Quantcast
Channel: MATUKIO NA VIJANA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 20290

MCHEZO WA NGUMI ZA KULIPWA WASITISHWA MPAKA MWISHO WA MFUNGO WA RAMADHANI

$
0
0
YASSIN ABDALLAH MWAIPAYA -USTAADH.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI -MICHEZO
NDG ZANGU WAPENDWA KTK MICHEZO, 
UONGOZI WA ORGANAIZESHENI YA NGUMI ZA KULIPWA TANZANIA (TPBO-LIMITED)
UNAPENDA KUWAJULISHA WADAU WOTE WA MCHEZO WA NGUMI ZA KULIPWA NCHINI TANZANIA ,KWAMBA KATIKA KIPINDI CHOTE CHA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI TUNASIMAMISHA SHUGHULI ZOTE ZA MCHEZO WA NGUMI ZA KULIPWA ZA ULINGONI MPAKA HAPO MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI UTAKAPOMALIZIKA.

HII HAINA MAANA KWAMBA OFISI ZETU ZITAFUNGWA BALI NYAKATI ZA KUFANYA KAZI ZA OFISI PIA ZITABADILIKA , ,BADALA YA OFISI KUFUNGULIWA SAA 2.00 ASUBUHI KAMA ILIVYO KAWAIDA HADI SAA 12.00 JIONI,

SASA KATIKA KIPINDI CHOTE CHA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI OFISI ZITAFUNGULIWA KUANZIA SAA 4.00 ASUBUHI HADI SAA 9.00 JIONI.

NA KATIKA KIPINDI CHOTE CHA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI TUTAKUWA TUNARATIBU MAPAMBANO AMBAYO YATAFANYIKA BAADA YA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI KUISHA [MUNGU AKITUJAALIA KUUMALIZA SALAMA TUKIWA HAI.

UONGOZI WA ORGANAIZESHENI YA NGUMI ZA KULIPWA TANZANIA [TPBO-LIMITED UNAWATAKIA WAISLAMU WOTE CHINI TANZANIA HERI NA BARAKA NYINGI KATIKA KIPINDI CHOTE CHA MFUNGO WA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI.

NA TUNAMUOMBA MWENYEZI MUNGU AIDUMISHE AMANI TULIYONAYO KATIKA KIPINDI CHOTE CHA MFUNGO WA RAMADHANI.

IMELETWA KWENU NAMI;-
YASSIN ABDALLAH MWAIPAYA -USTAADH
+255-713-644974 ,752-335584

Viewing all articles
Browse latest Browse all 20290

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>