Quantcast
Channel: MATUKIO NA VIJANA
Viewing all 20290 articles
Browse latest View live

ANGALIA PICHA MATESO ANAYOPATA MWENZETU,MSAADA UHAHITAJIKA.

$
0
0
Kijana Amos Ng’arare Sasi (21) mkazi wa kijiji cha Kizaru wilayani Musoma Vijijni  
Kwa kipindi hiki kijana Amos, ambaye anatoka Kata ya Mryaza, amelazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya matibabu, lakini matarajio ya kupona kwa tiba za hapa nchini hayapo hivyo njia pekee iliyobaki ni kwenda nchini India kwa matibabu zaidi.
Kijana Amos Ng’arare Sasi (21) mkazi wa kijiji cha Kizaru wilayani Musoma Vijijni amepoteza mwelekeo wa maisha baada ya ndoto yake ya kusoma hadi chuo kikuu kuishia njiani kutokana na matatizo ya ugomjwa wa ajabu ambao umemtesa kwa kipindi cha miaka 17.
Kwa kipindi hiki kijana Amos, ambaye anatoka Kata ya Mryaza, amelazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya matibabu, lakini matarajio ya kupona kwa tiba za hapa nchini hayapo hivyo njia pekee iliyobaki ni kwenda nchini India kwa matibabu zaidi.
Katika mahojiano na Mwananchi wiki iliyopita akiwa Wodi Namba 21, Sewahaji, Amos alionekana mwenye mawazo kupita kiasi.
“Ndoto yangu ya elimu itakuwa imeishia hapa. Sitegemei kurudi tena. Wenzangu niliokuwa nikisoma nao darasa moja, kwa sasa wapo kidato cha nne. Nilizaliwa nikiwa sina tatizo la aina yoyote kiafya na nililelewa na wazazi wote wawili. Kwa kweli kwa malezi niliyoyapata, sikuwahi kujiona tofauti,” anasema.
“Nikiwa na miaka minne baba alifariki dunia, nikabaki na mama ambaye alitulea mimi na kaka yangu kwa furaha akijishughulisha na kilimo cha jembe la mkono,” anasema Sasi.
“Baadaye tulibaki wawili tu, yaani mimi na mama baada ya kaka kuondoka kwa madai kuwa anakwenda kutafuta maisha. Ilikuwa mwaka 1998 na mpaka leo hatujawahi kumuona wala kusikia taarifa zake,” anasimulia Sasi.
Anasimulia kuwa alipofikisha umri wa miaka minne, usoni kwake kuliota kitu kama kipele ambacho alisema kilikuwa kinamuwasha sana.
Anaongeza kuwa mama yake alimpeleka hospitali ambako alipewa dawa za kupunguza maumivu tu.
“Nilipofikisha umri wa miaka tisa hali ilizidi kwa mbaya, maumivu na uvimbe ukazidi,” anasema.
“Mama alinionea huruma akawa halali pale anapoona nalia kutokana na maumivu makali. Aliamua kunipeleka hospitali ya Musoma lakini hakukuwa na mabadiliko. Mwaka 2010 alinipeleka Hospitali ya Bugando mkoani Mwanza, huko nilifanyiwa uchunguzi, lakini ugonjwa haukujulikana.”
Anasema wakati huo matokeo ya shule ya msingi yalikuwa yametoka naye alifaulu kwenda kidato cha kwanza, lakini alishindwa kutokana na kuzidiwa na maumivu.
“Nilirudishwa nyumbani, nikawa sipati huduma ya aina yoyote. Watu walioniona walinionea huruma, wengine wakawa hawataki kuniona mitaani. Walinitishia kuwa nikionekana, nitakamatwa na wachimba madini wanichinje wachukue viungo wakafanye manbo ya kishirikina wapate madini kwa wingi,” anabainisha.



“Baadhi ya wananchi walinionea huruma. Walinichangia fedha ili nije Muhimbili nipate matibabu.”
Anasema alifika Muhimbili Septemba, 2011 na madaktari walichukua vipimo na kumwambia arudi mwezi mmoja baadaye.
“Hata hivyo sikuweza kurudi kipindi hicho kutokana na kukosa nauli. Namshukuru mbunge wetu Nimrod Mkono na diwani wetu walinisaidia nauli ya kuja. Nikaja mwezi wa pili mwaka huu. Walinipima kwa mara ya pili na kunieleza kuwa kuna mshipa wa fahamu unapitisha damu nyingi hivyo natakiwa kufanyiwa upasuaji nchini India.
“Wakati fulani ninapata maumivu hadi napoteza fahamu. Nasikitika hali hii huwa inanikuta nikiwa peke yangu na mama anapenda sana kuja kuniona, lakini anashindwa kwa sababu ya kukosa nauli.
“Nawashukuru sana madaktari kwa kuwa karibu nami na kunipa dawa za kupunguza maumivu. Pia wauguzi wamekua nami kwa kunisaidia na kuniliwaza. Ninawapongeza ila kinachoniuma ni pale ninapowaona wagonjwa wanatembelewa na ndugu zao, lakini kwa upande wangu hakuna hata mtu mmoja,” anasema kijana huyo.
“Nawaomba Watanzania wanisaidie kwa msaada wowote hata kwa kuniombea, ili Mungu anisimamie nipelekwe India nitibiwe.
“Mimi ni kijana mdogo ninayetamani kurudi shule na kufanya shughuli nyingine za maendeleo.”
Kwa atakayeguswa na tatizo la mtoto huyu anaweza kuwasiliana na ofisi za Mwananchi au kupiga simu namba 0688551355.

GARI NDOGO AINA YA RAV 4 YASABABISHA AJALI MBAYA NA KUPELEKEA DERAVA WA BODABODA NA ABIRIA WAKE KUUMIA VIBAYA SANA.

$
0
0


 
Ajali mbaya imetokea muda mchache uliopita katika lango Kuu la kuingilia katika Mahakama ya mjini Tabora. Ajali hiyo imehusisha Gari ndogo aina ya Rav 4 yenye usajili wa namba T516 ALA ambayo ilikuwa inaendeshwa na Mama mmoja aliye tambulika kwa jina la Stumai Tambwe ambapo ameigonga Bodaboda iliyokuwa na Abiria na kuwasababishia kuumia vibaya san, na baada ya hapo Gari hilo liligonga mti na kumsababishia kuumia vibaya.



Majeruhi wote wamekimbizwa Hospitali kwa ajili ya Matibabu zaidi na hali zao wote mpaka sasa ni mbaya. 
 Majeruhi wakipata Msaada baada ya ajali hiyo kutokea mapema leo
 Majeruhi akikimbizwa kwa ajili ya huduma ya kwanza

 Gari baada ya kugonga Bodaboda liligonga Mti na ndipo mama huyo aliumia vibaya.








WAWILI WAFA KATIKA AJALI YA PRADO MBEYA

$
0
0

Watu wawili Rehema Mwamaso [30], mkazi wa Sumbawanga na mwanaume mmoja ambaye bado hajafahamika jina wala makazi yake,umri kati ya miaka 30-40, walifariki dunia papo hapo kufuatia ajali iliyotokea wakiwa katika gari T.620 CTL aina ya Toyota Land Cruiser Prado lililokuwa likiendeshwa na dereva Robert Jubery Mwaihoje [61],mkazi wa Sumbawanga.Tukio hilo limetokea tarehe jana majira ya saa 2:00 asubuhi huko katika kijiji na kata ya Nakawale,tarafa ya Ndalambo,wilaya ya Momba, mkoa wa Mbeya, barabara ya Sumbawanga/Tunduma. Katika tukio hilo watu wengine watatu walijeruhiwa akiwemo dereva wa gari hilo na wanawake wawili ambao bado hawajafahamika majina na makazi yao. Chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi, taratibu zinafanywa ili dereva afikishwe mahakamani. 


Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi Ahmed Msangi anatoa wito kwa madereva kuwa makini wanapoyumia vyombo vya usafiri kwa kuzingatia sheria na alama za barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika. Aidha anatoa rai kwa wananchi kufika katika kituo cha afya tunduma kwa ajili ya utambuzi wa marehemu na majeruhi.

RAISI:JK.AENDA KUMFALIJI SALVA NYUMBANI KWAKE KINONDONI

$
0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipa pole Bibi Isabela Salva Rweyemamu ambaye ni mama wa Marehemu Private Brian Salva Rweyemamu wakati alipokwenda kutoa pole nyumbani kwa marehemu Kinondoni jijini Dar es Salaam leo.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho kikwete akiwafariji Mkurugenzi wa Mawasiliano Ofisi ya Rais Ikulu Bwana Salva Rweyemamu na Mkewe Isabela Salva Rweyemamu ambao ni wazazi wa Marehemu Private Brian Salva Rweyemamu nyumbani kwao Kinondoni jijini Dar es Salaam leo.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na kuifariji familia ya Marehemu Private Brian Salva Rweyemamu nyumbani kwao Kinondoni jijini Dar es Salaam leo(picha na Freddy Maro)
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Ofisi ya Rais Ikulu Bwana Salva Rweyemamu Kinondoni jijini Dar es Salaam kufuatia kifo cha mwanaye Private Brian Salva Rweyemamu kilichotokea jana katika hospitali ya jeshi Lugalo jijini baada ya kuugua kwa muda mfupi. Marehemu Private Brian anatarajiwa kuzikwa kesho mchana(Jumamosi) katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

RATIBA YA MAZISHI YA PRIVATE BRIAN SALVA RWEYEMAMU NA WASIFU WAKE

$
0
0

TAREHE 17.05.2014

SAA      1.00  ASUBUHI CHAI

SAA 4.00-5.00  CHAKULA CHA MCHANA

SAA 5.00-6.00 KUAGA MWILI

SAA 6.00-7.00 MISA KATIKA KANISA KATOLIKI MWANANYAMALA

SAA 10.00 SHUGHULI ZA MAZISHI MAKABURI YA KINONDONI
---------------------------------------------------------------
WASIFU WA PRIVATE  BRIAN SALVA RWEYEMAMU



Rwechungura Brian Salva Rweyemamu, aliyefariki dunia alfajiri ya juzi, Alhamisi, Mei 15, 2014 ni mtoto wa kwanza wa Salva Rweyemamu na Isabella Kafumba Rweyemamu. Alizaliwa Desemba 27, mwaka 1987, katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar Es Salaam.
Alipata elimu ya awali katika Shule ya Awali ya Mama wa Kiganda, Kinondoni na Kwa Mama Kate eneo la Chang’ombe, Dar Es Salaam kabla ya kuhamia Kenya ambako alianza darasa la kwanza katika Shule ya Msingi ya Top Hill na Lukenya. Hatimaye alihamia kwenye mji Mkuu wa Ubelgiji wa Brussels ambako aliendelea na elimu ya msingi mwaka 1996.
Brian alijiunga na shule ya Bweni ya Trinity Exeter nchini Uingereza ambako aliendelea na kumalizia elimu ya msingi. Ili kumrudisha katika mazingira ya Kitanzania, Bwana Brian alirudia tena darasa la saba katika Shule ya Msingi ya Julius Nyerere iliyoko Mbezi Beach, Kinondoni, Dar Es Salaam, mwaka 1998.
Alijiunga na Shule ya Sekondari ya St. Albans ya mjini Pretoria, Afrika Kusini, mwaka 1999 ambako alikaa miaka minne kabla ya kujiunga na Shule ya Sekondari ya Kaboja nje kidogo ya mji mkuu wa Uganda wa Kampala ambako alimaliza kidato cha sita mwaka 2005.
Alijiunga na Chuo Kikuu nchini Malaysia ambako alichukua masomo ya International Trade, masomo ambayo yalikuwa bado yanamdai credits za semester ya mwisho kabla ya kuaga dunia.
Alijiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Kambi ya Mlale, Songea, 2010 na kumaliza kumaliza mafunzo yake mwaka 2011 na hatimaye alijiunga na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (TPDF) ambako alifanya na kumaliza mafunzo katika Kambi ya Mafinga mjini Iringa mwaka 06/12/2013 kabla ya kuajiriwa na JWTZ mwishoni mwa mwaka jana.
Aliomba na kupewa likizo yake ya kwanza ndani ya JWTZ wiki mbili zilizopita ambako alikaa nyumbani kwa siku chache kabla ya kushambuliwa na malaria kali wiki iliyopita. Alilazwa Jumamosi iliyopita tarehe 10/05/14 katika Hospitali Kuu ya Jeshi ya Lugalo akiwa na malaria na kupoteza fahamu.
Alianza kupata fahamu kwa mbali siku ya Jumanne usiku na kujaribu kuongea siku ya Jumatano. 

KAMBI RASMI YA UPINZANI YATOA MSAMAHA KWA JAJI WEREMA, SIKILIZA HAPA KAULI YAO

$
0
0

Kwa maneno ya siku hizi ni kwamba Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Fredrick Werema ‘amelikoroga na kulinywa mwenyewe’, baada ya jana kutoa kauli ya kuudhi alipomtaka mbunge kutoka Zanzibar akaulize swali lake visiwani humo, iliyosababisha baadhi ya wabunge kususia Bunge na kutoka. Lakini hatimaye leo kambi rasmi ya upinzani imetoa majibu ya msamaha baada ya msamaha huo kuwasilishwa na James Mbatia kwa niaba ya kambi hiyo, sikiliza hapa chini>>>


MAMA MARIA NYERERE AZUNGUMZIA MAISHA YA MWALIMU, AUNGANA NA VIJANA WAZALENDO

$
0
0
mama maria.Mama Maria Nyerere amezungumza na vyombo vya habari nyumbani kwake Msasani, na kuwataka vijana waliokwenda kumtembelea kuzunguka nchi mzima kuwaambia ukweli watanzania juu ya Maisha halisi ya mwalimu na mchango wake katika ujenzi wa Taifa huru la Tanzania.mama mariaVijana wazalendo na wapenda Amani ambao wamemtembea Mama Maria wakiongozwa na Kiongozi wao anayejulikana kwa Jina la Mohamed Nyundo, wamesema wako pamoja na familia hiyo na kwamba wamesikitishwa na kampeni inayoendelea ya kumchafua Baba wa Taifa, kumkebehi na kumtuhumu kwa Uzushi na uzandiki.

UJUMBE WA VIJANA KULAANI VITENDO VIOVU VYA KUMVUNJIA HESHIMA BABA WA TAIFA.
Kumekuwepo na kampeni yenye nia ovu iliyoasisiwa hivi karibuni ya kuharibu taswira na heshima ya Baba wa Taifa Mwalimu Kambarage Nyerere katika jamii ya kitanzania na kimataifa. Kampeni hiyo inayoendeshwa na vibaraka wa nchi za magharibi na Ulaya, wazandiki na maadui wa Amani ya Tanzania imeendelea kusambazwa kwa kasi na kwa gharama kubwa.
Kutokana na kuwepo kwa Kampeni hiyo, jumuiko la Vijana Wazalendo na wapenda Amani  tumeamua kutoa tamko hili la kulaani na kupinga vitendo viovu vya baadhi ya watu kumtuhumu, kumkebehi na kumtukana Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Kwa kutambua Mchango wa Baba wa Taifa kama muasisi wa Taifa hili, mpigania Uhuru shupavu, Shujaa aliyekuwa na mapenzi ya dhati kwa watu wake na kwa kutambua umahiri na jitihada za kujenga Taifa lenye Muungano, Umoja, Amani na Utulivu, jumuiko la Vijana wazalendo limeamua kuukumbusha Umma wa watanzania juu ya mchango wa utumishi uliotukuka wa Mwalimu Nyerere katika ustawi wa Taifa letu, lakini pia kuhamasisha watanzania hasa Vijana kuenzi kwa Vitendo moyo wa kujituma,weledi na busara za kiuongozi, pamoja na ushujaa na ushupavu wa Mwalimu Nyerere.
Sisi Jumuiko la Vijana wazalendo, tumeona ni vyema kuja kumfariji Mama yetu, Mama Maria Nyerere pamoja na familia nzima ya Mwalimu Nyerere na Kwamba sisi kama wananchi na Vijana makini tutaendelea kuwa pamoja na familia katika kupinga na kulaani vitendo hivyo viovu vya kejeli, matusi, tuhuma na kebehi zinazoelekezwa kwa Baba wa Taifa, marehemu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Kwa masikitiko makubwa, tumeshitushwa na kufadhaika kuona chombo kikubwa na taasisi muhimu ambayo ni muhimili mkubwa wa Serikali kama Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania linakuwa ndio uwanja wa matusi ya kumtukana muasisi wa Taifa hili, imetusikitisha na kutufedhehesha. Imefika wakati sasa, kwa Bunge Tukufu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kudhibiti na kuondoa kinga yake kwa wale wote ambao kwa ujinga na kutumika wameamua kuanzisha na kuendesha kampeni kabambe ya kutia doa taswira na heshima ya Baba wa Taifa.
Imetolewa na:                                            
Mohamedi Nyundo.
Kiongozi wa Jumuiko la Vijana Wazalendo na Mwenyekiti wa Vijana Mkoa wa Pwani.

ANGALIA TASWIRA YA MKUTANO WA UKAWA IRINGA

$
0
0

Profesa Ibrahim Lipumba akikaribishwa na Mchungaji Peter Msigwa (mbunge wa Iringa Mjini )kuhutubia mamia ya wakazi wa mji wa Iringa waliojitokeza
Huu ndio ulikuwa muitikio wao, wakisisitiza serikali tatu kama walivyotoa maoni yao kwa Tume ya Katiba
Mchungaji Msigwa akiamsha hali kwa wananchi hao
Profesa Lipumba akionesha rasimu iliyosainiwa na Rais Jakaya Kikwete kwa ajili ya kujadiliwa na bunge maalumu la katiba
Danda Juu wa NCCR-Mageuzi alikuwepo pia na akazungumza machache anayofahamu kuhusu rasimu hiyo, msisitizo ukiwa ni serikali tatu kama ilivyopendekezwa na katika rasimu

Sheikh Rajab Katimba wa Shura ya Imam alikuwepo na kuzungumzia umuhimu wa bunge la katiba kujadili maoni ya wananchi. Alisisitiza umuhimu wa kuwa na serikali ya Tanganyika kama ilivyo visiwani  ambako Zanzibar wana serikali yao
Diwani wa kata ya mivinjeni Iringa Mjini, Frank Nyalusi alikuwepo na akarusha lawama kwa jeshi la Polisi kwa kutisha watu ili wasipate katiba wanayotaka
Katibu wa Chadema Mkoa wa Iringa, Allein alikuwa mshehereshaji wa mkutano huo wa Ukawa
Moja ya mabango yaliyopamba mkutano huo na ujumbe wake kama unavyosomeka

IDADI YA WALIOFARIKI NCHINI KENYA KATIKA MILIPUKO GIKOMBA IMEFIKIA WATU

RAIS KIKWETE AONGOZA HARAMBEE KANISA LA KKKT BUMBULI

$
0
0
afsgsRais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo na Naibu waziri Mawasiliano Sayansi na Technolojia na mbunge wa Bumbuli January Makamba wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa la Bumbuli Shughuli hiyo imefanyika katika Hotel ya Golden Tulip (Ijumaa) Tarehe.16.05.2014makambaRais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia wimbo wa wanabumbuli mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa Hotel ya Golden Tulip kwa ajili ya harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa la Kilutheri la Bumbuli, Kushoto ni askofu mkuu wa KKKT Dr.Gerhas  Malasusa, Watatu Kulia ni Dkt.Steven Munga wa Lushoto na kulia ni mbunge wa Bumbuli ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na teknolojia Mh.January Makamba Katika harambee hiyo jZaidi ya Shilingi milioni mia tatu zilipatikana(picha na Freddy Maro).

ANGALIA PICHA MILIPUKO ILIYOTOKEA NAIROBI JANA NA KUUWA WATU 13

ASKOFU DALLU KUSIMIKWA RASMI KESHO

$
0
0
dalu_1b119.jpg
Balozi wa Baba Mtakatifu nchini Tanzania Askofu Mkuu Fransisko Montecillo Padilla, anataraji kuongoza Misa Takatifu ya kusimikwa kwake Askofu Mpya wa Jimbo Kuu la Songea, Mhashamu Damian Dennis Dallu (Pichani). 
Tukio hilo litafanyika katika Kanisa la Mtakatifu Mathias Mulumba Kalemba la Jimbo Kuu la Songea hapo kesho. Leo hii baadhi ya waumini wamesafiri mpaka katika mpaka wa Mkoa wa Ruvuma na Njombe kwa ajili ya kumpokea Askofu Dallu anayeingia Jimboni Songea na leo Jumamosi atafanyiwa Ibada ya kukabidhiwa Kanisa. 


Tukio hilo linalotaraji kuhudhuriwa na Viongozi wengi wa Madhehebu ya dini, litahudhuriwa pia na Rais mstaafu wa awamu ya tatu Mheshimiwa Benjamin Wiliam Mkapa.(


Bishop Damian Dennis Dallu was born on 26 Apr 1955 at Kiponzelo, in Iringa Diocese. He is the youngest child among the six children. His parents were Catholics who introduced him into the Catholic Faith. Damian went to school at Kiponzelo Primary School from standard one to four. Later he joined Kalenga Middle School from Standard five to seven.  After Primary school, Damian joined Mafinga Minor Seminary where he completed his high school in 1978.
After High School education, Dallu decided to continue on with his vocation to priesthood. In 1979 Damian went to Peramiho major seminary for Philosophy and Theology studies. Dallu was ordained a Priest on November 15th 1984.
Fr. Damian joined higher studies at Catholic University of Eastern Africa (CUEA) in Nairobi, Kenya. Later on, he went to Belgium for further studies in Moral Theology. After his studies, Fr Damian Dallu was appointed to teach at Segerea Major Seminary in Dar es Salaam.
Fr. Dallu was appointed a Bishop of Geita on 14 April 2000.  On 30 July 2000 Fr. Dallu was consecrated and installed the Second Bishop of the Diocese of Geita. The Principal Consecrator was H.E. Polycarp Cardinal Pengo, and the Principal Co-Consecrators were the late Bishop Aloysius Balina, by then Bishop of Shinyanga and Bishop Tarcisius Ngalalekumtwa, Bishop of Iringa.
SOURCE: Vatican Information Service and AMECEA Social Communications Office

UNYAMA WA KUTISHA MUME AMFANYIA UKATILI WA KINYAMA MKEWE

$
0
0

Bwana Gasto Edward na mkewe ambaye anadaiwa kumkata nyeti zake.

Gasto Edward (32) amemkata mkewe Mwelu Raymond sehemu zake za siri, Risasi Jumamosi lina simulizi hii ya kusikitisha. Tukio hilo lilitanguliwa na kumpiga mkewe huyo na kipande cha nondo kichwani hali iliyosababisha apoteze fahamu papo hapo na kutekeleza azma yake.Imeelezwa kuwa, tukio hilo lenye sura ya majonzi, lililovuta hisia za watu wengi lilitokea Jumatano ya wiki hii, huko King’azi, Kwembe – Mbezi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

KISA CHA YOTE
Habari zilizopatikana eneo la tukio zinadai kuwa, chanzo cha unyama huo ni wivu wa kimapenzi ulioingilia ndoa hiyo, ambapo Gasto alimtuhumu mkewe kuwa  na uhusiano wa kimapenzi na mwanaume mwingine anayeishi Temeke aliyejulikana kwa jina la Mgogo.
Chanzo chetu cha kuaminika, kwa sharti la kutotajwa gazetini kilisema: “Mwelu na Gasto wametoka mbali, wameishi kwa muda mrefu na wamebarikiwa watoto wawili, sema siku za hivi karibuni, Gasto alianza kumtuhumu mkewe kuwa anatoka nje ya ndoa.
Wananchi wakiwa eneo lilipotokea tukio hilo.
“Tena siyo tuhuma, anasema alikuwa akimwambia wazi kuwa ana mwanaume wake Mgogo ambaye yupo Temeke. Jamaa alikuwa analalamika kuwa mkewe alifikia hatua ya kumwambia amuache ili aende kwa mwanaume huyo anayejua kutunza.”
Akaongeza: “Unajua katika hali ya kawaida, kama ni kweli mke alikuwa akimwambia mumewe maneno ya hovyo kama hayo, yanaumiza. Ndiyo maana jamaa akaona kwa sababu chanzo cha yote ni penzi, akamkata nyeti zake.”
MJUMBE ANAFAFANUA
Mjumbe wa Mtaa wa King’azi, Amani Abdallah alikiri kupokea malalamiko hayo kutoka kwa Gasto, mwezi mmoja uliopita na kufanikiwa kusuluhisha.
Ujumbe alioandika bwana Gasto kabla ya kutokomea.
“Ni kweli walikuwa na tofauti na hili suala lilinifikia hata mimi. Gasto alikuja kulalamika kuwa mkewe siyo mtulivu na anamwonyesha dharau. Lakini tulisuluhisha yakaisha. Jana (Jumatano) ambapo tukio lilitokea, yule mkewe alikuja kulalamika kuwa mumewe amebadilika.
“Alisema amemuona akinoa kisu asubuhi, usiku ugomvi ukatokea akaamua kuja kulala kwangu, lakini baadaye akaniaga anakwenda kulala kwa jirani yao mama Mbonde, huko ndipo mumewe alipokwenda kumchukua na kumfanyia unyama huo.”
WOSIA MZITO
Baada ya tukio hilo, Gasto alitoroka lakini aliandika wosia uliomtaja mrithi wa mali zake kuwa ni watoto wake Edward na Editha ambapo alimchagua kabisa msimamizi wao kuwa ni mdogo wake aitwaye Kiriani.
Jalada alilofunguliwa Gasto.
Katika barua hiyo, Gasto alisema anakwenda kujiua kwa sababu amechoshwa na dharau za mkewe, ndiyo maana akaamua kuondoa sehemu zinazompa kiburi.
Kesi ya Gasto imeripotiwa katika Kituo cha Polisi Kwa Yusuph na kufunguliwa jalada nambari KWR/RB/4716/14 – KUJERUHI.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Camilius Wambura alipopigiwa na Risasi Jumamosi ili kuelezea tukio hilo, alikiri kupokea taarifa, akasema bado wanafuatilia.

ANGALIA PICHA YA MWANAMKE ALIYEBADILI DINI AMEHUKUMIWA KIFO KWA KITENDO HICHO NCHINI SUDAN.

$
0
0

 Mwanamke aliehukumiwa kifo kwa kubadili dini na kuolewa na mume Mkristo. Mahakama nchini Sudan imemuhukumu kifo mwanamke mmoja anayedaiwa kubadili dini yake na kuolewa na mwanaume mkristo.Daktari Mariam Yahya Ibrahim Ishg ambae baba yake ni muisilamu alishitakiwa kwa kosa la kuasi dini pamoja na kufanya zinaa kwa kuolewa na mwanamume mkristo kitu ambacho dini ya kiisilamu imeharamisha kwa Wanawake. 

BBC wamesema Mariam mwenye umri wa miaka 28 pia ni mjamzito na ataadhabiwa kwa kuchapwa mijeledi miamoja kwa kosa la zinaa. 

Unaambiwa Mariam alilelewa na mama yake mzazi ambae ni Mkristo lakini maafisa wa Sudan wanasema yeye bado ni Muislamu kwa sababu ndio dini ya baba.

Alipewa siku tatu baada ya kuhukumiwa aweze kurejea katika dini ya kiisilamu lakini akakataa na ndio maana adhabu ikabaki palepale kwa kuwa Wanawake Waislamu hawaruhusiwi kuolewa na Wanaume Wakristo ingawa Wanaume Waisilamu wanaruhusiwa kuwaoa wanawake wakristo. 

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu Amnesty International linasema kuwa Ishag alilelewa kama Mkristo muorthodoxi kwa sababu baba yake hakuwepo naye maishani mwake. 

Kesi ya Ibrahim ni ya kwanza ya aina yake kusikika nchini Sudan kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters na Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu, wamelaani uamuzi huo wa Mahakama na kuitaka serikali ya Sudan kuheshimu haki na uhuru wa watu kuabudu. 

Maafisa wa balozi za mataifa ya magharibi pia wamekemea vikali kesi hiyo na kuelezea asiwasi wao na kuwataka maafisa wa sheria nchini humo kuangalia kesi hiyo upya na kuhakikisha kuwa Mariam anatendewa haki. 

Waziri wa mawasiliano amesema kuwa sio Sudan peke yake ambako sheria za kiisilamu zinafuatwa na ambako sio sawa kwa mtu kubadili dini yake, hali hiyo pia ipo nchini Saudi Arabia na katika nchi nyngine zinazofata sheria za kiisilamu. 

Serikali ya Rais Omar al-Bashir inakabiliwa na changamoto nyingi za kiuchumi na kisiasa hasa baada ya kujitenga na Sudan Kusini ambako mafuta yake 

FA CUP: LEO FAINALI, KOMBE JIPYA UWANJANI-HULL CITY v ARSENAL!!

$
0
0


FA_CUP-FINAL-HULL_v_ARSENAL_LOGO

>>MEI 17, WEMBLEY STADIUM, LONDON, SAA 1 USIKU!
>>NAFASI MURUA KWA ARSENAL KUMALIZA UKAME MIAKA 9, JE….???
NAHODHA wa Hull City au Arsenal Leo Usiku Uwanjani Wembley Jijini London atabeba Kombe jipya kabisa la FA ikiwa Timu yake itaibuka kidedea kwenya Fainali ya FA CUP.
Hii itakuwa ni mara ya 3 katika Historia ya Miaka 143 ya FA CUP kwa kwa FA, Chama cha Soka England, kulibadili Kombe la FA na mara nyingine ni kwenye Miaka ya 1911 na 1992.
Kombe hili jipya linafanana kabisa na lile Kombe la Mwaka 1911 na limebadilishwa baada ya kuchakaa.
Kombe la zamani litabaki kwenye kumbukumbu za FA Uwanjani Wembley.

HABARI ZA AWALI:
KWA WACHAMBUZI wengi huko Uingereza hii ni nafasi murua kwa Arsene Wenger na Arsenal yake kumaliza ukame wao wa Miaka 9 bila ya Kombe lolote wakati Jumamosi watakapoingia Wembley Stadium Jijini London kuivaa Hull City kwenye Fainali ya FA CUP.
Arsenal wanapambana na Hull City ambao wamemaliza Msimu huu wakiwa Nafasi ya 16 kwenye Ligi Kuu England lakini kwa Meneja wa Hull City, Steve Bruce, Nguli wa Man United, faraja kubwa ni kukumbuka nini kiliwakuta Arsenal Miaka mitatu iliyopita walipotinga Wembley kwenye Fainali ya Kombe la Ligi na kuchapwa 2-1, bila kutarajiwa, na Birmingham City.
Wakiwa na Masupastaa kama kina Mesut Ozil, Santi Cazorla na Olivier Giroud, utabiri wote unanyoosha kidole kuwa Arsenal ndio Bingwa wa FA CUP na hasa ukizingatia Rekodi mbovu ya Hull City dhidi ya Arsenal ya kufungwa Mechi zote 2 za Ligi Kuu England Msimu huu na pia kutoifunga Arsenal tangu wakutane uso kwa uso kuanzia Mwaka 2009.
+++++++++++++++++++++++++
SAFARI KWENDA WEMBLEY
ARSENAL
Raundi ya 3
Arsenal 2 Tottenham 0
Raundi ya 4
Arsenal 4 Coventry 0
Raundi ya 5
Arsenal 2 Liverpool 1
Raundi ya 6
Jumamosi Machi 8
Arsenal 4 Everton 1
Nusu Fainali
Wigan 1 Arsenal 1
[Penati: Arsenal 4-2]
HULL CITY
Raundi ya 3
Middlesbrough 0 Hull City 2
Raundi ya 4
Southend 0 Hull City 2
Raundi ya 5
Brighton 1 Hull City 1
[Marudiano Hull 2 Brighton 1]
Raundi ya 6
Hull City 3 Sunderland 0
Nusu Fainali
Hull City 5 Sheffield United 3
+++++++++++++++++++++++++
Wenger anatarajiwa kufanya uamuzi nani amuweke Golini kati ya Kipa Lukas Fabianski, ambae amedaka Mechi zao zote za FA CUP Msimu huu, au Kipa Nambari Wani Wojciech Szczesny, ambae ametwaa Glovu za Dhahabu Msimu huu baada ya kuweka Rekodi ya kutofungwa katika Mechi 16 za Ligi Kuu England.
VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:
Arsenal: Fabianski; Sagna, Mertesacker, Koscielny, Gibbs; Ramsey, Arteta; Ozil, Cazorla, Podolski; Giroud
HULL CITY: Harper; Bruce, Chester, Davies, Figueroa, Rosenior; Livermore, Huddlestone, Elmohamady; Boyd; Sagbo
REFA: Lee Probert
+++++++++++++++++++++++++++++
THE FA CUP WITH BUDWEISER
MSIMU 2013-14
-NUSU FAINALI:
Jumamosi Aprili 12
Wigan 1 Arsenal 1 [Baada Dakika 120 1-1, Arsenal yasonga Penati 4-2]
Jumapili Aprili 13
Hull City 5 Sheffield United 3  
-FAINALI: Jumamosi Mei 17
Arsenal v Hull City 
 
MAN CITY YAADHIBIWA NA UEFA KWA KUKIUKA FFP! 

MAN_CITY-BINGWA_COC2014
MANCHESTER CITY imepewa Adhabu na UEFA kwa kukiuka Sheria za FFP [Financial Fair Play] ambazo zinataka Klabu zijiendeshe kwa Mapato yao wenyewe kwa kupigwa Faini ya Pauni Milioni 49 na Kikosi chao kubanwa kisizidi Wachezaji 21 na 8 kati yao ni lazima wawe Wachezaji Chipukizi waliokuzwa Nyumbani kwenye Mechi zao za UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu ujao.
Pamoja na hayo pia wametakiwa Msimu ujao wasizidishe Fungu la Fedha za Mishahara ya Wachezaji wao kupita lilivyo hivi sasa.
Kwenye Faini, City wametakiwa walipe Pauni Milioni 18 tu na nyingine kusimamishwa kuangaliwa mwenendo wao.
Mara baada ya kutangazwa Adhabu hiyo, Man City wamemesema wao hawakubaliani na uamuzi huo kwani wanaamini hawakukiuka FFP na hivyo watalipeleka mbele suala hili.
Vile vile, City wamesema kwenye Msimu huu wa UEFA CHAMPIONZ wao walitumia Wachezaji 21 tu hivyo hiyo Adhabu ya kuwabana wasizidishe Wachezaji 21 haitawaathiri sana.
Inaaminika Adhabu hiyo ni sawa na ile waliyopewa Paris Saint Germain kwa pia kukiuka FFP kama zilivyotolewa na Bodi ya Udhibiti Fedha ya UEFA, CFCB, [Club Financial Control Board].
Chini ya Sheria za FFP, Klabu zinatakiwa zisipate Hasara ya zaidi ya Pauni Milioni 37 katika Misimu miwili iliyopita.
Man City wao wamepata Hasara inayokaribia Milioni 149 kwa Misimu miwili iliyopita ikiwa ni Pauni Milioni 97 Mwaka 2012 na Pauni Milioni 51.6 kwa Mwaka 2013.
Man City na PSG ni miongoni mwa Klabu 9 ambazo zimetinga kwa CFCB na kupewa hadi mwishoni mwa Wiki hii kufikia makubaliano na UEFA  kuhusu Adhabu zao.
City wakikata Rufaa watasikilizwa na Jopo Maalum ambalo uamuzi wake hauna mjadala na upo uwezekano wa kuamuliwa Kifungo kwa City kutocheza Ulaya.

MAGAZETI YA MICHEZO NA BURUDANI

MAGAZETI YA UDAKU LEO

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI TAREHE 17.05.2014

ANGALIA PICHA ZA AJALI MBAYA ZILIZOTOKEA DAR

$
0
0
Toyota Coaster T 916 BQE  ikiwa imetumbukia mtaroni maeneo ya Sinza Mapambano.
Ikionekana kwa nyuma ilipokuwa ikivutwa baada ya kutumbukia mtaloni maeneo ya Sinza Mapambano.
Gari nyingine aina ya Toyota Coaster T 561 CJA  iliyoacha njia na kuingia mtaloni katika Barabara ya Mandela.
Ikionekana kwa nyuma mara baada ya kutumbukia mtaloni kwenye Barabara ya Mandela.
Gari ndogo aina ya Toyota Corolla iliyoharibiwa vibaya baada ya kugongwa na Coaster.
Wasamaria wema wakisaidia kulitoa gari, Toyota Corolla barabarani.
Gari moja lililokuwa likivutwa na ‘Breakdown’ mara baada ya kuharibika njiani. Haikufahamu gari hilo liliharibikia maeneo gani.
Ajalli mbaya zimetokea asubuhi hii maeneo ya Sinza Mapambano na baada ya gari kubwa (coaster) kuigonga gar ndogo (teksi) na kuingia mtaoni. Hakukuwa na watu walioumia vibaya.
Ajali nyingine imetokea katika Barabara ya Mandela ambapo coaster moja imeacha njia na kutumbukia mtaroni. Hakukuwa na abiria zaidi ya dereva peke yake ambaye hakuumia sana.
STORI NA PICHA: NYEMO CHILONGANI NA ANDREW CARLOS/GPL

MPENZI WA SAMIR NASRI AWAUDHI WAFARANSA BAADA NASRI KUACHWA NA TIMU YA TAIFA KATIKA FIFA 2014 BRAZIL

$
0
0
Chama cha soka cha Ufaransa kimepokea kwa hasira ujumbe ulioandikwa kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter na rafiki wa kike(Mpenzi) wa Samir Nasri.
Mapema wiki hii kiungo huyo wa Manchester City hakujumuishwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Ufaransa kitakachoenda Brazil kwenye michuano ya kombe la dunia licha ya kuonyesha uwezo mkubwa na kuisaidia klabu yake kushinda taji la ligi kuu ya Uingereza.
Mpenzi wake alitwaye,Anara Atanes alitumia mtandao wa Twitter kuonyesha hasira zake,ambapo aliandika,**** Ufaransa.Pia alimshambulia kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Ufaransa,Didier Deschamps.
Atanes aliandika: 
 F*** Ufaransa na f*** Deschamps! Nani s*** meneja!
Binti huyo alionyesha kukazia pointi yake,huku akirudi mtandaoni tena na kusema: 
 Kama huku soma tweet yangu vizuri..nitarudia binafsi…f*** Ufaransa na f*** Deschamps!
Mwanamitindo huyo alitumia tena Twitter siku ya Alhamisi usiku kuomba radhi kwa chochote alichokosea,ila alikataa kuomba radhi kwa Deschamps.
Huku akisisitiza:”Naomba msamaha kama nilimkosea mtu yeyote kutoka Ufaransa,ujumbe wangu kupitia Tweeter haukuwa lengo kwa nchi nzima kwa ujumla.”
Hivyo ikimaanisha kuwa ujumbe wa binti huyo ulimlenga moja kwa moja meneja wa timu ya Taifa ya Ufaransa pamoja na jopo lake la benchi la ufundi na sio kwa wananchi wa Ufaransa.
Didier Deschamps aliyewahi kuzinoa klabu za Monaco,Marseille na Juventus alishindwa kumjumuisha Samir Nasri kikosini kwa madai ya kwamba nyota huyo hana mchango kwenye timu ya Taifa ukilinganisha na klabuni kwake Manchester City.
Kitendo hicho kilizua maswali kwa watu wengi hususa kwa mashabiki wa klabu yake ambao walishuhudia kiungo huyo mshambuliaji akiisaidia vilivyo timu yao mpaka kufanikiwa kushinda makombe mawili msimu huu.
Nasri alipoulizwa alipokeaje taarifa za kutochaguliwa alisema,
 Nilijiandaa kabisa.Nilifahamu kabla,mara nyingine unakuwa na hisia.
Huku akielezea kuwa,
 Unapokuwa unataka kuzungumza na meneja,lakini yeye hataki kuzungumza na wewe,unafahamu kuwa hauendi kwenye kombe la dunia.
Viewing all 20290 articles
Browse latest View live