Mbunge wa viti maalum Magret Mkanga akikabidhiwa jiko na Range Jackson ambaye ni mwanafunzi mwenye mahitaji maalumu wakati alipotembelea katika banda la VETA, Katikati ni mwalimu wake Kintu Kilanga akishuhudia, Mafunzo ya Rangae yanakwenda sambamba na baba yake hayupo pichani.
Mbunge wa viti maalum Magret Mkanga akipewa maelezo na Mwalimu wa ufundi wa kuunga vyuma (Werding) Kintu Kilanga juu ya elimu inayotolewa kwa Range Jackson (kulia) mwanafunzi mwenye mahitaji maaalum(Matatizo ya akili katika kujifunza jamii imezoea kuwa ita Tahila) wakati alipotembelea katika banda la VETA lililopo kwenye maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam.
KAZANA UTAELEWA TUU,Mwalimu waufundi wa kuunga vyuma (Werding) Kintu Kilanga akimfuatilia mwanafunzi wake Range Jackson wakati alipokuwa akisaga chuma alichochomlea katika monesho ya 37 ya biashara ya Kimataifa Dar es Salaam, maarufu kwa jina la Sabasaba.VETA wamekuwa wakitoa elimu juu ya mafunzo wanaoyotoa katika chuo chao.
Range Jackson akiambaye ni mwanafunzi mwenye mahitaji maaalum(Matatizo ya akili katika kujifunza jamii imezoea kuwa ita Tahila) walimu wa VETA wanakataa kuwaita jina hilo kwa kuwainyesha kuwa wanafundishika ,Pichani akiwaonyesha askari Polisi waliotembelea katika banda lake kifaa maalumu kinachotumika kumsaidia kumfunza.
Kutokana na tatizo lake walimu wa VETA wamelazaimika kumfundisha mtoto na baba yake mzazi Jackson Range ili kumrahishia mafunzo yake kwa sababu baba atakuwa anakmkubushia masomo yake aikiwa nyumbani kwa sababu mtoto huiga mambo mazuri kutoka kwa wazazi .Katikati ni mwalimu wao Kintu Kilanga.Wananchi mnakaribishwa katika banda la Mafunzo ya Ufundi stadi VETA, mjionee mafunzo mbalimbali yanayotolewa na chuo hicho kwa vijana wetu.

Mke wa Makamu wa Rais Asha Bilal na mke wa Waziri Mkuu TunuNU Pinda wakiangalia moja ya nguo zinazotengenezwa na wanafunzi wa VETA wakati walipotembelea katika Banda hilo jana