ya mechi hiyo watakwea pipa kuelekea Lubumbashi DRC tayari kwa maandalizi ya mechi ya pili dhidi ya mahasimu wao AS Vita mei 25 mwaka huu.
Baada ya mechi hiyo na AS Vita ambapo wiki iliyopita walikutana nao katika mchezo wa mwisho wa ligi kuu ya DRC na kushuhudia vurugu kubwa ziliosababisha watu zaidi ya 15 kupoteza maisha, Samatta na Ulimwengu wataweza kupata nafasi ya kucheza mechi ya marudiano na Zimbabwe mjini Harare.

BRAZIL YAITA 23 KOMBE LA DUNIA, WAKONGWE KIBAO WAPIGWA CHINI

$
0
0

KOCHA Luis Felipe Scolari ametaja wachezaji 23 kwa ajili ya Kombe la Dunia akijumuisha wachezaji sita wanaocheza Ligi Kuu ya England, ingawa amewaacha nyota wawili wa Liverpool, Lucas na Philippe Coutinho.

KIKOSI CHA BRAZIL KOMBE LA DUNIA;

Makipa: Julio Cesar (Toronto FC, on loan from QPR), Jefferson (Botafogo), Victor (Atletico Mineiro)
Mabeki: Dani Alves (Barcelona), Maicon (Roma), David Luiz (Chelsea), Thiago Silva (PSG), Dante (Bayern Munich), Marcelo (Real Madrid), Henrique (Napoli), Maxwell (PSG).
Viungo: Oscar (Chelsea), Fernandinho (Man City), Willian (Chelsea), Paulinho (Spurs), Ramires (Chelsea), Luis Gustavo (Wolfsburg), Hernanes (Inter Milan).
Washambuliaji: Bernard (Shakhtar Donetsk), Neymar (Barcelona), Fred (Fluminense), Hulk (Zenit St Petersburg), Jo (Atletico Mineiro).
Wanapewa nafaso: Brazil wanapewa nafasi kubwa ya kubakiza Kombe nyumbani

JULIO AOMBA URAIS SIMBA SC NA 'KUMFUNGULIA MASHITAKA' RAGE

$
0
0

 http://3.bp.blogspot.com/-PjQ4FgLijBw/UXQryqyH9BI/AAAAAAAAA88/V9r5OyHV3hE/s1600/kiwelu.jpg

MCHEZAJI na kocha wa zamani wa Simba SC, Jamhuri Mussa Kihwelo ‘Julio’ amechukua na kurudisha fomu ya kugombea Umakamu wa rais wa klabu hiyo- lakini pia akasema yeye bado ni kocha halali wa timu hiyo.
Julio amechukua fomu ya kuwania umakamu wa Rais kwenye uchaguzi wa Juni 29, mwaka huu na akasema ataushitaki uongozi unaomaliza muda wake chini ya Mwenyekiti Alhaj Ismail Aden Rage kwa kumdhulumu haki yake.
Akizungumza  leo Julio alisema anaudai uongozi unaomaliza muda wake milionI 24 kama fedha za mshahara. Aliema tayari amekwenda mahakamani kuwasilisha malalamiko yake kuhusu fedha hizo.
Julio kikao kilichowatoa madarakani kilikaa chini  ya makamu mwenyekiti Joseph Itang’are kilikuwa batili.
 “Mimi bado ni kocha wa Simba kwa kuwa uongozi uliompindua Rage kikao chake kilikuwa sio haliali na mimi bado ni kocha halali wa timu hiyo.
Alisema Rage alirudishwa madarakani na rais wa TFF Jamal Malinzi kwa kusema kikao hakikuwa halali sasa na sisi pia ni makocha halali.
Chanzo:  Bin zubeiry

GIGGS AKUTANA NA VAN GAAL KUJADILI HATIMA YAKE MAN UNITED

$
0
0

Talks: Ryan Giggs (pictured with wife Stacey in Manchester) was in Holland for a meeting with Louis van Gaal

Showdown: Giggs was to meet with Van Gaal for crunch talks over his Manchester United future
 Giggs  alitakiwa kukutana na Van Gaal kujadili hatima yake ya baadaye katika klabu ya Man United

Meeting point: Noordwijk's Hotel van Oranje was the destination of choice for the pair
Sehemu ya mkutano: Hoteli ya Van Orange mjini, Noordwijk ndio sehemu ambayo Giggs alitakiwa kukutana na Van Gaal.
Classy establishment: Inside the hotel where Giggs was holding his talks with the Holland manager
Incoming: Van Gaal, expected to be announced as United boss this week, will talk with Giggs about his role
Mtarajiwa: Van Gaal anatarajiwa kutangazwa kuwa kocha wa Man United wiki hii.

ANGALIA PICHA KIJANA AKIPEWA KIPIGO KATIKA MKUTANO WA UKAWA MOROGORO

$
0
0

Njemba huyo akipokea kichapo kutoka kwa wafuasi wa Ukawa mkoani Moro.
NJEMBA mmoja amepokea kipigo kikali kutoka kwa wafuasi wa Ukawa waliokuwa na mkutano mkoani Morogoro jioni hii baada ya kudaiwa kuwa miongoni mwa waliomteka Mbunge Rose Kamli wakati wa kampeni jimboni Kalenga, mkoani Iringa.
Njemba huyo ambaye hakufahamika jina lake mara moja, aliangushiwa kipigo baada ya kuibuka na kuanza kumpiga picha Mwenyekiti wa Bavicha Taifa, John Heche. Baada ya kipigo cha nguvu, njemba huyo alinusuriwa na polisi waliomchukua kumtoa mikononi mwa wafuasi hao.
Mwenyekiti huyo wa Bavicha akithibitisha kumtambua kijana huyo anayedaiwa kushiriki kumteka mbunge wao kwenye uchaguzi mdogo uliofanyika Jimbo la Kalenga, lringa.
(PICHA NA DUSTAN SHEKIDELE / GPL, MOROGORO)

POLISI WAMGUNDUA KINARA WA MTANDAO WA WIZI KATIKA MABENKI JIJINI D’SALAAM

$
0
0

Kamishna kova leo alipoamua kuitoa hadharani picha ya mtuhumiwa huyo mbele ya wanahabari ili apatikane mara moja

Jeshi la Polisi Kanda Maalum D’Salaam limefanikiwa kumbaini mtuhumiwa mhimu ambaye ni kinara wa mtandao wa wizi katika mabenki ambaye anajulikana kwa jina la RONALD S/O MOLLEL umri miaka 37, mfanyabishara na mkazi wa Kimara Bonyokwa Jijini D’salaam.
          
           Mtuhumiwa huyu amekimbilia mafichoni mara baada ya tukio la ujambazi katika Tawi la Benki ya Barclays  Kinondoni lililotokea tarehe 15/4/2014 ambapo majambazi walifanikiwa kupora kiasi kikubwa cha fedha T.Shs.390,220,000/= , USD 55,000/= na EURO 2150/=.  Aidha sasa imefahamika kwamba mtuhumiwa huyu ni mume wa mtuhumiwa wa kwanza katika tukio la Barclays Benki aitwaye ALUNE D/O KASILILIKA @ ALUNE D/O MOLLEL , miaka 28,  Mkazi wa Kimara Bonyokwa ambaye ni Meneja wa Benki Tawi la Barclays Kinondoni.  Mtuhumiwa Mollel anatafutwa kwa kila hali kwa vile yeye ndiye alikuwa kinara wa kupanga tukio hilo la Barclays na mara baada ya tukio ametoroka na kiasi kikubwa cha fedha hizo zilizoibiwa.


RONALD S/O MOLLEL ambaye ndiye mtuhumiwa wa ujambazi katika mabenk mbalimbali hapa jijini dar es salaam
Zipo taarifa za kuaminika kuwa mtuhumiwa huyu amekuwa akipanga na kushiriki kikamilifu katika matukio mbali mbali ya uhalifu mkubwa ikiwa ni pamoja na kuongoza vikundi vya majambazi vilivyowahi kupora katika mabenki mbali mbali katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.  Mtuhumiwa huyo ni hatari kwani ana mtandao na watumishi muhimu katika matawi mbali mbali ya mabenki kwa lengo la kufanikisha uhalifu katika mabenki hayo.


Endapo utamona mtu huyu toa ripot mahali popote hata kwa mmiliki wa blog hii
Jeshi la Polisi limelazimika kutoa picha yake hadharani kwa kutumia dhana ya ulinzi shirikishi ili mtuhumiwa huyu akionekana akamatwe na taarifa zitolewe katika kituo chochote cha Polisi ikiwa ni lengo la polisi kupambana na uhalifu katika dhamira ya kuzuia uhalifu, kulinda maisha na mali za wananchi.   

    Zawadi nono ya fedha taslim itatolewa kwa siri kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa zitakazosaidia kukamatwa kwa mtuhumiwa huyu.  Pamoja na maelezo hayo mtuhumiwa mwenyewe sasa anapewa fulsa ya kujisalimisha katika kituo chochote cha polisi kabla ya kukamatwa kwa njia nyingine.

ANGALIA PICHA YA MWANAUME ALIYEHAI MWENYE MIAKA MINGI ZAIDI DUNIANI.

$
0
0
Dr_Alexander_Imich-main   
Guinness World Records wamethibitisha kuwa Dr. Alexander Imich wa mjini New York ndio mwanaume aliyehai mwenye miaka mingi zaidi duniani. Dr Imich anamiaka 111.
Dr. Imich amezaliwa February 4th, 1903. Mwaka 1951, Imich na mke wake walihamia Marekani kutokea Soviet Union na kuishi Manhattan akiwa mwenyewe toka mke wake afariki mwaka 1986.
Aliyekuwa akishikilia rekodi hii amefariki ni Arturo Licta wa italia, alifariki April 24th akiwa na miaka 111 na siku 357.

Dr-Alexander-Imich-with-Stuart-Claxton_500x333Misao Okawa wa Japan mwenye miaka  116 yupo kwenye rekodi ya Guinness kama binadamu aliyeishi miaka mingi zaidi duniani. Alizaliwa March 5, 1898 na anaishi Osaka.
Fahamu binadamu aliyewahi kuishi miaka mingi zaidi na kuweka rekodi liishi miaka 122 na siku 164. Alikuwa Jeanne Louise Calment wa Ufaransa.
credit : sam misago

HATIMAYE YULE MWANARIADHA WA SOUTH AFRIKA INAYOSEMEKANA ANA JINSIA MBILI ANATAKA KUMUONA GIRLFRIEND WAKE

$
0
0
Caster Semenya akiwa Violet Rasebova
Mwanariadha wa kike wa South Africa ambaye pia mshindi wa Medali ya Olypinc Caster Semenya imeripotiwa anataka kumuoa mwanariadha mwenzake Violet Rasebova.
Kwamujibu wa wa website ya Daily Sun, Semenya (23) aliwatuma wazazi wake wapeleke posa na kujadiliana kuhusu mahali. .......STORY ZAIDI

ANGALIA PICHA ZA VURUGU ZILIZOTOKEA KWENYE MKUTANO WA UKAWA MOROGORO

$
0
0
Kijana mmoja amepigwakutoka kwa wafuasi wa Ukawa waliokuwa na mkutano mkoani Morogoro jioni hii baada ya kudaiwa kuwa miongoni mwa waliomteka Mbunge Rose Kamli wakati wa uchaguzi mdogo jimboni Kalenga, mkoani Iringa.

Njemba huyo akipokea kichapo kutoka kwa wafuasi wa Ukawa mkoani Morogoro na baadaye kuokolewa na polisi.
Mwenyekiti wa Bavicha, John Heche akithibitisha kumtambua kijana huyo anayedaiwa kushiriki kumteka mbunge wao kwenye uchaguzi mdogo uliofanyika Jimbo la Kalenga, lringa.
Mmoja wa viongozi wa Chadema mkoa wa Morogoro, lnnocent Zawadi ambaye alikuwepo jimboni Kalenga naye akithibitihsa pia kumtambua kijana huyo.
Njemba huyo ambaye hakufahamika jina lake mara moja, aliangushiwa kipigo baada ya kuibuka na kuanza kumpiga picha Mwenyekiti wa Bavicha Taifa, John Heche. Baada ya kipigo cha nguvu, njemba huyo alinusuriwa na polisi waliomchukua kumtoa mikononi mwa wafuasi hao.
Mwenyekiti huyo wa Bavicha akithibitisha kumtambua kijana huyo anayedaiwa kushiriki kumteka mbunge wao kwenye uchaguzi mdogo uliofanyika Jimbo la Kalenga, lringa.

MAGAZETI YA MICHEZO NA BURUDANI

MAGAZETI YA UDAKU LEO

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI TAREHE 15.05.2014

ANGALIA PICHA MWANAMKE AUAWA KIKATILI KWA KUCHOMWA MOTO HADI AKAFA,

$
0
0
Hivi karibuni mwanamke mmoja huko Nchini Nigeria aliuawa na wananchi walioamua kujichukulia sheria mkononi baada ya kumtuhumu kuwa anaiba watoto wa shule na kuwapeleka kusikojulikana. 
Mwanamke huyu ambaye jina lake halikupatikana mara moja, alianza kupigwa na baadaye wananchi hao wakamuua kwa kumchoma moto. 

Inadaiwa kuwa mwanamke huyu alikutwa na watoto wawili wa kike ambao ni wanafunzi, akiongozana nao na ndipo wananchi walipompiga  na hatimaye kumchoma moto hadi akafa

BAADA YA SAMIR NASRI KUACHWA KATIKA KIKOSI CHA UFARANSA FIFA 2014, AZUNGUMZA YA MOYONI

$
0
0

Kiungo wa Manchester City,Samir Nasri amesema kuwa aliamini kwamba hata chaguliwa na timu ya Taifa ya Ufaransa kwaajili ya kombe la dunia. 

Meneja wa Ufaransa,Didier Deschamps aliamua kumwacha Nasri nje ya kikosi kitakachoshiriki michuano inayokuja ya nchini Brazil,licha ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 kuwa na msimu wa mafanikio na Manchester City.Na Nasri anafikiri kuwa kwasasa hana jinsi lakini anatazamia kufahamu mustakabali wake wa soka la kimataifa. 

Alipoulizwa alipokeaje taarifa za kutochaguliwa alisema
 Nilijiandaa kabisa.Nilifahamu kabla,mara nyingine unakuwa na hisia.

Huku akisisitiza
 Unapokuwa unataka kuzungumza na meneja,lakini yeye hataki kuzungumza na wewe,unafahamu kuwa hauendi kwenye kombe la dunia
 Nilikuwa nimejiandaa kiakili.Ulikuwa ni mshtuko lakini nilikuwa nimejiandaa kiakili hivyo niko sawa.

Mashabiki wengi wa Manchester City wameshangazwa kuhusu kuachwa kwa Nasri mara baada ya kumaliza msimu vizuri akifunga goli la kwanza Jumapili waliposhinda taji baada ya kuifunga West Ham 2-0. 
Nasri akaongeza kuwa
 Wakati watu wanazungumzia hilo,inamaanisha kwa baadhi ya pointi kuwa ulifanya kitu kizuri,hivyo ni jambo zuri.
 Nini naweza kusema?Naheshimu uchaguzi wake.Hakutaka kuniita mimi,ni jambo zuri kwake.
 Niitakia kila la heri timu ya Taifa ya Ufaransa na nahitaji kuchukua muda kadhaa sasa kufikiria kuhusu timu ya Taifa kwasababu inakuwa mara ya pili sasa wanaenda kwenye michuano ya kombe la dunia bila mimi kuwemo.

Deschamps alisema wakati anaelezea kwanini alimwacha Nasri:
 Ni muhimili Man City,kitu ambacho sio kesi na Ufaransa na alionyesha wazi kuwa hana furaha iwapo atakaa benchi hivyo naweza kukwambia wewe kuwa inaweza kuleta hisia tofauti ndani ya kikosi.

Lakini nasri alijibu,
 Ni kazi ngumu sana kukubali.
 Kila kitu ambacho amekuwa akisema.Unaweza ukaenda na kumuuliza mchezaji yeyote kama wanakuwa na furaha kuwepo kwenye benchi.Hakuna hata mmoja anaenda na kukwambia ndio.

Nyota huyo wa zamani wa Arsenal akadai kuwa,
 Kama hiyo ndiyo sababu pekee waliyoipata na kuitumia,ni kazi ngumu sana kukubali.
 Nahitaji kufikiria kwa kina,katika kipindi cha likizo kuhusu nini utakuwa mustakabali wangu kwenye timu ya Taifa.Kukosa michuano miwili ya kombela dunia,hakika ni kitu kigumu na kinaumiza kwa mchezaji.

ANGALIA KLABU ZILIZOTOA WACHEZAJI WENGI KWENDA KOMBE LA DUNIA

$
0
0
fifa_world_cup_2014_wallpaper1
Homa ya kombe la dunia inazidi kupanda zikiwa zimebaki takribani wiki zipatazo nne kabla ya michuano hiyo haijaanza kutimua vumbi kwenye viwanja tofauti nchini Brazil. Timu zote 32 tayari zimeshatangaza vikosi vyao kwa ajili ya michuano hiyo.

1613854_710679932328222_4444464783027608059_n
Katika vikosi vyote vya timu za taifa vilivyotajwa kwa ajili ya kombe la dunia Brazil 2014 – Klabu ya Bayern Munich ndio inaoongoza kwa kutoa wachezaji wengi – imetoa wachezaji 17 watakaowakilisha mataifa mbalimbali kwenye kombe la dunia.

Klabu ya Manchester United inashika nafasi ya pili baada ya Bayern na nafasi ya kwanza EPL kwa kutoa wachezaji wengi walioitwa kwenye timu za taifa zitakazoshiriki michuano ya kombe la dunia – UNITED imetoa wachezaji 16.
Chelsea ya England imeshika nafasi ya 3 kwa kutoa wachezaji 15, Napoli 14, Barcelona na Real Madrid wametoa wachezaji 13 kila timu, Juventus imetoa wachezaji 13.

MTANZANIA ADAM NDITI AONGOZA CHELSEA KUTWAA UBINGWA LIGIKUU UINGEREZA JANA USIKU UNDER 21,WAKIIBAMIZA MAN UNITED

$
0
0
Kikosi cha  Chelsea Under 21,Adam Nditi akiwemo wa tatu Kutoka Kushoto waliosimama.
Mtanzania Adam Nditi akipambana na Mchezaji wa Man UnitedWakishangilia Ubingwa baada ya Kuibamiza Man United bao 2 kwa 1 Mechi iliyochezwa Old Trafford.

ANGALIA PICHA KIJANA ACHOMWA MOTO HADI KUFA

ANGALIA PICHA NDEGE YAVUNJIKA KIOO IKIWA ANGANI.

$
0
0
Screen Shot 2014-05-07 at 2.49.08 AM
Ndege ya Delta Airlines aina ya Boeing 767-300 ilikua ikipaa urefu wa futi 38,000 angani na kisha ghafla rubani akawasiliana na abiria ili kuwajulisha kwamba ndege itatua kwa dharura Albuquerque ikitoka Atlanta kuelekea Los Angeles Marekani.



 Mmoja kati ya abiria wa ndege hiyo Jennifer Squires amesema “nilidhani kuna mtu ameumwa lakini baada ya muda kidogo rubani alisema sababu ni msukumo wa upepo kusababishia kioo cha mbele ya ndege kuvunjika kwa nje bila kuvunjika kwa ndani’
 “Niliposhuka kwenye ndege niliomba kuona sehemu iliyovunjika na kupiga picha hii, nashukuru rubani kwa kutushusha salama na kuweza kutoa habari hii kwa wananchi wengine pia ndege nyingine iliagiziwa kuja kutufata kutoka Los Angeles” – Jennifer.

ANGALIA PICHA ZA MAUAJI YA KUTISHA YALIYOTOKEA SUDAN YA KUSINI,TUITUNZE AMANI YETU.

$
0
0
http://www.ufukunyuku.blogspot.com/ 
Umoja wa Mataifa unasema kuwa vikosi vinavyoipinga serikali nchini Sudan Kusini viliwaua mamia ya watu kwa sababu ya kabila lao wakati vilipouteka mji wa Bentiu wiki jana.Kwa mujibu wa taarifa ya shirika hilo, watu hao walilengwa wakiwa katika maeneo salama walikokuwa wanahifadhiwa kama vile msikitini, makanisani na hospitalini.Umoja huo umesema kuwa watangazji katika baadhi ya vituo vya redio walitumia lugha ya chuki na uchochezi na kuwataka watu wa kabila fulani kuondoka mjini humo huku wakiwashauri wanaume kuwabaka wanawake.



MWANAMKE MUISLAMU SUDAN AMEHUKUMIWA KIFO NA BAKORA 100 KWA KOLA LA KUBADILI DINI NA KUOLEWA NA MWANAUME MKRISTO

$
0
0

Mahakama nchini Sudan imemhukumu kifo mwanamke mmoja anayedaiwa kubadili dini yake na kuolewa na mwanamume mkristo.

Daktari Mariam Yahya Ibrahim Ishag, ambaye babake ni muisilamu alishitakiwa kwa kosa la kuasi dini pamoja na kufanya zinaa kwa kuolewa na mwanamume mkristo , kitu ambacho dini ya kiisilamu imeharamisha kwa wanawake.
Mariam mwenye umri wa miaka 27 pia ni mjamzito na pia atapata adhabu ya mijeledi miamoja kwa kosa la zinaa. Maafisa wakuu wanasema kuwa icha ya Mariam kulelewa kwa njia ya kikristo yeye bado ni muisilamu kwa sababu hiyo ndiyo dini ya babake.
Kwa kawaida wanawake waisilamu hawaruhusiwi kuolewa na wanaume wakristo ingawa wanaume waisilamu wanaruhusiwa kuwaoa wanawake wakristo.
Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu Amnesty International linasema kuwa Bi Ishag alilelewa kama Mkristo muorthodoxi kwa sababu babake hakuwepo naye maishani mwake.
Viewing all 20290 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>