Quantcast
Channel: MATUKIO NA VIJANA
Viewing all articles
Browse latest Browse all 20290

KUELEKEA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI LOWASSA AZUA GUMZO

$
0
0
 
Na Mwandishi Wetu
ZIKIWA zimebaki siku chache kabla ya kuanza Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, picha za Mbunge wa Monduli kwa tiketi ya CCM, Edward Lowassa akiwa amevaa mavazi ya Kiislam ya joho na hagali zimezua gumzo kubwa kwenye jamii wengi wakitaka kujua kama Waziri Mkuu Mstaafu huyo amebadili imani au la!

Hata hivyo, asili ya picha hizo zilizombadilisha mwonekano Lowassa ni mtandao mmoja wa kijamii ambao umetupia picha na maelezo kwamba, mbunge huyo ambaye kasi yake ya kisiasa nchini haishikiki, alikuwa akipongezwa na Kiongozi wa Sunni al Jamaa Afrika Mashariki, Shariff Hussein al Badawi kwa kumvika joho na kilemba baada ya kufanikisha harambee kwa ajili ya Kituo cha Redio Ikra kinachomilikiwa na Baraza la Waislam Tanzania (Bakwata) Mkoa wa Mwanza. 

ENEO LA TUKIO
Ishu hiyo ilijiri usiku wa Ijumaa iliyopita katika Ukumbi wa Hoteli ya Gold Crest jijini Mwanza hivyo kuondoa utata kwamba, alivaa vazi hilo na kuzama nalo msikitini kitendo ambacho baadhi ya watu walisema si sahihi kama mheshimiwa huyo hajabadili imani yake. Lowassa ni wa imani ya KKKT.NA GLOBAL PUBLISHER









Viewing all articles
Browse latest Browse all 20290

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>