Tarehe 15 Mei miaka 238 iliyopita kama leo, ilitengenezwa meli ya kwanza yenye kutumia mvuke. Meli inayotumia nishati ya mvuke ilitengenezwa miaka 70 baada ya kuvumbuliwa nishati ya mvuke na mhandisi wa Kifaransa Denis Papin. Utumiaji wa nishati ya mvuke katika meli ulileta mabadiliko makubwa katika sekta ya usafiri wa baharini.
↧
MELI YA KWANZA DUNIANI ILITENGENEZWA MIAKA 238 ILIYOPITA
↧
UNYAMA KWA WATOTO WAZIDI KUSHIKA KASI : ,WABAKWA NA KULAWITIWA .

Binti aliyefanyiwa kitendo hicho kiovu cha ubakaji.
Kijana aliyejulikana kwa jina la Mfaume Kassim amesurika kuuwa na wananchi wenye hasira kali baada ya kutuhumiwa kuwalawiti watoto watatu wa kiume na kumbaka binti mmoja (majina yao yanahifadhiwa) kwa nyakati tofauti.
Tukio hilo lilitokea Chanika, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam ambapo wananchi hao walifikia hatua ya kumwangushia kipigo kwa madai kuwa, kila akikamatwa kwa vitendo hivyo, huachiwa baada ya muda mfupi na kuendelea kudunda mitaani.
Akizungumza kwa uchungu baba wa mmoja wa watoto waliofanyiwa kitendo hicho, Abdillah Mpacha (pichani), alisema tukio lilitokea Kigezi, Chanika ambapo mtoto wake alikuwa akitokea Madrasa.
Alisema, alipokuwa njiani kuelekea nyumbani alikutana na mbakaji huyo na kumlaghai kwa pipi na kashata kisha kumpeleka nyumbani kwake na kumfanyia kitendo hicho.
Hapa anafafanua zaidi: “Tulishangaa kuona mtoto hana furaha kama kawaida, huku akiwa na wasiwasi mwingi, baadaye akalalamikia maumivu ya tumbo.
“Tulipompeleka hospitalini, baada ya uchunguzi na vipimo alionekana kuwa ameharibiwa vibaya sehemu za siri, hapo ndipo akasema ukweli na kumtaja mbakaji akasema alificha kwa sababu alimwambia kama angesema angemchinja.”
Awali tukio hilo liliripotiwa kwenye Kituo cha Polisi Chanika na kufungiliwa jalada namba CHK/RB/718/2014 kabla ya kuhamishiwa Kituo cha Polisi Stakishari na kufunguliwa jalada namba STK/RB/3609/2014 KUBAKA.
Hata hivyo, wananchi wa eneo hilo wanasema kuwa, baada ya siku tatu, Mfaume alionekana nyumbani kwake akiwa hana wasiwasi jambo lililowatia hasira na kuamua kumshushia kipondo.
↧
↧
MTOTO WA MWAKA MMOJA AANGUKA KUTOKA GHOROFA YA 11 NA KUNUSURIKA KIFO
Mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja amenusurika kifo baada ya kuanguka kutoka orofa ya 11 ya jengo moja mjini Minnesota Marekani.
Vyombo vya habari katika jimbo hilo vimeripoti kuwa Musa Dayib, amevunjika mkono mara mbili na kwa sasa anapumua kwa usaidizi wa mashine japo madaktari wanamtarajia kuishi.
Musa aliteleza katikati ya mianya inayozingira sebule yao katika orofa ya 11 ya mjengo huo wenye nyumba na makazi ya watu.Muuguzi mkuu katika zahanati aliyolazwa amesema kuwa Musa anatarajiwa kuishi baada ya kuanguka katika eneo lisilo kavu sana.
Jamaa na marafiki wa familia hiyo ya kisomali wamepigwa na butwaa kutokana na tukio hilo.
Tukio hilo lilizua mjadala kama ni muujiza au la kuwa amenusurika kifo lakini watafiti wameelezea kuwa mtoto ananafasi nzuri zaidi ya kuishi hata baada ya kuanguka ama kupatwa na janga lolote lile kwani mwili wao bado ni mwororo na mifupa ya mtoto huwa bado ni laini kinyume na mtu mzima ambaye tayari mifupa yake ni kavu na mwili wake ni mkubwa na mzito.
Abdirizak Bihi alisimulia muujiza huo kwa gazeti la The Star-Tribune baada ya kushuhudia yaliyotendeka hapa ninahofia usalama wa wazazi wa mtoto ambao hadi kufikia sasa wamepigwa na bumbuazi hawazungumzi na yeyote.
Dakta Tina Slusher, aliyemhudumia mtoto Musa, alisema hakuna vile mtu mzima angenusurika baada ya kuanguka umbali kama huo.
Bila shaka huu ni muujiza wa Mwenyezi mungu kwa familia hiyo.
↧
ANGALIA PICHA CHA MKUTANO WA UKAWA MJINI MOSHI
↧
BAADA YA ALBINO KUTENDEWA UNYAMA SIMIYU, SERIKALI IMEOMBWA WAGANGA WA KIENYEJI WAFUTIWE VIBALI
Polisi nchini Tanzania wamewakamata waganga wawili wa kienyeji baada ya mwanamke mmoja mwenye ulemavu wa ngozi au Abino kuuwawa kwa kuchinjwa.
Moja ya miguu yake pamoja na vidole vilinyofolewa baada ya shambulizi hilo la hapo jana Jumanne katika mkoa wa Simiyu Kaskazini Mashariki mwa Tanzania. Kumekuwa na visa vingi vya mauaji ya albino katika eneo hilo hapo awali.Shirika la kutetea haki za watu wenye ulemavu wa ngozi Albino la 'Under the Same Sun limeiomba serikali ya nchi hiyo kufuta vibali na shughuli zote za waganga wa jadi kwa madai kuwa wao ndiyo chanzo cha kuuawa kwao.
Kuuawa kwa mwanamke Munghu Lugata mlemavu wa ngozi toka kijiji cha Gasuma mkoani Simiyu Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo kumeacha hisia na uchungu kwa walemavu wengine waliopata mikasa hiyo.
Akizungumza na mwandishi wa BBC Leonrad Mubali kwa uchungu na kilio, Mariamu Staford mlemavu wa ngozi Albino amesema kwamba tukio la kuuawa kwa Munghu Lugata mwanamke mwenye umri wa miaka 40 juzi linamkumbusha mkasa wake uliomkuta wa kukatwa mikono yake yote, zaidi ya miaka mitano iliyopita na sasa anatumia mikono ya bandia ya vyuma huku akisema malengo yake mengi yamekwama.
Albino wamekuwa wakihangaishwa sana nchini Tanzania ambako baadhi ya watu wanaamini kuwa dawa za miujiza zinazotengezwa kutokana na viungo vya miili yao zinaleta bahati nzuri.
Mashambulizi yamepungua katika siku za hivi karibuni lakini mauaji ya hivi punde yamepelekea shirika moja la kutetea haki za Albino kutoa wito kwa serikali kupiga marufuku waganga wote wa kienyeji.
Matukio mengi ya maujia ya walemavu nchini Tanzania yamekuwa yakihusishwa na imani za kishirikina huku waganga wa jadi wakihusishwa.
Mkoa wa Simiyu ni moja katika maeneo kaskazini magharibi mwa Tanzania yenye matukio mengi ya mauaji hayo.
Hivi karibuni nchini Tanzania umezinduliwa mnara maalumu unaoitwa NITHAMINI, mnara pekee duniani unaowakilisha kupinga mauaji ya albino huku Tanzania ikiwa ni moja ya nchi yenye matukio mengi ya ukatili dhidi ya walemavu hao
↧
↧
Serikali ya Tanzania imethibitisha mradi wa Treni za juu kama hizi kujengwa Dar hivi karibuni.
Waziri wa uchukuzi Dr. Harrison Mwakyembe ameongea na TBC1 na namnukuu akisema ‘mradi unaanza wakati wowote mapema iwezekanavyo manake wenzetu tayari wanazo pesa hivyo ni sisi kukimbia tuanze mara moja huu mradi, barabara za juu za treni zinatengenezwa viwandani moja kwa moja hivyo kazi ni kuzisimika tu barabarani ndio maana haitochukua muda mrefu kukamilika’
Elisha Elia alimuuliza Mwakyembe… Je umeme wa bongo tunavyoufahamu na historia yake utafaa kuuwezesha usafiri huo wa Treni kufanya kazi yake? manake treni hizi za kasi zinatumia umeme.Akajibiwa ‘hawatotumia umeme wa TANESCO, watatumia umeme wa solar na vyanzo vingine vya umeme ili isitokee treni ikasimama katikati manake umeme ni lazima uwepo kwa saa 24′
Kazi hii ya ujenzi wa barabara za juu za treni na treni zenyewe Dar es salaam itafanywa na jopo la wawekezaji ambao tayari wameshakubali kuwa tayari kuifanya hii kazi kwa kuanzia Dar es salaam, baadae Arusha kisha Mwanza na kwa Dar es salaam mradi huu kwa kuanzia utatoa ajira kwa zaidi ya watu elfu moja.
↧
ANGALIA PICHA MTOTO AFARIKI BAADA YA KUANGUKIWA NA JIWE KUBWA

Huyu ni baba wa mtoto, bwana Jackson Ismail akimwangalia mwanae kwa uchungu..
Wangali wakipata chakula hicho, baba aliwahi kumaliza na hivyo kuendelea na kazi hiyo ya kuponda mawe huku mkewe na watoto wakimalizia kupata chakula....
Wakati bwana Ismail akiendelea kuyaporomosha mawe hayo,ghafla alisikia mtikisiko mkubwa na hivyo kumtaka mkewe na watoto watoke haraka.....
Mama akiwa na mtoto mchanga waliwahi kunyanyuka na kutoka,lakini kabla binti Malaika mwenye umri wa miaka mitano hajatoka, jiwe kubwa lilimuwahi na kumkandamiza na kumfanya afariki dunia papo hapo....

Mwili wa Marehemu Malaika Jackson...![]()


Baadhi ya wananchi wakiwa eneo la tukio
↧
ORODHA YA WATUMISHI WALIOHAMA KWA VIBALI MAALUM - MEI 2014
Orodha ya watumishi walio hama kwa vibali maalim imetolewa na ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI. Orodha hiyo ndefu ya majina inapatikana katika tovuti ya TAMISEMI kupitia link hii hapa >>>> ORODHA YA WATUMISHI WALIOHAMA KWA VIBALI MAALUM
↧
RAIS KIKWETE AMUAPISHA BALOZI MPYA WA TANZANIA URUSI, NAIBU KATIBU MTENDAJI WA TUME YA MIPANGO
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha Luteni Generali Wyjones Kisamba kuwa Balozi wa Tanzania nchini Urusi Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 15, 2014

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimuapisha Mhe Paul Thomas Sangawe kuwa Naibu Katibu Mtendaji Tume ya Mipango Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 15, 2014

Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe, wakiwa na walioapishwa Luteni Generali Wyjones Kisamba na Mhe Paul Thomas Sangawe Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 15, 2014.PICHA NA IKULU
↧
↧
MASTAA WA BRAZIL WAMTAKA IBRAHIMOVIC KOMBE LA DUNIA

Wanasoka wa kale na wa sasa nchini Brazil wameanzisha kampeni iitwayo VemIbra (yaani Njoo Ibra) ili kuhakikisha mshambuliaji nyota wa Sweden Zlatan Ibrahimovic 32 anakuwepo Brazil kwa ajiri ya kombe la dunia mwezi ujao.Nyota hao ambao ni Dan Alves,Bebeto,Rai,Denilson na Ronaldo de Lima wametengeneza video fupi ili kumshawishi Zlatan kuja Brazil kushuhudia michuano hiyo.
Video hiyo inaanza kwa kuonyesha magoli ambayo Zlatan amefunga akiwa na klabu yake ya PSG msimu huu kisha kufuatiwa na goli la Christian Ronaldo lililofuta ndoto ya mswedeni huyo kuwemo katika michuano ya mwaka huu ya kombe hilo kubwa na maarufu zaidi duniani.
Baada ya goli hilo kukafuatiwa na nukuu ya Zlatan kufuatia kauli aliyoitoa isemayo
"Kombe la dunia bila mimi hainogi kutazama" Kauli hii ilikuja baada ya Sweden kufungwa na Ureno katika mchezo wa mtoano wa kusaka tiketi ya kombe la dunia.

Baada ya nukuu hiyo unafuata wimbo maalum toka kwa mlinzi Dan Alves akimsihi Zlatan kuja Brazil.
Wimbo huo unafuatiwa na ujumbe toka kwa nyota watajwa hapo juu (Rai,Ronaldo,Bebeto na Denilson) Baada ya Zlatan kuona video hiyo akaandika kwenye ukurasa wake wa Twitter
"Brazil!!Itanibidi kupangua ratiba ya likizo yangu" Tusubiri tuone kama kampeni hii itafabikiwa
↧
MAGAZETI YA MICHEZO NA BURUDANI
↧
MAGAZETI YA UDAKU LEO
↧
MAGAZETI YA LEO IJUMAA TAREHE 16.05.2014
↧
↧
WAZIRI CHIKAWE AKIWA NA WATENDAJI WAKUU WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI BUNGENI LEO



Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kulia) akiteta jambo na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ulinzi na Usalama, Mama Anna Abdalla, nje ya lango Kuu la Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Waziri Chikawe tayari amewasilisha Bajeti ya wizara yake katika Bunge la Bajeti linaloendelea mjini Dodoma. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.
↧
MHASHAMU BABA ASKOFU MKUU MTEULE DAMIAN DENIS DALLU APOKEWA KWA SHANGWE SONGEA
Mhashamu Baba Askofu mkuu mteule Damian Denis Dallu akiwa kwenye gari la wazi kwa ajili ya kuwasabahi wakazi wa mkoa wa Ruvuma waliojitokeza barabarani ikiwa ni ishara ya upendo baada ya kupokelewa kijiji cha Lukumbulu ambacho kipo mpakani kati ya mkoa wa Njombe na Mkoa wa Ruvuma
Mhashamu Baba Askofu mkuu mteule Damian Denis Dallu akiwa katika lango kuu la nyumba ya Askofu katika kanisa kuu la Mt.Mathias Mulumba Kalemba lililopo Mjini Songea
Waseminari kutoka Seminari kuu ya Peramiho wakitumbuiza katika mapokezi ya Mhashamu Baba Askofu mkuu mteule Damian Denis Dallu alipo wasili katika kanisa kuu la Mt. Mathias Mulumba Kalemba .
Baadhi ya waumini na wananchi waliojitokeza jioni hii katika mapokeze ya Mhashamu Baba Askofu mkuu
↧
MKONGWE RIO FERDINAND AMPIGIA PANDE VAN GAAL MAN UNITED, ASEMA JAMAA ANAFAA KINOMA!

BEKI mkongwe wa Manchester United, Rio Ferdinand anaamini Louis van Gaal ni mtu sahihi kukabidhiwa majukumu ya ukocha mkuu klabuni hapo.
Kutangazwa kwa Mholanzi huyo kama mirthi wa David Moyes kulistishwa jana alhamisi ili kumuacha huru wakati huu akiiandaa timu ya taifa ya Uholanzi kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Ecuador.
Van Gaal amewahi kuongeza klabu kubwa za dunia, hivyo beki huyo wa kati ambaye hatakuwepo Old Trafford msimu ujao baada ya kutangaza kuondoka majira ya kiangazi mwaka huu amesema kocha huyo anaweza kuleta mafanikio katika michuano ya ligi kuu.
“Anaonekana mtu imara sana na muelekezaji. Ana uelewa na ufahamu mkubwa kwa kila anachotaka kufanya. Unatakiwa kuwa hivyo katika klabu kama Man United,” Ferdinand aliwaambia waandishi wa habari.
“Katika klabu alizopita-Ajax, Bayern Munich, Barcelona- anaonekana kufanya mambo kwa falsafa yake na nadhani atafanya hivyo akiwa na Man United.”
Van Gaal ataelekeza nguvu kubwa ligi kuu ya England katika msimu wake wa kwanza kwasababu Ma United walishika nafasi ya 7 na kushindwa kufuzu michuano ya Ulaya, na Ferdinand anasema mazingira hayo yatawafanya warudi kwenye mbio za ubingwa”.
Ferdinand kwasasa anafirikiria wapi kwa kwenda kucheza. Beki huyo mwenye miaka 35 anahusishwa kwenda nchini Uturiki, lakini Asernal na Hull City zinaonesha nia ya kumtaka.
↧
BARCELONA HAWATASHEREHEKEA UBINGWA WA LA LIGA.....NAO ATLETICO WATASHANGILIWA NA MASHABIKI 447 TU, MOTO UTAWASHWA KESHO YAKE

Head-to-head: Barca na Atletico Madrid watakutana kesho jumamosi kwenye uwanja wa Nou Camp

LA LIGA: PAZIA KUFUNGWA KESHO
Siku ya mwisho kesho wapenzi wa soka watashuhudia Barcelona na Atletico wakichuana kwa mara ya tatu katika historia yao.
Barcelona wataweza kushinda taji kutokana na rekodi nzuri ya `head-to-head` kama watawafunga Atletico Madrid.
Sare itatoshwa kuwapa Atletico ubingwa kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 18.
HEAD-TO-HEAD
21 August: Atletico 1-1 Barcelona
(Spanish Super Cup)
28 August: Barcelona 0-0 Atletico
(Spanish Super Cup)
11 January: Atletico 0-0 Barcelona
(La Liga)
1 April: Barcelona 1-1 Atletico
(Champions League)
9 April: Atletico 1-0 Barcelona
(Champions League)
Kama Atletico Madrid watashinda taji kesho hakuna atakayelala ndani ya saa 48 ndani ya mji mkuu wa Hispania.
Mshabiki 447 ndio waliopata tiketi za kushabikia timu ya Atletico hapo kesho, lakini kama watashinda, moto utawashwa tena mapema jumapili nyumbani kwao Madrid.
Timu hizi mbili zitashangilia ubingwa kwa staili tofauti kabisa. Wakatalunya watamfuta kazi Kocha mkuu, Tata Maryino bila kujali kitakachotokea kesho jumamosi.
Mlinda mlango Victor Valdes atajiunga na Monaco. Dani Alves atamfuata nchini Ufaransa kwa kujiunga na PSG. Beki Carles Puyol atajiunga na kocha mpya anayekuja, Luis Enrique kwenye benchi la ufundi.
Alex Song, Javier Mascherano, Pedro na Alexis Sanchez wote wanauzwa na wanaweza kuondoka kama ofa nzuri zitapatikana, huku Barcelona wakijiandaa kumsajili beki wa Chelsea, David Luiz.
Barca wanaweza kuwashawishi Chelsea kwa kuwapatia Alex Song na Alexis ili kuinasa saini ya Luiz.



↧
↧
TFF YAOMBOLEZA VIFO VYA WASHABIKI DR CONGO
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amemtumia salamu za rambirambi mwenzake wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- FECOFA, Omar Constant kutokana na vifo vya washabiki.
Washabiki 12 walipoteza maisha uwanjani wakati wa mechi ya Ligi Kuu ya nchi hiyo kati ya TP Mazembe na AS Vita iliyochezwa kwenye Uwanja wa Tata Raphael, jijini Kinshasa.
“Tumeguswa na msiba huo mzito, tunatoa salamu za rambirambi kwako (Rais wa FECOFA), familia za marehemu pamoja na wadau wote wa mpira wa miguu katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo,” imesema sehemu ya barua hiyo ya Rais Malinzi.
↧
KOZI ZA UKOCHA LESENI A, B KUFANYIKA JUNI, KAYUNI, MADADI WALA SHAVU LA UKUFUNZI
![]() |
Salum Madadi atakuwa moja ya wakufunzi wa semia hiyo |
Na Boniface Wambura, Dar es salaam
Kozi ya ukocha wa mpira wa miguu kwa ajili ya leseni A na B zinazotambuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) zitafanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Juni 2 mwaka huu.
Ada kwa kozi zote ni sh. 300,000 ambapo wale watakaofanya ya A (equivalent) itaanza Julai 21-26 mwaka huu. Washiriki wa kozi hiyo ni wale wenye leseni B za ukocha za CAF.
![]() |
Sunday Kayuni naye atakuwa mkufunzi wa kazi hiyo |
Kwa wale watakaoshiriki kozi ya leseni B ambao ni wale wenye leseni C watakuwa na vipindi viwili. Kipindi cha kwanza ni kuanzia Juni 2-15 mwaka huu wakati cha pili kinaanza Juni 23 mwaka huu na kumalizika Juni 28 mwaka huu.
Wakufunzi wanaotambuliwa na CAF watakaoendesha kozi hiyo ni Sunday Kayuni na Salum Madadi kutoka Tanzania, na washiriki watajigharamia kwa kila kitu. Baadaye CAF watatuma Mkufunzi mwingine kwa ajili ya mitihani.
↧
LIONEL MESSI KUVUTA MKWANJA MREFU ZAIDI YA CRISTIANO RONALDO
Milionea: Messi amekubali kusaini mkataba mpya Barcelona ambao utamfanya awe mwanasoka anayelipwa zaidi ya wote duniani.
MSHAMBULIAJI Lionel Messi atakuwa akilipwa Pauni Milioni 16.3 kwa mwaka katika mkataba mpya aliokubali kusaini na klabu yake, Barcelona jambo linalomfanya Muargentina huyo kuwa mwanasoka anayelipwa zaidi duniani.
Baba wa mchezaji huyo Jorge alikutana na viongozi wa klabu hiyo Javier Faus na Antoni Rossich wiki iliyopita na kufikia makubaliano ya mkataba wa saba ndani ya miaka 11 ya mshindi huyo wa Ballon d’Or nne Barcelona.
Messi atafikisha miaka 27 June na mkataba mpya unatarajiwa kuweka Camp Nou hadi mwaka 2018.
Kwa mshahara huo mpya, Messi anampiku hasimu wake, Cristiano Ronaldo wa Real Madrid ambaye analipwa Pauni Milioni 15 kwa mwaka.
↧